Ukimchunguza kuku sana hutamla..............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
kuna msemo usemao......................ukitaka kumla kuku usimchunguze sana...................na kwenye mahaba mambo ndivyo hivyo...............tatizo la walimwengu huangaishwa na nafsi zao kutafuta kifaa kikamilifu...................wakati wao wenyewe siyo wakamilifu..................na ukweli ni kuwa hakuna mkamilifu bali Mwenyezi Mungu tu...........................

wengi huhangaika kufuatilia nyendo za zamani za mwenzi mtarajiwa bila ya kujua ya kuwa la muhimu siyo jana ila ni kesho yenu imekaa vipi........wateja wa jana hudai ya kuwa historia yaweza kujirudia yenyewe kwa hiyo inabidi wajihami............kwa kwenda na mitazamo hiyo huishia kusahau kuwa waswahili walikwisha kuwaasa ya kuwa "mavi ya jana hayanuki........"

achana na jana kwa sababu mahusiano ni juu ya kesho na leo kidogo sasa jana yakuashia nini?
 
Nafikiri si vibaya kujua tabia ya mpenzio ya zamani kwa ajili ya future yenu especially kama mna mapango wa kuwa wanandoa. Kuna wengine huwa wana background ambazo ni ngumu kubadilishika ktk hali ya kawaida, ambayo kama hutaifahamu mapema, then baada ya kuingia kwenye ndoa yaweza kulete mkanganyiko na kukosa amani ya moyo. Nafikiri ni better kujiridhisha mapema.

Niliwahi kusikia historia mbaya ya jamaa ambaye alioa mwanamke ambaye alizoezwa kufanyiwa michezo michafu. Huyo mkewe alivyopata mimba, siku ya kujifungua manesi walimzomea yule mume wa yule dada wakimlaumu kwa kumfanyia mkewe mchezo mbaya. Kumbe ukweli ni kuwa hakuwa kufanya hiko kitu, ila mkewe alikuwaga akifanyiwa hayo mambo mabaya kabla ya kuolewe na nje ya ndoa ....

It was really embarrassing, na I try to think laiti kama jamaa angefanya uchunguzi wa kina hapo kabla, yamkini matusi hayo yasingemkuta! :A S embarassed:
 
Mi naamini ni vema kujua tabia na mienendo ya mwenza wako kabla hamjawa na mahusiano na inapotokea umeshakuwa na mahusiano hakuna haja ya kuhangaika na ya nyuma kwa kuwa lazma yatavunja mapenzi mliyokwisha anza kuyajenga.
Chunguza kabla hujaingia na si baada ya kuzama kwenye mapenzi coz utajiumiza mwenyewe.
 
Ruta bana hii wiki hii sijui itakwishaje kwako maana nahisi umetendwa mbaya sana pole sana usijali yatakwisha tu
 
Niliwahi kusikia historia mbaya ya jamaa ambaye alioa mwanamke ambaye alizoezwa kufanyiwa michezo michafu. Huyo mkewe alivyopata mimba, siku ya kujifungua manesi walimzomea yule mume wa yule dada wakimlaumu kwa kumfanyia mkewe mchezo mbaya. Kumbe ukweli ni kuwa hakuwa kufanya hiko kitu, ila mkewe alikuwaga akifanyiwa hayo mambo mabaya kabla ya kuolewe na nje ya ndoa ....

wafikiri ukimchunguza haya utayajua........na hata kama ukiyajua huoni ya kuwa aweza kufanyia operesheni akapona na mambo yakawa mdundo kabisa...
 
Mi naamini ni vema kujua tabia na mienendo ya mwenza wako kabla hamjawa na mahusiano na inapotokea umeshakuwa na mahusiano hakuna haja ya kuhangaika na ya nyuma kwa kuwa lazma yatavunja mapenzi mliyokwisha anza kuyajenga.
Chunguza kabla hujaingia na si baada ya kuzama kwenye mapenzi coz utajiumiza mwenyewe.

wengi wanaonekana leo ni safi kesho hugeuka na kuwa bomu.....................wale ambao ni bomu leo kesho utashangaa wamekuwa watu swafi sana.........................utafiti moyo wake wewe mwenyewe.......................usisubiri majungu...........
 
Jana inajenga leo na tunajifunza kutokana na yaliyopita. Kutaka kujua ya kale sio kumchunguza kuku, ni kutaka kujua unadeal na mtu wa aina gani, there is nothing wrong with that.
 
kuna msemo usemao......................ukitaka kumla kuku usimchunguze sana...................na kwenye mahaba mambo ndivyo hivyo...............tatizo la walimwengu huangaishwa na nafsi zao kutafuta kifaa kikamilifu...................wakati wao wenyewe siyo wakamilifu..................na ukweli ni kuwa hakuna mkamilifu bali Mwenyezi Mungu tu...........................wengi huhangaika kufuatilia nyendo za zamani za mwenzi mtarajiwa bila ya kujua ya kuwa la muhimu siyo jana ila ni kesho yenu imekaa vipi........wateja wa jana hudai ya kuwa historia yaweza kujirudia yenyewe kwa hiyo inabidi wajihami............kwa kwenda na mitazamo hiyo huishia kusahau kuwa waswahili walikwisha kuwaasa ya kuwa "mavi ya jana hayanuki........"achana na jana kwa sababu mahusiano ni juu ya kesho na leo kidogo sasa jana yakuashia nini?
kuli..........koni ..........Ruta......!!!!!!..........
 
Jana inajenga leo na tunajifunza kutokana na yaliyopita. Kutaka kujua ya kale sio kumchunguza kuku, ni kutaka kujua unadeal na mtu wa aina gani, there is nothing wrong with that.

mbaya usimchunguze kupita kiasi............hutaweza kumla..............utamtapika.........
 
Jana inajenga leo na tunajifunza kutokana na yaliyopita. Kutaka kujua ya kale sio kumchunguza kuku, ni kutaka kujua unadeal na mtu wa aina gani, there is nothing wrong with that.

relationships is about the future not about the past.....................the past is only relevant if it helps building the future........not to destroy it.........good past may not necessarily translate into a promising future....................wengi hubadilika baada ya kufika kileleni kimahusiano..........wanaanza kuangazaangaza kujihakikishia ya kuwa kama hakuna wame-miss..........
 
Well kama ni mchafu kiasi hicho hatakiwi kuliwa.

uchafu husagwa na tumbo na kutoka nje....................kwa hiyo unachotakiwa wakati wa kumla ni kuondoa uchafu kwa maana ya kumchambua kama karanga....................halahala usitupe minofu minono eti kwa sababu imechanganyikana na uchafu.............msafishe mkatekate khalafu mwingize jikoni....................utamu wake utasimulia sana
 
Sasa kama anaweza akasafishika wasiwasi wa nini? Namchunguza, nagundua aliwahi kula uchafu, naangalia kama alisafishika tunaendelea, kama hakuweza namtupilia mbali.
 
Man: 'Tell me sweetie, how many relationships have you ever had?'
Woman: 'Sweetie, does it matter now that am with you?'......

......now thats what i call wisdom! yesterday doesnt really matter kihivyo na kama it does basi mbinguni hakuna atakayefika maana MUNGU huyu akianza kuyatilia maanani makosa ya jana ya kila mtu basi tumekwisha. 100
 
Nafikiri si vibaya kujua tabia ya mpenzio ya zamani kwa ajili ya future yenu especially kama mna mapango wa kuwa wanandoa. Kuna wengine huwa wana background ambazo ni ngumu kubadilishika ktk hali ya kawaida, ambayo kama hutaifahamu mapema, then baada ya kuingia kwenye ndoa yaweza kulete mkanganyiko na kukosa amani ya moyo. Nafikiri ni better kujiridhisha mapema.

Niliwahi kusikia historia mbaya ya jamaa ambaye alioa mwanamke ambaye alizoezwa kufanyiwa michezo michafu. Huyo mkewe alivyopata mimba, siku ya kujifungua manesi walimzomea yule mume wa yule dada wakimlaumu kwa kumfanyia mkewe mchezo mbaya. Kumbe ukweli ni kuwa hakuwa kufanya hiko kitu, ila mkewe alikuwaga akifanyiwa hayo mambo mabaya kabla ya kuolewe na nje ya ndoa ....

It was really embarrassing, na I try to think laiti kama jamaa angefanya uchunguzi wa kina hapo kabla, yamkini matusi hayo yasingemkuta! :A S embarassed:
kidogo umeniacha hapo kwene virangi rangi...
 
Sasa kama anaweza akasafishika wasiwasi wa nini? Namchunguza, nagundua aliwahi kula uchafu, naangalia kama alisafishika tunaendelea, kama hakuweza namtupilia mbali.

wengi wetu tunamtazamo kama wako lakini swali ambalo halina majibu kama kuchunguzana kungelikuwa kunasaidia mbona baada ya kumkubali yule uliyekuwa unamchunguza...............baadaye waanza kulalama ya kuwa laiti ungelijua kuwa atakubadilihia gia kinamna ungelimkataa.....................kiujumla si rahisi kumjua mwanadamu na ndiyo maana Jeremeiah 17:9 inatuuliza maswali ya kimsingi.............."The human heart is deceitful above all things and desperately wicked; Who can know it?"

kama umempenda mwenzio basi fuata roho yako acha mambo yake ya kale.................yawe mazuri au la.............yote yaweza kurekebishika................kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu............................na ndiyo maana waswahili husema "Kipya kinyemi ingawa kidonda".......................na wengine hulonga "Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika."
 
kidogo umeniacha hapo kwene virangi rangi...

amezungukazunguka sana lakni anachoongelea hapo ni kuwa alikuwa anatumiwa kwa TIGO...........sijui huo uchunguzi wake kama ungelishirikisha madaktari wampime....................kwa sabau haya mambao watu huwa wanayafanya halafu wanapiga ganzi kali sana....................wanakuwa bubu kwa hiyo hutayasikia mitaani yakiongelewa
 
Back
Top Bottom