Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajiriwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

Pia unaweza jielimisha juu ya ufugaji wa mifugo mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku kwa kusoma hapa
SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
 
Mkuu kama mayai yataweza kuhifadhiwa kwenye aircondition kama ulivyoeleza hapo juu yanaweza kukaa muda gani bila kuharibika?

Exactly life span yake kama ni miezi mingapi,hilo naomba uniachie nilifanyie utafiti kidogo nitakujibu,ila kinachojulikana kuwa mayai yaliyohifadhiwa kwenye air condition yana uwezo wa kukaa muda mrefu tu,na hii huwasaidia wafugaji pale ambapo soko la mayai linapokuwa sio zuri,wanayahifadhi ili kusubiri soka.
 
nimevutika na nimependa sana ushauri wako,ukizingatia mimi ni mwanafunzi wa chuo,na nategemea sana niweze kujiajiri mwenyewe ila nilikua sijajua niende kwenye field gani maana najihisi sina kipaji na sina uwezo mkubwa ila nimevutika na mraadi huu wa ufugaji kuku,mimi naitaji kujua haya yafuatayo

(1)jinsi gani nitapata elimu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na wapi kwa garama zipi,kwa sasa hivi mi nipo chuoni zanzibar ila naitaji kujua kwakua nipo kwenye semester ya mwisho na nikimaliza narudi home dar na kuelekea kijijini kwetu tayari kwa kulitumikia taifa kupitia kujiajiri kama hivyo,

Mh mafia boy, tuwasiliane kama utahitaji hiyo elimu, nitakuPM namba zangu.
 
Kwa wastani wa kama kuku 100 wa mayai, wanahitaji mabanda mangapi na makadirio ya gharama za ununuzi pamoja na ujenzi wa mabanda yaweza kuwa shilingi ngapi bwana mtaalamu?
 
Bradha kichwa mbovu, nitakutafuta kwani nina mpango kazi wangu wa kutaka kufuga kuku machotara, hawa wa kienyeji machotara kwa ajili ya mayai na nyama. Hasa nataka pia niwe natotoresha kwani nimeona vitotoresho (incubators) vizuri kwenye mtandao na havina gharama sana.

Ila la haraka ni hili naomba maelekezo ya namna ya kutengeneza chakula cha hao high breeds wa kienyeji mwenyewe nyumbani. Mengine tutatafutana as we go along humu JF - KISIMA CHA KUKOMBOANA.
 
Ndugu Papizo kwanza nikupongeze kwa maswali yako mazuri.
Umeuliza idadi ya kuku wa kuanza nao kama ni wengi au kidogo.Kwa swali hili nadhani kwanza itategemea na mtaji wako na uzoefu katika ufugaji.Inawezekana ukawa na mtaji mkubwa ukatosha kuanza na kuku wengi lakini huna uzoefu kwenye ufugaji wa hawa kuku matokeo yake kama utafuga kuku wengi watakufa.Ninachoshauri kama huna uzoefu ni vyema ukaanza na wachache ili kupata uzoefu kusudi utakapoingia kamili kwenye hii nyanja utakuwa tayari umegain uzoefu,au kama sivyo ni muhimu ukapata mafunzo ili utakapofuga kuku wengi hutakumbana na vikwazo.Kifupi ukianza na kuku wengi inalipa zaidi na kiwango kinachopendekezwa cha kuanzia angalu kuku 500 kama wewe unahitaji.Na kama unataka zaidi ya hapo basi ufugaji huo uende kwa awamu(batch)

Kuhusu eneo kutokuwa na umeme.Sikiliza, katika ufugaji wa kuku,umeme si mahitaji ya msingi sana kwa kuku.Kuku hasa anapokuwa kifaranga anahitaji zaidi joto na mwanga hasa katika kipindi cha wiki tatu za mwanzo.Baada ya hapo vitu hivyo havihitajika tena.Kwa ajili ya joto na mwanga kwa sehemu ambayo hakuna umeme, kuna vyanzo vingine vinaweza kutumika,mfano kwa ajili ya kupata mwanga unaweza kutumia taa ya za chemli,na kwa kwa ajili ya kutoa joto,unaweza kutumia majiko ya kawaida ya mkaa.

Kuhusu gharama ya kujenga banda lenye uwezo wa kuchukua kuku 500,hapo itabidi uwaone watu wa uthamini wa majengo, mimi ninachoweza kukupa ni eneo la square mita ambalo kuu 500 wanahitaj.Kimsingi square mita moja huchukua kuku 6,kwa idada ya kuku 500 unaweza kupata eneo linalohitajika kwa kurejea post za nyuma,ila kama hutaelewa utaniuliza.

Kwa upande wa biashara ipi inalipa zaidi kati ya kuku wa mayai au nyama,kuku wote wanalipa.Kuku wa nyama wanawafaa zaidi wale wenye mitaji midogo na wanapenda kuongeza mitaji yao kwa harakaharaka.Wenye mitaji mikubwa ufugaji wa kuku wa mayai unawafaa zaidi.

Kuhusu availability yangu kusafiri mkoa wowote kwa ajili ya kutembelea kukagua miradi na kushauri nk,niko available kwa yeyote anayenihitaji.Ndiyo kazi yangu ninayaifanya siku zote kuwaanzishia watu miradi ya ufugaji ,kuwaongoza na kuwasimamia mpaka watakapoweza kusimama wenyewe.

Na mwisho umeongolea masoko,masoko yapo tena mengi,ingawa changamoto iliyopo kwa sasa ni kuwa bei ya mayai hairidhishi sana ukilinganisha na bei ya chakula,ingawa kwa bei iliyopo haileti hasara.Pia kuna kipindi baadhi ya mikoa soko la mayai huwa lina sumbua kidogo kwa kuwa soko la mayai huwa mara nyingi linakuwa kama la msimu hivi na huwa siachi kuwashauri kuwa kama ni mfugaji na unaifanya kama kazi,ni muhimu ukawa na chumba maalum ambacho unakuwa umekiwekea aircondition na kuseti nyuzi joto 13-20 kwa ajili ya kuhifadhi mayai kwa muda mrefu.

Nashukuru sana mkuu wangu mwenyezi mungu akubaliki na itabidi basi nikutafute na tuangalie namna ya kufanya maana ushauri wako umeelezea na umekuwa deep zaidi tunashukuru sana, naona kumb hata kama sehemu hamna umeme hii kazi ni possible basi ni sawa kaka.

Na mwenyewe huwa sio mkaaji sana wa sehemu moja kutokana na shughuli zangu sasa hapo haito kuwa problem kweli?
 
Kwa wastani wa kama kuku 100 wa mayai, wanahitaji mabanda mangapi na makadirio ya gharama za ununuzi pamoja na ujenzi wa mabanda yaweza kuwa shilingi ngapi bwana mtaalamu?

Swali zuri sana nadhani nitapata na mimi majibu kutoka kwenye hili swali
 
CHANJO NA KINGA DHIDI YA MAGONJWA MBALIMBALI YA KUKU WA MAYAI,NYAMA(BROILERS) AU CHOTARA(CROSSED BREED)

UMRI
KATIKA
SIKU/WIKI
AINA
YA
UGONJWA
CHANJO/KINGA
NJIA YA UTOAJI
WA
DAWA
Mara baada ya kutotolewa
Marek's
HVT
SINDANO(Kiwandani)
1
Kuondoa uchovu
Glucose
Maji
2-6
Pullorum
Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin'total au Broiler booster
Maji
7
Mndondo
Newcastle vaccine(Lasota)
Maji
14
Gumboro
Gumboro (Bursine vaccine-IBD)
Maji
16-20
Coccidiosis
Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin
Maji
21
Mdondo
Newcastle vaccine(Lasota)
Maji
23-27
Kinga dhidi ya magonjwa mengi
OTC 20%+Dawa ya vitamin yoyote
Maji
28
Ndui
Fowl pox vaccine
Sindano kwy mabawa
35-39
Mafua
Coridix,Tylosine75%+dawa yoyote ya vitamin
Maji
56-60
Kinga dhidi ya magonjwa mengi
OTC 20%+Dawa yoyote ya vitamin
Maji
WIKI YA 12
Taifodi(Fowl typhoid)
Gentamyzine sulphate
Sindano
Wiki ya 13
Minyoo
Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin
Maji
WIKI YA 15
Ukataji midomo
Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi
Maji
WIKI YA 16
Kipindupimdu (fowl cholera)
OTC 20% Injection
Sindano
WIKI YA 17
Mafua (Infectious coryza)
Tylosine Injection
Sindano
WIKI YA 18
Taifodi(Fowl typoid)
Gentamizine sulpate
Sindano

MUHIMU

· Dawa ya minyoo irudiwa kila baada ya miezi 3 toka ilipotolewa awamu ya kwanza .
· Dawa ya mdondo irudiwa kila baada ya miezi 3 toka ilipotolewa siku ya siku ya 21.

KIASI CHA CHAKULA ANACHOHITAJI KUKU KUANZIA WIKI YA 1 HADI
MWISHO WA UTAGAJI WIKI YA 80

AINA
YA
CHAKULA
CHICKS'
STARTER
GROWERS'
MASH
LAYERS'​
MASH​
UMRI/
WIKI
0-8 9-20
21-80​
CHAKULA/
KUKU
2kg 6kg 52kg
CHAKULA/
KUKU 500
1000kg 3000kg 52kg
MIFUKO@
50Kg/KUKU 500
20 60 520

MUHIMU
· Kuanzia wiki ya 18-20, kuku wanapaswa kupewa chakula cha Growers kilichochanganywa na Layers.
 
Photo-0186.jpg

Layers parentstock wakionekana katika hali ya uchangamfu na wenye afya njema.
 
Bradha kichwa mbovu, nitakutafuta kwani nina mpango kazi wangu wa kutaka kufuga kuku machotara, hawa wa kienyeji machotara kwa ajili ya mayai na nyama. Hasa nataka pia niwe natotoresha kwani nimeona vitotoresho (incubators) vizuri kwenye mtandao na havina gharama sana.

Ila la haraka ni hili naomba maelekezo ya namna ya kutengeneza chakula cha hao high breeds wa kienyeji mwenyewe nyumbani. Mengine tutatafutana as we go along humu JF - KISIMA CHA KUKOMBOANA.

Tuwasiliane tu nitakupatia.
 
Kwa wastani wa kama kuku 100 wa mayai, wanahitaji mabanda mangapi na makadirio ya gharama za ununuzi pamoja na ujenzi wa mabanda yaweza kuwa shilingi ngapi bwana mtaalamu?

Nitakujibu kukicha,kwa sasa muda umenibana kidogo mkuu.
 
Kwa wastani wa kama kuku 100 wa mayai, wanahitaji mabanda mangapi na makadirio ya gharama za ununuzi pamoja na ujenzi wa mabanda yaweza kuwa shilingi ngapi bwana mtaalamu?

Kuku 100 wanahitaji chumba kimoja tu chenye ukubwa wa mita 6 kwa mita 3.

Siwezi kukupa gharama halisi ya ujenzi wa mabanda kwani gharama inatofautiana kati ya mahali na mahali.Nitakachofanya ni kukupa mahitaji ya ujenzi wa banda la kuku lenye vyumba 2 na stoo 1 kwa ajili ya kuhifadhia dawa,chakula na mayai, kila chumba kikiwa na uweza wa kubebe kuku 100.

MAHITAJI KWA UJENZI WA NYUMBA YA KUKU

  1. Tofali za block 5000 au tofali ndogo za kawaida zilizochomwa 12000
  2. Bati 68x2mita.
  3. Kenchi 24x2"x3"x12"
  4. Boriti kwa milango na madirisha 12x12"x1"x12'
  5. Lati 12x25"
  6. Vipande vya lati kwa kuwekea makasha ya kuku 8x12'
  7. Futi 100 za waya kwa kugawa vyumba na kunga madirisha.
  8. Mifuko20 ya saruji.
  9. Kilo 5 za misumari ya bati na kilo 7 ya Misumari ya waida
  10. Mchanga Lory 2
  11. Dazan1 ya bawaba
  12. Komeo 3 na kufuli moja.

Kwa kutumia data hizi mfugaji ana weza akajua gharama za ujenzi wa nyumba ya kuku.
 
Mkuu kwa experience yangu tofali 5000 ni nyingi sana hiyo mbona ni ghorofa kabisa? nadhani tofali 1000 zinatosha kabisa kumbuka mabanda ya kuku huwa na madirisha makubwa sana na halina complications zozote
 
Hizi data nimezikopy kutoka kwenye kitabu kinachoitwa Ufugaji bora wa kuku Tanzania kilichochapwa na Peramiho printing press cha mtafiti mmoja anaitwa Joseph Goodwin.Hizi data kwa mujibu wa mwandishi ni kwa ajili ya maeneo ya baridi na hasa mkoa wa Iringa.Niliweka hizi data kusudi kuwapa mwanga wafugaji, but kwa hili la ujenzi wadau wenyewe wa mifugo mna ujuzi zaidi.

Mimi mara nyingi huwa napenda kutoa zile specification,yaani kuku wangapi na wanahitaji kiasi gani cha eneo la mita square,sifa za mabanda ya kuku na pia kutoa sketch za ramani ya mabanda ya kuku. Nitajitahidi nitake time kwenye kufanya evaluation ya gharama kwenye ujenzi wa mabanda.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom