Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Suala la mikopo ya chap chap yenye riba kubwa maarufu 'kausha damu' limejitokeza katika mkutano wa hadhara wa Katibu wa NEC, Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ambapo wananchi wa Singida Mjini wamemuomba kiongozi huyo kuwasaidia.
Leo Alhamisi Januari 25, 2024 Makonda akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya zamani ya mabasi wilayani Singida amepokea kilio cha kausha damu kutoka kwa mmoja wa wakazi wa wilaya hiyo, Shaban Itambusa aliyesema mikopo ya aina hiyo inawatesa wananchi.
Baada ya maelezo hayo, Makonda alimuita Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba aliyekuwa katika meza kuu kwenda jukwaani kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
Akijibu maswali hayo, Dk Mwigulu amesema ni kweli wakopesha wa kausha damu wamepewa leseni na riba wanayoipata ni kwao si Wizara ya Fedha au waziri anayenufaika.