Uhawara miaka 10

Kwa kweli mambo yamebadilika sana siku hizi, hapo hao mahawara wanaona ni kitu cha kawaida kabisa na mtu akienda kuwashauri watamuona wa ajabu na kapitwa na wakati...Kwa kweli inatakiwa tumtegemee Mungu kwa kila jambo na hasa hapa kwenye kutafuta wenza ambao hawatakuwa na tamaa na ambao tutaendana nao.
 
Haya mambo bwana,
Mi nasema tu kama Mungu yupo na kama kweli tunavyoamini ndiye anayetupatia mume/mke mwema basi na atuhurumie tu, atukutanishe na wale watu ambao nafsi zetu zinaendana nao!!

Vinginevyo haya mambo sio marahisi kabisa!!

na kweli atuhurumie, manake..mmmmmhh
 
Kinachowafanya mahawara kudumu kwa muda mrefu ni kile kitendo cha kutoonana na kugandana muda wote kama wanandoa. Kinachowakutanisha zaidi ni starehe (ngono). Mbaya zaidi hapa ndio kila ufundi huonyeshwa. Binadamu angekuwa na ufahamu zaidi ya alio nao japo kidogo tu angeweza kugundua dawa ya tatizo hili. Sehemu ya tatizo ni kuwa mke anafanywa kuwa mke na mume kadhalika badala ya rafiki fulani hivi.

Suppose yale anayotendewa hawara akitendewa mke/mume yataleta mabadiliko?
 
wengi wanafanya kuona kama desturi yaani lazima ufanye hivyo ndio mana ndoa zimekuwa ndoano!
 
Wabongo kwa kuoa na kuolewa tu hamjambo, ndoa zimepitwa na wakati achaneni nazo jamani!
 
kuna kale kamsemo kanasema hawala hawaachani ila wanatengana tu.
 
Mara nyingi watu huwa wanaingia kwenye ndoa na watu ambao hawana vigezo wavyo kuwa wakivihitaji, ndio anapo kuja kuona mtu mwenye vigezo vile anatokea kuanza kumpenda kuliko hata yule aliyenaye.

Nani kakuambia vigezo ni static? vigezo vinabadilika kila kukicha ndio maana watu wanatoka............soma post ya Michele utaona sababu kibao watu wanatoka................Suluhisho ni kuomba msaada wa Mungu na kuamua kusema huyu ananitosha basi.
Say No to Tamaa
 
Kuna wadau wawili mwanamke na mwanaume. Wote wana ndoa zao. Wameanza kuchakachuana tangu 2001 hivi na hadi leo hawana dalili za kubandukana. Mke mumewe anajua kinachoendelea ila kachemka kuzuia. Sasa hawa wagoni ndio kwamba wanapendana sana? Ndio kusema wangeoana wasingechakachua? Nadhani unapotafuta mwenza tafuta anayekuvutia ili kuepuka haya.
RF hapo kwenye nyekundu,unajua kuna watu wanalazimisha kupenda,minafikiri inatakiwa kupenda to the maximam mpaka unahisi kuchanganyikiwa na huyo mwenzi nae anatakiwa ajisikie hivyo hivyo sio kama unapenda penda hivi but sio sana, siku utakapokuwa nae 24/7 atakukinai.
 
tatizo ndo linaanzia hapo. Anayependwa kwa kulazimishiwa nae anamuonea huruma halafu huruma ikiisha vinaanza vitimbi
 
Duuu huo msiba ndugu yangu kulazimika kupenda kisa unamwonea huruma mtu,yani point hii bwana ni black and white kama mtu humfeel unamweleza tu kabla kufika mbali.

kuna watu wameumbiwa huruma ndugu. Esp hawa dada zetu. Ila ikishaisha muda wake na kama haujui namna ya kuihuisha (renew) hiyo huruma utajiju kwa nini ulibembelezea
 
Ndoa hizi bana aaaarghhh ila ndio hivyo tena yatubidi tumuombe mungu sana atusaidie vinginevyooo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom