Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Maisha ya hapo zamani mtu akikuta begi kama hili na kuliacha, watu walimshangaa sana kwamba kapitwa na bahati na bahati haiji mara mbili,
Ila kwa siku hizi mtu akiliacha begi kama hilo ana akili sana, wala si wa kumcheka.
Teknolojia ya GPS tracking imekuwa kubwa sana, Begi lenye maburungutu ya hela ni kawaida sana kuwekwa gps inayoonyesha movement zote za begi, Gps ndigo ya ziada inaweza kuwekwa kwa ustadi katikati ya pesa zilizobanana, hata begi likitupwa location ya mzigo inaonekana.
Gps trackers itaonyesha sehemu lilipo begi na movements zake, hivyo ukiliokota na kwenda nalo nyumbani kwako, watajua lilipo na kulifuata, kibongo bongo utapewa kipigo kikali sambamba na kupewa kesi ya ujambazi.
Watu wanaweka gps kwenye pikipiki na magari na yakiibiwa wanayapata sembuse mabegi yenye maburungutu ya hela ? hilo swali ujuilize sana.
Njia pekee ya kuiba hilo begi labda uwe na jammer wanazotumia majambazi wa kisasa kuiba pikipiki na magari, gps jammer ni kifaa maalum cha kublock mawimbi ya gps tracker.
Begi ukikimbia nalo kwa muda mfupi ukiwa na furaha utasema maisha umeyapata lakini kifuatacho baada ya hapo kinaweza kufanya maisha yako yawe ya majonzi sana.