Nivea
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 7,459
- 4,748
inabidi ununue spishi ya maji chumviSamahani kwani nikiwa na bwawa la maji chumvi litafaa kufugia samaki?
inabidi ununue spishi ya maji chumviSamahani kwani nikiwa na bwawa la maji chumvi litafaa kufugia samaki?
kaka tayari nimekutumia Email kupitia PMToa mail address yako nikusukumie manual za jamaa wa Kenya na Uganda ambao wanafuga.
Kambale kwa mazingira ya kisasa ( yaani ukitengeneza bwawa kisasa mara nyingi hawazai, ni sawa na Kanga), wanataka mazingira asili zaidi.
Nimepata kambale ( Wild african cat fish ) kama 470 hivi, 20 july nimewapata 230 na 22july nimewapata 240 wakiwa wakubwa size ya kidole gumba,nimewaweka ktk ponds mbili tofauti, hakuna aliyekufa mpaka mchana huu. Nitawalisha vizuri kwa miezi sita nione ukuaji wake. Naanda pond ya tatu ili nifikie kambale 700 kwa kuanzia.
Nitayafanya (ponds) mabwawa haya yapate uasili kidogo hata kwa kuchelewa ili niweze kuzalisha fingerlings za mbegu pia. Hawa kambale nimewapata ktk mazingira asilia kabisa kwa kukausha vidimbwi kando ya mto Mduzi huko Shungubweni. Mpango ni kuhamisha kambale wote ktk vidimbwi vile kila baada ya msimu wa mafuriko/mvua unapopita. Kwa kufanya hivi nitaokoa gharama za kwenda Mbegani,kinguluira kuwanunua.
Naamini wengi watapata mbegu toka kwangu ya kambale asilia.
kaka tayari nimekutumia Email kupitia PM
kuhusu hao kambale pia mimi huku nimewaona wengi sana tena nimetaambua kuwa kuna aina mbili ya kambale kuna wengine aambao hawakui kabisa wenyeji wa huku wana waita shingugu.
Jamani, mimi niko Dar. Nitapata wapi ushauri wa kufuga samaki? Moro naona mbali kwangu
Wadau nina mpango wa kufuga samaki kwa ajili ya kula na biashara,nina eneo la heka moja mkoani Morogoro ambalo nafanya ujenzi,ila nimetenga robo heka kwa ajili ya zoezi la ufugaji wa samaki,me sina utaalamu kabisa na ufugaji wa samaki,kwa hiyo naomba kujua yafuatayo: je robo heka itatosha kweli kwa ufugaji wa samaki kwa ajili ya kitoweo na biashara,pili je ni aina gani ya samaki mbali ya kambare na perege, wanaweza stawi na kukua vizuri kwa hali ya hewa ya Morogoro?asanteni wadau
Mfano mtu mwenye kufanyakazi ya ufugaji ktk kiwango cha biashara na ana chakula kizuri kama pellet au punje za chakula kilichotengenez wa rasmi kwa ajili ya samaki, unaweza kumshauri aweke samaki 4 kwa mita 1 ya mraba na hivyo bwawa la 900 m2 kama hili unaweka samaki 900 x 4 = 3,600 kujumlisha tahadhari ya 5% ambao ni sawana samaki 180.
Habari za leo wana JF
naomba msaada kwa anaefuga ama kujua ufugaji wa samaki maji baridi.
Na uandaaji wa mabwawa unakuwaje?
asanteni sana
Habari za leo wana JF
naomba msaada kwa anaefuga ama kujua ufugaji wa samaki maji baridi.
Na uandaaji wa mabwawa unakuwaje?
asanteni sana
Mkuu Strawberry, samaki maarufu sana wa maji baridi wanaofugwa hapa Tanzania ni Sato (Tilapia).
Labda, kwa kuanzia, hebu angalia article hii naona itafaa kuwa mwongozo wa mwanzo katika azma yako hii.
Kweli kabisa,
Ila avumaye ni Sato lakini African cat fish wapo, na hata wild african cat fish wanafugwa.
Hawa cat fish nasikia kuwa hawazaliani kirahisi kwenye bwawa. Sasa kuna mbinu gani za kuwafanya wazaliane wakiwa kwenye bwawa ?
Pia kuna samaki wanaitwa 'kitoga', hawa pia ni jamii ya cat fish ?
Habari wanaJF
Naombeni msaada wa ushauri na maelezo ya kina juu ya ufugaji wa samaki kwa yeyote anayejua kuhusu hili.
1.Ningependa kujua kiasi/mtaji wa kuanza nao.
2.Ni aina gani ya samaki wanalipa wakifugwa.
3.Upatikanaji wa mbegu au samaki wenyewe.
4.Ujenzi wa mabwawa
Kwenye bwawa la kujenga kama haya yetu hawazaliani, lakini ktk bwawa la asili wanazaliana sana. Nimewakamata cat fish watoto toka ktk vidimbwi kando ya mto na nimeviweka pamoja ktk bwawa ili nione kama hawatazaliana. Hiki kibwawa kinazidi kupata uasili fulani kwa sababu sitaki kukitibua kabisa ili nione haya maneno kama ni kweli.
Kitoga wapo zaidi Morogoro, sina hakika kama generation ni moja, pia kuna samaki anaitwa Mjonga, huyu hupatikana Kilombero huko Moro pekee duniani. Tatizo hawa samaki ( kitoga, mjonga,mkunga na wengine wa asili ni) wagumu kufugika na kuzaliana. Majaribio yanaendelea juu ya samaki aitwae black basa ( spelling sijui), huyu anazaliana na growth rate ni kubwa, ni wa maji baridi, anafugwa sana Igowole Mufindi, alitokea Songea ni mtamu sana.