Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Kuku 100 wanahitaji chumba kimoja tu chenye ukubwa wa mita 6 kwa mita 3.

Siwezi kukupa gharama halisi ya ujenzi wa mabanda kwani gharama inatofautiana kati ya mahali na mahali.Nitakachofanya ni kukupa mahitaji ya ujenzi wa banda la kuku lenye vyumba 2 na stoo 1 kwa ajili ya kuhifadhia dawa,chakula na mayai, kila chumba kikiwa na uweza wa kubebe kuku 100.

MAHITAJI KWA UJENZI WA NYUMBA YA KUKU
  1. Tofali za block 5000 au tofali ndogo za kawaida zilizochomwa 12000
  2. Bati 68x2mita.
  3. Kenchi 24x2"x3"x12"
  4. Boriti kwa milango na madirisha 12x12"x1"x12'
  5. Lati 12x25"
  6. Vipande vya lati kwa kuwekea makasha ya kuku 8x12'
  7. Futi 100 za waya kwa kugawa vyumba na kunga madirisha.
  8. Mifuko20 ya saruji.
  9. Kilo 5 za misumari ya bati na kilo 7 ya Misumari ya waida
  10. Mchanga Lory 2
  11. Dazan1 ya bawaba
  12. Komeo 3 na kufuli moja.
Kwa kutumia data hizi mfugaji ana weza akajua gharama za ujenzi wa nyumba ya kuku.

Mkuu Kichwa hivi ulivyo Orozesha hapa ni vya Kujenga Nyumba kabisa ya Kuishi, Kwa Banda la Kuku 100 hayo makadirio yako juu mno
 
Hizi data nimezikopy kutoka kwenye kitabu kinachoitwa Ufugaji bora wa kuku Tanzania kilichochapwa na Peramiho printing press cha mtafiti mmoja anaitwa Joseph Goodwin.Hizi data kwa mujibu wa mwandishi ni kwa ajili ya maeneo ya baridi na hasa mkoa wa Iringa.Niliweka hizi data kusudi kuwapa mwanga wafugaji,but kwa hili la ujenzi wadau wenyewe wa mifugo mna ujuzi zaidi.Mimi mara nyingi huwa napenda kutoa zile specification,yaani kuku wangapi na wanahitaji kiasi gani cha eneo la mita square,sifa za mabanda ya kuku na pia kutoa sketch za ramani ya mabanda ya kuku.Nitajitahidi nitake time kwenye kufanya evaulation ya gharama kwenye ujenzi wa mabanda.

Okay nina experience na ujenzi wa mabanda ya kuku kwa DSM hizo tofali ni nyingi sana na hayo makadirio ni makubwa sana ila ni vizuri mtu akajiandaa kwa makubwa na chenji ikabaki kuliko kujiandaa kwa madogo then akaishia njiani ujenzi wa mabanda ya kuku hauna gharama sana
 
Mkuu Kichwa hivi ulivyo Orozesha hapa ni vya Kujenga Nyumba kabisa ya Kuishi, Kwa Banda la Kuku 100 hayo makadirio yako juu mno

Ni kwa kuku 200.Kunakuwa na vyumba viwili,na stoo moja.Hizi data ni kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya kudumu ya kuku kwa maeneo ya baridi mfano Iringa.Nyumba za maeneo hayo huwa zinapanda juu sana ili kuzuia baridi.Madirisha yanakuwa madogo na yanakuwa juu pia.

Kama ambavyo nimesema,hizi data ni kwa ajili tu ya mwongozo.Nimezitoa kwa mtafiti mmoja anayeitwa bwana Joseph Goodwin.Natumai kwa maeneo ya joto mfano Dar es salaam tofari zitatumika idogo sana.Kwa kule njombe,aliyebahatika kufika kwenye kumpuni moja ya kutotoa vifaranga matembwe village company ltd,atakuwa amejionea aina ya ujenzi wa mabanda ya kuku.Wao wamejenga nyumba kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: YJS
Mkuu, vipi kuhusu hawa wanaoitwa kuchi?. Je ufugaji wake unaweza kufanyika kwa namna gani?

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
Mkuu, vipi kuhusu hawa wanaoitwa kuchi?. Je ufugaji wake unaweza kufanyika kwa namna gani?

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
Ufugaji wa Kuchi hauna tofauti na ufugaji wa kuku wengine wa kienyeji au wa kisasa kwai njia za ufugaji na management kwa ujumla ni zile zile. Kuchi kwa kwetu Tanzania ni kosaafu bora sana ukilinganisha na kuku wa kawaida wa kienyeji.Ni kuku wenye uwezo wa kukuhakikishia faida kubwa kutokana na maumbo yao kuwa makubwa.
 
kichwa mbovu Ubarikiwe kwa kushare nasi ujuzi huu. Mimi nategemea kuanza mradi wa kufuga kuku wa kisasa wa mayai mwaka huu mwezi Juni. Na nimepanga kuanza na kuku 120. natumaini nitajifunza mengi hapa, once again thax for this opportunity mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Nakushukuru mama Joe kwa kunipa likes,hii inaonyesha una appreciate kile ninachofanya kwa niaba ya wenzangu.

Kuhusu kuwa contracted inawezekana na huwa tunafanya,mara nyingi visiting inafanyika mara 1 kwa mwezi kwa ajili ya kumonitor maendeleo ya mradi, kwa case ya emmegence hapo any time haiangalii ratiba, gharama ni negotiable,kwani lengo ni kuwafanikisha watu watimize malengo yao.Mara nyingi gharama zetu zinakuwa kubwa kidogo kwa mara ya kwanza unapotuita kwa ajili ya kukuconsult,lkn baada ya hapo unakuwa kama mwanachama wetu,hivyo utainjoy huduma kwa gharama nafuu.
kwan

Big Mama Joe kwa maswali mazuri. kichwa mbovu Je, haiwezekani wafugaji walioko eneo fulani mfano dsm wakaji organize kwa makundi mfano (wale wanao anza) wakachanga fedha mkaja kwa ajili ya mafunzo muhimu ya kuanza mradi?

Unaweza kufanya need assesment hata humu humu JF! ni mtazamo wangu.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nina maswali mengi sanaaaaa. Nitaanza kuuliza kidogo kidogo, Lakini Mtaalamu wetu kwanini unajiita kichwa mbovu ?? why not Kichwa nzuri? Uko vizuri sana.
 
Last edited by a moderator:
big Mama Joe kwa maswali mazuri. kichwa mbovu. Je, haiwezekani wafugaji walioko eneo fulani mfano dsm wakaji organize kwa makundi mfano (wale wanao anza) wakachanga fedha mkaja kwa ajili ya mafunzo muhimu ya kuanza mradi?

unaweza kufanya need assesment hata humu humu JF! ni mtazamo wangu.

Mkuu inawezekana,mara nyingi wafugaji wanafanya hivyo ili kupunguza gharama,nakumbuka mara ya mwisho tuliendesha mafunzo kwa wafugaji wa kuku mabibo hostel, wafugaji walijikusanya wakaandaa sehemu ya kufanyia mafunzo kisha tukaitwa.

Hivyo naomba nitumie fursa hii kwa wafugaji wanao hitaji kupata mafunzo na mbinu bora za ufugaji wa kuku nk mnaweza kujiorganize then mkaniambia baada ya kuwa tayari.

Siyo mbaya pia mkanipa vipaumbele vyenu ambavyo mngependa mfundishwe.
 
kichwa mbovu asante kwa kutoa data muhimu kuhusiana na banda coz nimepata jibu la swali nililotaka kuuliza.

Asante pia kwa mchanganuo wa mahitaji ya chakula kwa kuku wa mayai.

Je, unaweza kutupatia mchanganuo wa utoaji wa chanjo na madawa muhimu kulingana na umri wa kuku?? Hii inaweza kusaidia wafugaji kupunguza changamoto ya vifo. Natanguliza shukrani
 
Last edited by a moderator:
Mimi nina maswali mengi sanaaaaa. Nitaanza kuuliza kidogo kidogo, Lakini Mtaalamu wetu kwanini unajiita kichwa mbovu ?? why not Kichwa nzuri? Uko vizuri sana.

Shukran mkuu neggirl,kichwa mbovu just ni jina la utani tu,hata lisikupe taabu,ni kama yalivyo majina mengine.Mifugo ndio professional yangu.Sio kuku tu ni mifugo yote inayofugwa.
 
Mkuu Kichwa hivi ulivyo Orozesha hapa ni vya Kujenga Nyumba kabisa ya Kuishi, Kwa Banda la Kuku 100 hayo makadirio yako juu mno
.
Chasha labda tumwombe Mtaalamu wetu kichwa mbovu atupostie picha ya banda la kisasa la kuku.. na kwa kuwa ameshatupa data za ukubwa wa banda kulingana na idadi ya kuku natumaini haitakuwa na shida kujenga ukimpatia fundi data hizo.
 
Last edited by a moderator:
kichwa mbovu asante kwa kutoa data muhimu kuhusiana na banda coz nimepata jibu la swali nililotaka kuuliza.

Asante pia kwa mchanganuo wa mahitaji ya chakula kwa kuku wa mayai.

Je unaweza kutupatia mchanganuo wa utoaji wa chanjo na madawa muhimu kulingana na umri wa kuku?? Hii inaweza kusaidia wafugaji kupunguza changamoto ya vifo. Natanguliza shukrani

Asante,nadhani mchanganuo wa utoaji wa chanjo na kinga nimeshatoa tayari jaribu kupitia post za nyuma kidogo mkuu.
 
Mkuu inawezekana,mara nyingi wafugaji wanafanya hivyo ili kupunguza gharama,nakumbuka mara ya mwisho tuliendesha mafunzo kwa wafugaji wa kuku mabibo hostel,wafugaji walijikusanya wakaandaa sehemu ya kufanyia mafunzo kisha tukaitwa.
Hivyo naomba nitumie fursa hii kwa wafugaji wanao hitaji kupata mafunzo na mbinu bora za ufugaji wa kuku nk mnaweza kujiorganize then mkaniambia baada ya kuwa tayari.Siyo mbaya pia mkanipa vipaumbele vyenu ambavyo mngependa mfundishwe.

Asante mkuu.. ni matumaini yangu kwa wafugaji wa kuku wanafuatilia huu uzi, na kwa nondo ulizotoa wahitaji watakuwepo. Mimi niko DSM na kwa kweli ningependa mkija DSM nisipitwe na fursa hiyo. Labda utoe wito kwa wadau wa Dsm wanaohitaji wa ku- pm then kulingana na idadi ya wahitaji tunaweza kuleta mapendekezo ya mada za kujadiliwa.

Ni mtazamo wangu. Wengine pia wanaweza kutoa mawazo ili kufanikisha hili.
 
kichwa mbovu Namna gani ya kuweza kuhakikisha kuku wanapata hewa safi nawakati huo huo wanapata joto wanalohitaji?

Na joto linapimwaje ili kuhakikisha halizidi wala kupungua?
 
@kichwa Mbovu Namna gani ya kuweza kuhakikisha kuku wanapata hewa safi nawakati huo huo wanapata joto wanalohitaji ?
Na joto linapimwaje ili kuhakikisha halizidi wala kupungua?
Asante neggirl kwa swali lako zuri,kifupi joto linahitajika zaidi kwa vifaranga wenye umri kati ya siku moja hadi wiki tatu.Baada ya wiki tatu vifaranga hawatahitaji tena joto kwa kuwa tayari wanakuwa wameshaota manyoya ambayo huwasidi kuwapa joto.
Joto hupimwa kwa kipima joto(thermometer) lakini kwa wafugaji wengi huwatutumii hiki kipimo bali tunatazama tu kwa macho.

Kama joto litakuwa limezidi kwenye banda,vifaranga watakaa mbali na chanzo cha joto.Kama kutakuwa na baridi vifaranga watajikusanya wengi sehemu pamoja.Na kama kutakuwa na upepo mkali vifaranga wataonekana kwenye makundi makundi makundi.

Ili kuku waweze kupata hewa safi kwa maeneo ya joto ni muhimu kukawa na madirisha makubwa pande zote mbili ili kuruhusu mpishano wa hewa,madiriha hayo yaanzie usawa wa tumbo ili kuweza kukinga upepo mkali.Kwa maeneo ya baridi madirisha yawe madogo na yewekwe juu sana ili kuzia baridi kuingia ndani.
 
kichwa mbovu Kuna baadhi ya wafugaji wanasema kuwa changamoto kubwa pia inayowakabili wafugaji wa kuku ni madawa feki, uchakachuaji wa vyakula(vyakula visivyo kizi viwango), vifaranga dhaifu (vilivyototolewa bila kufuata taratibu bora za kitaalamu) unalizungumziaje hili? Ushauri tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
kichwa mbovu . ... kuna baadhi ya wafugaji wanasema kuwa changamoto kubwa pia inayowakabili wafugaji wa kuku ni madawa feki, uchakachuaji wa vyakula(vyakula visivyo kizi viwango), vifaranga dhaifu (vilivyototolewa bila kufuata taratibu bora za kitaalamu) unalizungumziaje hili? ushauri tafadhali

Uko sahihi sana mheshimiwa neggirl, ndiyo maana tunashauri ni muhimu sana mfugaji akawa anatengeneza chakula mwenyewe kwani atazingatia mahitaji halisi ya formula bila kuzidisha wala kuacha ingriedient yoyote.Kwa upande wa madawa ni muhimu ukawa wasiliana na wataalam wa mifugo kusudi upate dawa bora. Na vifaranga pia ni vyema ukaagiza kutoka kwenye makampuni yanayojulikana na yenye sifa, vinginevyo utakuwa mwenye kupata hasara siku zote. Uchakachuzi ni mkubwa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom