Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

jokaKuu

well said my brother.

NOTE: kule wilayani kwa Mramba Rombo kulikuwepo kiwanda cha VIBIRITI, (pale Mkuu) nafikiri kilifungwa kwa sababu ya soko...........ni ktk kuweka sawa moja ya para za hiyo post yako #1264
 
Mashirika Makubwa Bongo na Wakurugenzi wake
Especially yalio chini ya Wizara ya Fedha na Viwanda
TRA -Kilimanjaro Mkapa's Legacy
Bank ya Posta Kilimanjaro
NSSF - Coastal Area
PPF -Kilimanjaro Mkapa's Legacy?
CRDB- Alishinda Interview (Kilimanjaro)

Mawasiliano na Uchkuzi
DAHACO/Swiss Port- Kilimanjaro
Tanzania Aiport Authority- Kilimanjaro
Civil Aviation-Kigoma
TANROADS- recently Appointed Wa Mlima ( sasa Sijui ni Shemeji au Rafiki
BIMA-Nyakyusa
Sigara- watu wa njee na Local Partners sijui ni wa wapi??
VODACOM- Sa na Local Partners Majority?
Serengeti Breweries- Hindi na Sukuma?
TBL-SA na Local Kileo???
Inter-Consult???
TAn-Consult
TISCAN- Karamagi na Coastal
Machimbo ya Dhahabu- Watu wa Nje na Local Parners Wengi Legacy ya Mkapa na Yona.
TANESCO- Net Group Shemeji's Legacy?
Total Net Flow of Wealth na other Development Activities in The country from one end of the country to Another or to a particular Area is Equal or not Equal to????
Ukabili???
 
august,
Inter-Consult ni kampuni binafsi iliyoanzishwa na ndugu wawili wa Kichaga. Hao jamaa ni pioneers ktk consulting business Tanzania. Huo ndiyo UJASIRIMALI aliokuwa akiuzungumzia Mkapa.

Badala ya kuwasimanga Eng.Mosha na Eng.Njiu ni bora tukajifunza toka kwao. Hawa waliona kazi za serikali tunazokabana makoo nazo hapa JamboForums hazina maana. Wakaamua kuchukua RISK na kuanzisha a CONSULTING BUSINESS, and today they are MULTI-MILLIONAIRES.

Tan-Consult pia ni kampuni binafsi imeanzishwa na Eng.George Alliy. Sifahamu jamaa ni mtu wa wapi. i consider Consulting to be an ethical business where the money is "clean." So kudos to Eng.Alliy.

PPF DG wao anaitwa Erio. Wengi wetu tulifikiri jamaa ni mtu wa Kilimanjaro. Member mmoja wa jamboForums alitulihakikishia kwamba Erio ni Mmakua, na ni mpwa wake Mkapa.

Hivi umeshapata kujiuliza kwanini Nyerere,Mwinyi,Mkapa wote hao wameshindwa kusafisha hii takataka inaitwa "Kilimanjaro?" Wote hao wameshindwa kuteua ma-DG wa makabila mengine ili Watanzania tusinungunike na kusononeka?

.....tuache blah-blah tujenge nchi!!!

NB: Dr.Ramadhani Dau, ni mzaliwa wa Dar lakini baba yake ametokea Mafia.
 
Joka Kuu
Kuweka Inter or Tan Consult ni ktk kujaribu kuongeza Sample size, kama Serengeti Breweries etc, ningeweza kuweka hata COSEKE BML, na nyingine nyingi tu za watu Binafsi kama IPP , SHIRECU,
 
Nyerere alijitahidi, kwa kuwaachia Bima Mwaikambo, na Nsekela NBC, Sigara Msangi, TIB Rubambe, Railways Bakilana, Janguo Harbours, CRDB Swai, Pamba Shindika etc, Tanesco Salvatory Mosha na Then Mhavile, then Luhanga.
Nyerere alikuwa ana namna yake ya ku-balance the equation.
BOT Nyirabu
 
ndio maana zanzibar hawataki mambo ya ukabila hakuna mzenji akakwambia kabila lake lakini hivi tu karibuni ndio imeingia fitna na kupandikishwa chuki ndio leo utasikia mpemba na muunguja hakuna jambo baya kama kitu ukabila au udini
 
ndio maana zanzibar hawataki mambo ya ukabila hakuna mzenji akakwambia kabila lake lakini hivi tu karibuni ndio imeingia fitna na kupandikishwa chuki ndio leo utasikia mpemba na muunguja hakuna jambo baya kama kitu ukabila au udini

..unafikiri hatujui watu wanavyopeana vyeo na madaraka kwa kujali wametoka upande gani wa unguja?

..huo ni sawa na ukabila pia!
 
hayayayayayayayayaya
yawezekana pakawepo na ukabila serikalini kama mnavyosema, lakini kumbuka kwamba kusoma sana sio kuelimika. watu wengi wamesoma lakini ukiangalia ufanyaji kazi wao ni wa hovyotu, tuna baadhi ya mawaziri na viongozi wa serikalini, utshangaa hata ukisikia statements zao!
mfano kikwete ana shahada ya uchumi, lakini angalia anavyocheka akiwa jukwaani!
statemenets zake juu ya ongezeko la ushuru wa mafuta zinatia shaka kama kweli huyu ni msomi wa uchumi au la!, kwa hiyo pamoja na degree zetu bado kunahitajika akili ya kuzaliwa na sio ya skull tu!
 
mfano kikwete ana shahada ya uchumi, lakini angalia anavyocheka akiwa jukwaani!

Practce ni kitu muhimu pia, practice inajenga experience. Experience is the best teacher.Nafikiri JK uchumi hajapractice siku nyingi.

kuhusu ukabila:Kilimanjaro wao wamefumbua macho siku nyingi kuhusu elimu. Angalia idadi ya shule Mtwara, Shinyanga linganisha na mikoa ya kaskazini etc. then what do you expect?
Muheshimiwa shija kama mbunge na waziri ameusidiaje mkoa wake kielimu? nasikia shinyanga ilikuwa haina shule ya serikali ya wavulana kabla ya huu mpango wa MMES.

Katika ubinadamu wetu unapokuwa mkurugenzi,wamekuja vijana wawili kuomba kazi, wote wanaqualification sawa, lakini mmoja wao unafahamu asili yake si mbali sana na wewe ulikotoka.Ni dhahili huyu unayemfahamu kijujuu ndiye utakayempa kazi.

Na si hapa Tanzania kote hata katika Mashirika makubwa ya UN, ni hivyo hivyo. ili uweze kuingia huko ni lazima uwe na kachain fulani ka kutambulika.
Huo ndio ubinaadamu.
 
Practce ni kitu muhimu pia, practice inajenga experience. Experience is the best teacher.Nafikiri JK uchumi hajapractice siku nyingi.


.


ukweli ni kuwa muheshimiwa rais baaada ya kumaliza degree yake ya BA Economics..alijiunga moja kwa moja na TANU kama msaidizi wa katibu msaidizi wa TANU zanzibar ..kabla hajajiunga na jeshi kuchukua mafunzo ya uongozi ya jeshi..uafisa..baada ya hapo aliendelea kuwa jeshini kama kada na pia kwa nyakati tofauti akawa katibu wa CCM wa wilaya za singida,lindi..kabla ya kupewa ubunge wa kuteuliwa na mzee mwinyi..na unaibu waziri wa nishati.......so kwa kifupi hajapata kupractice uchumi..kama ajira labda kama siasa...
 
Ukabila upo kila mahali. The old cliché holds true: "It's not what you know, it's who you know." Most people really do get their jobs because of who they know. It doesn't mean everyone in those posts got there because they new someone but like any other human being I prefer to work with someone I am confortable with. So besides credentials when I have to make a choice btn 2 individuals with same capabilities, I will pick someone I can relate to after all I have to work with them and as we all know we spend most of our time at work. Why not with someone I am confortable with.
 
Jamani Naona Watanzania,,, Mmeamua,ila Kwenye Swala La Ukabila Naomba Niwapinge Kwa Hili
Ndugu Zanguni Makabila Mliotaja Sio Tu Wamesoma Wanamuelekeo Wa Maisha ,,na Mumngu Naweza Kusem Amewap Vipaji Maalum.,,waachen Wachaga Wawaongoze Tra,,nani Asiejua Waliwekwa Wasukuma Kule Kila Mtu Akataka Kuhamishia Tra Mbeya,,sasa Wachaga Pesa Zinaonekana Wamesoma,,na Kuiba Wanakuibia Vilevile,,wahaya Nani Asiejua Ndio Wanaowapa Watu Na Ajira,,,nani Ajui Vijana Wa Kihaya Wnatengeneza Certificate Mpaka Za Birngham University??
Swala Nawashauri Makabila Wenzetu Twendeni Shule,,mwinyi Alisema Hili Kwa Nani Aahh Sijui????
Msiposoma Wajameni Wak@#$^&* Wataendelea Kukamata Kila Kiti,,sasa Jamaa Ameingia Mwacheni Afanye Equalization Hata Kwa Wachache Waliosomoa

Ahsanten
 
ukweli ni kuwa muheshimiwa rais baaada ya kumaliza degree yake ya BA Economics..alijiunga moja kwa moja na TANU kama msaidizi wa katibu msaidizi wa TANU zanzibar ..kabla hajajiunga na jeshi kuchukua mafunzo ya uongozi ya jeshi..uafisa..baada ya hapo aliendelea kuwa jeshini kama kada na pia kwa nyakati tofauti akawa katibu wa CCM wa wilaya za singida,lindi..kabla ya kupewa ubunge wa kuteuliwa na mzee mwinyi..na unaibu waziri wa nishati.......so kwa kifupi hajapata kupractice uchumi..kama ajira labda kama siasa...

Sasa kama rais anatakiwa awe qualified economist na watendaji wake watakuwa na kazi gani? Rais kazi yake ni kutoa vision na yeye anaamini kuwa Vision ya Mkapa haikuwa na umakini katika kumsaidia Mtanzania mwenzake kama homeboys zake kule Bagamoyo na Chalinze. Hivyo ni wajibu wake kutoa vision yenye kulenga kubadili ama kuboresha njia ili nao pia wafaidike.

Sasa kama njia hizo zinakuwa tofauti na misingi ya ki9uchumi tunayosomeshwa darasani hilo ni kosa la watendaji ambao wanapaswa kuhakikisha kuwa wanakuja na njia bora itakayowezesha kutimiza vision ya Rais lakini bila ya kuharibu zaidi uchumi wetu.

Lakini yote muyaonayo kama ni dalili mbaya naamini alama ya kuwa mfumo wa kisiasa wa nchi yetu una mapungufu mno kiasi ya kwamba kunatokea mgongano mkubwa wa kiufanisi kati ya dira (vision) ya kongozi wa nchi, sera za nchi na utekelezaji wa yote hayo mawili, yaani dira na sera.

Tufanyeje, hilo ndio swali tunalopaswa kuja na majibu yake na kuacha kulalama na kuishia kujiona kuwa sisi ndio wajuvi na tuliyempa urais wa nchi ndiye mwenye mapungufu.

Tanzanianjema
 
... na hizi NGOs za kiraia wanaojitangaza kuwa ni vyama vya kitaifa? kwa mfano ukiangalia wanaharakati hawa; viongozi wao, wanachama wao na ushabiki wao kisiasa?

Wanaharakati waandamana kumtetea Kabwe
Na Boniface Meena

WANAHARAKATI wa Haki za Binaadamu wa Mitandao ya Jinsia na Maendeleo Tanzania (FemAct) wameandaa maandamano ya amani yatakayofanyika leo, kupinga adhabu ya kusimamishwa kwa Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari 2008.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya, alisema maandamano hayo yatafanyika kuzunguka viwanja vya TGNP, Mabibo jijini Dar es Salaam, karibu na Chuo cha Usafirishaji.

Alisema mbali na kupinga adhabu hiyo, nia ya maandamano hayo pia ni kutafakari kwa kina juu ya mwenendo mzima uliotumika katika kutoa adhabu hiyo kwa Zitto Kabwe.

Alisema pia watajadili hali ya kisiasa Tanzania katika muktadha wa mchakato unaoendelea kuleta demokrasia nchini, pamoja kujenga wigo mpana wa majadiliano juu ya utungaji na uundaji wa sheria na sera nchini Tanzania.


http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=1141
 
... na hizi NGOs za kiraia wanaojitangaza kuwa ni vyama vya kitaifa? kwa mfano ukiangalia wanaharakati hawa; viongozi wao, wanachama wao na ushabiki wao kisiasa?

Kikalenda sifikiri, kila kitu ukiangali namna hii, mimi sio Chadema, wala si Mtu wa Mlima, lakini kille kilicho tokea Bungeni si hala. That is fact. Sasa kila kitu ukikiweka kwa misingi hii hatutafika.
Ndio mfano wa kula wenyewe kwa wenyewe unakuja.
uwe mkristo au muislamu etc ukitetea upuuuzi upo siku uta kudhuru wewe mwenywe, sasa sijui utasemaje hapo?
Nafikiri umenielewa.
Leo utafurahi mjomba wako kaniibia mimi, kwa sababu ni nduguyo, badala ya kuona kwamba mjomba kaiba. sasa akija kukuibia wewe uzalendo unakutoka, unataka mimi niwe shahidi wako.
 
mwanakijiji, nashukuru sana kwa kazi nzuri uliyofanya; hoja yangu ni kuwa hivi wale watu wa kabila moja wanaokutwa ofisi moja wana qualificasions wanazositahili kuwa nazo? kama wanazo basi hamna ubishi ni vigumu kudhibitisha kama kwenye interview kuna wengine walikuwa wanamzidi? ni upumbavu kuhukumu kwa kuangalia majina kuwa huyu ni Mushobozi, huyu ni Mwakisu, na huyu ni Mushi. nyerere aliwai kusema mwaka 1968 wakati NBC imekosa wafanyakazi wenye qualifications za kutosha baada ya kuibinafsisha na kufukuza wazungu:

to employ the indignous to replace the foreigners is a good thing, but to employ a person who is not qualified on the grounds of patriotism is not self reliance but stupidity.
 
Back
Top Bottom