Ujumbe kwa wale wote mnaoagiza magari kutoka nje. Usipite bila kusoma hapa

BROKE BOYS

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
13,220
39,061
Ndugu habari za jion, Kuna jambo nimeona tuambiane ukweli ili tuelimishane kidogo.

Kuna watu watu wanaagiza magari nje kupitia agents au mawakala mbalimbali mbaya zaid kuna agents wengine sio waaminifu kabisa.

Mtu anakwenda kwa agent amchagulie gari, amsaidie malipo yaani kila kitu anafanya agent wewe unasubir gari tu ifike upewe tena unakuta gari umeiangalia juujuu kisa unamwamni agent wako acha ufala asee.

Sasa mambo yanayofanyika ni hatari mpaka huruma yani hawa jamaa wanabadili vitu vingi sana watu wanapigwa hela nje nje kama unavojua watu wengi hatuna elim ya magari. Inauma sana kwakweli.

Hawa jamaa wanawabadilishia taa , fan na time belts, battery nk hivi ndo nashuhudia live. Mimi nimefungua ofisi yangu mitaa ya huku sokoine karibu na port view sasa huku ndo gari zilizotoka bandarin ndo zinazagaa sana unakuta gari inakaa mpaka wiki 2 kwa wakala unajiuliza ina maana mwenye gari hana taarifa? Kama ni ishu za tbs jamaa anashindwa kufix tatizo mapema?.

Hapa ofisn mimi nafanya polishing, painting, nauza lubricants nk sasa wengi huwa wanakuja kupata huduma, juzi kuna jamaa kaja na crown athelete kupiga ribiti sasa jamaa akampigia simu mwenye gari, maongezi yao yalikua hivi nanukuu “ tajir mambo vipi gari yako imefika toka juzi sasa nimeshamalizana na TRA bado TBS kwasababu gari betri imekufa na belts zote zimeisha tumeambiwa tuchange ili gari ipewe certificate ndo tukafanye usajili na gari ikiendelea kukaa hapa bandarin inachajiwa mkuu”

Jamaa akapaniki “ndomana nimekupa kazi betri sh. Ngap jama akamwambia chukua la mtumba la crown kama yako jamaa anauza achana naya dukani bei 250k na belts 270k za mtumba crown original, jamaa akasema nakutumia chap, jamaa anaongea ukituma mapema leo leo gari inatoka mpaka plate No. . Jamaa hakuchukua hta dk5 akatuma hio pesa walichofanya jamaa wakaisafisha ile betri wakabandika plate No. hao wakasepa boya kashaliwa. Ikabandikwa pale DXM kumbe gari ilikua imesajiliwa tyr.

Mwingine huyu alikua dada amepigwa kama
Laki6 kweli kupiga ribiti, kuosha engine na kufanya service laki6??. Jamaa anakuagizia gari imepauka hatari ikifika bongo anakupigia polish inanga’a fresh hizi gari kila siku tunapiga polishi na kurudia rangi ,au kama kuna michubuko anarudia rangi wewe huwezi jua. Ni matukio mengi siwez sema yote.

Sasa gari ambazo zinafanyiwa ma service ya ajabu ni hzi BMW na marcedes nyingi utakuta mara power window imekufa, sijui nn nilimuuliza jamaa akasema wengi wanaagza hizi gari kwa mihemuko anachukua ya bei rahs ilimradi na yeye awe na bmw matokeo yake gari inafika na matatizo lukuki.

Ushauri wangu agiza gari mwenyewe mpe agent kazi ya kufanya clearing tu, fatilia meli ilobeba gari yako mwanzo mwisho ikifika tu lazma agent anajua fatilia hatua zote anazofanya kama gari inashida mara nyingi tbs mtasumbuana kwenye tairi kama unachochote wape usipoteze muda kama una pesa mwambie atoke na gari wewe ichukue gari yako usimwachie kabadili tair hapo gari ushaichek angle zote.

Kama unatumia agent hakikisha anakupa picha za gari zote na malipo fanya wewe usimpe yeye afanye malipo hapa wengi wanalizwa, agent atakuagizia gari ya kawaida ili apate faida zile high quality hawezi sababu bei ni kubwa itamkata. Ogopa sana huu utapeli kuagza toyota ist ni 13.5m awamu ya kwanza utalipia 7m afu utamalizia 6.5m ogopa sana huu utapeli.

Kuna agent wengine ni waaminifu ila tatizo la wale wanaokwenda kule kufanya clearing bossy hawez kwenda bandarin atatuma vijana watu hawaaminiki asee watu wanajiongeza sana. Watu wana njaa nyie kuna jamaa tulimwambia tunataka taa za subaru OG akasema nipeni siku3 kuna gari inatoka soon kweli akaleta taa
Unafikiri katoa wapi?

Sema nini watu wanashusha mandinga makali sana asee daah .
 
Watanzania wengi wamezoea spoon feeding..... kwenda tu website ya befoward kuchagua gari kwa hitaji lake, anamwachia agent na wengine wanamkabidhi cash eti agent ashughulike kila kitu tunayo safar ndefu sana
What do expect, utaambulia aina ya gari, habari ya Ubora na vingine ni juu yako.
 
Kuna muda huwa naona hata hawa viongozi serikalini tunawalaumu kuwa ni wezi ila kiukweli watanzania wengi hatujapata upenyo wa kutia mpigo.

Hii nchi na kizazi chake kina vinasaba vya wizi kwa kila mmoja hii ni laana kwa taifa inahitajika maombi ya kufunga juu ya hii dhambi ambayo ni adui mkubwa wa maendeleo
 
Sana tu...hata wewe jamaa lazima katika kuutafuta ugali kwa kazi unayofanya huwa una mafekechee yako...

Mara kibao huwa mnatupiga za macho kuwa mnang'arisha taa zinarudi kuwa kama mpya, wiki mbali taa zinarudi kuwa za njano

Ukiona hvo jua hawajatumia mashine wametumia dawa, ukitumia mashine inadumu sana we leta gari yako
 
Hahah...
Ndio maneno yenu hayo, utasikia nipe buku 10 nikusafishie kwa mashine...wale wa kibirika au dawa ya kupaka wanakosea

Mkuu mimi ni kampuni lazima nitoe huduma nzuri kuna tofauti na wale wa chini ya mti. Mimi nakupa na warranty mkuu sifanyi kazi kwa kubahatisha. Polish vipi? Gari haijafubaa bado
 
Back
Top Bottom