kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 711
Kauli ya kukataza uhamisho kutoka vijijini/miji midogo kwenda mjini kaitoa Waziri Ummy Mwalimu na sio wasaidizi wake
Style ya kufanya kazi za serikali kwa matamko yasio ya kisheria iliasisiwa kwenye awamu iliyopita. Kila mtu alikua anatoa maagizo ili kumridhisha "Mkuu" ikiwemo ya ma DC na Ma RC kuweka watu ndani!
Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Miji pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya nao wanatoa matamko kwa watumishi kwamba hakuna kwenda likizo mpaka wakamilishe ujenzi wa madarasa ambao unakadiriwa kuchukua hadi miezi saba!!!!
Ajabu ni kwamba hawawalipi hizo likizo zenyewe ambazo zipo kisheria. Inapotokea kufuta likizo ya mtumishi kuna taratibu zake ikiwa pamoja na kuinunua
Huyu Ummy Mwalimu hivi karibuni alitoa tamko la kuwazuia wakuu wa mikoa kutoka nje ya mikoa yao bila kibali cha Rais au Makamu au Waziri Mkuu!!! Hii haikubaliki na ni uvunjaji haki za binadamu na kanunu na taratibu za utumishi wa umma
Huku ni kudhalilishana kwakweli! Unamzuia mtu kutoka nje ya mkoa amekua ni mtuhumiwa ambaye yupo chini ya uangalizi wa mahakama au polisi?!!! Kwani isingetosha kuwapa malengo ya Wizara na wakawaacha na uhuru wao kama watu huru tena viongozi wa umma!!! Hizi ni athari mbaya kabisa za mind set za watawala zilizoachwa na awamu ile.
Acheni upotoshaji enyi vijana wa Ufipa. Hebu rudia kusikiliza ile speech yake vizuri. Ummy Mwalimu hajasimamisha Uhamisho amesitisha kwa muda tena ni Uhamisho kwenye Majiji, Miji na Manispaa kwa ajili ya kufanya msawazo wa watumishi.
Kilichopo ni kwamba kwenye Maeneo hayo Watumishi wamezidi ni wengi sana na wanaohitaji kuhamia huko bado ni wengi kitu kinachopelekea upungufu kwenye halmashauri za Pembezoni.
Hata Hivyo uhamisho wa kubadilishana unaruhusiwa
na ule wa kuhamia kwenye Halmashauri za Wilaya unafanyika kama kawaida. Kitaalamu wanaita kubalance Ikama.