Ujenzi wa barabara za mwendokasi una ufisadi ndani yake?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Mipango yetu mibovu inatufilisi, natafakari kimoyomoyo kisha kwa sauti kuhusu ni nani anahusika katika kuliingiza taifa masikini kama la kwetu kwenye hasara hizi za kubomoa barabara mpya ambazo hazijachoka ili kupisha ujenzi wa barabara za magari yaendayo haraka, BRT.

Barabara zetu zinazojengwa sasa zinaachwa matoleo ya kupitisha barabara za usafiri wa haraka lakini hawajengi vituo vya magari ya usafiri huo.

Hii inasababisha siku ya kuvijenga vituo hivyo kulazimika kuzibomoa na kuzijenga upya barabara za magari ya kawaida hata kama barabara hizo bado zinapitika.

Mfano, huwa nawaza siku kipande cha barabara cha Morocco hadi Mwenge kilichomalizika juzi tu kujengwa kitapotifuliwa na kujengwa upya tena wakati ukifika wa kujenga stendi za mabasi yaendayo haraka kwenye kipande hiki. Pesa nyingine itahitajika kuibomoa na kuijenga upya kama tunavyoshudia sasa kwenye kujenga BRT.

Hivi mipango yetu kwanini inatutia hasara au kuna ufisadi kwenye kujenga barabara? Kwanini anaejenga barabara, mfano zile za Ubungo Kimara hadi KIBAHA na Morocco hadi mwenge asiepushe gharama kwa walipa kodi kwa kujenga kabisa vituo vya BRT badala ya kuacha matotoleo tu ya njia hizo?

Hela ya kubomoa tena na kujenga barabara ambayo haijachoka kwanini zisipelekwe kujenga barabara kwenye maeneo ambayo yana shida ya barabara?

Watu wa mipango mnatufisadi bila ya kukusudia pengine, fanyeni yote kwa pamoja iliwezekana.
 
Back
Top Bottom