SI KWELI Ukikutana na Simba, ukimtazama machoni huona aibu na kuondoka

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na kuondoka? Bado siamini hili jambo naona hawa vijana wa ovyo wanataka kuniingiza chaka siku nikikutana naye mbashara nisichukue njia nyingine za kujiokoa eti nimtizame.

Hivi kweli Simba huyu kweli wa kumwonea aibu binadamu kisa kumuangalia machoni ana kwa ana kwa ujasiri.

Wakuu naombeni taarifa sahihi kuhusu hili jambo, huenda mada ikawa kichekesho lakini hili jambo linasemwa sana mtaani.

simba.png
Simba 1.png

 
Tunachokijua
Simba ni mnyama mkubwa jamii ya paka anayeishi porini, hii ina maana kwamba simba hufanana na paka mkubwa, chakula cha Simba ni nyama (carnivore) . Simba hupatikana kwenye kundi la mamalia yaani huzaa na kunyonyesha. Tofauti na paka wengine, Simba huishi na kuwinda katika vikundi vyenye Simba 10-20.
images

Je, ni kweli ukimuangalia Simba machoni anaona aibu kama alikuwa anakufuata ataondoka kwa kuwa wana aibu sana?

Pia, kama akiendelea kukufuata basi unatakiwa kuweka mawe kwapani yakipata harufu ya jasho ukiyaweka chini mawe hayo yatamzubaisha nawe utapata nafasi ya kukimbia?

JamiiCheck ilizungumza na Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja ambaye alijibu suala hilo kuwa:-

Hiyo ni dhana tu, watu huwa wanadhani kwamba Simba wana aibu, lakini katika uhalisia Simba siyo mnyama mwenye aibu kama inavyofirika, Simba ni mnyama mwenye ujasiri mkubwa sana na haogopi.

Ila inategemea na umemkuta katika hali gani, kama Simba umemkuta ameshiba hana tatizo lolote atakutazama tu na kukuangalia tu unataka kufanya nini kwa sababu hana njaa, basi atakuangalia na kuondoka zake.

Lakini ukimkuta mwenye njaa, na hana Altenative(Mbadala) ya kupata chakula basi usitegemee hiyo itakuwa silaha ya kumfanya yeye aweze kurudi nyuma hapo naomba watu waelewe.


Kuhusu kuweka mawe kwapani yapate harufu, Mhifadhi alisema:-
Hiyo ni imani tu, na masuala ya imani hatuwezi kuyaongelea, lakini kisayansi, hakuna kitu kama hicho kwamba mawe yakikaa kwapani yanamfanya mnyama Simba aweze kuzubaika, au ukiyaweka chini ndio azubaike hayo ni mambo tu ya imani.

Unajua haya mambo huwa yanatokea tu katika jamii kila jamii ina imani zake juu ya wanyama, kwa mfano Fisi, watu wana imani zao wengine wanawatumia kama usafiri, hiyo ni dhana tu.


Nini cha kufanya ukutanapo na Simba?

Beatus Maganjai amesema ukutanapo na Simba unatakiwa kufaya afuatao:
Katika maeneo yale ambayo korofi, yaani maeneo ambayo yana wanyama hawa korofi,

Kama umekutana na Simba ana kwa ana,
simama firmly(Imara), bila kutikisika, au kutikisa kiungo chochote huku ukiwa unamtazama.

Simba huwa ana kawaida ya kupima ujasiri wa mtu, ukisimama ukamtazama, kwa maana ya kuwa umesimama imara bila kutikisika, anaweza kuamua kughairi na kuondoka zake.

Unapofanya movement(mijongeo au mitikisiko), yeye hisia zake zinamuijia kwamba unataka kumletea madhara fulani, yeye atatafuta namna yoyote ya kuhakikisha kwamba anakufanyia kitu chochote ambacho ataona kinakufaa. Kwa hivyo unasimama Farmly bila kufanya movement za aina yoyote kama huna namna.

Na hiyo inategemea na umbali, upo umbali kiasi gani, umekutana naye katika umbali gani, kama upo mita 30 hivi, umekutana naye mita 30, mara nyingi Simba hawana muda na binadamu huko maporini kwa sababu wana wanyama, wanyama wala nyasi ndio chakula chao, hata sisi wahifadhi huwa tunakutana nao, wakati mwingine hata sisi hatujui. Wakati umerudi doria umekaa chini ndio unajua alaaa! Hapa alikuwepo Simba hapa, hapa alikuwepo chui.

Tunawashauri wakazi wanaoishi maeneo mbalimbali ambayo wanaweza kukutana na wanyama hao waweze kuchukua hatua kama hizo.


Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja wanyama pori, JamiiCheck imeona kuwa suala la Simba kuwa na aibu si la kweli
Simba ni muoga na aibu anayo

Masai Ngorongoro anamswaga simba kwa fimbo na Simba anakimbia mbio

Vitabu au Sayansi haiwezi kusema ukweli wote
Ila simba ana uoga na udhaifu sana sio mbabe kama tu avosoma kwenye vitabu

Simba hamchokozi fisi au mbwa mwitu anamwogopa mno
 
Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na
Mimi akili itanijia siku hiyo nikikutana nae. Kama vipi nimevaa jezi ya Al-Ahly nitampa makofi mawili matatu na kuchimba zangu.
 
Itakuwaje ukutane na Simba Jike mwenye upwiru.. wana mtindo wa kugauza mgongo wao
 
Hilo somo nani aliwahi kufanya hayo ikawa hivyo?

Kwanza tu ile kukutana nae sidhani kama utakumbuka mbinu hizi mlizipost!

Yaani kila mtu ajue mwenyewe namna atajiokoa lakini sio nimkazie macho simba kabisa ili aone aibu aniache asinidhuru sidhani labda huyo awe kashiba
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom