CCM yaiweka mfukoni CHADEMA

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,327
9,748
Ndugu zangu Watanzania,

Nilishawaambieni humu jukwaani kuwa ukongwe wa CCM na uwepo wake madarakani mpaka leo hii unatokana na uimara wake,mfumo wake imara katika kujiendesha kitaasisi, pamoja na kujaa na kusheheni kwa manguli wa sayansi ya siasa ndani ya chama hicho wenye uwezo wa kuvianzishia Ajenda vyama vya upinzani na kuvifanya muda wote vibakie na kuendelea kuwa vipaza sauti wa CCM na mambo yake.

Embu angalia mfano kete na karata iliyochezwa kwa sasa ya kumleta Makonda wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani pamoja na ule wa 2025. Sasa chadema nzima kuanzia ngazi ya msingi mpaka Taifa wamebaki kuwa watoa na waeneza taarifa za Makonda na hotuba zake.kila mmoja ndani ya CHADEMA anajitahidi kuwa wa kwanza kuripoti habari za Makonda.

Angalia hata humu jukwaani tu namna mada mbalimbali zinazomhusu Makonda namna zilivyoteka jukwaa lote na kila ukurasa unakuta habari za Makonda na CCM tu.viongozi na wanachadema kwa ujumla wao wanafanya mashindano ya kuwa wa kwanza kuripoti habari za Makonda na CCM juu ya maagizo ya chama kwa serikali katika utekelezaji wa ilani yake, ili kuhakikisha kuwa watanzania wanapata huduma bora na stahiki bila ubaguzi wa aina yoyote ile.

Ukija mitaani ndio kabisaaaa unakuta ni Makonda tu na CCM Ndio wameteka mijadala yote ya kisiasa.ukienda kwenye vyombo vya habari,magazeti,TVs,magari,vijiwe vya kawaha, boda boda,bajaji unakuta ni habari za CCM na Makonda wake kwa namna alivyoleta mchakamchaka na matumaini kwa wanyonge kusikilizwa na kuhudumiwa vizuri.kila mtu anashauku yakutaka kumuona Makonda na kumsikiliza juu ya kile serikali yao imefanya na inakwenda kufanya.

Matokeo yake ni kuwa kwa sasa husikii habari za CHADEMA zikizungumzwa popote pale maana hata wanaotakiwa kuzisema na kuziandika wapo Bize kuripoti habari za CCM na Makonda komandoo wa vita vya ardhini. Wapo Bize kwelikweli na hawakauki wala kutulia.

Hiyo ndio maana ya chama cha siasa kinachoijuwa siasa na namna ya kucheza na akili za watu na kuwepo midomoni, barabarani, mitaani,majukwaani na kila eneo lenye mkusanyiko wa watu.kwa sasa CCM ipo kila eneo na inazungumzwa kwa mema kila sehemu na kusambazwa habari zake na kila mtu bila kujali itikadi za kisiasa kwa kutumia watu mbalimbali wakiwepo wapinzani ambao nao sasa wapo na kibarua cha kuisemea CCM,kuitangaza na kuinadi kila dakika.

Sasa CHADEMA ipo mfukoni mwa CCM na haionekani popote pale wala kusikika kwa kuwa hakuna anayeweza kuona kitu kilichomfukoni ikiwa hakijatolewa na aliyekiweka. Hii imeonyesha nguvu ya CCM kimikakati,kimipango, kijasusi, kisayansi,kimbinu na kimaono.

Hakuna chama chenye uwezo wa kuitikisa CCM Katika nchi hii,hakuna mtu wala kikundi chenye uwezo wa aina yoyote kwa misingi ya aina yoyote chenye uwezo wa kuisumbua CCM hiii ya Rais Samia.ndio maana Inaendelea kusalia madarakani na kuchaguliwa kila uchaguzi kwa Kishindoo kikuu,.hii inatokana na ukweli kuwa vyama vya upinzani vya hapa nchini ni vyama visivyo na ajenda wala sera za kugusa maisha ya watu, havina maono wala Dira wala kitu ambacho kinamgusa mtanzania mpaka aone umuhimu wa kuviunga mkono vyama vya upinzani.

Kila mtanzania anaona vyama vya upinzani ni mkusanyiko wa wasaka tonge,wachumia tumbo,watu wasio na malengo mahususi kwa ustawi wa Taifa letu.ndio maana hakuna aliye tayari kuwaunga mkono upinzani .ndio maana hata matamko yao au maazimio yao huwa yanapuuzwa na watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Usichojua ni kuwa CCM kama Chama hakina uimara wowote kwa miaka mingi sasa, kinachoisaidia ni Polisi na katiba mbovu inayowapa wateule wa rais ambaye ndio MWENYEKITI wa Chama hicho mamlaka ya kusimamia na kutangaza matokeo ya urais, wabunge na madiwani.

Kama kungekuwa na fairness ground kwenye hilo CCM ingeshakuwa kama KANU siku NYINGI tu ila pia kumbuka kauli yao kuwa watatumia Dola kubakia kwenye Dola....kwa maana ya kutawala kwa mkono wa chuma.

Matibabu ya haya yote ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi
 
Usichojua ni kuwa CCM kama Chama hakina uimara wowote kwa miaka mingi sasa, kinachoisaidia ni Polisi na katiba mbovu inayowapa wateule wa rais ambaye ndio MWENYEKITI wa Chama hicho mamlaka ya kusimamia na kutangaza matokeo ya urais, wabunge na madiwani.


Kama kungekuwa na fairness ground kwenye hilo CCM ingeshakuwa kama KANU siku NYINGI tu ila pia kumbuka kauli yao kuwa watatumia Dola kubakia kwenye Dola....kwa maana ya kutawala kwa mkono wa chuma.

Matibabu ya haya yote ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi
Hata ije katiba mpya au Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu,kwa kuwa CCM hupita na kuchaguliwa kwa kishindo kutokana na ubora wa sera ajenda zake zenye kugusa maisha ya watanzania.kuwa na ilani yenye kubeba mambo yenye kugusa mahitaji ya makundi yote na kuendana na wakati.lakini pia utekelezaji wake wa ilani umekuwa ni wakiwango kikubwa na chenye kutia matumaini. lakini vyama kama CHADEMA havina uwezo hata wa kuandaa tu ilani yake au mgombea Urais tu,ukitaka uamini hili angalia kilichotokea 2015 ndio utajuwa kuwa nchini hatuna vyama vya upinzani zaidi ya wasaka tonge na wachumia tumbo tu.
 
Ila kama ukweli vile
Huo ndio ukweli wenyewe.angalia hata humu jukwaani tu uone namna wana chadema walivyo bize kuripoti habari za Makonda na CCM. nenda Twitter au Facebook au Instagram utakuta Chadema wanashindana uafisa habari wa habari za CCM na kuachana kabisa na habari za chama chao.
 
Back
Top Bottom