Ukata wa Fedha na Migogoro ndani ya CHADEMA waiondoa majukwaani na kuiweka mfukoni mwa Mbowe

Nilishakwambia mdogo wangu SAGAI GALGANO kuwa achana na hiyo mibangi unayovuta kupita kiasi kama mwendawazimu. Inakuharibu akili yako.
Wewe ni taahira tu kwani unashindwa kufanya tathmini kama unachofanya kinakulipa au la. Unajidhalilisha tu kujaza mabandiko yako humu na simu unaweka lakini hawakupigii. Kwa ujinga huu huwezi kuteuliwa.
 
Wewe ni taahira tu kwani unashindwa kufanya tathmini kama unachofanya kinakulipa au la. Unajidhalilisha tu kujaza mabandiko yako humu na simu unaweka lakini hawakupigii. Kwa ujinga huu huwezi kuteuliwa.
Wewe ndiye unayejidhalilisha kwa kushinda humu ukiporomosha matusi yako muda wote.
 
Nilishakwambia kuwa achana na mibangi yako na maliza matibabu ya magonjwa ya akili.
1700196962994.jpg

Hayo ndiyo matunda ya CCM
 
Tena ni CCM tupu lakini ni aibu nyumba za tembe tupu
Kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa mwananchi na siyo kuja kukujengea nyumba huku wewe ukikesha huku jukwaani kutukana matusi kama Mwendawazimu.fanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa.lima kwa bidii upate hela
 
Ndugu zangu Watanzani,

Wanasema chama cha siasa kilicho hai na uhai ni lazima kiwe mabarabarani na majukwaani. ni lazima kiwe midomoni mwa watu muda wote,ni lazima kitetewe vijiweni,magengeni,masokoni, viwanjani na sehemu yoyote yenye shamrashamra za watu.ni lazima kiwe kwenye ndoto za watu ,kwamba mtu akilala usingizi anajikuta anakiota chama husika na harakati zake huku yeye akiwa msitari wa mbele kukitetea ,kukipigania na kukisemea wakati wote kinaposemwa vibaya.

Ili chama kifikie hatua hiyo na kuwa na uwezo huo wa kuteka mioyo ya watu na kuwa midomoni mwao ni lazima kiwe kinaaminika mbele za watu ,kiwe na viongozi wenye Taswira na tabia nzuri katika macho ya jamii,ni lazima kiwe na safu ya uongozi madhubuti, imara, shupavu,yenye umoja , mshikamano, kauli moja na wenye msimamo wa pamoja usiyo yumba wala kuyumbishwa.ni lazima kiwe na Dira,muelekeo na shabaha maalumu.

Kufanikisha haya ni lazima viongozi husika wakubali kuumia, kujinyima,kujitoa na kujitolea ,kuteseka,kupoteza baadhi ya vitu au uhuru wao au marafiki zao au mali zao pamoja na maslahi yao binafsi ili kukifikisha chama katika kilele cha upendo wa mioyo ya watu. ni lazima wakiweke chama na maslahi yake mbele kuliko matumbo yao binafsi na maslahi yao.

CHADEMA kwa sasa imekosa vitu na mambo yote hayo niliyoyaeleza hapo juu,haina mshikamano wala muunganiko miongoni mwa viongozi wake,kila mtu anapigania tumbo lake ,kila mtu anaangalia upepo unavuma je,hayupo ambaye yupo tayari kupoteza kwa ajili ya chama,hayupo ambaye yupo tayari kuona kila senti inayopatikana inakwenda kukinufaisha chama moja kwa moja pasipo kumega kidogo.

Sasa CHADEMA imeshuka majukwaani na kupotea katika harakati za kuimarisha chama na kuwafikia wafuasi wake.hii ni baada ya kukumbwa na ukata mkubwa sana wa pesa pamoja na kutokuwepo kwa maelewano mazuri baina ya viongozi wa ngazi za juu hasa mwenyekiti na makamu wake ambao matokeo yake yamewagawa hadi wafuasi wake ,ambapo wapo walio upande wa mwenyekiti na wengine kwa makamu.

Huku chanzo kikubwa kikielezwa kuwa ni kutofautiana kwa misimamo na mitizamo juu ya masuala mbalimbali yanayopelekea kutuhumiana sana. Sasa CHADEMA imepotea katika vinywa na midomo ya watanzania,haipo barabarani wala mitaani wala masokoni wala akilini mwa watanzania.

Chama hakina pesa na hakielewi kipate wapi pesa.kurudi kwa wanachama kuomba misaada na michango hakiwezi kwa kuwa wanachadema wameshagoma kusikia habari za michango na badala yake wanataka ukaguzi maalumu wa fedha na mali zote za chama hicho.wanataka pesa za join the chain ielezwe zipo wapi? Zilikusanywa na kupatikana shilingi ngapi? Zimefanya kazi ipi na kwa utaratibu upi?

Sasa viongozi maji ya shingo wanaanza kuitana nyumbani kwa mwenyekiti kujaribu kuzimazima moto pasipo majibu ya msingi. Jambo ambalo linaendelea kukuza migogoro zaidi ,kwa kuwa viongozi wengine wanaanza kujiuliza mbona sisi hatujaitwa? Kwahiyo walioitwa ndio wenye thamani ndani ya chama? Ndio wenye umuhimu? Ndio wenye nguvu? Ndio sauti ya chama? Kwanini mwenyekiti anahamishia ofisi nyumbani kwake? Kwanini wasikutanie ofisini? Kwanini visiitwe vikao rasmi vya chama kuliko kuitana kwa kubaguana na kuangaliana sura?

Kwa hiyo kwa sasa inaonekana chama kimetupiwa mfukoni mwa Mbowe,yeye ndiye amebaki anatembea nacho popote aendapo na ndio maana anageuza makazi yake kuwa ofisi za chama na kuamua amwite nani na nani waende kwake na wajadili nini na wale nini na kiasi gani. Kwa hiyo ukiwa kwake hutakiwi kuanza kuleta ubishi ubishi na vurugu zako kwenye masofa yake aliyoyanunua kwa hela zake.unatakiwa kuwamtulivu na kukubali kila kitu kama kasuku na kuunga mkono kila mkakati.

Chama kimetekwa mateka na kimegota kifikira na kumtegemea mwenye kigoda tu. Tuendelee kuangalia kinachoendelea hapo ufipa na kuwaombea wenzetu ambao walishachukuliwa kama wajinga kwa kubadilishiwa gia hata mahali pasipo stahili kubadilisha gia.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Wewe utakuwa na shida sana. Hiyo Chadema ni chama cha siasa chenye viongozi na wanachama. Usitegemee kusiwepo kutofautiana. Ni sawasawa tu na jinsi ilivyo ndani ya CCM. Niambie Makonda, Kinana na Chongolo wako sawa? Kinana mwenyewe anatishia kuvua jezi baada ya m/kiti kuwakera kwa kumteuwa yule muuwaji. Nyumbani kwako ni pachafu usiangaike na madoa ya nyumba ya jirani.
 
Wewe utakuwa na shida sana. Hiyo Chadema ni chama cha siasa chenye viongozi na wanachama. Usitegemee kusiwepo kutofautiana. Ni sawasawa tu na jinsi ilivyo ndani ya CCM. Niambie Makonda, Kinana na Chongolo wako sawa? Kinana mwenyewe anatishia kuvua jezi baada ya m/kiti kuwakera kwa kumteuwa yule muuwaji. Nyumbani kwako ni pachafu usiangaike na madoa ya nyumba ya jirani.
CCM Ni moja na ndani ya chama kumetamalaki umoja na mshikamano na ndio maana unaona shughuli za chama zinakwenda vizuri kabisa huku chama kikiwa midomoni mwa watu.
 
Kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa mwananchi na siyo kuja kukujengea nyumba huku wewe ukikesha huku jukwaani kutukana matusi kama Mwendawazimu.fanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa.lima kwa bidii upate hela
Mjinga wewe kwani mi nipo Singida? ni hao wajinga wenzako wanaipenda CCM matokeo yake inawapelekea nyumba za tembe tupu
 
Uwe unasema ndugu zangu CCM sio ndugu zangu Watanzania, Mimi sina ndugu anayejipendekeza namna hii, wote tuna haso zetu hatujidhalilishi ili mkono uende kinywani.
 
Hoja hupingwa kwa hoja na siyo viroja au hasira au matusi.unatakiwa uthibitishe uongo wangu upo wapi?
Acha upimbi, mlivyopiga marufuku mikutano ya kisiasa mlikuwa mmelewa na hamkumbuki? Sasa leo unaposema chama kiwe mabarabarani na majukwaani unamaanisha nini?
Hovyo kabisa.
 
Uwe unasema ndugu zangu CCM sio ndugu zangu Watanzania, Mimi sina ndugu anayejipendekeza namna hii, wote tuna haso zetu hatujidhalilishi ili mkono uende kinywani.
Watanzania wote ni ndugu labda kama wewe ni li hamiaji haramu.
 
Acha upimbi, mlivyopiga marufuku mikutano ya kisiasa mlikuwa mmelewa na hamkumbuki? Sasa leo unaposema chama kiwe mabarabarani na majukwaani unamaanisha nini?
Hovyo kabisa.
Kwa hiyo baada ya kuishiwa hela mmeakua mtafutie kichaka? Ninyi si mseme tu ili nyumbu wawachangie? Ninyi ni matapeli sana
 
Back
Top Bottom