Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,598
- 215,315
Wengi tunapofikiria kufungua frame ya duka, unawaza mahali Pa kuweka bidhaa na dirisha la wateja kuona na kununua bidhaa. Mambo ya muhimu tusiyo yazingatia ni mahitaji ya binadamu anaehudumia duka.
Mhudumu anahitaji kula, anahitaji kwenda haja. Haya ni mambo ya muhimu kwa kila binadamu. Unapoweka frame weka na jiko, choo na sehemu ya kuhifadhia bidhaa. Jikoni unaweza kuweka jiko la kupikia chakula, microwave na fridge. Mhudumu akipata mapumziko ya chakula anaweza kupasha kiporo chake cha wali maharage alichotoka nacho nyumbani au akaja na mchuzi wa kuku au mchicha wa nazi na akaweza kupika ugali wake pale na siku ikaendelea
Choo kitamsaidia mhudumu au hata wateja wako wachache. Fikiria mtu anafanya manunuzi ya milioni nne ana kutaarifu traffic ilikua kubwa barabarani amekaa njiani masaa matatu na anawahi kurudi. Kama anahitaji huduma ya choo unaweza kumpisha.
Ukiweka store ya ziada unawsza kuhifadhi bidhaa za ziada na pia kitanda cha mtu wa kulinda duka kwa ndani.
Unajenga frame choo kiko nje cha shimo, unamuona mhudumu anakwenda uwani na kopo la maji na akitoka huko aje akupimie sukari.!!