salmin siraj
Senior Member
- Oct 10, 2017
- 198
- 204
Habari zenu ndugu zangu wajf leo nimeamua kuanzisha hii thread inayohusu ufugaji wa ng'ombe wa kisasa /maziwa kwa minajiri ya kujaribu kusolve changamoto mbalimbali zinazowakumba wafugaji wa sector hii kupitia uzoefu wangu mashambani na shuleni (SUA) hivo karibuni tusharee mawazo tupate kujifunza njia na namna tofauti ya kuzitatua hizi changamoto kitaalamuna kiasili ili ufugaji huu uweze kua yenye tija kwetu na jamii kiujumla.
Tuanze mwanzo kabisa kujua aina ya ng'ombe wa maziwa na sifa zake mbalimbali.
Friesian
Sifa
-Hawa ni wale wenye rangi meusi na nyeupe (rangi yeyote inaweza kutawala kuliko nyingine).
-Wana maumbo makubwa kuliko aina (breed) nyingine.
-Wanasifa ya kuwa na uwezo wa kutoa maziwa mengi kuliko aina nyingine zote za ng'mbe wa kisasa.
-Kutokana na kua na umbo kubwa wanafaa pia kutumika kama ngombe wa nyama.
Changamoto
-Sio wastahimilivu wa magonjwa hasa magonjwa ya kupe na ndorobo.
-Wanamahitaji makubwa ya chakula kutokana na kua na uzito mkubwa .
-Sio wastahimilivu kwenye mazingira ya joto sababu ni rangi nyeusi inaakisi joto zaid ya rangi nyingine.
Arshire
-Hawa wanamchanganyiko wa rangi nyekundu na nyeupe .
-Wanaumbo la wastani ukilinganisha na friesian (ni wakubwa kuliko aina ya jersey na guernsey.
-Ni wastahimilivu wa mazingira magumu mfano maeneo yenye joto.
-Kinga kwa maginjwa ipo juu ukilinganisha na fresian.
-Pia Wanatoa maziwa mengi yenye wastani asimilia 4% ya fatty(mafuta).
Changamoto
-Wanamatumizi makubwa ya chakula na maji.
Guernsey
-Hawa wanataka kufanana na arshire ila wao wanaumbo madogo na rangi zao ni kama njano hivi au red yenye brown ilochanganyika na rangi nyeupe
Sifa
- Wanatoa maziwa ya wastani ukilinganisha na arshire na friesian
- Maziwa yao yana asilimia ya fatty (mafuta ) 4.3%
- Mahitaji ya chakula ni wastani
Changamoto
- Awatoa kiasi kikubwa cha maziwa kama friesian na arshire
Jersey
- Sura zao ukiziangalia ni kama dish (sura kama imebonyea) na macho ya prominent (yametoka nje)
- wanaumbo dogo zaid kuliko aina nyingine.
- Wanatoa maziwa mazuri zaidi, mazito yenye kiasi kikubwa cha mafuta(fatty 4.8%)
- wako very fertile (uwezo mkubwa wa kushika mimba na kuzaa kuliko aina nyingine .
- Wanamature haraka sana (kupevuka).
Changamoto
-Wanatoa kiasi kidogo cha maziwa kuliko aina nyingine za ng'mbe wa waziwa
Aina nyingine zitumikazo ni
1. Brown swiss
2. Mpwapwa breed
Note
Ng'ombe wetu wengi Tanzania ni crossbreed yani ni mchanganyiko wa mbegu za kisasa na kitanzania sio pure breed.