Ukimwi unaniuwa kwa haraka jamani

ninmwezi mmoja tu tambu ni fanye mapenzi na dada ambaye baada kumfanya tulienda maabara kupima maana nilimuona anavutia sana na alikuwa na umri wa miaka 19 tu hivyo nikaamini atakuwa mzima. Baada ya kumfaidi nikajenga hoja ya kujua afya zetu na tulivyopima sikuamini matokeo binti alikutwa na UKIMWI na hakuwa na wasiwasi kabisa akaanza kunipa pole.

Naomba msaada wandugu kama kunaaina ya kipimo ambacho naweza kufanya nikawa na uhakika wa afya yangu maana mala tumbo, kichwa, usingizi saa 8 unakatika, kichefuchefu, mafua na kikohozi, mwili kuwasha. hayo ni machache tu kwa dalili na magonjwa niliyonayo.

haja yangu sio kujianika kwa umalaya wangu bali nimeamua kuandika hapa nikijieleza kwa DR ili niweze kupata msaada wa aina ya kipimo maana rapid test inaonyesha hakuna tatizo lakini mpaka miezi mitatu ndipo huwa na uhakika lakini iwapo kunakipimo ambacho naweza kujua hali yangu ndani ya hizi wiki 6 tangu nikutane kimwili na yule dada nitafurahi.
mh! yaani hata hodi hakuna jameni...unaingia tu na kuja na stori zako za kugegedana kavukavu! lkn pole!
 
China kuna watu walishawahi kuugua na kuoneesha dalili zote za ngome,lakini walikuwa kila wakipiMwa ni negative.Wataalam wanasema Ukiwa unawaza kuwa umeambukizwa ukimwi bila kupima,na mawazo hayo yakaendelea kwa muda wa mwezi mzima,UTAANZA KUUGUA DALILI ZOTE ZA NGOMA HAPA CHINI,kumbuka hizi ni dalili za HIV na sio AIDS.
  • Lack of energy
  • Weight loss
  • Frequent fevers and sweats
  • Persistent or frequent yeast infections
  • Persistent skin rashes or flaky skin
  • Short-term memory loss
  • Mouth, genital, or anal sores from herpes infections.

Mkuu sijakuelewa vizuri hapo pekundu.Ungefafanua vizuri kwa faida ya wengi.
 
Yaani mwezi mmoja tu uanze kupata magonjwa nyemelezi?!!.
Wewe utakua umepanick.

Hofu ni ugonjwa mbaya sana,ndugu yangu tuliza akili yako.Uliposikia mdada ni mwathirika ulipanic.Ndicho kinachokusumbua nenda angaza watakupa ushauri mzuri sana.
 
Mkuu sijakuelewa vizuri hapo pekundu.Ungefafanua vizuri kwa faida ya wengi.



Mtu mwenye ukimwi/AIDS ana dalili zinazoonekana dhahiri ndizo kazitaja hapo juu. Kwa hali ya kawaida dalili hizo husababishwa na HIV. Sasa kuna baadhi ya wagonjwa wana dalili zote hizo lakini wanapopimwa hawakutwi na HIV ... Soma post zangu nyuma nimesama kuna uwezekano.. EMOTIONAL PARASITES ...

Utaelewa zaidi uki google " AIDS WITHOUT HIV" ukasoma kwa makini...
 
Pole ana ndugu yangu, unajua si vizuri kuchanganyikiwa hali hujahakikisha kwamba u mgonjwa au umeathirika, nachoamini mimi ni kwamba, kujua kwamba u mzima au mgonjwa ni tiba tosha ndugu yangu .fanyavipimo uweze jua kisha ujitunze.
 
Elisa test haiwezi kuonyesha results kwa hiyo time frame,thats why anaonekana bado hana kitu kwa kuwa yenyewe inaangalia antibodies,ila PCR(Polymerase Chain Reaction) inaweza kuonyesha hata kama ni few days but ni expensive na si hospital zote wana machine hizo.

Mkuu asante kwa msaada wako, naomba kujua pia ghalama zake maana nilifika hapa Singida rufaa wakasema hakuna zaidi ya hizo za miezi 3. Nikijua ghalama zake naweza kujipanga na kuja Dar maana ndipo karibu kutoka hapa Singida. Asante tena
 
Pole sana ndugu yangu yangu kwa hilo,ila mimi nina mambo kadhaa ya kuksema:

Kwanza sio kila unapofanya mapenzi na mtu mwenye VVU utaambukizwa. Kumbuka tumekuwa tunafanya mambo haya mara kadhaa na watu wenye VVU bila kujua na hakuna shida yoyote tunayopata;ni bahati nzuri tu kwamba nyie mlienda kupima soon after hilo tendo..huo ni ujasiri wa hali ya juu na unastahili kupongezwa.

Pili,huna haja ya kukosa amani kiasi hicho.Hilo limeishatokea,limetokea,unachotakiwa ni kufocus mbele na kuendelea na maisha yako kama awali.Najua hii ni chungu kumeza,lakini je ikiwa umeambukizwa,what next?! Hakuna haja ya kuhangaika mahospitalini kutafuta kipimo,unaweza kukipata kwa gharama ya juu sana,maana inaonekana uko radhi kutoa kiasi chochote cha pesa mradi tu ujue afya yako.Swali,sasa ukishajua umeambukizwa,nini kinafuata?! Na je ukiambiwa hujaambukizwa,unadhani itakuwa kinga ya kuzuia kuambukizwa tena?! Nachotaka kusema hapa ni kwamba wewe endelea na maisha yako kama kawaida huku ukisubiri hiyo miezi 3 ipite ukapime tena ili kujiridhisha..

Inavyooneka wewe ni kijana na yumkini upo chuoni,unachotakiwa kujua ni kwamba bado unayo safari ndefu ya kuishi.Utakumbana na mengi tena mazito kuliko hili,jaribu kuwa mstahimilivu.Hili limetokea hivi leo,hujui mwaka kesho utakuja hapa na lipi,so kwa muda huu wewe concetrate with what you're doing.Usije ukapoteza hata unachokifanya,halafu mwisho wa siku unapima unakutwa uko salama..

Asante sana mkuu kwa kuchukua muda wako na kunishauri mambo mengi muhimu. Mkuu tangu nijue hali ya yule kimwana sasa ni wiki ya 6 na siku 5 yaani zimepita siku 40. Sio rahisi sana kufika hapa maana niko vibaya emmotionally na sioni tumaini japo nadhani nikijua hali ya afya yangu naweza jua nini chakufanya.

nikijua nimeathirika inakuwa hakuna namna tena nitakubali matokeo na itanilazimu kuishi maisha ya virusi. Tafadhali iwapo unafanya kazi katika vituo vyenye huduma hii nisaidie kipimo mkuu nijifahamu.
 
Hapana ndugu.
Hii ni post yake ya kwanza,anaonekana amejiunga leo tu. Tatizo ninaloona kwake ni kwamba,mbona amepost kisha amejiweka pembeni kimya? Hakuna response tena.

sijaamua kukaa pembeni mkuu tatizo sina computer ya kuwa online muda wote. Nisaidie na endelea kufanya hivyo
 
Hapana ndugu.
Hii ni post yake ya kwanza,anaonekana amejiunga leo tu. Tatizo ninaloona kwake ni kwamba,mbona amepost kisha amejiweka pembeni kimya? Hakuna response tena.
wengine hufungua id mpya,maybe ni mtu mzoefu humu jf.pole kijana.wasiwasi pekee unaweza ukajihisi una dalili zote kumbe ni wasiwasi tu huo.ugonjwa uusikie tu kwa mwenzako,maana hiyo presha yake huwa si ndogo.na mara nyengine mwengine anajiamini kabisa kuwa huu ugonjwa hatoupata,na anawanyooshea wengine vidole.bila ya kutegemea unapima na kupata majibu kuwa umeathirika.kibaya zaidi ni kudeal na watu wako wa karibu,kuna watakaokusema,kuna watakaokuonea huruma.mradi kila mtu na lake
 
We unaumwa zaidi saikplojia... acha uoga. Zaidi ya 55% ya wanaume wanaofanya mapenz na wanawake waathirika kwa mara moja hawapati maambukizi. Hii ina maana kuwa una 55% probability ya kuwa hujaathirika. Pili, hata kama umeathirika, una zaidi ya miaka 5 kabla hujaanza kupata magonjwa nyemelezi (CD4 kushuka sana). Tatu, hata baada ya CD4 kushuka sana, una zaidi ya miaka 15 ya kuwa na afya njema kwa kutumia ARVs.

Kwa hiyo, Kwanza 55% kuwa hujaathirika, pili, miaka 5 kabla hujaugua, tatu miaka 15 au zaidi ya kuishi na afya kwa ARV..
miaka 5+15=20... hiyo ni minimum... ina maana hata kama kwa bahati mbaya uliambukizwa, una zaidi ya miaka 20 ya kuishi. Hivi hadi miaka 20 ijayo, tiba ya HIV itakuwa haijapatikana kwa kweli? Mi nadhani itakuwa imepatikana...

So, ondoa hofu mdogo wangu... miaka 20 inakutosha kutimiza ndoto zako zote za maisha. By the way unaweza shangaa hata kama usingeathirika na HIV, ndani ya hiyo miaka 20 (au zaidi, maana tafiti zinazidi kugundua dawa imara kila zaidi kila siku), ungekufa labda kwa moyo, cancer au ajali... so kifo kipo tu hata usingeambukizwa...

In addition, kwa nchi zilizoendelea kama ulaya wanatumia 3rd generation ya HIV, inayompa mtu uhakika wa kuishi zaidi ya miaka 40 baada ya kuathirika. Kwa Tanzania kwa sasa tunatumia ARV duni kwa sababu ya ukata wa serikali. Hata hivyo ARV hizo bora zimeanza kushuka bei huko duniani, na bila shaka ndani ya miaka michache, Tz itaanza kuzitumia, na utahakikishiwa kuishi hadi miaka 50 kutoka sasa... Sasa mdogo wangu una miaka mingapi sasa hivi... kama utaishi miaka 50 ijayo, kuna haja ya wewe kuwa na wasiwasi?

Nikuambie kitu... kama unasoma, au unafanya kazi, basi fanya bidii ili baadae uwe na ela ya kutosha kula na kugharamia dawa. Pia kama unasoma, soma kwa bidii ili baadae usilazimike kufanya kazi ngumu na hatarishi, zitakazoyaweka maisha yako hatarini...

Sawa e? Dont worry... wengi unaowaona humu, au huko uliko wanacheka, wanaishi kwa furaha ni waathirika, but hawana wasiwasi na wanaishi maisha mazuri na yenye afya zaidi ya maelfu ya wengine ambao hawajaathirika...

Lastly... Why worry if you can pray? Mungu wako hawezi kukuadhibu na kukutelekeza kwa dhambi moja bana... kula maisha... nothing has changed in you

By the way we ni mzima... hujaathirika...

Asante sana kiongozi kwa maneno ya faraja kubwa sana maishani mwangu, maana hata aliyekuwa mpenzi wangu baada ya kumwambia hii kitu aliniacha gheto na hajawahi kunipigia simu tena. Lakini wewe unenifariji kwa dhati ya moyo wako mkuu wangu.

nimepata nguvu mpya ya kuishi kwa miaka mingine mingi tuu hata zaidi ya 50 za ulaya endapo nitakuwa nimeoza na virusi.

Lakini pia Mungu akinisaaidia kuwa salama UMAYA sasa itakuwa basi. Nitaanza maisha ya uaminifu sana na kujenga familia yangu , lakini pia nikiwa nao nitakubali matokeo na niutunza ndani yangu pekee maana sio vyema sana kuwaingiza wengine kwenye janga hili. Maana watakuwa hawakutendewa haki nami.
Asante tena Mkuu maana kama wangenipa PEP pia yamkini ningekuwa salama maana nilipima baada ya saa moja tangu nitoke mtamboni
 
ninmwezi mmoja tu tambu ni fanye mapenzi na dada ambaye baada kumfanya tulienda maabara kupima maana nilimuona anavutia sana na alikuwa na umri wa miaka 19 tu hivyo nikaamini atakuwa mzima. Baada ya kumfaidi nikajenga hoja ya kujua afya zetu na tulivyopima sikuamini matokeo binti alikutwa na UKIMWI na hakuwa na wasiwasi kabisa akaanza kunipa pole.

Naomba msaada wandugu kama kunaaina ya kipimo ambacho naweza kufanya nikawa na uhakika wa afya yangu maana mala tumbo, kichwa, usingizi saa 8 unakatika, kichefuchefu, mafua na kikohozi, mwili kuwasha. hayo ni machache tu kwa dalili na magonjwa niliyonayo.

haja yangu sio kujianika kwa umalaya wangu bali nimeamua kuandika hapa nikijieleza kwa DR ili niweze kupata msaada wa aina ya kipimo maana rapid test inaonyesha hakuna tatizo lakini mpaka miezi mitatu ndipo huwa na uhakika lakini iwapo kunakipimo ambacho naweza kujua hali yangu ndani ya hizi wiki 6 tangu nikutane kimwili na yule dada nitafurahi.

We unaujua ukimwi au....jishauwe tu na mahekaya ya abunuwasi haya unayoandika humu kuna siku utaupata kweli jasho litakutoka
 
Mhhhh....uko kwenye window period, subir baada ya 3 months ukafanye full blood picture ;)
 
Elisa ni kipimo cha uhakika ila unaweza ukajijuapia.

Kama baada ya ngono ulipata homa kama ya flu, au mwili ukawa kama una surua vile, uwezekano kama umepata maambukizi ni mkubwa.

lakini wewe, watu wanaimba nyimbo, michezo ya kuigiza, filamu matangazo kila aina, documentaries zote unaona ni bure?
Huna huruma kabisa kwa watu wanaokupenda.
Sikunyanyapai lakini hustahili moral support kwani haionyeshi kama ni bahati mbaya bali ulifanya makusudi ukijua fika hatari ya ngono zembe.
Hata hivyo I hope uko salama, nisingependa mtu yeyote apate maambukizi. I have been affected so many times by AIDS in the FAMILY

Surua ndo unafeel aje?
 
Namshukuru mkuu Ngahekapahi hapo juu kailezea vizuri sana...

Niliwahi kumtania dk mmoja kuwa kama PEP inasaidi, then mtu ukisex labda katika mazingira ambayo hukujikinga (hasa ulevi), je unaweza kwenda hospitalini kesho yake ukapewa... akacheka, akasema ukipewa itakusaidia, but sio rahisi kwa madaktari wa kibongo kukuelewa...

Nadhani kuna haja ARV zianze kuuzwa pharmacy kama aspirin...

Mkuu kwani hiyo PEP unapewa ARV utumie? Nataka nijue tu mkuu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom