Taswira ya mbunge wa iramba magharibi,nd mwigulu Nchemba imezidi kuharibika jimboni kwake iramba.Kuharibika kwa taswira ya Mwigulu,kumeongezeka baada ya ziara yake iliyoanza jana hapa iramba,kuambatana na tukio baya lenye harufu ya kigaidi,la kuchomwa moto kwa nyumba ya katibu wa chadema kata ya kidaru,ndugu Philipo Manguli na kuteketea kabisa pamoja na tv,thamani za ndani na vifaa vya uenezi kama bendera na kadi.Mwigulu nchemba amekuwa akimtisha kiongozi huyu wa chadema,hasa baada ya kazi nzuri anayoifanya ya kuelimisha wananchi.Usiku wa kuamkia leo vitisho vyake vimeanza kutimia baada ya kuteketezwa kwa nyumba yake na yeye mwenyewe manguli na familia yake kunusurika kifo.Hivi karibuni alimtisha jeska kishoa.