teddy isaac
New Member
- Jun 4, 2012
- 4
- 0
ndoa cyo majaribio ts a lyftym commitment, so ni bora kuoa au kuolewa na m2 umpendaye sana coz ni rahic kumvumilia kuliko ucye mpenda sana.
Mtizamo wangu ni kwamba oa au olewa na m2 anayekupenda kwa sababu ni rahis kujlazmisha kumpenda m2 usiyemfeel kuliko kumbadilisha acyekupenda akupende.
ndoa sio kitu cha mchezo wala majaribio..... Unapaswa kuoa/olewa na mtu unayempenda......
Unadhani kuishi na mtu ambaye huna mapenzi nae kivile ni mchezo?
BadiliTabia...Sikubaliani nawe moja kwa moja kwa haya uyasemayo. Wasichana/wanawake wengi hapa Bongo siku hizi hawaolewi na mtu eti kwa sababu wanampenda; hapana, ila wanafuata material things. Haswa ukiangalia idadi kubwa ya wanawake wanao olewa na hawa vijana wa kuuza unga, unataka kuniambia they are there for the love? Heck no, but they'll do anything na watakubali kunyanyasika ili waonyeshe kuwa wako serious na ndoa zao. Mwanamke gani mwenye akili timamu anakubali kuwa a spare tyre? Nasema hivi kwa sababu vijana wengi wenye mahela machafu hapa Bongo, yaani asilimia 100 ni malaya na wake zao wanajua hivyo lakini wanavumilia because they are there for the ride. Kutoka kwenye ndoa zao hawawezi kwani walishatambia wenzao kabla ya kuolewa, na akitoka hapo ataenda wapi kwenye matanuzi kama aliyonayo? Binafsi, najua jamaa kama watatu hivi wameoa na wapigaji mademu hodari sana hapa jijini. Cha kusikitisha wake zao wote wanajua na mara nyingi huwa wanawambia waume zao mwenzangu tafadhali jichunge huko nje na kina mama, au utasikia shemeji tafadhali muonyeni rafiki yenu jamani kwani najuwa vitu vyake huko nje. Karne hii ya 21 hakuna love Bongo, kama wewe una mapenzi Mungu akubariki ila pia nakusitikia kwani kina mama wengi kama wewe ndio wanaopelekeshwa kwenye ndoa zao na huishia kujiua kwa kutovumilia manyanyaso ya ndoa. Pole sana yasije kukukuta dada yangu ila ukweli ndo huo.
Katika hali ya kawaida mtu huweza kushangaa hoja hii. Ukweli ni kuwa watu wengi wanafikiri wakioa au kuolewa na watu wanaowapenda sana maisha huwa ya furaha sana lakini wengi wamekuwa wakilazimika kufanya mambo hata nafsi zao hazipendi kwa kuwa tu wanaogopa wampendae atachukia au atamwacha. Ni vyema basi mtu kuoa au kuolewa na mtu umpendae wastani ili kuwa na kuambiana tunavyopenda na tusivyopenda vinginevyo tutaogopa kuwaudhi watu tunaowapenda kupita kiasi.
WEWE UNAONAJE? NI VYEMA AU SI VYEMA KUOA AU KUOLEWA NA MTU UMPENDAE KUPIATA KIASI?