Mkuu Signature Yako inanikata sitimu kabisa,
Ok ngoja niitaute make ndo na pata internet nilikuwa far, Ila maelezo yake ni ya kidhungu, nitayaweka baadae nikiwa na laptop,

Mkuu Chasha, na Wakuu wote; Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Mkuu Chasha bado nasubiri upate laptop ili niendelee kufaidi, maana ilikuwa tarehe 10 leo tarehe 15.

Kuhusu signature ni imani, na kila imani imekamilika na ina Mungu wake.
 
Hakika naendelea vizuri na ufugaji wa kuku hapa nataka kutotoresha vifaranga kwa mashine hakika nawaza jinsi ya kuwakuza.
Je nataka kuku wangu wakuwe haraka nifanyaje?
 
Hakika naendelea vizuri na ufugaji wa kuku hapa nataka kutotoresha vifaranga kwa mashine hakika nawaza jinsi ya kuwakuza.
Je nataka kuku wangu wakuwe haraka nifanyaje?

Jidhatiti uwape chakula bora, mazingira bora ya kuwakuzia, kinga na madawa ya uhakika na kufuata maelekezo ya kitaalamu. Tulia upitie thread mbali mbali za ufugaji kuku aina mbali mbali humu JF utapata darasa tosha.
 
Wakuu wote (Kubota et al), Mwenyezi Mungu awabariki sana kwa kutupa wajasiriamali uzi huu.
Mkuu Chasha; leo ni tarehe 17 bado naendelea kukusubiri. Ubarikiwe.
Asante Mkuu kutuamsha maana tumesinzia kidogo, tunaendelea kusikilizia feedback, wakubwa wengine mnaendeleaje huko na ufugaji?
 
Kwa hali ya kawaida unapokuwa na kuku wachache wasiozidi 20 mazingira ya majumbani kwa kiasi fulani hutosheleza mahitaji ya kuku! Kuku na vifaranga huzurula huku na kule wakiokoteza wadudu, mabaki ya chakula na majani hata matunda pia! Vifaranga hukua vizuri tu na kama kuna vifo vya vifaranga vifo hivyo husababishwa na mambo mengine na siyo lishe!

Lakini unapoamua kufuga kiujasilia mali kuwa na kundi kubwa ndiyo lengo, kuku wakiwa wengi zaidi utahitaji eneo kubwa zaidi ambako kuku husambaa mbali zaidi wakiokoteza! Kwahiyo wale wanaoishi sehemu zisizokuwa na mbanano wa makazi ya watu wanafursa kubwa sana ya kuzalisha kuku wa kienyeji kwa gharama ndogo. Kuku wakiwa wengi sana hufikia wakati wanakuwa wameshaokota mabaki yote na wadudu wote! Kundi la kuku linapokuwa kubwa kama huwezi kupata eneo kubwa zaidi unalazimika kuwapa chakula cha ziada ni lazima kuwatafutia chakula.


Mimi nilikuwa nikifugia eneo ambalo majirani zangu kulia na kushoto walikuwa umbali wa nusu ya urefu wa kiwanja cha mpira, huku mbele ya makazi yangu na nyuma ilikuwa ni mashamba. Hofu kwangu ilikuwa ni vicheche na wanyama wabaya ambao baadae niliwadhibiti kama nitakavyosimulia huko mbeleni.


Niliamua kujidhatiti kutengeneza chakula. Kipaumbele kikubwa ilikuwa kutengeneza chakula cha vifaranga, kwa sababu sikutaka wazurule! Kuwaacha kuku wenye vifaranga wazurure vifaranga wengi huliwa na maadui, matokeo yake kuku hawaongezeki. Nilinunua kinu kwa ajili ya kutwangia mashudu ya alizeti na dagaa, nilinunua unga wa mifupa, madini ya chokaa, vitamin, nilinunua mahindi na kuyapalaza. Wakati mwingine nilinunua vumbi la dagaa na pia kunamashine zilikuwa zinauza mashudu ya alizeti yaliyosagwa tayari. Nilichanganya mchanganyiko huo kwa kufuata formula ambazo zipo. Kuna aina nyingi tu za formula za kuchanganya vyakula vya kuku hata humu JF ukifuatilia wadau walishazishusha kwa wingi tu! Hiki chakula kwa ajili ya vifaranga ndiyo hiki hiki pia nilikuwa ninawawekea kuku wanaoatamia kwa kuwa hiki chakula kimekamilika kwa lishe na hao kuku waatamiao hawatoki nje kwa hiyo ilikuwa lazima walishwe chakula bora.


Naomba nitumie fursa hii kuwa muwazi na nikiri kabisa kwamba pamoja na umakini wangu wa kutengeneza na kuchanganya chakula kwa ajili ya vifaranga na pamoja na kutumia formula nilizokuwa nazipata kwenye maonyesho ya 8-8 NILICHEMSHA !!


Vifaranga walikuwa wanapukutika baada ya siku 10 au wiki 2. Sikuelewa kwa nini na nilikuwa naona kizunguzungu! Nilifanya kila nilichotakiwa, niliwapa chanjo, niliwapa madini niliwapa antibiotics lakini vifaranga walikuwa wanapukutika! Vifaranga walikuwa wanatotolewa sana na kwakweli ilifikia hatua wala nilikuwa sifurahii huo utotoaji mkubwa maana nilijua hatimae watakufa! Nihadithi ndefu sana kusimulia nilivyohangaika kujua chanzo cha tatizo hilo! Nilikutana na mtaalamu akanieleza kuwa huwezi kuchanganya ingredients za chakula cha kuku kwa mikono ukapata mchanganyiko mzuri! Aliniambia uchanganyaji ni changamoto kubwa! Aliniambia fumba macho nunua chakula cha vifaranga! Chick Marsh!

Kwa kuwa vifaranga ni chimbuko la ukuaji wa kundi la kuku, nilinunua mfuko mmoja wa chakula cha vifaranga Chick marsh kwa ajili ya kuwavusha vifaranga mwezi mmoja tu, kisha baada ya hapo niliendelea kuwalisha chakula changu cha SIDO (cha kutengeneza mwenyewe)!! Kuanzia hapo nilisahau rasmi kushuhudia vifo na kutupa vifaranga. Ndege ya mafanikio ya ufugaji wa kuku wa kienyeji hapo ilianza kupaaa! Kusema kweli kwa kuwa nilishahangaika sana wadau JF kama kuna aliyefanikiwa kutengeneza chakula cha kulisha vifaranga na anafanikiwa kuwakuza vifaranga ninampongeza sana na tusaidiane utaalamu huo maana mimi hapo nilishanyoosha mikono.


Mwezi wa kwanza wa uhai wa kuku ni mwezi wa muhimu sana. Ni huo mwezi wa kwanza hufanya wafugaji wengine kusonga mbele na wengine kukata tamaa! Kuwavusha vifaranga mwezi ule wa kwanza ni hatua kubwa sana! Kuku wakishafikia hatua ya kuota manyoya unakuwa umepita kipindi kimoja kigumu sana! Ni ushindi! Hadi sasa nilishaamua kwa ule mwezi wa kwanza huwalisha vifaranga wa kuku wa kienyeji chakula bora kisichokuwa na mashaka kwa kununua Chick Marsh.

Kwa ndugu zangu mlioko maeneo ambako chakula hiki cha kununua hakipatikani, nawashauri acheni kuku wenye vifaranga wachunge wenyewe huko wanapata balanced diet kulikoni kuwafungia! Labda kama tutapata msaada wa ujanja wa kutengeneza chakula cha vifaranga hapa JF


Masimulizi ya Chakula cha kuku YATAENDELEA…..

Dah mkuu hii ni kweli kabisa hata mie nilipata shida sana wa vifaranga kufa katika earlier stage na hili lilikuwa tatizo la kudumu nilipoanza kuwanunulia kile chakula chao tatizo liliisha sasa hivi niko juu kabisa
 
Dah mkuu hii ni kweli kabisa hata mie nilipata shida sana wa vifaranga kufa katika earlier stage na hili lilikuwa tatizo la kudumu nilipoanza kuwanunulia kile chakula chao tatizo liliisha sasa hivi niko juu kabisa

Mkuu Ureni nakushukuru sana kwa feedback yako. Watu wengi sana huelimika kwa ushuhuda kama wako na si kwa hadithi niliyosimulia, itakuwa vema sana iwapo wasomaji wetu mtaendelea kutoa maoni yenu kwa mfano alioutoa Mkuu Ureni. Karibuni sana.
 
Wakuu nafahamu ukarimu mkubwa wa wanaJF linapokuja suala la kubadilishana uzoefu na kuelimishana. Kuna ishu moja hadi sasa hakuna mrejesho uliopatikana utakaosaidia kujua ufumbuzi wa changamoto ya kujitengenezea chakula cha vifaranga. Nilishasema kujitengenezea chakula cha vifaranga cha kuwavusha mwezi wa kwanza ni changamoto ambayo imepelekea tukubali kununua chakula spesho ambacho ni ghali sana. Hadi niandikapo leo hii hajawahi kujitokeza mtu hapa JF akatuthibitishia kuwa amefaulu kumudu kujitengenezea chakula cha vifaranga (home made). Kufaulu kufanya jambo hili ni hatua kubwa (breakthrough) kwenye ufugaji huu. Kwa hiyo kwa ukimya uliopo ni dhahiri kuwa hii bado ni changamoto kubwa na kwahiyo kwa lishe ya uhakika ya vifaranga wa kienyeji kwa wanaotaka kuongeza idadi kubwa ya kuku wa kienyeji ni kununua Chick marsh madukani, hakuna jinsi!
 
Mama Timmy, Mama Joe, Asigwa, LiverpoolFC, Guta, n.k, upweke umenizidi, mko wapi wakubwa? Feedback zije wajameni!
 
Mama Timmy, Mama Joe, Asigwa, LiverpoolFC, Guta, n.k, upweke umenizidi, mko wapi wakubwa? Feedback zije wajameni!


Kubota habari ya asubuhi Mkubwa! Hakika upweke umetawala thread hii ila nina IMANI ya kwamba member tajwa wote wana afya njema kwa kudura zake MUNGU,nipo chaka nyakati hii na nikitua ndani mambo yote nitarudisha hewani hakika!
 
Last edited by a moderator:
Nilianza na chotara25 wakafa23nikanunua2kienyeji wametotoa vfaranga12 nachanganya stata na pumba wanaendele vzuri.

Mkuu asante sana kwa kutujuza. Hapa tena tunashuhudia jinsi feed back ilivyokitu chenye thamani kubwa kwenye kuelimishana. Asante mkuu kwa kushea nasi uzoefu huo, kuanguka daima ni darasa kubwa na hasara ni ada ya shule. Kusema kweli sijawahi kufuga chotara ila niliwahi kuwaona chotara wa broiler kwa jirani yangu, ukweli kuku walikuwa wanakua kwa kasi kubwa sana kuliko kuku wa kikwetu lakini ukweli unabaki pale pale kwamba kuku halisi wa kienyeji wanahimili mikiki mikiki kuliko kuku wa kisasa na chotara. Ukweli umeuona mwenyewe, hata hivyo ukiwamudu kuku wa kienyeji baadae unaweza kurudia hao chotara maana wanakua haraka na utagaji mkubwa sinauhakika kama huwa wanauwezo wa kuatamia mayai, wadau tuelimishane kwa hili.
 
Kubota; mbwa wangu wanakula kuku tatizo nini? unawapa dawa gani ya kuwafanya wakae kwenye lindo wasizulure usiku?

Mkuu umenivunja mbavu zangu natamani ungeniona. Kwamba mbwa anakula kuku na hakai kwenye lindo! Mkuu Ibra6 mbwa nao wako wa kila sampuli na tabia pia. Kunajambo moja naomba uelewe hapa, mimi niliwahi kustajaabu sana kuku wangu kutokuzurula acha mbwa! Nilikuwa naona jinsi kuku wa majirani walikuwa wakienda miji ya mbali kuzurula na wengi walikuwa wanashinda nyumbani kwangu na kuchangia kutaga kwenye viota vyangu. Kuku walikuwa hawazuruli kabisa na ndivyo walivyokuwa mbwa wangu! Kama mbwa ukimpenda, kumjali na kumpa chakula kizuri na akashiba kabisa mbwa anajua kujipendekeza kwa Master wake hakuna mfano!! Mbwa si rahisi kukuangusha eti akazurule usiku? mimi haijanitokea!

Ufugaji mwingi wa kiswahili wa kuku na mbwa ni wa kuwaacha viumbe kujitafutia wenyewe. Mbwa wana akili, wakishaona nyumbani wao ni kupigwa tu na kupewa mabaki ya chakula wasishibe vizuri nafasi yao nzuri kushiba ni usiku kuzurula kuokoteza. Ili kuhakikisha mbwa wako hazuruli mchana na usiku anza kwanza kuhakikisha wanapata balanced diet. Wasagie dona, nunua dagaa, ugali mseto na dagaa! Mimi siyo mtaalamu wa mbwa ni uzoefu tu. Nakumbuka nikiwa mdogo kwetu mbwa alikatiwa ugali au alipikiwa ugali wa pumba, chakula cha aina hii humshibisha tumbo tu lakini ki afya hakina ukamilifu hapo mbwa lazima azurule kujazia lishe. Mbwa wako akishiba hatawinda kuku wako na wala hatazurula usiku. Hiki kitu kinaitwa protein ni muhimu sana kwa mifugo, tusikazanie kuwalisha mifugo wetu vyakula vya wanga pekee!

Njia nyingine ya kuzuia mbwa asizurule usiku ni kufuga dume na jike. Ukiwa na jike unanafasi kubwa ya kupata msaada wa walinzi kutokana na wachumba watakaokuwa nanakuja kumendea jike.
Njia nyingine ambayo sina uthibitisho wa kitaalamu ila kwa hisia zangu nadhani kumfungia mbwa mchana ili asizurule yaweza kusaidia kupunguza uzurulaji wakati wa usiku. Mbwa wangu wanaminyororo, mchana huwafunga kwenye kivuli. Mbwa anapokuwa hazuruli sana anakuwa hana uenyeji sana na hana mbwa marafiki wa kuwatembelea usiku! Ni hisia zangu lakini. Kama tulivyowatu wanyama nao wako hivyo hivyo.

Pia njia nyingine nzuri ni ya kununua mbwa watoto unawakuza mwenyewe, mbwa wanapokulia kwako ukawalisha na kuwafuatilia matunzo vizuri mbwa hujua hadi unayowazia maana wamekulia kwako wanakufahamu vema kuliko unavyozania, mimi mbwa wangu nikikaribia nyumbani hunikimbilia! Sijawahi kuwavutisha bangi wala madawa yoyote lakini mbwa wangu wamevuma mtaani kwamba ni wakali hakuna mfano! Haya mambo yananifanya nashangaa sana!! Jamani unachoipa dunia hii ndiyo hicho hicho dunia itakurudishia! Kama umamtunza vema mbwa wako lakini anakutia maudhi piga bei ujue ni hajatulia huyo na mbwa wapo wa hivyo.


Naomba nimalizie hapa kwa kusema kwamba nilishashikwa na mshangao sana lakini mwishowe nilielewa ni kwa nini. Tunapokula chakula nyumbani kwangu ni mimi tu huwa nasumbuliwa sana na paka wetu, akitaka nimpe chakula na hata kupanda miguuni kwangu kwa kujiamini, wenzangu huona paka ni msumbufu humpiga au kumkamata na kumfungia sehemu, mimi huwa natambua huyu ni mnyama anaenitegemea, akililia chakula mara moja lazima nimkatie msosi wa nguvu, kwa kufanya hivi nimejenga urafiki wa ajabu na mifugo, nimeshuhudia paka akiwakimbia baadhi ya member wa nyumbani kwangu kila anapowaona, mbwa wangu pia ni hivyo hivyo, nikifungua mlango asubuhi mbwa wapo kunirukia rukia, wengine wanasema paka ukimpa msosi hakamati panya wanasahau kuwa kunawakati panya huwa wajanja kiasi kwamba paka huwa haambui kitu! Matokeo yake paka anabadilika tabia anaanza kula vifaranga!

Samahani Mkuu kwa maelezo marefu sana hii ni hulka yangu sikujaliwa kuwa na maneno mafupi nivumilieni tu.
 
Asante sana,dog nlpata mdogo akala kuku akazaa watoto nao wakala kuku,nkawachapa usku wanenda kuvnja mabanda ya majiran
 
Mkuu Kubota kufuga nimeelewa.sasa naomba utaratbu wa biashara awam na mauzo ya kuku wako.tupate na mbinu za kuuza pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom