Vichaa wa siku hizi wamekuwa legelege sana, wapole na wavivu

kidole cha simba

JF-Expert Member
Jun 3, 2022
1,290
1,656
Naomba niandike kitu kama pumba flani lakini inafikirish kidogo.

Nakumbuka zamani nilipokuwa mdogo kule kijijini kwetu msinga-kibosho marehemu bibi yangu (ndo nilikuwa nikiishi nae, wazazi wangu na wadogo zangu wao waliishi Dar) alikuwa akiniasa wakati akinituma, "usipite mtaa ule kuna kichaa mkali sana si unamfahamu kichaa PAULO? "naitikia ndio.....si unajua anapiga watu? basi tafadhli usipite pale.

Na kweli kichaa Paulo alikuwa noma na alikuwa na pumzi ya ajabu, alikuwa na uwezo wa kukimbia siku nzima bila kupumzika, pia mara chache shangazi yangu aliyekuwa akiishi pale mjini moshi, wakati wa likizo alikuwa akinichukua kwenda kupumzika kwake.

Sasa pale mjini Moshi kulikuwa na vichaa wengi sana na ajabu wengi wao walitokes sehemu iitwayo URU, unaopatikana sehemu iitwayo kishumundu, sio kwamba nazodoa, hapana watu wa URU wana akili sana ndo manake wengi wao ni maingeneer. Sasa wale ambao hawakuendelea na shule ili akili zipoozwe ndo walikuwa wakidata.

Anyway ilikuwa ni vurugu, huwezi toka mpaka uongozane na mkubwa. Hata ukisoma Biblia, YESU alimkuta kichaa mkali sana, unaambiwa kwa mujibu wa maandishi huyo chizi alikuwa na nguvu za ajabu na alikuwa na mapepo kibao kichwani (sijui ndo majini)

Unaambiwa YESU likomaa nao mpaka ikabidi ayaamrishe yale majini yaende kuwaingilia nguruwe, na waliwaingilia nguruwe nao nguruwe walichizika kama wamekula msuba, wote walikimbilia mtoni.

Sasa tuje kwenye vichaa hawa wa DOTCOM, vichaa hawa bwana wamekuwa wavivu sana, hawakimbii tena. Hata kutembea kwao wananyata, kuongea hawaongei achana na kupiga kelele kama vichaa wa longi, kutwa wamelala majalalani. Yaani sasa hivi kama kichaa kalala barabrani unamkamata mguu na kumvutia kando ya barabara huku yeye akikuangalia kwa jicho la huzuni!

Vichaa wa sasa hivi ni wembamba kama miwa, tofauti na wa zamani waliokuwa na kifua kama mandonga. Vichaa wa siku hizi hawabaki akina dada kama wa zamani wala hawapigi punyeto kama wa zamani, wala hawatembei uchi kama wa zamani!

Lakini katika kutafakari sana nikagundua jambo moja. Inawezekana utitiri wa makanisa ya walokole na kuongezeka kwa walokole na mikesha yao ya usiku na mchana, imesababisha hawa majini wanaoshi ndani ya vichwa vya hawa vichaa, kupooza na kunyon'gonyea kabisa, au nimekosea mazee?
 
Zamani kulikua na vichaa OG, sasa hivi ugumu wa maisha + madeni mtu anaona bora ajifanye chizi tu.
ina maana vichaa wote ni kwa sababu ya ugumu wa maisha ndo manake wamelegea???,,,kichaa wa zamani alikuwa anapokonya vitu au anachukua kibabe kwani kichaa afanyi kazi,biashara wala kulima,,,,sasa imekuaje?
 
Uandishi wako changamoto.

Anyway ninakumbuka miaka ya 90 kule Kibosho Manushi Sinde kuna kichaa alikuwa mkali sana na alimuua mtoto mmoja aliyekuwa anateka maji chemchem iliyokaribu na Shule ya Msingi Manushi Chini.

Ninamkumbuka huyu mtoto (age mate wangu wakati huo) aliitwa Kadadaa(RIP).

Vichaa wa zamani walikuwa tishio sana.
 
Uandishi wako changamoto.

Anyway ninakumbuka miaka ya 90 kule Kibosho Manushi Sinde kuna kichaa alikuwa mkali sana na alimuua mtoto mmoja aliyekuwa anateka maji chemchem iliyokaribu na Shule ya Msingi Manushi Chini.

Ninamkumbuka huyu mtoto (age mate wangu wakati huo) aliitwa Kadadaa(RIP).

Vichaa wa zamani walikuwa tishio sana.
uandishi wangu ni mmbovu manake wakati naandika nilikuwa nimekunywa double kick!!!,,,so mikono ikawa inacshake na kalam yangu ilikuwainaishia wino,,,so nikawa naandika chapchap wino usiishe!!
 
Nilishawahi temewa mate na chizi na sikumfanya chochote miaka ya 2000 mwanzoni.
 
ungepata supu kidogo ili mikono ikakamae
nimepewa supu hapa,,ila kila nikishika kijiko supu inamwagika na nikimamata bakuli naogopa supu yote itamwagika,,,,so,,,mama muuza kaniomba nisubiri kidogo mume wake aondoke{kajamaa kana wivu sana],then ataninywesha!!
 
Back
Top Bottom