Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Hebu nifahamishe inakuwaje samaki wankuwa hawakui?

Nimejaribu mara tatu na ninafuata maelekezo ya kitaalam lakini hakuna mafanikio
 
Hebu nifahamishe inakuwaje samaki wankuwa hawakui ?
Nimejaribu mara tatu na ninafuata maelekezo ya kitaalam lakini hakuna mafanikio
Haa itabagumba mi nakaa mbugani pale......

Ulishaji wako ukoje?unawapa chakula inform of unga au pellets?vipi maji ya bwawa unayarutubisha?na je huyo aliekuuzia mbegu performance yake shambani unaijua?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Haa itabagumba mi nakaa mbugani pale......

Ulishaji wako ukoje?unawapa chakula inform of unga au pellets?vipi maji ya bwawa unayarutubisha?na je huyo aliekuuzia mbegu performance yake shambani unaijua?
tunajitahidi kufuga kisasa maelekezo yote tunafuatia labada hilo la muuzaji lakini tumenunua vifaranga sehem tofauti

Karibu mrumoni
 
Uchimbaji wa bwana unategemea na ukubwa wa bwawa,ukitaka kazi na bwawa likae vizuri inakuhitaji uwe na excavators ila pia wapo watu wanachimba ila wanachukua mda mrefu sana. Kwa mfano nimechimba na excavator size ya 43mx15m kwa shilling 700,000 arusha.
 
mambo samahan mm nko Arusha na natamani sana kuona jinsi ufugaji wa samaki unavyofanyika naweza kuja kutembelea eneo lako kwaajl ya study tour am interested kufanya hiyo kazi nahitaji sehem ya kujifunza kwa ukarb pls if u can naomba namba zako myn is 0713276076
 
Natamani Sana kufuga kwa kisasa wenzentu nchi zilizoendelea kunakitu kinaitwa AQUAPONIC agriculture niliipenda Sana cjajua hapa kwetu kama kunawataalam hz mambo
 
Wakuu mimi Ndio nimekwisha jaribu biashara hi ya samaki nimechimba mabwawa mawili nakueka samaki elfin5 tano kwasasa wanamuda wa miezi miwili kamili TATIZO NI UPATIKANAJI WACHAKULA NINAPATA ILA BEEIPO JUU SANA YANI KILO 20 KWA TSH 50'000/= NAOMBA ANAYE JUA UPATIKANAJI WAKE KWA BEI NZURI TUWASILIANE
 
Wakuu mimi Ndio nimekwisha jaribu biashara hi ya samaki nimechimba mabwawa mawili nakueka samaki elfin5 tano kwasasa wanamuda wa miezi miwili kamili TATIZO NI UPATIKANAJI WACHAKULA NINAPATA ILA BEEIPO JUU SANA YANI KILO 20 KWA TSH 50'000/= NAOMBA ANAYE JUA UPATIKANAJI WAKE KWA BEI NZURI TUWASILIANE
Mkuu hongera sana. hapa kwenye chakula ulaji wa samki pananichanganya kidogo. kwa siku kwa hao samaki 5000 wanakula kiasi gani? hicho chakula cha 50,000 (20kg) wanakitumia kwa mda gani?

Nafikiri kuna gharama kubwa san kwenye chakula kwani mtaalamu hapa kasema wakiwa wadogo wanakula 5% ya uzito wao. maana yake kwa hao 5000 tuseme wana uzito wa 20kg watakula 5000g kwa siku sawa na 5kg. kwa mwezi watakula 150kg kwa mwezi ambayo itakuwa 450,000tsh kwa bei ya 3,000tsh kwa kilo. sasa kwa miezi mitatu ya mwanzo itakuwa zaidi ya 1.4M kumbuka uzito unazidi kuongezeka.

sasa kwa miezi ya 4-7 ambapo watakuwa wanakula 5% ya uzito sema wamefika 400g+ maana yake mmoja atakula 20g kwa siku. 5000 watakula 100kg kwa siku.. sasa kwa miezi 3 itakuwa ni 9,000kg ambazo ni 27,000,000tsh ( kwa bei ya 3,000tsh kwa kg)

sasa faida itakuwa wapi mkuu?
Naomba kuelimishwa hapa wakuu
 
Kwenye chakula tunaomba mtupe mchanganuo.. Wataalamu wanavyosema akiwa mdogo (SATO) miezi mitatu anakula 5% ya uzito wake na akikua 4months + anakula 3% ya uzito wake nikipiga hesabu kwa samaki 5000 mfano gharama ya chakula kwa kuweka bei ya 3,000 kwa kilo ni kubwa sana.

Naona inaenda milioni 25+.
Je hili mnalionaje? Waliofuga na wanaofuga tafadhali
 
naomba ushauri wa kitaaram, ningependa kujua garama za
1. kuchimba bwala la futi12 by 10
2. garama za kujenga na cement
3. wanaenda samaki wangapi???
4. garama za kuwahudumia hadi kufika kuwauza

nitashukuru sanaa kwa msaada wenu
 
Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).



Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

N:B
Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.
naomba namba yako
 
tembelea gereza la moshi karanga, wako vizuri na wana mabwawa ya aina tofauti
mambo samahan mm nko Arusha na natamani sana kuona jinsi ufugaji wa samaki unavyofanyika naweza kuja kutembelea eneo lako kwaajl ya study tour am interested kufanya hiyo kazi nahitaji sehem ya kujifunza kwa ukarb pls if u can naomba namba zako myn is 0713276076
 
Samaki wenyewe kumbe wanakua kwa miezi tisa? Bora Kufuga Kuku...
Kama Mimba ya Binadamu...

Idea Zingine unaweza kugeuka Masikini kwa muda mfupi.... Gharama zote hizo siku unavuta unaishia kulipa madeni... Deal kama hizi uwe na kipato kingine cha kuendesha Maisha
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mbona bei yako ya vifaranga iko juu sana mkuu, kuna huyu jamaa anauza kwa bei poa kabisa au inakuwaje hapo?
Ufugaji wa samaki kwenye bwawa ~ MUUNGWANA BLOG
 
Mbona bei yako ya vifaranga iko juu sana mkuu, kuna huyu jamaa anauza kwa bei poa kabisa au inakuwaje hapo?
Ufugaji wa samaki kwenye bwawa ~ MUUNGWANA BLOG
Kingolwira ni kituo cha serikali ambacho kinauza kwa bei ya ruzuku. Hata hivyo muda mrefu walikuwa katika ukarabati bila kizalisha
 
Back
Top Bottom