Kazi ambazo ni rahisi kukuingiza kwenye laana wewe na familia yako kama hutokuwa makini

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kazi ni shughuli yoyote halali inayokuingizia kipato. Shughuli hiyo lazima izingatie haki za wengine yaani kutodhulumu au kuharibu haki za wengine. Hiyo ndio huitwa kazi. Sio uuze madawa ya kulevya au uwe mwizi au fisadi au kahaba uiite hiyo ndio kazi. Hakuna kitu kama hicho. Hizo sio kazi.

Kijana, utakapokuwa mkubwa na ukatafuta shughuli ya kufanya itakayokuwa kazi kwako lazima uzingatie kuwa haimdhulumu mtu yeyote haki zake ikiwemo wewe mwenyewe. Ninakuhakikishia utakuwa na Furaha na amani siku zote za maisha yako.

Haki ni pamoja na Riziki. Riziki ni kupata kile anachostahili kulingana na ulichofanya. Hiyo ndio maana ya Riziki. Kushukuru kwa haki uipatayo kwa kile ulichofanya (riziki yako) ni kujipa Haki katika nguvu na jasho lako. Kuzidisha riziki yako isivyo halali ni kudhulumu haki za wengine.

Watibeli hatuoni aibu wala haya kuwa na maisha ya aina yoyote ile ikiwa tuu ni haki yetu. Mathalani, mtu anaweza akawa amesoma sana lakini akakosa kuajiriwa akaanza kulaumu na kujidhulumu nafsi yake.

Unakuta mtu anajiambia au kusema Haya sio maisha yangu. Sikupaswa kuwa hivi nilivyo. Huo ndio huwa mwanzo wa kudhulumu wengine au kujidhulumu.

Watibeli kwetu maisha mazuri ni kuishi kwa Haki, kutowatendea wengine mabaya lakini kuukataa ubaya kwa nguvu zote. Na hii haimaanishi kuwa sisi ni watakatifu. Bali ni kuhakikisha wajibu wetu wa kutoa na kutenda haki unafanyika kwa sababu huo ndio ukweli, upendo na Akili.

Zifuatazo ni kazi ambazo usipokuwa Makîni utajikuta unajiingiza kwenye Laana wewe na familia yako;

1. Upolisi
Upolisi ni kazi nzuri lakini ipo katika mazingira hatarishi ya kumfanya mtu atende dhulma. Polisi usipokuwa makini kujiingiza kwenye laana ni dakika sifuri tuu.

Hata hivyo hakuna kisingizio hata kimoja cha mtu kutotenda HAKI. Mtu yeyote anayefanya dhulma mara nyingi huamua kuchagua dhulma. Polisi husingizia kuwa Wanaagizwa kufanya mambo na waliapa kutii wakubwa zao lakini hakunaga kiapo cha kumtii shetani.

Polisi, UNAOWAJIBU wa kutii mkubwa wako anayekuagiza HAKI. Huko sio kumtii huyo mkubwa wako hali kumtii akiyekuumba, na kujiheshimu wewe kama Mtu. Kumtii mkubwa wako anayekuagiza kufanya dhulma ni kumtii Shetani na kujidharau utu wako na kudhulumu haki za Wengine.

Niliwahi kuandika pia kuwa wakubwa hukutuma kazi za dhulma wakishakuona wewe ni wadhulma dhulma. Huwezi kuwa polisi wa Haki alafu kisabengo fulani kisa kina cheo kukuzidi kikutume kazi chafu never ever kwenye huu ulimwengu.

Kikawaida Wakubwa wenyewe wanajua kuwa wewe ni mtu wa aina gani. Hivyo wanakupa kazi kulingana na wanavyokuona na ulivyojionyesha kwao.

Sasa mtu umdhulumu mtu haki yake kisa kazi ya mshahara wa milioni moja. Hata mtu mjinga hawezi kufanya hivyo. Ni bora uache kazi kuliko mkuu wako wa kazi kukuingiza kwenye dhulma na anakutishia kukufukuza kazi.

Haya kuna ile unadhulumu kwa maamuzi yako. Yaani hujatumwa na mtu. Unachukua jasho la mtu mwingine. Unabambikia kesi Watu. Familia zao zinateseka ili yako ile. Yaani mkeo na watoto wanakula jasho na machozi ya Watu wengine na wewe unajihisi Comfortable. Hiyo ni laana Mpumbavu wewe.

Watibeli, hawawezi kuoa au kuolewa na Polisi ambaye hatendi HAKI. Kwa Watibeli ni mara elfu kuwa maskini na kuishi maisha ya dhiki kuliko kujilaghai na furaha ya uongo kwa kuumize wengine.

Maisha yana maana kubwa kwa Watu wanaotenda Haki na wenye UPENDO, lakini siku zote, maisha ni ubatili na hayanaga maana kwa Watu waovu na wenye kudhulumu.

2. Uwakili na Uanasheria
Taikon ni mwanasheria kiasili. Watibeli wote ni wanasheria kiasili. Huwezi kuwa Mtibeli bila kuwa mwanasheria. Zipo sheria za wenye haki na zipo sheria za waovu. Watibeli lazima sheria zote hizo tuzijue, za wenye haki na waovu.

Taaluma yako ni sheria. Upo kwaajili ya kutetea Haki, kufundisha na kuelekeza jamii haki. Badala ya kuitetea haki unakuwa Wakili wa kutetea wahalifu na waovu walioamua kuwa wahalifu kimakusudi. Hiyo ni LAANA kubwa. Huwezi furahia maisha kwa kufanya dhulma.

Siku zote muovu huona siku zinakimbia kwa sababu hana subira. Huona maisha ni mafupi kwa sababu ya ubinafsi ndio maana hufanya haraka na kujikuta kwenye kufanya dhulma.

Huyu kaua, au Kabaka, au katiba, au kafanya uhalifu fulani. Na Wakili imeshakuwa jambo hilo. Jukumu lako sio kumtetea awe huru bali jukumu lako ni kutetea haki ya mkosaji apewe kile anachostahili. Sio kumlinda, huwezi kulinda uovu na waovu. Huwezi kumlinda shetani na Ushetani.

Ni jukumu lako kuhakikisha kuwa Mahakama haimuonei mkosaji kwa kumpa adhabu kubwa kupita kiasi au ndogo. Bali uhakikishe mahakama inampa huyo mteja wako haki yake.

Ni laana kumficha mhalifu na kupotosha haki ya aliyeonewa. Huko ni kuwa mtumwa wa shetani. Ni kujitesa mwenyewe. Na kuiingiza familia yako kwenye laana kwa vipande vya fedha kama Yuda.

Wewe ni msaliti kama wasaliti Wengine.

3. Hakimu, jaji, kadhi na watoa Hukumu.
Hakuna kazi nzuri kama hiyo. Yaani kutoa hukumu ni kazi nzuri kwa sababu upo kama Mungu. Umebeba uwakilishi wa Mungu yaani wewe ni wakili wa Mungu. Kuhakikisha Haki inafanyika kwa gharama yoyote ile.

Kumlinda mhalifu na Muovu kimakusudi ni laana. Unapotosha hukumu. Yaani Jaji unaona kabisa haki iko hapa lakini unaipindisha kimakusudi kwa visingizio vya kijinga. Mara sijui nitafukuzwa kazi. Huwezi kufukuzwa kazi ya Mungu boya wewe.

Mungu ndiye mtoaji wa kazi. Yeye ndiye anakupa kazi ili akupe riziki yako. Ajira unapewa na Watu ila kazi utapewa na Mungu. Ukifanya yasiyostahili kwa kazi aliyokupa Mungu ndio basi tena. Mungu akikúfukuza kazi hutokuja upate popote pale.

Yaani unaweza kuwa na ajira lakini usiwe na kazi. Kwa sababu ajira haikupi riziki, lakini kazi inakupa riziki.

Kuna mambo Watu hawayaelewi acha nitoe ufafanuzi Kidogo.
Riziki inasifa zifuatazo:

i) Riziki inayotoka kwa Mungu lazima ifanye lengo utakalolipanga. Yaani kama ulipanga jambo fulani lazima ulitimize.

ii) Riziki huleta furaha ndani ya familia. Yaani unatimiza malengo yako. Kama kujenga nyumba na magari na vyote unavyofanya vinakupa amani na furaha. Hiyo ndio Riziki lakini Ajira inakupa Ujira ambao unaweza usiwe Riziki.

Sio ajabu mtu anaajira na analipwa Ujira mkubwa lakini Riziki yake ni ndogo. Ukitaka kujua jambo hili utaangalia mambo yafuatayo;

1. Anapata ujira inaweza kuwa mkubwa lakini haoni malengo yake yakitimia kwa Wakati. Hii ni kwa sababu anaharaka kuliko wakati wa Muumba wake. Kwa hiyo anazidisha kuwa mdhulmati ili atimize malengo kwa haraka.

2. Akitimiza malengo yake hayampi furaha. Yaani anaona alikuwa anapoteza muda. Na mara zote malengo yake yaliyotimia lazima yamuumize. Mfano anaweza kujenga nyumba nzuri na nyumba hiyohiyo mkewe akawa anafanywa na Watu wengine.

Au anaweza kujenga nyumba lakini muda wa kukaa ndani ya nyumba hiyo hana. Na siku akikaa ndio siku atakayokuwa anaumwa magonjwa mazito ambayo yatamfanya asione umuhimu wa ukubwa na fahari ya nyumba yake hiyo.

Kitu ambacho hakitoki kwa Mungu yaani sio riziki lazima kikusumbue na kihakikishe unateseka kwa sababu ni dhulma.

Shida ya dhulma ni pale ambapo Watu wa nje wanakuheshimu lakini wale unaotaka wa kuheshimu hawakushemu ili ikuume. Ni kawaida kukuta mke wa mdhulmati akimtesa mumewe kwa namna yoyote ile iwe kumbambikia watoto, iwe kulala na shamba boy, iwe kumnyima unyumba na mateso mengine kama hayo. Huwezi kuwa mwenye haki Maisha yakakusumbua, never ever.

4.
Kwa leo niishie hapo. Acha nipumzike sasa. Kama unataka maisha yasikupe shida yàani yawe kama unakunywa uji basi penda na fanya Haki, upendo, ukweli na Akili.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
uroho wa kutokutosheka ndo mbaya lakini dhulma kuna muda inabidi/inakulazimu

yaani mungu huyohuyo kakuweka kwenye maisha duni mpaka unafika kwenye dhulma halafu wewe ndo ulaumiwe sio yeye? laana ni imani potofu za washamba

kiujumla sheria haipo kwenye haki wanasema 'the law is not right, it is just' kuna hukumu nyingi za kisheria watu hawakubaliani nazo

sheria ni ngumu sana kuijadili katika muktadha wa haki na dhulma, kwahiyo hapo kwenye wanasheria na mahakimu, labda utafute mmoja uzungumze nae
 
Kila kitu kinamakadirio.
Unaweza ukawa umezaliwa kwenye mazingira duni lakini ukifanya kazi kwa bidii, juhudi na akili kwa haki mabadiliko polepole ya mafanikio yanatokea na sio lazima uwatie wengine kwenye dhiki ili ujinasue kwenye shimo ulilomo.
 
Sidhani kama unaweza toboa kwenye uchumi wa CCM bila dhulma. Hili tutabishana wee ila ni ukweli. Bidii na kujituma havitokufikisha mbali

Kuna matatizo mtu akiyapata akafanya dhulma kujikomboa ni sawa

Labda ushauri watu waridhike na maisha duni
 
Wapo wengi
Wachungaji
Waalimu
Viongozi wa siasa,wenyeviti wa mtaa
Askari wanyamapori
Nesi
Ndugu wa karibu
Wote wote
Sister ,padre
Shahid wa uongo
Msema uongo yeyote
Shehe
Waumini
Wevi
Madalali
Wala rushwa wote
Madereva
Majambazi
Walawiti
Wasinguziaji
 
Raana ni vitu vyakufikilika tu ni km uchawi ukiamini uchawi upo bas utauona na madhara yake utayaona ila ukiamin akuna uchawi huto uona na madhala yake utoyaona wala kuyahisi

Una raaniwaje na mtu usomjua unapataje rahana kwa kufanya kazi na majukumu yako uloajiliwa au kusomea kuyafanya
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kazi ni shughuli yoyote halali inayokuingizia kipato. Shughuli hiyo lazima izingatie haki za wengine yaani kutodhulumu au kuharibu haki za wengine. Hiyo ndio huitwa kazi. Sio uuze madawa ya kulevya au uwe mwizi au fisadi au kahaba uiite hiyo ndio kazi. Hakuna kitu kama hicho. Hizo sio kazi.

Kijana, utakapokuwa mkubwa na ukatafuta shughuli ya kufanya itakayokuwa kazi kwako lazima uzingatie kuwa haimdhulumu mtu yeyote haki zake ikiwemo wewe mwenyewe. Ninakuhakikishia utakuwa na Furaha na amani siku zote za maisha yako.

Haki ni pamoja na Riziki. Riziki ni kupata kile anachostahili kulingana na ulichofanya. Hiyo ndio maana ya Riziki. Kushukuru kwa haki uipatayo kwa kile ulichofanya (riziki yako) ni kujipa Haki katika nguvu na jasho lako. Kuzidisha riziki yako isivyo halali ni kudhulumu haki za wengine.

Watibeli hatuoni aibu wala haya kuwa na maisha ya aina yoyote ile ikiwa tuu ni haki yetu. Mathalani, mtu anaweza akawa amesoma sana lakini akakosa kuajiriwa akaanza kulaumu na kujidhulumu nafsi yake.

Unakuta mtu anajiambia au kusema Haya sio maisha yangu. Sikupaswa kuwa hivi nilivyo. Huo ndio huwa mwanzo wa kudhulumu wengine au kujidhulumu.

Watibeli kwetu maisha mazuri ni kuishi kwa Haki, kutowatendea wengine mabaya lakini kuukataa ubaya kwa nguvu zote. Na hii haimaanishi kuwa sisi ni watakatifu. Bali ni kuhakikisha wajibu wetu wa kutoa na kutenda haki unafanyika kwa sababu huo ndio ukweli, upendo na Akili.

Zifuatazo ni kazi ambazo usipokuwa Makîni utajikuta unajiingiza kwenye Laana wewe na familia yako;

1. Upolisi
Upolisi ni kazi nzuri lakini ipo katika mazingira hatarishi ya kumfanya mtu atende dhulma. Polisi usipokuwa makini kujiingiza kwenye laana ni dakika sifuri tuu.

Hata hivyo hakuna kisingizio hata kimoja cha mtu kutotenda HAKI. Mtu yeyote anayefanya dhulma mara nyingi huamua kuchagua dhulma. Polisi husingizia kuwa Wanaagizwa kufanya mambo na waliapa kutii wakubwa zao lakini hakunaga kiapo cha kumtii shetani.

Polisi, UNAOWAJIBU wa kutii mkubwa wako anayekuagiza HAKI. Huko sio kumtii huyo mkubwa wako hali kumtii akiyekuumba, na kujiheshimu wewe kama Mtu. Kumtii mkubwa wako anayekuagiza kufanya dhulma ni kumtii Shetani na kujidharau utu wako na kudhulumu haki za Wengine.

Niliwahi kuandika pia kuwa wakubwa hukutuma kazi za dhulma wakishakuona wewe ni wadhulma dhulma. Huwezi kuwa polisi wa Haki alafu kisabengo fulani kisa kina cheo kukuzidi kikutume kazi chafu never ever kwenye huu ulimwengu.

Kikawaida Wakubwa wenyewe wanajua kuwa wewe ni mtu wa aina gani. Hivyo wanakupa kazi kulingana na wanavyokuona na ulivyojionyesha kwao.

Sasa mtu umdhulumu mtu haki yake kisa kazi ya mshahara wa milioni moja. Hata mtu mjinga hawezi kufanya hivyo. Ni bora uache kazi kuliko mkuu wako wa kazi kukuingiza kwenye dhulma na anakutishia kukufukuza kazi.

Haya kuna ile unadhulumu kwa maamuzi yako. Yaani hujatumwa na mtu. Unachukua jasho la mtu mwingine. Unabambikia kesi Watu. Familia zao zinateseka ili yako ile. Yaani mkeo na watoto wanakula jasho na machozi ya Watu wengine na wewe unajihisi Comfortable. Hiyo ni laana Mpumbavu wewe.

Watibeli, hawawezi kuoa au kuolewa na Polisi ambaye hatendi HAKI. Kwa Watibeli ni mara elfu kuwa maskini na kuishi maisha ya dhiki kuliko kujilaghai na furaha ya uongo kwa kuumize wengine.

Maisha yana maana kubwa kwa Watu wanaotenda Haki na wenye UPENDO, lakini siku zote, maisha ni ubatili na hayanaga maana kwa Watu waovu na wenye kudhulumu.

2. Uwakili na Uanasheria
Taikon ni mwanasheria kiasili. Watibeli wote ni wanasheria kiasili. Huwezi kuwa Mtibeli bila kuwa mwanasheria. Zipo sheria za wenye haki na zipo sheria za waovu. Watibeli lazima sheria zote hizo tuzijue, za wenye haki na waovu.

Taaluma yako ni sheria. Upo kwaajili ya kutetea Haki, kufundisha na kuelekeza jamii haki. Badala ya kuitetea haki unakuwa Wakili wa kutetea wahalifu na waovu walioamua kuwa wahalifu kimakusudi. Hiyo ni LAANA kubwa. Huwezi furahia maisha kwa kufanya dhulma.

Siku zote muovu huona siku zinakimbia kwa sababu hana subira. Huona maisha ni mafupi kwa sababu ya ubinafsi ndio maana hufanya haraka na kujikuta kwenye kufanya dhulma.

Huyu kaua, au Kabaka, au katiba, au kafanya uhalifu fulani. Na Wakili imeshakuwa jambo hilo. Jukumu lako sio kumtetea awe huru bali jukumu lako ni kutetea haki ya mkosaji apewe kile anachostahili. Sio kumlinda, huwezi kulinda uovu na waovu. Huwezi kumlinda shetani na Ushetani.

Ni jukumu lako kuhakikisha kuwa Mahakama haimuonei mkosaji kwa kumpa adhabu kubwa kupita kiasi au ndogo. Bali uhakikishe mahakama inampa huyo mteja wako haki yake.

Ni laana kumficha mhalifu na kupotosha haki ya aliyeonewa. Huko ni kuwa mtumwa wa shetani. Ni kujitesa mwenyewe. Na kuiingiza familia yako kwenye laana kwa vipande vya fedha kama Yuda.

Wewe ni msaliti kama wasaliti Wengine.

3. Hakimu, jaji, kadhi na watoa Hukumu.
Hakuna kazi nzuri kama hiyo. Yaani kutoa hukumu ni kazi nzuri kwa sababu upo kama Mungu. Umebeba uwakilishi wa Mungu yaani wewe ni wakili wa Mungu. Kuhakikisha Haki inafanyika kwa gharama yoyote ile.

Kumlinda mhalifu na Muovu kimakusudi ni laana. Unapotosha hukumu. Yaani Jaji unaona kabisa haki iko hapa lakini unaipindisha kimakusudi kwa visingizio vya kijinga. Mara sijui nitafukuzwa kazi. Huwezi kufukuzwa kazi ya Mungu boya wewe.

Mungu ndiye mtoaji wa kazi. Yeye ndiye anakupa kazi ili akupe riziki yako. Ajira unapewa na Watu ila kazi utapewa na Mungu. Ukifanya yasiyostahili kwa kazi aliyokupa Mungu ndio basi tena. Mungu akikúfukuza kazi hutokuja upate popote pale.

Yaani unaweza kuwa na ajira lakini usiwe na kazi. Kwa sababu ajira haikupi riziki, lakini kazi inakupa riziki.

Kuna mambo Watu hawayaelewi acha nitoe ufafanuzi Kidogo.
Riziki inasifa zifuatazo:

i) Riziki inayotoka kwa Mungu lazima ifanye lengo utakalolipanga. Yaani kama ulipanga jambo fulani lazima ulitimize.

ii) Riziki huleta furaha ndani ya familia. Yaani unatimiza malengo yako. Kama kujenga nyumba na magari na vyote unavyofanya vinakupa amani na furaha. Hiyo ndio Riziki lakini Ajira inakupa Ujira ambao unaweza usiwe Riziki.

Sio ajabu mtu anaajira na analipwa Ujira mkubwa lakini Riziki yake ni ndogo. Ukitaka kujua jambo hili utaangalia mambo yafuatayo;

1. Anapata ujira inaweza kuwa mkubwa lakini haoni malengo yake yakitimia kwa Wakati. Hii ni kwa sababu anaharaka kuliko wakati wa Muumba wake. Kwa hiyo anazidisha kuwa mdhulmati ili atimize malengo kwa haraka.

2. Akitimiza malengo yake hayampi furaha. Yaani anaona alikuwa anapoteza muda. Na mara zote malengo yake yaliyotimia lazima yamuumize. Mfano anaweza kujenga nyumba nzuri na nyumba hiyohiyo mkewe akawa anafanywa na Watu wengine.

Au anaweza kujenga nyumba lakini muda wa kukaa ndani ya nyumba hiyo hana. Na siku akikaa ndio siku atakayokuwa anaumwa magonjwa mazito ambayo yatamfanya asione umuhimu wa ukubwa na fahari ya nyumba yake hiyo.

Kitu ambacho hakitoki kwa Mungu yaani sio riziki lazima kikusumbue na kihakikishe unateseka kwa sababu ni dhulma.

Shida ya dhulma ni pale ambapo Watu wa nje wanakuheshimu lakini wale unaotaka wa kuheshimu hawakushemu ili ikuume. Ni kawaida kukuta mke wa mdhulmati akimtesa mumewe kwa namna yoyote ile iwe kumbambikia watoto, iwe kulala na shamba boy, iwe kumnyima unyumba na mateso mengine kama hayo. Huwezi kuwa mwenye haki Maisha yakakusumbua, never ever.

4.
Kwa leo niishie hapo. Acha nipumzike sasa. Kama unataka maisha yasikupe shida yàani yawe kama unakunywa uji basi penda na fanya Haki, upendo, ukweli na Akili.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Daah! Nakubaliana na wewe
 
Back
Top Bottom