Mwanamke mpumbavu hupiga kelele

Showmax

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
6,594
12,579
MWANAMKE MPUMBAVU HUPIGA KELELE.

Kabla hatujatafuta mchawi wa mahusiano yetu, tunapaswa kujichunguza sisi wenyewe kwanza tupo sawa au tuna shida mahali ila hatujui kama hilo ndilo linatufanya tushindwe kuwa na amani kwenye mahusiano yetu.

Ukiwa kama binti, unaweza usiwe na tabia zingine mbovu unazojua wewe kama vile zinaa ila ukawa na kitu hichi, "kelele/makelele" unashangaa kila baada ya muda fulani mahusiano yako ya urafiki/uchumba yakikaa huwa yanavunjika.

Unaweza ukapata bahati ya kuambiwa shida yako na aliyekuacha, baada ya kukuonya mara nyingi huko nyuma, ama unaweza kuachwa kimya kimya bila kuambiwa shida yako ni nini.

Ukiwa kama mke, unaweza kuharibu ndoa yako kwa sababu hii, "kelele/makelele" kwa mume wako. Hasa ukiwa umeolewa na mwanaume ambaye hajasimama vizuri kwenye imani, na ambaye hajaokoka.

Ni rahisi sana mwanaume kuchoshwa na mke mwenye makelele/kelele, na kutoka nje ya ndoa yake. Sio njia ya kumaliza tatizo ila kwa mwanaume ambaye hajaokoka kwake haiwezi kuwa tabu kufanya hivyo.

Tunaweza kulalamika sana kuhusu waume zetu wanaochelewa sana kurudi nyumbani ila ukweli ni kwamba, kelele zetu ndio zinawafanya waume zetu waone ni heri kuchelewa nyumbani, kuliko kuwahi nyumbani ukakutana na kelele zisizo na mwisho.

Japo kuchelewa nyumbani hakuwezi kuondoa tatizo, wanaume wengi huona njia hiyo inawasaidia wao kuepuka kelele za wake zao. Sasa huko nje huwezi kujua huyu mwanaume anashindia wapi.

Ndio maana wanawake wengi huanza kuhisi vibaya waume zao, kwa kuwaambia wana wanawake wengine nje. Si unajua kusingiziwa kila siku kitu ambacho hukifanyagi huwa inauma na mtu mwingine inaweza kumwathiri. Na kuamua kufanya kweli, hasa kwa yule asiye na hofu ya Mungu ndani yake.

Kelele zisizoisha ndani ya ndoa zinaweza kuharibu kabisa ndoa ile, wawili hawa wanaweza kuonekana kwa nje wapo pamoja ila ukweli humo ndani hawapo pamoja.

Hebu tuangalie maandiko matakatifu yanasemaje kuhusu hili, huenda umepata ukakasi wa hili fundisho kutokana na kichwa cha somo hapo juu.

Rejea: Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.MIT. 9:13 SUV.

Mwanamke yeyote anayepiga sana kelele ni mpumbavu, na ni Mjinga, yaani ana sifa zote mbili, ya upumbavu na ya ujinga. Tena andiko likaongeza mkazo zaidi, HAJUI KITU.

Kwa lugha nyingine mwanamke wa namna hii, huwa mjuaji sana, kila kitu yeye anajua, yupo juu kwa kila kitu, kujishusha kwake ni hakuna. Mume wake hakuna anachoweza kuzungumza akaeleweka, yeye ni anachojua sana ni kelele.

Wanawake wa namna hii, huwa wanakimbilia wapewe haki SAWA, yaani 50 kwa 50, si unakumbuka ni kwa sababu HAWAJUI KITU! Ni andiko limesema hivyo, wanaojua kitu hawezi kupigizana hizo kelele.

Rejea: Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.1 KOR. 11:3 SUV.

Kichwa cha mwanamke ni mwanaume, na sio kichwa cha mwanaume ni mwanamke... huu sio ukabila. Maana kuna watu hawachelewi kusema huo ni ukabila/utamaduni wa watu fulani, hili ni andiko ndani ya Biblia.

Wanawake mtaponya ndoa zenu wenyewe, acheni kelele ndani ya nyumba zenu, ndoa inajengwa kwa hekima ya kiMungu iliyo ndani yako. Si kwa kelele zako ndani ya nyumba.

Rejea: Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. MIT.14:1 SUV.

Wasiosikia, endeleeni kuzibomoa ndoa zenu wenyewe huku mkilalamikia wanaume, utasema wewe hujui tu ninayoyapata, kwani wakati unaolewa naye hukujua hayo. Si hadi kuna watu walikuja kukunasua ukaona wanakufuatilia maisha yako! Basi tulia, acha kelele.

Tena tabia yake mbaya ulikuwa unaiona kwake ukasema Mungu atambadilisha akiwa ndani ya ndoa, kwa hiyo Mungu ameshindwa hiyo kazi? Jibu ni kwamba, ujuaji wako, upumbavu wako, Ujinga wako, na kutokujua kwako ndio kulikuingiza kwenye mahusiano yasiyo yako. Acha kelele.

Turejee kwa Mungu.

NDOA INAHITAJI USAFI WA ROHO NA MWILI

Uchafu ni kitu cha kuchukiza sana. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuchukuliana na mazingira machafu labda awe hana akili. Usafi ni asili ya Mungu, Mungu hachangamani na uchafu wa aina yoyote. Usafi wa kiroho kwa lugha nyingine ni utakatifu. Mungu wetu ni Mtakatifu, chochote kinachotokana naye ni kitakatifu. Yeye alikusudia kila alichokifanya kidumu katika utakatifu.

Ndiyo maana akakamilisha kazi yake yote ya uumbaji katika utakatifu (dhambi ilikuwa haijaingia duniani). Ndoa ya kwanza ilifungwa na Mungu mwenyewe, na ilifanyika katika usafi wote (Adamu na Eva walikuwa safi walipounganishwa na Mungu) na Mungu akawaagiza waendelee kudumu katika usafi na kuepuka kula atunda ya mti wa mema na mabaya.

Usafi (wa rohoni na mwilini) ni nguzo ya ndoa. Ikiwa wanandoa hawajasimama katika huo, hakuna uwezekano wa kufika mbali. Uchafu husababisha maradhi, harufu mbaya, na kudharauliwa. Heshima ya ndoa inategemea jinsi ambavyo wanandoa watadumu katika usafi. Uchafu wa rohoni hudhihirika kwenye matendo, maneno na mawazo; uchafu wa mwilini hudhihirika kwenye mwili, malazi, mavazi na kwenye mazingira (ndani ya nyumba na nje). Mtu anaweza kuwa na:

1. Midomo michafu
Hii ni ile hali ya kutoa maneno machafu ambayo husababishwa na yale yalioyoko moyoni. Isaya aliuona uchafu huu alipomwambia Mungu “mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu” (Isaya 6:5). Bila shaka utaelewa kwamba midomo michafu hapa haimaanishi midomo ambayo haijasafishwa (hajapiga mswaki); maana yake ni kule kuwa na maneno machafu, kunena mabaya (uovu, masengenyeo, matusi na mengine). Ili ndoa isimame inahitaji maneno mazuri yenye kujenga, maneno ya kutia moyo, maneno matamu, maneno ya staha, maneno yaliyojaa neema ya Mungu. Ndoa nyingi zimeharibika kwa sababu ya midomo michafu.

Ukikuta mke ni mtukanaji, au ni msengenyaji au ni mgomvi asubuhi, mchana na jioni, ujue hakuna ndoa hapo. Hata kama ataishi na mume, yatakuwa maisha ya taabu sana. Mithali inasema “Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi. (Mithali 21:19) Unaona, nchi ya nyika ni mahali pa shida (hapana maji, jua kali, hapana chakula) ila mateso yake hayafikii mateso ya kukaa ndani na mwanamke mgomvi na mchokozi. Je, mdomo wako unautumiaje? Kusudi la Mungu ni kwamba wanandoa watiane moyo, wajadili mambo yao kwa upendo, wapeane maneno yenye kujenga. Siyo kutukanana, kuitana majina ya wanyama, kugombana, na kuchokozana.

Mwanaume anayeutumia mdomo wake kama silaha ya kumpiga mke wake naye haijengi ndoa yake. Mwanaume ni mshauri wa familia, ni mwalimu, ni baba, ni kiongozi na ni mlinzi wa mke na watoto. Maneno ya ukali na matusi au ugomvi, hurarua mioyo ya watoto na mke. Ni muhimu mwanaume kujifunza Kwa Mungu, Baba. Yeye ni Mungu wa Upendo, hata wanawe tukikosea huturidi (hutuadhibu) kwa upendo. Kila wakati anatuwazia yaliyo mema, hajawahi kuwaza kutuumiza au kutuangamiza. Hata tukimkosea atakasirika lakini tukishuka na kumwomba msamaha yeye hutusamehe.

Hivyo ni muhimu tukahakikisha midomo yetu ni misafi, yaani tunaongea maneno mema siku zote. Paulo anasema “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.” (Wakolosai 4:6) Mke akijua jinsi ya kumjibu mumewe na mume akajua jinsi ya kuongea na mkewe na wote wakaungana kuongea na Mungu maisha yatakuwa mazuri sana. Hata mwenzi wako akikosea, ongea naye kwa maneno ya kujenga. Maneno yana uwezo wa kubomoa kabisa mahusiano, kumbuka Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. (Mithali 18:21). Maneno yanaweza kuua au kuhuisha ndoa yako, Mwombe Mungu akitakase kinywa chako kama ukiona kina shida.

2. Moyo uliojaa uchafu

Maandiko yanasema, “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano” (Mathayo 15:19). Moyoni mwa mtu ndimo mlimo hisia, mawazo, na maamuzi, hivyo ili maisha ya mtu yawe salama ni lazima moyo uwe salama. Kwenye mithali tunasoma, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. (Mithali 4:23. Moyo uliochafuka ni makao ya shetani, kila aina ya uharibifu utatoka ndani yake. Kama mwanadoa mmoja wapo ataacha moyo wake wazi na shetani akaujaza uchaffu wake (chuki, husuda, matukano, uzinzi, uasherati, uongo na mengine) ndoa haitaweza kusimama.

Upendo wa kweli huletwa na Roho Mtakatifu ndani ya mtu, hivyo kama moyo ni mchafu Roho Mtakatifu hawezi kukaa na upendo wa kweli hauna nafasi. Suluhisho ni kurudi msalabani na kumtwika Yesu mizigo ili kupata raha moyoni (nafsini) – Mathayo 11:28. Moyo wa mtu hujazwa kwa vile anavyovisikia, anavyovisoma na kuviona.

Je, huwa unasoma nini? Huwa unasikiliza nini? Huwa unatazama nini kwenye runinga au ‘smartphone’ au kipakatilishi chako? Moyo wako ndio uliobeba ndoa yako, na ukilemewa na uchafu hakika utaiharibu ndoa. Dhambi ilipowalemea Adamu na Eva, walianza kulaumiana mbele za Mungu. Linda moyo wako, linda ndoa yako.

Dunia hufanya kazi katika mfumo hatari ambao hauwezi kutusaidia kudumu katika mahusiano. Kimsingi, dunia huhamasisha ubinfsi, chuki, kiburi na tamaa ambavyo ni hatari sana kwa ndoa. Yohana anasema, “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. (1Yohana 2:16). Mambo haya yaani “taama ya mwili, tama, na kiburi” kazi yake ni kuvuta uharibifu na kututenga na Mungu.

Uasherati ni uchafu mbaya, unaua roho na kuharibu mwili; ni lazima kujiepusha nao kama kijana unayempenda Mungu. Mabinti wanaojua thamani ya ubinti wao na vijana wanaojitambua hujilinda kabisa na uchafu huu. Ndoa nyingi zimevurugika kwa sababu ya uasherati ambao wanandoa waliufanya kabla ya ndoa. Wengine katika uasherati wao wakapata watoto ambao wamekuwa chanzo cha vurugu na chuki katika ndoa. Uchafu wa uasherati huchochea uzinzi katika ndoa, japo si mara zote. Ila mara nyingi watu ambao hawakuwa waaminifu kabla ya ndoa hushindwa kuwa waaminifu kwenye ndoa.

Usifanye tendo la ndoa kabla ya ndoa, na baada ya ndoa baki na mume wako kama Mungu alivyoamuru; ndoa yako haitatikisika.

Ni muhimu sana wanandoa wakadumisha usafi mioyo yao, na wasijichafue kabisa kwa uzinzi au picha za ngono. Kuaminiana huletwwa na usafi. Kila mmoja akikubali na kuamua kwa moyo wa dhati kumtii Mungu na kuwa wasafi na waaminifu kwa ndoa yake, maisha ya ndoa yatakuwa ya Baraka sana. Usafi ni msingi wa muhimu sana katika ndoa.

3. Mikono (michafu) iliyojaa damu

Unaitumiaje mikono yako? Wengine wameitumia kuwapiga wenzi wao. Wengine wameitumia kubeba vitu ambavyo ni hatarishi kwa wenzi wao. Je, mikono yako ni salama? Mungu ametupa mikono ili kwamba tuweze kujipatia kipato kwayo, tena tuitumie kuwasaidia wengine sio kuwaumiza. Mume au mke ambaye mikono yake ni myepesi kuleta madhara hawezi kuishi na ndoa yake kwa usalama. Mtume Yakobo akasema, “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.” Hapa anazunggumza juu ya kuitakasa mikono na mioyo ili kuweza kuwa karibu na Mungu. Usafi huu ni wa muhimu sana.

4. Mwili na mavazi
Usafi wa mwili na mavazi una uzito sana kwenye mahusiano. Tuliyoyaona hapo juu ni mambo ya rohoni, hivyo matokeo yake huja taratibu na ni ya ndani. Swala la mwili na mavazi ni la wazi na halifichiki. Watu wengi wamevuruga mahusiano yao ya ndoa kwa sababu ya uchafu. Baadhi ya maeneo ya kutilia mkazo zaidi ni:
Nguo za ndani yani brazia, chupi, boksa, soksi, vesti n.k. hakuna kitu chenye kero kama harufu mbaya. Na kwenye ndoa ule ukaribu wa wanandoa huweza kuathirika sana kama kutakuwa na harufu mbaya inayotoka kwa mmoja wapo. Kukimbiana na kutokufurahiana huanzia hapo, mwisho michepuko hubisha hodi. Usafi wa mavazi ni kivutio kikubwa sana kwa mwenzi wako, usikubali kuwa mchafu bila sababu za msingi.

Mwili: Sehemu za siri, kinywa, kwapa nk; Haya nayo yamevuruga ndoa nyingi. Mume au mke ni mtu wa karibu sana na mara nyingi meneo haya kwake ni ya msingi, hasa kwenye eneo la tendo la ndoa. Hivyo yakiwa machafu yanamsababisha anapata haaki yake kwwa mateso badala ya furaha. Mwisho anaweza kupoteza kiu kabisa au akafanya kama wajibu tu bila kuonyeha furaha na kuridhika. Hii ni hatari kwa ndoa.

5. Mazingira ya ndani na nje

Haya nayo yana umuhimu wake, kimsingi nyumba yenye mandhari masafi ni bustani yenye kuvutia kwa wanandoa. Usafi huleta unadhifu na hamasa kwa wanandoa wenyewe na wageni. Maeneo ya msingi ya kuangalia kwenye eneo la usafi wa ndani na nje ni:

Usafi wa nyumba na mpangilio wake. Nyumba ikisafishwa na kupangiliwa vizuri huwavutia sana wanaume, wanawake nao hufurahia kuona wanakaa na waume zao nyumbani ili kujenga ndoa. Usafi na mpangilio mzuri wa nyumba ndiyo siri ya mafanikio katika hili.

Chumba na malazi; Chumba cha wanandoa ni cha muhimu sana, yaani ni mahali ambapo wanashikiana katika tendo la ndoa. Hivyo ni mahali wanapafurahia kuliko pahali pengine pote. Ni bustani ya amani na furaha kwa wandoa.

Usafi wa chumbani ni wa msingi sana. Na hili linawahusu wanandoa wote japo mke ndiye msimamizi mkuu wa jukumu hili. Mashuka yafuliwe kwa wakati, chumba kisafishwe, neti ifuliwe, vitu vipangiliwe vizuri, pawepo na kapafyumu kazuri, yaani mambo yatakuwa mazuri sana. Mke usikubali mumeo atamani kukaa chini ya miti kwa sababu chumbani hapakaliki. Jitahidi kwa uwezo ulionao ufanye usafi.

Maandalizi ya chakula na vyombo: Chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi na kutengwa kweye vyombo visafi, ni kivutio kikubwa. Hata hamu ya kula huja ghafla kwa ule usafi tu. Ndoa inaguswa na eneo hili pia, ili mume au mke ale na afurahie chakula usafi unahitajika.

Chooni na bafuni na Mazingira ya nje, nayo pia yanahitaji usafi ili kuifanya nyumba iwe ya kuvutia zaidi. Watoto hujifunza sana kwa wazazi, hivyo usafi ukitiliwa mkazo utawajengea watoto tabia njema na utajenga sifa njema kwa ndoa.

Kumbuka uchafu wa aina yoyote ile huleta dharau, hakuna mwanandoa yeyote anayependa kudharauliwa kwa sababu ya mwenzake. Mume hupenda kusifiwa kwa sababu ya mkw wake na mke vivyo hivyo. Kiujumla, usafi ni msingi wa muhimu sana kwa wanandoa. Ona mstari huu unavyosema “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.” Waebrania 13:4. Katika mafundisho ya Paulo kwa Timotheo, Paulo alikazia sana kuhusu usafi pia (1Timotheo 4:12), hivyo usafi ni lazima utiliwe mkazo kwa vijana, ili wakafanye vizuri kwenye ndoa zao pia.
AMINA
 
Baada ya mnyama dorphin mwanaume ndie mnyama wa pili asiyenda kelele. Kelele ni nini. Kelele ni mpangilio wa sauti zenye maneno yasiyo na mpangilio katika hali ya kupayuka payuka hovyo.

Mwanamke mpenda kelele hana afya nuru njema sababu, roho yake ni chafu imejazwa vitu vichafu. Ana hitaji msaada wa kiroho Ili kuisafisha roho yake kwa jiki, roho ikiwa safu. Nuru na siha njema utokeza.
 
Baada ya mnyama dorphin mwanaume ndie mnyama wa pili asiyenda kelele.
Kelele ni nini. Kelele ni mpangilio wa sauti zenye maneno yasiyo na mpangilio katika hali ya kupayuka payuka hovyo.
Mwanamke mpenda kelele hana afya nuru njema sababu, roho yake ni chafu imejazwa vitu vichafu. Ana hitaji msaada wa kiroho Ili kuisafisha roho yake kwa jiki, roho ikiwa safu. Nuru na siha njema utokeza.
kama katika makanisa yao yaleeee ya makorokocho rakataratakataaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaparakshaaaaaarukutuuuuuuu rikaraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaarruruyruuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, ni wapuuzi sana wale.
 
Mwanamke mpumbavu upiga kelele, madhara ya kelele.

1.Wanaume kuchelewa kurudi nyumbani, wengi hushinda bar kuliko nyumbani na familia kuzikimbia kelele.
2.Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, tendo ni hisia panapo makwazo msisimko haupo.
3.Kuchepuka,wengi utumia kama sehemu ya kuondolea stress ambapo ni chanzo cha kumsambaratika kwa familia, KWA sababu Hakuna mwanamke mfariji kama mwanamke kahaba/ mchepuko ndie mwanamke anaejua mwanaume anataka nini maadamu kama pesa ipo. Michepuko ndio uyatumia mafundisho ya ndoa kwa vitendo Ili kutekea wanaume za watu hali wake za watu mafundisho ya ndoa uyachia mlangoni mwa seminar ya ndoa.

4.Chanzo cha magonjwa mfano mfadhaiko, kushuka moyo, kupooza, pressure, nk sababu ya ukosefu wa utulivu nyumbani.

5.Kushuka KWA uzalishaji. Ili mwanaume awe na maendeleo inategemea na amani na utulivu wa mke nyumbani. Labda tu mwanaume awe na elimu ya kutosha kuhusu saikolojia na mambo ya emotional intelligence. Yaani uwezo binafsi wa kublock makelele yasiingie kichwani mwake kumuharibia siku. Sisi tuliokula somo la matusi kelele hazitupi shida, tupo positivity masaa 24.

Yalipo mafanikio ya mwanaume mwanamke mwenye kibali yupo nyuma yake na kinyume chake pia yaani alipo mwanaume masikini.

6.Chanzo cha kuporomoka KWA maadili ya familia.
Watoto kukosa amani na utulivu sababu ya makelele ya mama hivyo ukimbilia vijiweni kutafuta faraja.

7.Chanzo cha magonjwa ya kiroho mfano mikosi,laana,nuksi, hasira, sababu ya ukosefu wa amani.
Maana pana familia huwa na furaha mama asipokuwepo nyumbani.

8.Chanzo cha vipigo,na vifo vya wanawake wengi hapa usiombe mwanamke mpiga makelele na ana mdomo usio na chujio.

Mdomo mchafu Ndio chanzo cha vifo vyao toka kwa mwanaume mpumbavu.
Mwanaume mpumbavu umpiga mkewe.

9.Chanzo cha wanaume kuoa mke wa pili wao uona dawa ya mwanamke fedhuli ni mwanamke mwenzake.

10.Chanzo cha ndoa za mbalimbali,hapa wanaume wasiotaka shali ukaa mbali hata mkoa mwingine KWA kisingizio cha utafutaji biashara au kazi hii ufanywa na wanaume wenye busara,Ili kulinda watoto, heshima ya wakwe pia kuepuka magonjwa kama stress, pressure, kupooza,nk.

Inaitwa kukeep distance huja mara moja moja weekend au KILA baada ya mda fulani kuona watoto.
Pana dada fulani aliambia yeye na mume wake hawawezi kaa dakika pamoja ni lazima wagombane thus KILA mmoja anaishi mkoa mwingine.

11.Ni chanzo cha talaka kwa wanawake wengi sana.
Wapo wanaume awataki kabisa usumbufu, dakika sifuri mbele wao kumuacha mke ni SAwa na kunywa maji

Huwezi kuta mwanamke hata awe mpumbavu vipi anampigia kelele mwanaume fyatu, mwanaume mpigaji.Uogopa kupondwa. Wahanga wa makelele ni wanaume waungwana waliokosea kuoa

Waliposema mwanamke mpumbavu ubomoa nyumba yake mwenyewe waliona mbali.
Mwanamke mwenye hekima uijenga nyumba yake.
Waliposema mdomo sumu Wana maana yao.
Laana na baraka ya mtu ipo kwenye ulimi wake chunga Sana ulimi kama huwezi kunyamaza ni bora ukae kimya.
Ulimi ni moto wa gesi.
 
kama katika makanisa yao yaleeee ya makorokocho rakataratakataaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaparakshaaaaaarukutuuuuuuu rikaraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaarruruyruuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, ni wapuuzi sana wale.
Zile hazina madhara labda kwa wenye mapepo
 
Wakati mwingine Mwanamke kupiga kelele inasababishwa na uwezo wa mwanaume kusimama kwenye nafasi yake

Nimesema wakati mwingine😉😉😉
 
Pia kuna wanaume wapumbavu kuna somo lake. Hawa uweka dhahabu kwenye banda la nguruwe. Yaani amempata mwanamke wa kibiblia kabisa lakini mwanaume ndie mpumbavu.
 
kama katika makanisa yao yaleeee ya makorokocho rakataratakataaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaparakshaaaaaarukutuuuuuuu rikaraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaarruruyruuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, ni wapuuzi sana wale.
Aaaah hapa shetani anakuwa anapelekewa moto
 
Wakati mwingine Mwanamke kupiga kelele inasababishwa na uwezo wa mwanaume kusimama kwenye nafasi yake

Nimesema wakati mwingine😉😉😉
Unapima madhara ya kelele angalia zisimkimbize kabisa, hata hicho kidogo kikakosekana kabisa.
Mwanadamu atoishi KWA mkate tu
 
Unapima madhara ya kelele angalia zisimkimbize kabisa,hata hicho kidogo kikakosekana kabisa.
Mwanadamu atoishi KWA mkate tu

Madhara ya kelele yanatokana na aina ya kelele😀 anayepigiwa kelele kufanya maendeleo sio sawa na anayepigiwa kelele kuombwa pesa ya mkorogo na madela
 
Back
Top Bottom