"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

Lulu ni #1 suspect na Seth ni #2 hakuna jinsi hapo!

na kama lulu alijichana chana baada ya kugundua keshaua tayari, hilo unalisemeaje? Pia yawezekana Kanumba alimrudisha Lulu ndani kwa nia nzuri tu na mtoto kafika ndani kareact na kujaribu kukimbia tena. Na hapa inawezekana ndiyo alimsukuma kwa nguvu sana ili ampishe. Katika hali ya kawaida Lulu hana nguvu ya kumsukuma Kanumba hadi apasuke kichwa na kufa. Na hapa ndiyo panapokuja suala la uchunguzi zaidi. Yaweza kuwa alimrudisha chumbani na tayari kikawa kinataka kwenda kwa yule jamaa mwingine na hapo kikamvizia na kumpiga na kitu kizito kisogoni. Kwanza siyo rahisi kuanguka na kupata jeraha kama ni kuanguka kwa kawaida tu chumbani. Hapo kuna maswali mengi. Sitetei upande wowote mpaka uchunguzi ukamilike. Utata ni zaidi ya tuwazavyo.
 
Mimi naona maelezo yaliyopatikana ni ya pande mbili,yaani Lulu na Sethi.Lakini sikuona sababu ya lulu kuondoka eneo la tukio mapema kiasi hicho kwasababu mtu aliyokuwa anamuogopa tayari alikuwa hana fahamu.Angesubiri mpaka daktari aje waondoke na mwili mpaka hospitari.

Tatizo hapa ni kwanini alitoweka eneo la tukio mapema kiasi hiki,kitendo hicho ndicho kinapelekea wadau wahisi kama pengine alihusika.

Mdogo wa marehemu yaani Sethi,amenukuliwa akisema alisikia sauti za malumbano, lakini alishindwa kuingia ndani kwasababu mlango wa chumbani ulikuwa umefungwa.Kwa mujibu wa kauli hii inaonyesha kuwa sauti zilizokuwa zinasikika zilikuwa za kawaida kiasi kwamba hazikumfanya apige keleke kuomba msaada kutoka nje.

Mtazamo wangu ni kwamba kama Marehemu angekuwa hai angetoa maelezo ya makovu yaliyokutwa kwa lulu kuwa yametokana na kipigo kutoka kwake au alikuja nayo; Lakini kama Lulu ndiye aliyetoa taarifa kwa Sethi kuhusu kudondoka kwa Kanumba,Basi hata Sethi anaweza kutoa ushuda wake kwa namna alivyo muona Lulu pindi alipompa taarifa, kwamba alimuona ana makovu au laa.

Ushauri wangu ni kwamba, hakuna tukio lisilokosa sababu,na ajali haina kinga; Fundisho hapa tuwe na kiasi kwa kila jambo:Simu za mkononi ni nzuri kama zitatumika kwa uaangalifu mkubwa,lakini ni mbaya kama zitatumika vibaya. Mimi naamini hakuna mpenzi asiye na wivu kwa mwinzi wake hasa kama anampenda, cha msingi tuwe makini na hivi vilonga longa

Jibu dogo hapa, She just panicked,
Mkuu kuna incidence zikitokea unaweza usijue umefikaje hapo ulipo.
Reference: Waathirika wa mabomu Gongola Mboto
 
Nimeisoma thread yako kwa umakini mkubwa kabisa na nimeielewa vizuri sana. Unajua jambo kubwa lililosababisha Lulu kuonekana kuwa amehusika na mauaji ya Kanumba ni pale alipokimbia baada ya kumuita Seth. Kwa kawaida sidhani kama inawezekana kumuacha mtu unayempenda kwa dhati katika hali ya umahututi na kukimbia zako hata kama walikuwa wamegombana. Inawezekana pengine alikimbia kwa sababu alichanganyikiwa kutokana na yale yaliyotokea huko chumbani na akili yake ilimtuma kukimbia kwa wakati huo.

Kitu kingine ambacho kinamfanya Lulu aonekane kuwa amehusika na mauaji hayo, ni kutokana na sifa mbaya ya umalaya aliyonayo ya kuwa na wanaume wengi kuliko nguo alizonazo kitu ambacho kinamfanya aonekane kuwa hana upendo wa kweli kwa wapenzi wake hivyo ana uwezo wa kufanyia kitu chochote kibaya wapenzi wake bila kujali uhusiano wao.

Sitaki kuamini kama lulu ameua na hata kama atakuwa ameua mimi naamini hakukusudia kufanya hivyo ila maelezo yangu ya aya ya kwanza yananishawishi niamini kuwa Lulu amehusika na mauaji hayo.

Ila yote hayo amejitakia yeye mwenyewe. Kama asingejihusisha na umalaya na kubadilisha wanaume kama chupi sidhani kama yote hayo yangemkuta. Alikanywa lakini hakusikia na ndio maana waswahili walisema Asiyesiikia la mkuu huvunjika guu na asiyefunzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu.
 
Duh.. haya maoni ya wana JF..! Ila ninavyojua kutokana na maelezo ya mwanzo.. Lulu ni Prime suspect lakini maelezo ya daktari ni ya muhimu sana.. So far inasemekana Kanumba hakuwa na majeraha kokote na wala uvimbe.. Hii ina maana hakujigonga sehemu ambayo labda ingesababisha concussion kwa kichwa.. Kinachofuata hapa Daktari achunguze.. inawezekana Kanumba alipatwa na labda ugonjwa wa moyo..? Kuna kitu Lulu alisema kikampa mshtuko Kanumba..? Kuna tetesi kwamba Kanumba alikuwa amekunywa whisky.. Jee ni kwa kiasi gani..? Jee kanumba alikuwa under any medication..? Tetesi nyingine ni kwamba Kanumba alikutwa ametokwa na mapovu mdomoni.. Hii yote itamalizwa na autopsy ambayo au itahalalisha Lulu kuachiwa huru.. au kushtakiwa kwa kosa la mauaji ya kuua bila ya kukusudia..
 
Nadhani ni muhimu jeshi la polisi likafanya uchunguzi kwa uhuru na usawa. Naamini watabaini tu nini kilichotokea. Ila sioni uwezo wa Lulu kufanya mauaji kama hayo. Inaweza kuwa ni ajali tu kuwa marehemu alidondoka na kuumiza kichwa chake kwenye kitu chenye ncha kali na kupoteza maisha. Ni msiba mkubwa kwetu sote, na si vyema kuufanya ukasababisha msiba zaidi hata kwa wengine.
 
je lulu ana mafunzo yoyote ya martial arts?

Je lulu ana historia ya kupiga watu?

Je lulu ana historia ya kutishia kuua?

Hivi lulu alilelewa na wazazi wake wote?

Lulu akiwa shuleni alifanya matukio gani ya ajabu?
 
Pia si inasemekana marehemu alikuwa amekunywa pombe kali....sasa kama hiyo ni kweli basi huenda pia ilipelekea yeye kuwa na aggression zaidi na pia labda kupoteza equilibrium yake na hivyo kudondoka na kujibamiza kichwa kwenye kitu kigumu.

Ila pia, matatizo ya kutokuwa na emergency systems za uhakika ndiyo matokeo yake haya. Ingekuwa kwenye nchi za watu mdogo wake angeweza tu kupiga simu 9-1-1 na watu wa EMT, Fire and Rescue, pamoja na polisi wote wanakuja kwa wakati mmoja.

Hii inahakikisha at least eneo la tukio litahifadhiwa kwa evidence collection (zitapigwa picha, itaandikwa ripoti , n.k.) huku mtu akipata matibabu ya dharura kabla hajapelekwa hospitali.

Sasa sina hakika hata kama marehemu alipelekwa huko Muhimbili akiwa kwenye gari la kubebea wagonjwa na sijui hata hao polisi walifika kwenye hilo eneo la tukio baada ya muda gani!!
 
je lulu ana mafunzo yoyote ya martial arts?

Je lulu ana historia ya kupiga watu?

Je lulu ana historia ya kutishia kuua?

Hivi lulu alilelewa na wazazi wake wote?

Lulu akiwa shuleni alifanya matukio gani ya ajabu?

Nashukuru sana Jack kwa maswali yako ..naamini hata wenzetu
wanaohusika na upelelezi wamo humu na pengine
wataweza kuona haya na kuyachukua yawasaidie ili haki itendeke.
 
Nadhani ni muhimu jeshi la polisi likafanya uchunguzi kwa uhuru na usawa. Naamini watabaini tu nini kilichotokea. Ila sioni uwezo wa Lulu kufanya mauaji kama hayo. Inaweza kuwa ni ajali tu kuwa marehemu alidondoka na kuumiza kichwa chake kwenye kitu chenye ncha kali na kupoteza maisha. Ni msiba mkubwa kwetu sote, na si vyema kuufanya ukasababisha msiba zaidi hata kwa wengine.

I think the police have bungled their investigation from the get go.
 
LULU HAKUPANGA KUMUUA KANUMBA!

1.katika mazungumzo yake na mkasi,hakupenda kugusia kama ana mahusiano na Kanumba.pia sikuona kama alishtushwa na swali hili.lakini tusisahau kuwa swali hili lingeweza kumkumbusha mabaya(ubakaji) aliokuwa akifanyiwa na marehemu labda kwa kisingizio cha kumtoa kimaisha.

2.kama lulu angepanga kumuua kanumba asingeweza kutumia ugomvi kwa sababu asingekuwa na uhakika wa kumshinda kanumba kimabavu.

3.kama lulu angepanga kumuua kanumba sitegemei angefanya hivyo nyumbani kwa kanumba tena kwa kutumia ugomvi.

4.pia kama lulu angepanga kumuua kanumba asingetoka na kumuambia seth kuwa kanumba kaanguka.angesubiri mpaka afe na baadaye kuondoka kimya kimya.

..........ngoja niendelee kufikiria!

Jackbauer nakuheshimu sana lakini hiyo namba moja is the poorest analysis of the year kwangu.
Ila kwa kuwa umesema unaendelea kufikiri sio mbaya sana, nadhani unaweza kuwaza zaidi ya hapo.
 
Jackbauer nakuheshimu sana lakini hiyo namba moja is the poorest analysis of the year kwangu.
Ila kwa kuwa umesema unaendelea kufikiri sio mbaya sana, nadhani unaweza kuwaza zaidi ya hapo.

labda ungefafanua ni kwa nini umesema ni poorest analysis na mimi nikufafanulie kwa nini nimeiweka.
 
Naanza na kutoa Pole kwa watanzania wote, hasa ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa Kanumba The Great (R.I.P) kabla sijatoa mchango wangu kuhusu hili jambo zito na nyeti ambalo limetawala maongezi katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka. Mengi yamesemwa na pia kuna mengi pia hayajasemwa, moja wapo likiwa "ujinai" wa Lulu katika kifo cha Kanumba.

Katika mukatadha wa sheria, tunaona kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye kuuweka uwajibikaji kijinai kuwa chini ya UMRI wa miaka 18 kwa kuweka miaka 10 kama umri ambapo mtu anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai. (Linganisha na Kenya miaka 8, Zimbabwe -7,Zambia 8,Africa Kusini 10) n.k. Ina maana kwamba mtu (mtoto) aliye chini ya umri huu hawezi kushtakiwa labda ithibitishwe kuwa alikua anajua kabisa anachokifanya. Lulu hafit kwenye kundi hili hata kama ana umri wa miaka 17 kama ambavyo Mh Halima Mdee ame tweet leo baada ya kumtembelea LuLU Oysterbay Polisi.

Tukiacha sheria na matakwa yake, kwa kuzingatia yale yanayosemwa kuhusu mkasa huu wa kifo cha Kanumba (R.I.P), inatupasa tuone kuwa kila hadithi ina pande mbili. Hadithi ya Kanumba ambaye kwa sasa hayupo kuelezea, na hadithi ya Lulu aliye mahabusu. Inasikitisha sana kwamba kifo kimetokea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.

Kama watanzania wengine napenda niseme kwamba , nahuzunika kama wengine kumpoteza Kanumba na pia kuona ndoto zake kama msanii zikizimwa ghafla. Aidha wapenzi wake wamekatishwa ile raha ya kuendelea kuburidika na filamu zake. Pamoja kuwa na huzuni kuu, pia najaribu kuangalia upande wa pili – Lulu! Huyu binti wa miaka 17/18 kijamii bado ni msichana mdogo japo kisheria hasamehewi kuwajibishwa kijinai. Lakini uwajibishwaji huo utakuja pale upelelezi utakapokamilika. Kufuatana na waliobahatika kumuona huyu binti, ana majeraha kuashiria kuwa alipigwa na kuumizwa na marehemu. Ingekuwa marehemu hakufa, basi nadhani kesi hii ingekuwa ya aina yake kama ingefika kunakohusika. Wote walijeruhiana. Lakini mazingira ya kujeruhi huko ni yepi?

Tumeambiwa na hata kusoma kwamba:

1. Lulu alienda kwa Kanumba usiku mkali mishale ya saa 6, kusudi watoke kwenda kucheza muziki kwa msanii Chaz baba – Mashujaa band ( Kanumba alishapiga simu kutaka andaliwe viti na sehemu maalum ya kukaa yeye na marafiki zake na pia akiomba hata wimbo maalum atakapofika)
2. Lulu alitoka nje kusikiliza simu – Kanumba akamfuata na kumrudisha ndani ili aeleze anaongea na nani.( Hapa tunaona kabisa Kanumba akianzisha shari yeye mwenyewe badala ya kuepuka shari)
3. Kanumba alimfungia Lulu ndani wakawa wanagombana. Aggressor hapa ni Kanumba na siyo Lulu.Kelele za ugomvi ziliashiria vurugu na kwa vile mlango ulifungwa na ufunguo, ilikuwa vigumu Lulu kukimbia tena au hata watu nje kuja kutoa msaada.
4. Lulu alitoka nje kwenda kumwita Seth na kumwambia Kanumba kaanguka.Lulu alikimbia akiwa na majeraha.Hii haionyeshi kuwa Lulu aliua vinginevyo angetoka kimya kimya akatokomea.

Sasa ndugu zanguni, kwanini Lulu anaonekana alifanya mauaji ya kukusudia? Ikiwa Kanumba alianguka katika purukushani na kuponda kichwa na kufa, Lulu kaua vipi? Kukamatwa na polisi na kushikiliwa ili kusaidia uchunguzi ni utaratibu wa kawaida sana. Nimewahi kushuhudia mtu kajiua, ndugu yake na mkewe waliomgundua kajining'iniza walikamatwa wakakaa ndani ili wasaidie uchunguzi Ilahali mtu kajiua mwenyewe. Ilisikitisha sana kwa maana wafiwa walitiwa misukosuko kwa kifo ambacho marehemu alijiletea kwa kujitundika. Walikaa masaa kadhaa kabla ya ndugu kwenda kuwatetea na kushinikiza waachiwe!

Kwenye hii kesi ya Lulu, bahati mbaya sana Lulu ana sifa mbaya kwenye jamii kiasi kwamba hakuna mtu anathubutu kumtetea na kumsaidia angalau aweze kujipanga kukabiliana na siku za kusubiri hatma baada ya upelelezi. Kibaya zaidi kuna statements za watu wazito ndani ya jamii, statements ambazo zenyewe tu zimeshapasisha kwamba Lulu ndio muuaji. Kibaya zaidi, unyeti wa hali inayozunguka msanii maarufu kipenzi cha wengi utaathiri hata mwenendo mzima wa upelelezi na kitakachojiri to the detriment of Lulu.

Nadhani kwa vile hii haijawa kesi ya kimahakama, na kwa vile jamii inazungumzia hiki kifo, hakuna ubaya tukawa na scenario zote.

Sijaandika haya kwa vile nataka kumsemea Lulu asiwajibike kama anahusika kijinai bali najaribu kupanua mjadala.

Nawasilisha.
WoS.

Nimefuatiliana tukio hili mpaka sasa, lakini bado sijajua Lulu alipokamatiwa? Naomba kuuliza Lulu alikamatiwa wapi na Polisi? hili ni swali muhimu sana, alafu tuendelee.
 
labda ungefafanua ni kwa nini umesema ni poorest analysis na mimi nikufafanulie kwa nini nimeiweka.

Kwa sababu imejaa speculation na ambayo haiwezi kuthibitika mkuu. Ulivyoisema is as if una uhakika nayo wa 100% wakati ni kitu ambacho umekiwaza tu kwenye akili yako.
Nadhani kwa mtu muelewa huwezi kuleta jukwaani analysis ambazo zimekua influenced na individual subjectvism/ guess. Katika hali halisi hiyo namba moja ndivyo ilivyo unless uniambie una uthibitisho kwamba Kanumba alikua anambaka huyu binti.
 
Uchunguzi ufanyike kwa Hali ya juu, weledi wa hali ya juu utumike. Kufikiri na kutafakari ni jambo muhimu.

Nawaomba Polisi watumie wataalamu wa Sociology na psychology Chuo kikuu cha UD.

Pia inatakiwa SETH aapishwe ili aseme ukweli, ili asije kusema uwongo kumsingizia Lulu.

Pia Lulu ahojiwe taratibu na wanasaikolojia. Wanasaikolojia wana maswali yao maalum ya kutambua ukweli.

Pia Historia yao ya afya iangaliwe.
 
Naanza na kutoa Pole kwa watanzania wote, hasa ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa Kanumba The Great (R.I.P) kabla sijatoa mchango wangu kuhusu hili jambo zito na nyeti ambalo limetawala maongezi katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka. Mengi yamesemwa na pia kuna mengi pia hayajasemwa, moja wapo likiwa "ujinai" wa Lulu katika kifo cha Kanumba.

Katika mukatadha wa sheria, tunaona kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye kuuweka uwajibikaji kijinai kuwa chini ya UMRI wa miaka 18 kwa kuweka miaka 10 kama umri ambapo mtu anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai. (Linganisha na Kenya miaka 8, Zimbabwe -7,Zambia 8,Africa Kusini 10) n.k. Ina maana kwamba mtu (mtoto) aliye chini ya umri huu hawezi kushtakiwa labda ithibitishwe kuwa alikua anajua kabisa anachokifanya. Lulu hafit kwenye kundi hili hata kama ana umri wa miaka 17 kama ambavyo Mh Halima Mdee ame tweet leo baada ya kumtembelea LuLU Oysterbay Polisi.

Tukiacha sheria na matakwa yake, kwa kuzingatia yale yanayosemwa kuhusu mkasa huu wa kifo cha Kanumba (R.I.P), inatupasa tuone kuwa kila hadithi ina pande mbili. Hadithi ya Kanumba ambaye kwa sasa hayupo kuelezea, na hadithi ya Lulu aliye mahabusu. Inasikitisha sana kwamba kifo kimetokea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.

Kama watanzania wengine napenda niseme kwamba , nahuzunika kama wengine kumpoteza Kanumba na pia kuona ndoto zake kama msanii zikizimwa ghafla. Aidha wapenzi wake wamekatishwa ile raha ya kuendelea kuburidika na filamu zake. Pamoja kuwa na huzuni kuu, pia najaribu kuangalia upande wa pili – Lulu! Huyu binti wa miaka 17/18 kijamii bado ni msichana mdogo japo kisheria hasamehewi kuwajibishwa kijinai. Lakini uwajibishwaji huo utakuja pale upelelezi utakapokamilika. Kufuatana na waliobahatika kumuona huyu binti, ana majeraha kuashiria kuwa alipigwa na kuumizwa na marehemu. Ingekuwa marehemu hakufa, basi nadhani kesi hii ingekuwa ya aina yake kama ingefika kunakohusika. Wote walijeruhiana. Lakini mazingira ya kujeruhi huko ni yepi?

Tumeambiwa na hata kusoma kwamba:

1. Lulu alienda kwa Kanumba usiku mkali mishale ya saa 6, kusudi watoke kwenda kucheza muziki kwa msanii Chaz baba – Mashujaa band ( Kanumba alishapiga simu kutaka andaliwe viti na sehemu maalum ya kukaa yeye na marafiki zake na pia akiomba hata wimbo maalum atakapofika)
2. Lulu alitoka nje kusikiliza simu – Kanumba akamfuata na kumrudisha ndani ili aeleze anaongea na nani.( Hapa tunaona kabisa Kanumba akianzisha shari yeye mwenyewe badala ya kuepuka shari)
3. Kanumba alimfungia Lulu ndani wakawa wanagombana. Aggressor hapa ni Kanumba na siyo Lulu.Kelele za ugomvi ziliashiria vurugu na kwa vile mlango ulifungwa na ufunguo, ilikuwa vigumu Lulu kukimbia tena au hata watu nje kuja kutoa msaada.
4. Lulu alitoka nje kwenda kumwita Seth na kumwambia Kanumba kaanguka.Lulu alikimbia akiwa na majeraha.Hii haionyeshi kuwa Lulu aliua vinginevyo angetoka kimya kimya akatokomea.

Sasa ndugu zanguni, kwanini Lulu anaonekana alifanya mauaji ya kukusudia? Ikiwa Kanumba alianguka katika purukushani na kuponda kichwa na kufa, Lulu kaua vipi? Kukamatwa na polisi na kushikiliwa ili kusaidia uchunguzi ni utaratibu wa kawaida sana. Nimewahi kushuhudia mtu kajiua, ndugu yake na mkewe waliomgundua kajining’iniza walikamatwa wakakaa ndani ili wasaidie uchunguzi Ilahali mtu kajiua mwenyewe. Ilisikitisha sana kwa maana wafiwa walitiwa misukosuko kwa kifo ambacho marehemu alijiletea kwa kujitundika. Walikaa masaa kadhaa kabla ya ndugu kwenda kuwatetea na kushinikiza waachiwe!

Kwenye hii kesi ya Lulu, bahati mbaya sana Lulu ana sifa mbaya kwenye jamii kiasi kwamba hakuna mtu anathubutu kumtetea na kumsaidia angalau aweze kujipanga kukabiliana na siku za kusubiri hatma baada ya upelelezi. Kibaya zaidi kuna statements za watu wazito ndani ya jamii, statements ambazo zenyewe tu zimeshapasisha kwamba Lulu ndio muuaji. Kibaya zaidi, unyeti wa hali inayozunguka msanii maarufu kipenzi cha wengi utaathiri hata mwenendo mzima wa upelelezi na kitakachojiri to the detriment of Lulu.

Nadhani kwa vile hii haijawa kesi ya kimahakama, na kwa vile jamii inazungumzia hiki kifo, hakuna ubaya tukawa na scenario zote.

Sijaandika haya kwa vile nataka kumsemea Lulu asiwajibike kama anahusika kijinai bali najaribu kupanua mjadala.

Nawasilisha.
WoS.
ahsante kwa taarifa dada muhishimiwa
 
.......Huyo Halima Mdee alikuwa wapi zamani kumuonya Lulu? Leo ajifanye ana huruma naye? Nani asiyejua kwamba Lulu ni mapepe......kila siku alikuwa anaanikwa kwenye magazeti ya Shigongo, ina maana Halima hakujua tabia za huyo binti?

Hata kama yupo 17, je alilazimishwa kuhusiana kimapenzi na Kanumba? Kama si hiyari yake kwa nini hakumshtaki marehemu basi kuwa nalazimishwa kuhusiana naye!!

Huyo binti ana akili timamu I mean ni mtu mzima, na sheria ifatwe kama inavyotakiwa. Akikutwa na kosa haya, asipokutwa na kosa haya. Hata mie namuonea huruma sana Lulu, najua yupo katika kipindi kigumu. Ila sheria lazima ifuatwe.

Sorry WoS, nimechangia hii post yako bila kumaliza maelezo yako hapo juu. Sasa ngoja nisome umesema nini.
 
Kweli kabisa umesema points@Woman of Substance nimekusoma vilivyo mie sio mwanasheria lakini kuna makosa mengine yanasomeka kabisa na kama yakisimamiwa kisheria pasipo kupindishwa mbona kinaeleweka kabisa kama hii issue ya Elizabeth Michael(Lulu)ni kwamba iko wazi sana sema tu watu wanamuona Elizabeth ni muuaji tusimhukumu Lulu jamani tusubiri uchunguzi na pia ingekuwa pia hata Bosco angekuwa ndani kwa uchunguzi zaidi maake kwa kubaki kweke nje uanaweza haribu uchumguzi ninavyofahamu mie hata mbele kama mtu kafariki kw nyumba then ndani mko watu zaidi ya 2 wote mtasombwa.So kimsingi Elizabeth Michael anahitaji msaada sana tu,siwezi kumlaumu Kanumba kwani muda umekwisha wa kumlaumu lakini moja kwa moja alikuwa na makosa kwanza kutembea na Under age hata kama wanasema she is 18 lakini watakuwa hawajaanza juzi ati Kanumba atakuwa amemtumia Elizabeth Michael(Lulu)for long time may be kuanzia ana miaka 15 or 16 hapo moja kwa moja ana makosa japokuwa marehemu anakuwa na kipaumbele kuliko aliyebaki imagin angefariki Elizabeth Michael je Jamii ingemchkuliaje Kanumba?Je haya yote yangesemwa?
Wajamen nawaomba tusimhukumu Lulu kwani kwanza hajafahamu yaliyotokea yangekuwa mauti so inaweza kutokea kwako wewe au kwangu mia kumbuka sote ni binadamu.Ningekuwa mwanasheria ningejitokeza kumsaidia Elizabeth Michael ile apatiwe haki yake,tuachane na ushabiki usio wa maana oooh kauwa kauwa kumbuka aliyesababisha yote ni Marehemu asingemvuta mpenzi wake kwa ajili ya wivu na kujifungia chumbani huenda huyu binti kwa jinsi alikvyozidiwa na kibano angetoka nduki so sema tu ndio hivyo mashabiki wa Bongo movie viherehere vingi mbona wapo wengi u wanafikwa na mikasa hii hawasemi au kwa kuwa ni Bongomovie.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom