Ufisadi Bila Majibu: Rais Kikwete na Lowassa sasa jiuzuluni ndani ya siku 90 kupisha uchunguzi huru

Gamba la CCM, vitunguu au si vitunguu, hebu Rais Kikwete na Mhe Lowassa wote wajiuzulu kwanza tukawachunguze kupitia tume huru ya taifa. Tuhuma za ufisadi dhidi ya si tu tuhuma za ki-chama bali ni makosa kwa taifa zima.
 
Maendelea ya maana kamwe hayawezi kupatikana chini ya serikali inayokumbatia UFISADI na kutembeza bakuli kila kona ya dunia bila kuonyesha kujiheshimu kimatumizi na kuwaheshimu walipakodi wake.
 
Gharama hii kubwa ya kupindukia kufanyia BIRTHDAY YA TANGANYIKA yetu huenda ikatuponza kwa nchi wahisani hivi karibu.

Nchi msikini kama yetu hata unaposherekea kitu unachokipenda vipi wala si sababu ya kukufuru kwa kiasi cha kutumbu hadi zaidi ya Tshs 50bn/- wakati mi-hospitalini hali si yenyewe, ajira hola, mikopo kwa wanafunzi vyuoni ni mbinde na mishahara ya wafanyakazi serikalini ni hadi tarehe 68 ya miezi huko mbelembele sana huko.

Benno Ndulu, kweli mambo yenyewe ndio kama hivi kweli???? Vipaumbele vyetu kama taifa vimekaeje jamani na matumizi ya kodi zetu???
 
Ushauri mwingine ni vichekesho kweli. Hivi mtu anategemea kuwa JK atamsikiliza na kujiuzulu.
Hata kama hatasikiliza lakini ujumbe umefika na yatakayotokea nchini hatakuwa na wakumlaumu isipokuwa ni yeye mwenyewe, JK tuonee huruma sisi wananchi tunataabika jamani maisha magumu!
 
BAADA YA KUJISHEHEREHESHA KWA MA-BILIONI KITAJIRI KIASI KILE BENNO NDULU NA MUSTAFA MKULLO SASA TUPENI MAREJESHO YA AFYA YA SHILLINGI NA UCHUMIWETU

Kwa kawaida kwa kipindi ambapo kuna mfumuko mkubwa wa bei katika nchi, yaani muonekano fulani ambapo kuna hela kibao mifukoni mwao BAADHI YA WANANCHI (sana sana MAFISADI) wananchi ikifukuzia idadi ndogo ya bidhaa na huduma finyu katika soko, tahadhari ya kwanza ni kuzuia kumimina fedha zaidi katika mzunguko.

Kwetu sisi ndio kwanza tunachukua hatua ya kujisheherehesha kifalme kuliko hata nchi tajiri kama Uchina - ripoti zimenakiliwa zikiweka hizo fedha za kujisherehesha kwa siku moja tu kuwa huenda ikazidi Tshs 50bn/-.

Na kama hiyo tu haitoshi kutuvuruga kabishakiuchumi na kuweka uwezo wa 'kula vinono' kuwa ni hifadhi tu ya wachache wenye nazi huku kule Mbagala tukiendelea tu kula ugali na picha ya samaki ukutani, ndipo tena tunakutana na mchumi mwingine aliyebobea nchini kwa jina la SHIBUDA akishauri ikulu kuwaongea MATAJIRI WABUNGE kodi zetu ili wao waendelee kutumbua maisha huku Walalahoi wa nchi hii tukiendelea tu kuwabeba juu zaidi kwa kodi zetu na hata kuwaimbia nyimbo za furaha ili vinono visiwapalie kinywa.

Mhe Rais nasema sipendi tena sitamani kusikia hata tone wana-Uchumi uchwara kama huyu Shibuda anaposhauri Ikulu na kupuuza maoni ya kitaalam kama za wachumi wetu pale Benki Kuu yetu na Hazina. Tahadhari ni kwamba tunapoendelea kuendesha uchumi nje ya kanunizinazojulikana kote duniani basi kuchomoka kwenye umasikini tusahau.

Ni kutokana na sababu hizo hizo ndizo zinazonifanya sasa nione sababu ya kuomba tathmini juu ya faida na hasara kufuatia hii sherehe ya kukata na shoka nchini ambapo laiti Mwalimu Nyerere angelikwepo na tukawa tumemwalika ninayo uhakika yule baba asingekbali hata chembe kuonekana sura yake hapo kwa jinsi UMASIKINI wetu kweli ulivyokua unamuuma toka rohoni.

Mara baada ya shamrashamra hizi zote mwisho wa siku Mhe Mkullo na Benno Ndulu tungependa sasa mtupe marejesho sisi kama waheshimiwa walipakodi juu ya mpango mzima hapo juu.

Ndio, tunaomba kujua kwamba, licha ya hali tete kiuchumi nchini na mfumuko mkali wa bei ya kila kitu hivi sasa, Wa-Tanzania tutakua tumetumia kiasi gani cha fedha KUJISHEREHESHA kwa siku moja hii na kwamba kuna mambo mengi kiasi gani yenye vipaumbele kitaifa ambavyo hivi sasa utekelezaji wake umedoda.

Nijuavyo mimi ni kwamba msikini anaposheherekea jambo lolote lile lenye faraja kwake kamwe hapashwi kusahau kwamba kuna KESHO na makucha yake.
 
Siku zote BUSARA ZA MTU / NCHI MASIKINI hupimwa vema kwa kuangalia matumizi yake pale anapo / inapobahatika japo ka-neema fulani hivi ya dinero zaidi ya 30 mfukoni.

Na sana sana watu wenye akili nhusubiri kukutathmini pale kunapotokea kitu sherehe na jinsi unavyoenenda nayo kwa kujibana na kipato kiduchu katikati ya bahari kubwa la mahitaji yasioweza kusubiri wala kuahirishwa.

Hadi hapa, naona shida kubwa kwa nchi yetu pindi tutakaposogelea meza ya nchi wahisani na ki-bakuli chetu kile kile kilichomkere Rais Mstaafu Benjamin Mkapa hapo nyuma kidogo.
 
Sio siri tena kwamba nchi yetu hivi sasa ni namba moja kote duniani kwa kusheheni VILEMA KIBAO VYA UFISADI kama ambavyo maaskofu wetu walivyose hapo jana.
 
NI NINI SIRI YA UTAJIRI WA KUPINDUKIA WA MA-IGP WETU WA ENZI ZA VYAMA VINGI HIZI UNAOKINZANA KABISA NA HLE YA WENZAO KATIKA CHEO HICHO HICHO LAKINI ENZI ZA CHAMA KIMOJA TANZANIA?:A S 465:

Duh, mkuu umenikumbusha mbaali sana kuhusu zile sanaa za msanii maarufu nchini enzi hizo kwa jina la Omar Mahita.

Kama kuna mtu alituchezea akili nchi hii na kutufanya tukichukie kabisa Chama Cha Wananchi CUF (licha ya kuwemo Mtambo wa enzi hizo - Prof Lipumba), mtu huyo ni yule Kada wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Alhaji Omar Mahita, ambaye hivi sasa ni tajiri wa kupindukia akiendesha biashara ya msururu wa mabasi ya BUFFALO kote nchini eti alizozinunua KWA MSHAHARA TU WA KI-POLISI hata kabla ya kustaafu na kupewa kiinua mgongo.

Ndio, ni hizi hizi janja za Kova alizokua nazo huko Rungwe, Chunya na Tunduma huko ndizo hizo ambazo hata naye Alhaji alizitumia kukiua kabisa CUF huku bara.

Basi mambo yakawa vurugu tu fujo tu mara leo aibuke na mitoroli ya mapanga yaliopakwa TOMATO SAUCE na kutuaminisha kwamba CUF ni chama cha fujo na kwamba kinachinja watu, mara kesho CUF Ngangari na yeye Ngunguri - basi ikawa ni sinema tuuuu hadi anapomaliza mchezo akiwa tajiri kuliko hata Ndg Regnald Mengi mfanyabiashara aliyeagana na usingizi mwanana siku nyingi ili apate tu kugema kile tu kilicho chake ki-halali.

Wanabodi, kumbukumbu zangu hizo zinatufikisha hadi kwenye swala mama la: INAAKUA VIPI MA-IGP WA JESHI LA POLISI ENZI HIZI ZA VYAMA VINGI HUSTAAFU WAKIWA NA MALI KUZIDI KI-PATO CHAO MARA 100 ZAIDI UKILINGANISHA NA WENZAO WALIOWAHI KUSHIKA WADHIFA KAMA HUO HUO LAKINI CHINI YA CHAMA KIMOJA??

Mzee Jenerali Ulimwengu, Saed Kubenea, na Steven Chuwa na Maggid Mjengwa mpo hadi hapo?????????????? Kwa kuweka tu sawa rekodi, IGP Mstaafu (enzi za chama kimoja) Mzee Mgaya ni mtu wa kawaida kabisa kule Msasani tena kwa kujibidisha kwa tu ili asiadhirike na maishi kaamua kuwa Mlinzi Mkuu wa kampuni tu ya Ulinzi iliokua Group Four pale Masaki kwa maana ya kuwa mjumbe wa bodi tu ili mkono uende kinywani.

Je, hawa wenzake akina Omaari Mahita na wengine wanaoendelea kushika wadhifa huo ni kwamba wamegundua mgodi gani pale Wizara yetu ya Mambo ya Ndani mpaka watajirike kuliko hta waziri mwenye dhamana?

Au bidha wanayoiuza pale ndio hizi hizi ya 'NIKINGE VEMA NA HAO AKINA HAJJI DUNI NA KAMANDA LEMA' na baadaye nitakutupia jicho kukufanya ADADI RAAJAB Ubalozini au tukamalizana kabisa Cash Cash mkononi kama huna talanta ya mambo hayo ya kidiplomasi kama Omari Mahita??????


teh teh teh! Juzi kova kafungua ghala na kuchukua risasi 240 na bunduki 5 za kiviti, kama kawaida press conference, ''tumewakata majambazi 12 sugu wa drs.

Jamani saikolojia za kitoto. Eti kuthibiti uhalifu kipindi hiki cha kusheshekea miaka 50.
:nerd:
 
Mtu masikini busara zake hubainika wazi kwa kutazama tu jinsi anavyojisherehesha pindi apatapo tu-hela.

Je sisi kama Wa-Tanzania tukitazama gharama kubwa ajabu zilizotumika majuzi kwa ajili ya furaha ya siku moja hivi tunajikuta upande gani wa mzani wa masikini na tahadhari zake stahiki kwenye matumizi ya busara?
 
Nimependa majibu yako kwa huyu ndugu yetu Mwita25.

Hata kama hatasikiliza lakini ujumbe umefika na yatakayotokea nchini hatakuwa na wakumlaumu isipokuwa ni yeye mwenyewe, JK tuonee huruma sisi wananchi tunataabika jamani maisha magumu!
:canada:
 
Baada ya shamrashamra hizi zote za taifa masikini kama yetu kujisherehesha kitajiri mpaka kuziliwa sherehe zima na majirani zetu wote wa Afrika Mashariki, sasa turudi kwenye kazi ya kujivua gamba na kuruhusu uundwaji wa katiba mpya ya wananchi wakiwa usukani huku tukisubiri kiswahili kirefu toka kwa Membe kuhusu kitu gani kilichotokea mpaka wageni wetu wote hawa wasitokee kwenye hafla muhimu kama hii.
 
Kwa hivo unakobaliana na hoja ya Mh Lowassa kwamba Gamba la Ufisadi CCM ni sawa yake magamba ya vitunguu yalivyojipanga sio?

Mkitaka ajiuzuru basi wote wataisha maana hata makatibu wakuu wote alioshauliana nao kuhusu Richmond wataondoka, basi kama ni hivyo awahi sana maana Ruhanjo bado siku chache , naye tunataka hii jiuzuru imkute ili akose mafao ya kustaafu.
 
Mwana-Bodi uko wapo mbona hatukuoni jukwaani?

Nimechukua muda mwingi sana kupitia nyuzi kadhaa ulizochangi ili nipate picha ya wewe kuwa ni mtu wa aina gani na kwa nini lugha yako ikose staha kiasi hicho hapo chini kabisa mwa posti hii.

Tayari umesomeka, karibu tena kwenye hizi serious discussions badala ya kushinda kwenye kurasa za umbea.


-----------------------



Nyege zinakusumbua wewe tafuta mwenza ukalalwe then utaacha kufikiri kwa kutumia makalio na kuota ndoto za alinacha na alinanuswe!!
 
... eti hospitali ya rufaa lakini bila vifaa lakini posho maradufu kwa waheshimiwa wabunge yaonekana yafaa tena bila hata ridhaa??????????
 
mi nazani mwenye post hii anawazo zuri sema jinsi gani ya kulieleza imekuwa shida kidogo,sote tunamachungu hayohayo mkuu sema hii sio njia sahihi ya kulinusuru taifa kwa hao kujiuzuru afu tuwe tunawahudumia tena kama viongozi wastaafu,hahahahahahaha HAPANA kwa herufi kubwa,hapa ni kwenda barabarani kama tunisia ili jamaa wakimbie wenyewe,
 
KATIKA HILI LA KUKEJELI SERA NA MSIMAMO WA CHAMA KUZUIA WANANCHI KUTOKUONGEZEWA MIZIGO ZAIDI YA POSHO KWA WABUNGE, CHADEMA KAMPUMZISHENI SHIBUDA KWA 'MASLAHI YA UMMA' NA HICHO KITI CHA UBUNGE TUTAKIPATA VILE VILE

Nakubaliana na mtoa hoja hapo juu. CHADEMA tukampumzishe Shibuda harakakwa maslahi ya umma kwa kumuondolea udhamini wa chama kuwa mbunge kwa kuwa anapingana na sera halali za chama na wajibu wake kama mbunge kutetea chema kwa wapigakura bungeni badala ya kukimbilia maslahi binafsi hivi.

Ndio, katika hili ni wakati mwafaka na ni vema tena inakipasha CHADEMA kuitikia kilio cha wananchi, kuchukizwa kwetu na matumizi mabaya ya rasilmali zetu chache kama vile kodi kwa ajili ya watu wachache kuendelea kujineemesha nazo kadiri wapendavyo, kwa kufanya maamuzi magumu na ya kijasiri ili kuendelea kutetea MASLAHI YA UMMA kwa vitendo, HESHMA, HAKI NA UTU WA MTANZANIA bila kuyumbayumba. Shibuda kamwe hafananii na CHADEMA na kama kuna kazi alitumwa humu sawa na huyu Mzee Wasira wa le kwa NCCR-Mageuzi ya miaka ile hapa nchini basi kafeli vibaya sana.

Ni sawa kabisa, Shibuda atoke, Shibuda aende na huo umashuhuri wake wa mambo ya KIUCHUMI kushauri ikulu kulipa wabunge wa CCM posho kwa kupitisha Muswada wa Makinda katika kipindi kigumu kama hiki nchini ambapo mfumuko wa bei haushikiki; nasema Shibuda rudi ulikotoka ukapewe ubunge wa kuteuliwa huko au kazi ya balozi huko Dominican Republic ulikotembelea majuzi. Nenda Shibuda nenda!!!

Aheri kuwa na wabunge wawili watatu hivi tu kama CHADEMA au NCCR-Mageuzi wanaoonekana kuumwa na umasikini wetu tena wanaosikika hadharani wakitetea maslahi yetu ndani na nje ya bunge kuliko kuwa na idadi kubwa ajabu ya wabunge kama CCM lakini wanaojikita zaidi katika kutetea ama MASLAHI YA CHAMA au MASLAHI BINAFSI kujilimbikizia utajiri wa kupindukia katika bahari kuu la wananchi masikini kama sisi.

Mbunge yeyote anayeonekana kupenda sana gonjwa hili la UFISADI dhidi ya Umma na wakati mwingine hata kujichukulia hatua kujitosa mle na kuonekana hata kulitetea kwa nguvu zake zote sawa na Shibuda badala ya kutetea maslahi ya Waheshimiwa Wapigakura wa Maswa, mbunge kama huyo hatufai hata kwa dawa!!

Kwa matamshi yake kuwa wanaopinga Posho ni madomokaya na hiyo ikiwa ndiyo sera ya CDM, Sasa CDM wanaweza kumfukuza shibuda.

Yupo nje ya bunge anapinga sera za chama chake, wanaweza kumwajibisha kama chama kwa utovu wa nidhamu kama kanuni za chama zina kipengele hicho. Hapa kinga ya bunge ilivyoainishwa kwenye katiba kifungu cha 100 hakimlindi hata kidogo.

Yupo nje ya bunge na anakashifu sera za chama chake. kama kuna provision ya hivyo katika katiba/ kanuni za nidhamu za cdm. This is an opportunity to flush him out of cdm
 
Nasema hongo ya POSHO kwa wabunge na nishani spika kama malipo yao kwa kazi ya kupitisha sheria ya PROJECT-MEMBE kamwe haikubaliki mchana hata usiku; Shibuda toka, nasema nenda kwani wewe si fanania yake CHADEMA!!
 
Inakua vipi Bunge kutuzwa nishani na posho kwa kudhulumu haki za wananchi kinyume na katiba inavyotamka?
 
...AND WHY ARE WE PEOPLE ALL THIS BUSY CRUSIFYING MWL NYERERE'S GOLDEN PAST LIKE 'NO-MAN'S LAND' JUST LIKE THAT SURELY?

... soon after I had just read the last line of thi most darling piece of writing on JF wall, I just found myself with an unpreventable all-time question so dear to my heart in ages that goes;

HON PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE, WHY ARE YOU AND YOU COHOURT OR THE CHOSEN-FEW SO BUSY LIKE THIS IN CRUCIFYING THE LATE MWALIMU NYERERE'S GOLDEN PAST AND PEOPLES JUST LIKE A NO-MAN'S-LAND LIKE THAT? SHALL OUR HISTORY BE ANY KINDER TO YOUR CROP AND STYLE OF LEADERSHIP SOME YEARS TO COME? Dr Bnna, WHYYYY?????????????

... na kweli inasikitisha sana; kila kitu na kila mahali wimbo murua ni UFISADI dhidi ya umma wa Tanzania - kisiwa cha amani ambacho hakikuwahi kujua machungu ya kudhulumiwa na serikali yake yenyewe mchana kweupe kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni ya kitapeli kimataifa.

Hebu vijana kote nchini tuendelee kuzidi kuendelea kusema hapana kwa dhuluma zaidi!!!!!!!!!!!

Look how Tanzania played catch-up after Mwalimu

By Firoze Manji
THE EAST AFRICAN

Posted Saturday, December 10 2011 at 15:39


How to celebrate half a century of Independence of a country whose name remains inextricably linked with that of Julius Kambarage Nyerere, the first president of Tanzania? Known to us all as Mwalimu, his death in 1999 left a cavern in our consciousness, if not in our conscience. The 50th anniversary of Independence is both a cause for celebration as well as a time for reflection on the reversals of so many of Mwalimu's achievements that set Tanzania apart from so many of the post-Independence countries of Africa.

Mwalimu's influence went well beyond the territory that he led to Independence. Perhaps the tragedy of all great people is that they are truly recognised for their achievements only after their passing. As Tanzanian people today reel under the impact of the concessions subsequent governments have made to the international finance institutions, as they suffer the assault of neo-liberal policies, as the commons that Nyerere fought so hard to retain as a public right is privatised, it is really only now that many have begun to realise the extraordinary achievements of the Nyerere years.

Whatever criticism many of us may have had - and continue to have - about some of his policies during his lifetime, there is no getting away from the transformations that he brought about.

One has only to look at the scale of theft and pillaging, the failure of the national project, the politicisation of ethnic identity, the open collusion with transnational corporations in the plunder of resources, that characterise neighbouring countries to understand what efforts Mwalimu had made to prevent the same happening in Tanzania. One only has to look at the speed with which Tanzania has played catch-up once Mwalimu ended his term as president in 1985, to be reminded how different things were.

"Kambarage Nyerere," sang Neema Ndunguru in Africa's Liberation: Nyerere's Legacy:
"How we wish you were here.
…
But dear Mwalimu, why didn't you tell us, expose and prepare us
For the turmoil and struggles that have now engulfed us?"


Nyerere was not simply a player on the national terrain. He was a pan-Africanist and an internationalist - not only in thought and writing, but crucially in his praxis. The support and refuge that Tanzania provided to the liberation movements was unprecedented.

His
commitment to welcoming and integrating refugees into Tanazanian life was extraordinary. And his willingness to speak out loud against injustices across the world, including Palestine, marks him out from the many so-called leaders who have come to be known more for their betrayal than any commitment to political principles.


And consider the extraordinary act of solidarity in seeking to break the isolation of Zambia through the building of the TanZam railway - an extraordinary logistical enterprise that was a demonstration of South-South co-operation involving Zambia, Tanzania and China. There can be few comparable ventures in the history of the continent.

We should not be shy in celebrating Tanzania's achievements. But at the same time, Mwalimu would have been the first to condemn any attempts to romanticise his period in office.

It is a time both to celebrate Tanzania but also reflect on the tragedy of the reversal of so many gains in the early years of Independence. In 1970, for example, a massive national effort was undertaken to eradicate rampant illiteracy - such that, according to Salma Maoulidi, by 1986 (i.e., around the time Tanzania began adopting development prescriptions set by Bretton Woods Institutions) illiteracy for the population aged 13 years and above was systematically reduced to 10 per cent.

By 1997 illiteracy for the population aged 13 years and above rose to 16 per cent. The 2002 census data revealed that for adults aged 15 years and above the literacy rate is 70 per cent (78 per cent for men and 62 per cent for women). Currently about 28.6 per cent of Tanzanians cannot read and write in any language. Illiteracy is higher among women (36 per cent compared with 20.4 per cent for men).

But as unemployment grows, and more land is grabbed by international corporations, as more and more people become impoverished, and as a minority accumulate wealth at unprecedented levels, a young generation of the disenfranchised seeks desperately to find alternatives to the policies that make Tanzania just another impoverished African country. They would do well to reflect on the legacy of Nyerere and to retrieve the values of self-determination and self-sufficiency that so marked the glory years of the republic.

Firoze Manji is editor-in-chief of Pambazuka News and publisher of Pambazuka Press


 
KWANI KUNA AJABU GANI YAKOBO (ROSTAM AZIZI aka 'Mpiganaji wa Ukweli') AKIPEWA TUZO YA HESHIMA NA ISAKA HUKU ESAU (KAMANDA DR MWAKYEMBE) MWENYE KUSTAHILI AKIENDELEA KUUGUZA TARATIBU VIDONDA VYA NDANI KWA NDANI VYA SUMU??

Mzee Malecela wala usisononeke kwani MASHUJAA wa taifa hili ambao hawakuitwa ikulu hawana idadi.

Ndio, huyu baba ni kati ya Wa-Tanzania wachache waliotukonga nyoyo na tayari Umma wa Tanzani tumewaona na tunawaheshimu kupita maelezo hata wengine wasipowatambuahuko. Hawa ni pamoja na:

1. Wazee Sinde Warioba - HAKI KWA WALALAHOI,
2. Salim Ahmed Salim - DIPLOMASIA ILIOTUKUKA,
3. Getrude Mongela - MWANAMAMA ALIYETANGAZA TANZANIA MI-JUKWAA YOTE KIMATAIFA

4. Mzee Butiku / Shivji - KWA KUENDELEA KUKOKA MOTO WA MWALIMU NYERERE KATIKATI YETU
5. Prof Kironde - Mwelimishaji wa taifa asiyechoka hata uzeeni
6. Mengi / Bakhresa - Ajira za kumwaga kwa Wa-Tanzania kupitia ugumu ajabu huku mkipigwa vita na Masilingi.

7. Yule Konda wa Mbagala - Aliyeonyesha uaminifu wa ajabu kurudisha mamilioni ya fedha kwa abiria wake licha umasikini wake.
8. Kijana wa Kikosi cha Moto - Alivyojitolea maisha yake kuokoa Dar es Salaamna hatari kubwa ya janga la moto Ubungo.
9. Prof Baregu / Marandu - Kwa kulea wazo na mienendo ya 'Vyama vya USHINDANI' mpaka somo likaeleweka Tanzania.

10. Jenerali Kihwelu - Kwa kutuokoa na ujangili wa miaka nenda rudi Msitu wa Biharamulo.

11. Kamanda Maghufuli - Kwa kututoa Matongotongo kwa kutujengea barabara sehemu nyingi sana nchini na kuvipa heshima wizara za pembezoni na miradi ya mabilioni ya hela kupitia mikononi mwake LAKINI BILA KULAUMIWA UFISADI (Ulistahili kuzaliwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe wewe)

12. Samuel Sitta - Kwa kutuletea aina ya Bunge lenye hadhi, heshma, utunzi wa sheria nyingi zaidi, na ulinzi wa mali ya umma kwa namna ambavyo itatuchukua miaka mingi kuliona tena maishani.

13. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya - Kwa kutumia busara hadimu kuokoa maisha ya Wa-Tanzania wenzetu wamachinga wasiuawe kama mauaji ya kusikitisha Igunga na Arusha huku akiwaacha waandamane kwa amani kumaliza hasira yao dhidi ya dhuluma kote nchini.

14. Mzee Edwin Mtei - Kwa kuzingatia kanuni za taaluma yake kumpa Mwalimu Nyerere njia mbadala ya kuendesha uchumi na kulinda hadhi ya shilingi yetu hadi kila sarufi kikawa kina thamani na kutumika; Nidhamu ya usimamiaji wa shilingi yetu.

15. Charles Keenja - Kwa kubadili mfumo wa uendeshaji wa Jiji la Dar es Salaam kwa mafanikio toka kwa akina Mzee Kitwana Kondo.
16. Wachezaji wa Taifa Stars walioitumikia timu miaka nenda rudi kwa mafanikio kama vile Mwameja, Steven Nemesi, Athumani China, Madaraka Selemani Mzee waKiminyio, Mtendawema, Sanifu Lazaro Tingisha, Machinga, na waanariadha wale waliotukuka.

17. Jaji Mwalusanya na Kisanga - kwa kuacha rekodi nyuma isiotikisika kwa kutokufanya uzembe katika kupitia sheria na hukumu nyingi mno huko duniani ndipo wapate kutoa hukumu usio na maswali hata baada ya miaka mingi na haki kuonekana kutendeka.

18. Mr II, Bananna Zoro, 20 per cent, Mrisho Mjomba, Prof J - kwa kuvumbua njia mpya ya kutuelimisha dhidi ya ukimwi na umasikini.

19. Ole Njolay / Arnold Kileo - Kwa utumishi uliotukuka
20. Dr Slaa - Kwalikwepesha taifa na machafuko hata baada ya kuchakachuliwa.

21. Jenerali Ulimwengu / Saed Kubenea / Rioba/ Mzee Simbeye kwakuchora upya ramani ya taaluma yao nchini

... listi bado ni ndefu mno.
 
Back
Top Bottom