Wakuu nawasalimu kwa jina la JMT.
Jana nilifanikiwa kufika Wilayani Mwanga katika Kijiji cha Mangyo, kitongoji cha Vongo B. Kuna Mama mwenye umri wa zaidi ya miaka 80, ambaye tarehe 01/11 majira ya saa 1:45 Usiku, wakati akipika chakula chake cha usiku, alivamiwa na kuchinjwa shingo yake kama kuku! Haijaishia hapo, watu hao walimpiga mume wa marehemu kichwani na kumkata mkono, na baada ya mauaji hayo watuumiwa walitokomea kusikojulikana!
Cha kushangaza baada ya polisi kupewa taarifa, walifika 2/11 na kiuchukua mwili na kuupeleka mochwari ya Kijiji inayoitwa Kifula, na 3/11 ndugu wa marehemu waliofuatilia hilo suala wakaambiwa na CID wa wilaya kwamba wanaweza wakauzika huo mwili!
Msaada hii familia inayohitaji ni ifuatayo:
1. Kwanini police iruhusu mwili uzikwe angali upelelezi/majibu ya mauaji hayajakamilika/hayajatolewa kwa familia?
2. Mauaji haya siyo ya kwanza kwani Kuna watu wengine walishauliwa katika mazingira kama haya na hakukuwa na ufuatiliaji wa polisi, hivyo inaonekana mauaji haya Yana baraka ya polisi/Mkuu wa wilaya!
3. Diwani wa eneo hilo (Maradona), wiki mbili kabla ya mauaji haya, aliitaka familia hii imrudishe marehemu nyumbani kwake kwani aliwahakikishia usalama wake, na baada ya marehemu kurudi tu, ndipo mauaji haya yakafanyika! Je bwana Maradona hajahusika katika mauaji haya? Pia izingatiwe kuwa Maradona ana undugu na watuhumiwa (mfano ni urafiki/ukaribu wake na bwana Mashauri ambaye ni kati ya watuhumiwa wa mauaji haya), hivyo anatumia cheo chake cha udiwani kuiangamiza hii familia.
4. Je, usalama wa hiyo familia itakuwa mikononi mwa nani? Ikizingatiwa hii familia inaendelea kupokea vitisho kutoka katika familia ya Mashauri? Ikumbukwe, mume wa marehemu ni mgonjwa Sana baada yakukatwa kichwani na kuvunjwa mkono, pia mtoto mkuwa wa marehemu (Judika Yohana Mfinanga) anaendelea kupokea vitisho toka Kwa bwana Mashauri.
Maziko yanatakiwa kufanyika kesho juma tatu, ila chondochonde Mheshiwa Rais, naomba uingilie kati mauaji haya na ikiwezekana marehemu asizikwe kesho mpaka uchunguzi wakina ufanyike.
CC:
1. Mkuu wa wilaya ya mwanga
2. CID mwanga
3.Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro
4. @PaulMakonda
5. Waziri Mkuu Kasim Majaliwa
6. Mh. Rais
7.Vyombo vya habari mkoa wa Kilimanjaro
NB: Samahani kwa uandishi mbaya.