Uwenda Huyu ni Aina ya Mtu Unaemuhitaji Katika Biashara Yako

Jan 13, 2023
92
99
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 taaluma yangu ni ufugaji samaki kiwango cha elimu ni Diploma (Diploma in Aquaculture Technology)

Nina uzoefu wa miaka 4 kwenye hii industry nimefanya kazi katika miradi kadhaa katika mikoa ya Pwani, Shinyanga, Mwanza na Tabora. Kwa sasa nimejikita kama mshauli (fish farming consultant)

Nipende kutumia jukwaa hili kukutanishwa/kumtafuta mtu au watu wemwenye uhitaji wa mtaalamu ufugaji samaki iwe ni kwa ajili ya kupata muongozo wa kitaalamu juu ya ufugaji samaki kibiashara, usimamizi wa miradi, kufanyiwa survey, kuzalisha vifaranga (Sato na Kambale) na mambo yote yanayo husiana na ufugaji samaki

Au naomba nipate mtu ambaye anataka kuboresha au kutanua mradi wake kwa kuongeza mradi wa ufugaji samaki, au kama kuna mtu alikuwa akifuga samaki kimazoea nashauli unitumie mimi kufanya ufugaji wa samaki kisasa

Mbali na taaluma yangu mimi pia ni kijana mpambanaji ambayenaweza kufanya kazi yoyote nje ya taaluma yangu, mimi ni mbunifu, mwenye nidhamu, ninayejutuma, mwenye mawazo chanya na pia nafundishika kwa haraka

Uzoefu na sifa za ziada
• Uzoefu katika mauzo na masoko
• Kuandika na kuongea Kiingereza kwa ufasaha
• Niko vizuri kwenye matumizi ya computer
• Leseni ya udereva
• Kusimamia miradi midogo na miradi ya kati

Kwa yoyote ambaye anaona anaweza kunitumia katika shughuli zake ambaozo ziko ndani au zile ambazo ziko nje ya taaluma yangu karibu PM tujadili

Nina utayari wa kufanya kazi Mkoa na Wilaya yoyote ndani na hata nje ya Tanzania

Call/WhatsApp: +255758779170

Ahsante 🙏
 
Nashukuru, naendelea kupambana ndani na hata nje ya taaluma yangu nikiamini one day yes
Yaani usiamini, pambana upate, umri wako hadi moyo wangu umesisimka. You have to.
Ukitaka uamini nenda ajira portal kaangalie umri wa ajira kwenye kada mbali mbali.
 
Yaani usiamini, pambana upate, umri wako hadi moyo wangu umesisimka. You have to.
Ukitaka uamini nenda ajira portal kaangalie umri wa ajira kwenye kada mbali mbali.
Napambana sana kaka nimeshafanya kazi nyingi hadi kufikia sasa hivi naomba nielezee kwa ufupi

Baada ya kumaliza chuo ngazi ya diploma nilitaka kuendelea na bachelor ila nilikosa mkopo na familia yangu aikuwa na uwezo wa kuniendeleza

Option pekee niliyokuwanayo ni kutafuta kazi ili baadae nijiendeleze

Nilianza kujitafuta kuanzia wakati huu

Baada ya kukosa ajira rasmi nilifanya kazi kama kondakta kwenye gari ya mizigo, kazi ilikuwa tukisafirisha mbuzi tunatoa vijijini tunapeleka mpakani (Kenya)

Hii kazi ilikuwa ni hatari kwasababu zifuatazo kwanza dereva wangu alikuwa mgomvi na mlevi

Pili, kazi ilikuwa ni ya magendo tulikuwa tuanasafirisha mbuzi kwenda nchi jirani kimagendo, nikona nikiendelea kufanya kwa muda mrefu ni risk kwangu uwenda nikaishia pabaya

Ikabidi nifanye kwa malengo hela niliyokuwa napata nilikuwa nasave baada ya muda nilipata 700,000niliona hii inatosha kabisa kwa mimi kuanza biashara nikaacha kazi

Nilikuwa na uzoefu na biashara ya dagaa wa ziwa Victoria

Nikajiajili, nikaanza biashara ya dagaa nilikuwa nanunua dagaa Musoma natuma Mbeya kwa rafiki yangu anauza faida tunagawana

Nifanya kama miezi mitatu hivi, baada ya hapo nikamtumia jamaa mzigo, mzigo ukafika jamaa akauza lakini hela hakunitumia hadi leo ananipiga sound, ndio nikawa nimezurumiwa hivyo na mtaji ukaishia hapo

Nikarudi kutafuta ajira za kuajiriwa ili niweze kusurvive, mimi ndio kaka mkubwa kwenye familia nilijiona najukumu kubwa nyuma yangu

Nilipambana hadi nikapata kazi, nikaajiriwa kama patron nilifanya kazi kama patron kwenye shule moja hivi ya primary & secondary nilifanya kwa muda mfupi nikaacha kutokana na malipo kidogo na mazingira ya kukaa shule muda wote kama mwanafunzi niliona yanazidi kunidumaza

Wakati huu moral yangu ilikuwa juu nlikuwa na kiu yakujifunza na kujua vitu vingi nilitaka pia kusafiri nikutane na watu tofauti tofauti ili nipate exposure

Walivyofunga tu shule mwezi wa 12 mimi sikurudi nilisafiri kwenda Dar, nikafikia kwa Uncle nikakumbana na changamoto kibao na dharau toka kwa watoto wa Uncle ila nikafumilia na kufocus na kile kilichonileta

Baadae nikapata kazi nikaajiliwa kama mwalimu kwenye kishule flan hv cha day care, kazi ilikuwa na maslahi madogo lakini ilibidi nikubali kufanya ili tu nitoke kuwa tegemezi kwa Uncle

Naendelea
 
Naendelea

Nilianza kufundisha kama mwalimu wa day care wakati huo nikitafuta kazi ya taaluma yangu au yoyote tu yenye maslahi mazuri, bahati nzuri nilipata kupitia hii Jf

Kazi nilipata Tabora, nilisafiri nikaenda Tabora nikafanya kazi kama farm manager, hapa kiasi flani nilisettle na maisha yalikuwa mazuri

Baadae mkataba uliisha, nirudi Dar kujitafuta haikuchukua muda nikapata kazi Pwani nikaenda kufanya kazi kama assistant farm manager kwenye mradi wa ufugaji samaki

Hapa nilifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja, ikafika kipindi mradi ukasimama kutokana na upungufu wa maji na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, baadhi ya wafanyakazi nikiwemo na mimi tukapunguzwa

Kikaamua kujiajiri kufanya kazi kama consultant wa maswala yote yanayousiana na ufugaji samaki

Hii kazi haikuwa na uhakika kupata hela ni hadi pale nilipokuwa napigiwa simu na watu wanaohitaji huduma. Nilifanya jitihada kubwa za kujitangaza ili kuwafikia watu wengi

Wengi wanaonicheck wanaishia kuulizia tu juu juu nawapa ABC baada ya hapo wanahaidi kunitafuta ila miezi inapita "kimyaa"

Wachache ndio uwa wanawekeza nakunitumia mimi kuover view miradi yao

Mbali na kuwa consultant lakini pia niliingia kwenye tourism industry nikajifunza na kuwekeza huko

Kazi zangu zilivyoyumba class mate wangu aliniambia niende Moshi nikapambane kwenye issue za utalii

Wakati huu alikuwa amefungua website inayohusu tourism, baada ya kwenda tuliakaanza kuipambania kwa kufanya marketing ili tupate wageni wanaotaka kuja Tanzania kutalii mbugani au kupanda mlima Kilimajaro

Nilijifunza kufanya marketing na kufanya kazi kama tour operator pia nilisoma driving course nakukata leseni baada yakuona fursa kwenye udereva ila hadi sasa hivi sijapata gari.

Website tuliipambania sana tulipata wageni wa 3 tu kwa muda wa mwaka mzima, hiii kazi ilishindwa kabisa kuendesha maisha yetu

Hela iliyopatikana iliishia kulipa expenses kulipa maIT waliokuwa wanasaidia kwenye kufanya maintenance ya page na kulipia Blue host ili account izidi kuonekana online

Sikuwai kuacha kufanya consultation kwasababu kwa nyakati zote ndio ilikuwa ikinisaidia kusolve issues mahitaji yangu na kuwahudumia wategemezi wangu

Jamaa yangu baada ya kuona mambo ayaendi akijikita kwenye issue za transfer kubeba wageni (pick up na drop off) pale KIA - Kilimajaro International Airport.

Mimi nikaendelea kukomaa kupush website, season hadi imeisha "ngoma ngumu"

Upande wa taaluma yangu Sasa hivi kazi zimekuwa chache ndio maana natumia platform hii kutafuta kazi nyingine nje ya hii ili niweze kuishi nikiendelea kuzipigania ndoto zangu
 
Kwa nini samaki wa kufugwa huwa na ladha tofauti na wale wa ziwani (maji baridi)
Samahani naomba nikusahihishe

Asilimia kubwa ya samaki wakufugwa Sato na Kambale wanafugwa kwenye maji baridi

Kuhusu ladha kuna sababu zifuatazo

Sababu ya kwanza uwa ni maji, mfano maji ya bwawani uwa ni machache kuliko ya mtoni au ziwani hivyo uchafuka haraka nakutoa harufu inayoathiri hadi ladha ya samaki

Sababu nyingine uwa ni mtazamo hasi walionao watu wengi, baadhi ya watu wakishajua huyu ni samaki wa kufugwa huo mtazamo unaathiri saikolojia yao automatically wanaona sio watamu kama samaki wa asili

Kisayansi amna utofauti mkubwa wa ladha kati ya samaki wa kufugwa na samaki wa asili, tofauti iliyopo ni ya kimazingira
 
Kwa nini samaki wa kufugwa huwa na ladha tofauti na wale wa ziwani (maji baridi)
Samaki wa mazingira ya asili wanakuwa na kiwango kidogo cha mafuta kwasababu wild fish are constantly moving and trying to find food to eat ukilinganisha na samaki wakufugwa ambao wanakuwa na mafuta mengi kwasababu hawana movement nyingi za kutafuta chakula
 
Nashukuru sana kufahamu hili, kuwapanda mpaka kuwavuna huchukuwa muda gani? Let say Sato!
 
Naendelea

Nilianza kufundisha kama mwalimu wa day care wakati huo nikitafuta kazi ya taaluma yangu au yoyote tu yenye maslahi mazuri, bahati nzuri nilipata kupitia hii Jf

Kazi nilipata Tabora, nilisafiri nikaenda Tabora nikafanya kazi kama farm manager, hapa kiasi flani nilisettle na maisha yalikuwa mazuri

Baadae mkataba uliisha, nirudi Dar kujitafuta haikuchukua muda nikapata kazi Pwani nikaenda kufanya kazi kama assistant farm manager kwenye mradi wa ufugaji samaki

Hapa nilifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja, ikafika kipindi mradi ukasimama kutokana na upungufu wa maji na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, baadhi ya wafanyakazi nikiwemo na mimi tukapunguzwa

Kikaamua kujiajiri kufanya kazi kama consultant wa maswala yote yanayousiana na ufugaji samaki

Hii kazi haikuwa na uhakika kupata hela ni hadi pale nilipokuwa napigiwa simu na watu wanaohitaji huduma. Nilifanya jitihada kubwa za kujitangaza ili kuwafikia watu wengi

Wengi wanaonicheck wanaishia kuulizia tu juu juu nawapa ABC baada ya hapo wanahaidi kunitafuta ila miezi inapita "kimyaa"

Wachache ndio uwa wanawekeza nakunitumia mimi kuover view miradi yao

Mbali na kuwa consultant lakini pia niliingia kwenye tourism industry nikajifunza na kuwekeza huko

Kazi zangu zilivyoyumba class mate wangu aliniambia niende Moshi nikapambane kwenye issue za utalii

Wakati huu alikuwa amefungua website inayohusu tourism, baada ya kwenda tuliakaanza kuipambania kwa kufanya marketing ili tupate wageni wanaotaka kuja Tanzania kutalii mbugani au kupanda mlima Kilimajaro

Nilijifunza kufanya marketing na kufanya kazi kama tour operator pia nilisoma driving course nakukata leseni baada yakuona fursa kwenye udereva ila hadi sasa hivi sijapata gari.

Website tuliipambania sana tulipata wageni wa 3 tu kwa muda wa mwaka mzima, hiii kazi ilishindwa kabisa kuendesha maisha yetu

Hela iliyopatikana iliishia kulipa expenses kulipa maIT waliokuwa wanasaidia kwenye kufanya maintenance ya page na kulipia Blue host ili account izidi kuonekana online

Sikuwai kuacha kufanya consultation kwasababu kwa nyakati zote ndio ilikuwa ikinisaidia kusolve issues mahitaji yangu na kuwahudumia wategemezi wangu

Jamaa yangu baada ya kuona mambo ayaendi akijikita kwenye issue za transfer kubeba wageni (pick up na drop off) pale KIA - Kilimajaro International Airport.

Mimi nikaendelea kukomaa kupush website, season hadi imeisha "ngoma ngumu"

Upande wa taaluma yangu Sasa hivi kazi zimekuwa chache ndio maana natumia platform hii kutafuta kazi nyingine nje ya hii ili niweze kuishi nikiendelea kuzipigania ndoto zangu
Wewe ni mpambanaji usichoke. Alafu kingine, sikuelewa kama hii ni Kama update tu. I thought unataka kujikita tu huko. Ila la pili. On your time embu Fatilia open university ujikuze mdogo wangu. Umri wako wa thamani sana
 
Asante kwa kunitia moyo

Hii ni Kama update ya kufanya watu wawe aware juu ya huduma ninayotoa, kukutana na wadau

Pia kufungua milango kwa mtu anaeweza kunitumia kwa shughuli yoyote ambayo anaona nina fit in

Mwaka huu nimepanga kujiendeleza na lengo ni kusoma hadi masters in the near future
 
kisiwa cha mafia kina mazao bahari mengi sana yanayofamika na yasiyofahamika, wachache wanaofahamu ndio wanaokula mkate huo...hata hao huishia mikononi mwa wachina wahuni.

Kuna viumbe wa aina nyingi amabao bado jamii haijatambua umuhimu wake kibiashara (research hamna). Hata kwa mazao yanayofahamika soko limekuwa shida na ubabaifu mwingi.

Baadhi ya mazao. Jongoo bahari (sea cucumber), mwani (sea moss), kaa (crabs), kambakoche (lobster), pweza (octopus), chaza (oysters) na species nyingi za maua na mboga za chini ya bahari. Hizi ni kwa uchache, inahitajika utafiti wa soko ndani na nje ya mipaka yetu
 
Back
Top Bottom