Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,478
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu,
Napenda kukufahamisha matatizo matatu kuhusu Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF), kama ifuatavyo:
Mosi, mikataba yote kati ya NHIF na vituo vya Afya inacho kifungu kinachovunja sheria ya mikataba, kanuni za utawala bora, na heshima ya utu wa wamiliki wa vituo. Kinasomeka hivi:
"24.2.5. The Fund also may terminate Agreement if: the Fund in its sole discretion and for any reason whatsoever decides to terminate this Agreement."
Ushauri: Mwagize Mkurugenzi Mkuu kurekebisha dosari hii. Tanzania ni Jamhuri ya Kidemokrasia, na Katiba yake inataja kanuni za utawala bora ambazo haziruhusu ulevi wa madaraka wa kiwango hiki, hata kama NHIF wanayo monopoly katika sekta ya bima ya afya.
Pili, NHIF inatumia kifungu nilichokitaja hapo juu kuwatesa wagonjwa wasio na hatia pale inapovifungia vituo vya Afya kiholela. Kuna orodha ya vituo vya afya vilivyofungiwa inasambaa mitandaoni. Nimeambatanisha.
Baadhi ya vituo vinatoa huduma za kibingwa, kiasi kwamba wagonjwa husika wasopokwenda kwenye vituo hivyo, ama watakufa au watalazimika kwenda kwenye hospitali zinazowataka kugusa mfukoni, lakini wanakwama kwa sababu ya kukosa fedha taslimu.
Ushauri: Adhabu ya kufungia vituo kiholela zikomeshwe, na zitafutwe adhabu mbadala kwa vituo vinavyokiuka utaratibu. Kufungiwa huduma ya NHIF iwe hatua ya mwisho.
Ukweli ni kwamba, siwatetei wamiliki wa vituo vya afya wakorofi. Ninachosema ni kwamba, uwepo mfumo wa udhibiti usiowaumiza watu wasio na hatia. Kwa mfano, uwepo mfumo wa kusimamia nidhamu ufuatao:
- Kwanza, onyo kwa mmiliki.
- Pili, mmiliki apigwe faini ya kifedha,
- Tatu, mmiliki apigwe faini ya kupunguziwa baadhi ya huduma zilizosajiliwa na NHIF kwa muda
- Nne, mmiliki apigwe faini ya kufungiwa kwa muda,
- Na hatimaye, tano, mmiliki apewe adhabu ya kufungiwa kabisa.
Makosa mengine katika mfumo wa kompyuta yanatokea inadvertently kwa sababu ya computer iliteracy.
Na tatu, ni kuhusu service delivery cycle: Uongozi wa NHIF unafanya kazi kwa kasi ya konokono.
Tangu kituo kinapopeleka maombi ya kuingia mkataba hadi mkataba huo upatikane inachukua muda mrefu, jambo ambalo pia ni mzigo kwa wagonjwa. Kuna shida mbili hapa.
Kwanza, NHIF wanafanya kazi ya kukagua hospitali kana kwamba wao ni "health service regulator," yaani District Medical Officer (DMO), badala ya kufanya kazi ya "health insurance service provider," ambaye anafanya maamuzi kwa kuzingatia maamuzi ya DMO.
Hata ukisoma mikataba kati ya NHIF na vituo vya afya utaona tatizo hili. Neno "ukaguzi" limerudiwa zaidi ya mara 20.
NHIF Wakiacha ukiritimba, kazi ya NHIF inaweza kufanyika "remotely" kwa kutumia "NHIF service portal" na maombi kukamilishwa ndani ya masaa 24 pekee.
Ushauri: Waziri komesha huu ukiritimba na uporaji wa madaraka ya DMO. Watanzania wanataka huduma, sio ubabe na hali ya kutotabirika inayoighubika NHIF kwa sasa.
Nawasilisha.
Ukipita "Sumbawanga Town" tuwasiliane jamani.