Ufisadi Bila Majibu: Rais Kikwete na Lowassa sasa jiuzuluni ndani ya siku 90 kupisha uchunguzi huru

... Makinda naye bana, eti sitogombea 2015 wakati anajua fika KURA ZA CHUKI zinavyokisubiri hiki chama cha MAFISADI wasiovulika gamba ifikapo mwaka huo.
 
KAMA VIONGOZI WETO WOTE WAMEAMUA KWA DHATI KUSALITI 'HAKI YA KUISHI NA USALAMA WA MALI ZETU' KIASI HIKI SASA SERIKALI YENYEWE INAKUA NA MAANA KWA VIONGOZI WENYEWE AU SISI WANANCHI WALIPA KODI???????

Kijana umeongea kwa uchungu wa hali ya juu sana na yote ulioyataja humu ni ROBO TU ya jinsi gani tunavyowaona zaidi ya asilimia 98 % ya mbegu ya viongozi tulionao hivi sasa katika nchi yetu.

Mpaka hapa hakika mjue ya kwamba pindi mnapoendelea hata kwa robo hatua kwa kutuambia eti mchote tena kodi zetu ziwe posho zaidi kwenu, eti maisha Tanzania hii sasa ni magumu tu kwa hawa viongozi wanaofilisi taifa letu ...,

... nasema tunapoendelea kusikia eti hata MAFISADI waliokubuhu nao bado wanaendelea kuonekana wakirandaranda mitaani kutaka wakatuongoze tena badala ya kujivua gamba ...,

... kwa uhakika pindi vijana wa taifa hili tunapoendelea kushuhudia eti wengine wakiagiza polisi watuue raia na kutubandika nembo za WAHUNI pindi tunapoandamana kudai HAKI YA KI-KATIBA NA JUKUMU NAMBA MOJA YA serikali kutulinda na mali zetu ...

Mpaka hapo wenzetu ni kama vile akili zinataka kuturuka vile, ni kama vile wengine tunatamani kwenda kuondoa kabisa uozo wa aina hii kwa mikono yetu bila kuendelea kuhesabu vifo zaidi nchini; mkoa baada ya mkoa. Rai Kikwete kwa uhakika, kachukuwe hatua za dharura KUKOMESHA hii hulka mpya ya DOLA kuwaua raia kinyama kiasi hiki.

Mpaka hapa ni kwamba tungependa ieleweke kwamba HATUTOPENDEZEWA kuona vifo zaidi ya raia hata mmoja wakati kodi zetu polisi na jeshi letu wakiendelea kulipwa kila mwezi.

Nasema kwamba wala haitusaidii kitu kuendelea kuwa na viongozi sanamu sawa na picha tu ukutani kwa jina la Vuai Nahodha, Saed Mwema, Mkuu wa Mkoa, Wilaya na RPC huko Ruvuma wakati raia tukiendelea kuchinjwa na waajiriwa wetu wenyewe kwa mtaji wa kodi zetu!!

a.
Wanaharakati mko wapi au mnasubiri tu kuja kuandika mi-ripoti ndefu mara baada ya familia kadhaa nchini kupoteza zaidi y nusu ya ukoo wao?

b.
UDASA huu ukimya wenu tafsiri yake ni kujiunga na mdhulumishi au tuwaelewe vipi?

c.
Tangnyika Law Society ndio tuseme mpaka O'Campo awe ametoa neno ndio mtiririko wote huu wa mauaji katika mkoa mmoja baada ya nyingine ipate kuwagusa?

d.
Akina Mama kwenye taasisi zenu zote kama vile UWT inamaana uchungu wa mtoto wa mke mwenzio wala haukuhusu kitu isipokua ni jukumu la Mama Nkya na Kijo Bisimba peke yao sio?

e.
Enyi wanafunzi wa vyo vikuu nchini mliopata kua VIWAKILISHI VYA SAUTI YA HAKI KATIKA JAMII, mnaona ni vema hadi afe mtu wa ngapi tangu Mauaji ya raia Mwembechai, Pemba, Arusha, Igunga, Musoma, Uyole-Mbeya, na sasa Songea, ndio mpate hata kuguna tu juu ya mwenendo wote huu wa mambo?

f.
Kamisheni na taasisi zote za haki za binadamu nchini, inamaana hata kukemea tu muaji haya yote ni mpaka kupatikane mfadhili kutoka nje ya nchi ndio akawape fedha ndio mpate kutekeleza majukumu yenu?

g.
Vyombo vya maamuzi ya Juu nchini kama vile NEC-CHADEMA, NEC-CCM, Baraza la Mawaziri na Taasisi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi kweli vikao vya dharura mtaweza kuviitisha tu pindi mambo ya kisiasa yanapowaendeeni vibaya kwa njia moja au nyingine na wala si kule KUTOLEWA ROHO Mtanzania mwenzetu??

h. Hivi kweli Tanzania tumefika mahala ambapo uhai wa raia ni sawa tu na uhai wa inzi na wala halichukuliwi kwa uzito wake kama ambavyo tumewahi kusikia enzi hizo Mzee Mwinyi alipokua Waziri wa Mambo ya Ndani?

i.
Wazee wetu tunaowaheshimu saaana katika taifa hili; Joseph Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Benjamin Mkapa, Edwin Mtei, Bob Makani, Mufti Mkuu Sheikh Simba, Mwashamu Askofu Polycarp Pengo, Jenerali Ulimwengu, Rejnald Mengi, Mzee Bahresa ...

... je ukimya wenu wote huu wakati Dola ikiendelea kuua mkoa hadi mkoa ndio tuseme ni usaliti au usahihi wa msimamo wenu kutetea jukumu mama kikatiba kulinda uhai wa kila Mtanzania na mali zake au mpaka vurugu zije zitukumbe ndio mje kuanza kukatisha kushoto kulia.

Kamati ya kutumu ya Bunge kuhusu ulinzi na usalama, tunaomba maelezo kuhusu mauaji yote haya huku Rais Kikwete yeye akiendelea tu na safari zake za huko na kule kama vile hakuna cha ajabu kinachotokea ndani ya nchi yetu.

Kwa kweli kwa jinsi mambo yanavyoeneda hivi sasa na kwa usahihi ambao huyu Ndugu KweleaKwelea wa JF ameweza kubainisha kero za ndani kabisa wa kila kijana ndani ya nchi hii, napenda kusema kwamba NAUNGA MKONO karipio kali kwenye hotuba ya Mhe Dr Slaa, alioitoa hapo jana jijini Dar es Salaam, neno kwa neno na nukta kwa nukta bila ajizi!!


Well, simlaumu sana mama yetu lakini anawakilisha mawazo ya kizazi kilichopita chenye uvivu wa kujituma na kumtumikia kafiri bora mkono uende kinywani....

Ni kizazi ambacho hakina matumizi makubwa ya kichwa.... hakiwezi hata kuset priorities za taifa..... ni kizazi cha hunters and gatherers...... hakijafikia hata stage kuitwa horticultural societies.........

1. Kizazi hiki huona bora kiue kiwanda cha kiatu ili kinunue viatu vya ulaya.....
2. kizazi hiki huona bora kiue ginerry na vyama vya ushirika ili products zikawe processed ulaya.....

3. Kizazi hiki hudhani kuwa kutembelea 4 wd za gharama kutainua uchumi kuliko kujenga barabara bora....
4. Kizazi hiki hupenda kwenda kupumzika ulaya na si kuendeleza mambo mazuri ili kipimzikie nyumbani....

5. Kizazi hiki hupenda sana dili za muda mfupi mfupi hata kama zina gharama kwa taifa...
6. Kizazi hiki hakioni umuhimu wa huduma ya reli kuwa bora na umuhimu wa huduma hii kuwa chini ya state.....

7. Kizazi hiki ni hopeless.... ni hopeless kuliko kile cha chifu mwangunga kwani kimeenda shule lakini mambo yao kama kinavuta bangi mbichi......

NOTE: it is high time tulijipanga kwenye forum zetu kuwa tupigane mshahara wa mbunge uwe as high as the university professor....ili ONLY COMMITED PEOPLE TO GET IN PALE MJENGONI.........

Kwa heshima na taadhima NINAWAOMBA WABUNGE WOTE WAZEE WAFUNGASHE NA WAIGE MFANO WA MAMA MAKINDA (ambaye kwa kauli hii nimemuheshimu sana)....

Pia nawaomba wale wabunge vijana wanaofikiri kwa kutumia masaburi pia waunge bogi.....
lets leave the brilliant DOT COMs produce the new cadre to save our sunking Tanzania....
such that hakutakuwa na KULOGANA tena kwa ajili ya hii position......

kiasi kwamba B**** letu limekuwa kambi la wachawi.....

mAMA YETU KASOMA ALAMA ZA NYAKATI...she is brilliant!

Mungu mbariki Makinda...

Mungu ibariki Tanzania...

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake ...
 
Ni ajabu na kweli; yaani vifo vya raia Songea lakini Rais Kikwete yeye anaendelea kujisherehesha na Makirikiri Botswana.

Safari ya nyuma kidogo ilikua ni vifo hospitali zote nchini kufuatia mgomo wa Madaktari (ambao kuna kila dalili kujirudia tena kwa kuwa siku 30 za ahadi ya serikali kwao ndio hizo zinayoyoma bila mabadiliko yoyote), huku yeye akiwa anakula good time mawinguni kuelekea Davoa Uswisi.

Ndio sasa mtu amkumbushe kutuma salamu za rambirambi hivi sasa wakati wale wanaouuwa ni sawa tu na inzi tena waliobandikwa jina WAHUNI na kiongozi mwandamizi mojawapo huko serikalini??????

kwakua mheshimiwa umekua unatufariji mara kwa mara hasa kwenye misiba iwe ya raia ua viongozi bila kuja kujali itikadi za vyama vyetu.tunakuomba uwakumbuke na wananchi wa songea hasa ukizingatia kuwa jeshi letu la polis limekiri udhaifu kwa kutumia nguvu nyingi bila sababu za msingi kwa kuuwa raia wasiokua na hatia
 
SERIKALI INACHUNGUZA KITU GANI ZAIDI KWA AFYA YA DK MWAKYEMBE NJE YA RIPOTI YA MATOKEO YA KITAALAM ILIOTOLEWA NA JOPO LA MADAKTARI BINGWA WANASANSI WA HOSPITALI MAARUFU DUNIANI LA APOLLO NCHINI INDIA???????

I.
SERIKALI ICHUNGUZE SWALA LA 'NANI AU AKINA NANI WANAAHUSIKA NA SUMU KWA MWAKYEMBE' NA WALA SI KUCHUNGUZA 'KAMA ALILISHWA SUMU AU LA'

Serikali iache mara moja kupoteza kodi za wananchi eti kuchunguza KAMA DR MWAKYEMBE ALIPEWA SUMU AU LA, kwa kuwa yeyote anayeendelea kujikita katika mstari huu ajue kwamba kwanza anatupotezea muda, napoteza rasilmali za taifa kwa malengo butu yasiokua na tija si kwa Umma wa Tanzania wala kwa Dk Mwakyembe mwenyewe kwa kuwa majibu ya hilo swali tayari tunayo kitaalam zaidi toka Apollo Hospital wa kule nchini India.

Kwa mantiki hiyo, hoja yangu hapa ni kwamba uchunguzi wa serikali ni sharti sasa ulenge kutafuta majibu ya maswali zaidi juu ya sakata hili la 'Gogoro la Afya la KUCHONGA' ambayo mpaka sasa hayapata kujibiwa. Kwa msingi huu, hivo ijulikane wazi kwa serikaali hii ya Kikwete kwambaa sisi wananchi ambao ndio wenye dhamana wanayotumikia wote hapo serikalini tunapenda kusikia kwamba kodi zetu zinatumika kwa njia ya kuleta majibu mapya yenye tija kwetu na familia ya Dk Mwakyembe na wala si kufanya kazi za kurudufu shughuli ambazo taayari yako wazi mitaani.

Kwa matarajio yetu, swala jipya na zito zaidi kuhitaji majibu mapya ni 'JENI NANI AU AKINA NANI HAO WANAOHUSIKA NA ULISHWAJI SUMU KWA DK MWAKWEMBE NA WANAFANYA HIVO KWA NJIA ZIPI NA MALENGO GANI NA KITU GANI KIFUATE', full stop!!! Hatutaki mizunguko zaidi, miduara zaidi na kule kutupiana kwingi mpira kati ya maafisa waandamizi na vyombo vyao vilivyokwishaonyesha ubutu wa kustaajabisha toka huko nyuma.

Hivyo, mpaka hapa, ni kwa kuendeleza matarajio hayo hayo ya wananchi juu ya sakata hili ambapo tungependa kuaagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulika na maswala ya Afya na Usalama wa Raia, ifanye hima kuunda kamati murua itakayo kuna chombo huru, chenye weledi zaidi na hadidu za rejea za wazi kwenda kuchunguza swala zito zaidi kwamba 'NI NANI AU AKINA NANI HAO WANAOHUSIKA NA ULISHWAJI SUMU KWA DK MWAKWEMBE NA WANAFANYA HIVO KWA NJIA ZIPI NA MALENGO GANI NA KITU GANI KIFUATE', full stop!!!

Haya yote yanatokana na ukweli kwamba taarifa zozote juu ya afya wa kiongozi yeyote wa umma ni mali na na haki ya walipakodi wa nchi hii kuujua tena ki-undani zaidi.

Msingi wa hoja yangu hii ni kwamba mtu anapokua kiongozi anapewa dhamana na umma na pindi inapotokea kwamba ameugua tena ni umma hiyo hiyo ndiyo hugharamia tiba yake mwanzo mpaka mwisho. Hadi hapo si haki kwa mtu yeyote kuficha taarifa zozote mbali na umma kwa kuwa ndiye mwenye dhamana yake pamoja na ufadhiliya kiongozi yeyote

Kama haitoshi, nasema swala la serikali kupanga kuendelea kuchunguza sakata juu ya afya ya Dk Mwakyembe KAMA NI SUMU AU SI SUMU hadi hivi sasa ni AN IRRELEVANT ENDEAVOUR isiomsadia mtu yeyote yule ndani y nchi hii. Hivyo endapo kuna mtu au chombo kuna chombo (pengine CCM) kinataka kujiridhisha zaidi juu ya hilo bali kiendeshe uchunguzi binafsi kwa gharama binafsi na matokeo hayo yaje yatumike kwa kukidhi matakwa yao binasi huko mbali na macho yetu.

Katika eneo hili la pili nako hoja yangu nzito sana ni kwamba hadi sasa ni wazi kwamba jopo la Madaktari Bingwa na Wana-Sayansi wa hospitali Maarufu sana duniani, Apollo Hospital kule nchini India, wao walitumia MUDA MFUPI UNAOJULIKANA kuchunguza vipimo toka kwa Dokta Mwakyembe na KUTUWEKEA JIBU HADHARANI.

Katika msururu mzima wamambo ya uchunguzi wa kitibabu na kisayansi huko Apollo Hospital, katika ulimwengu wa sheria, tunatambua wazi kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa niaba ya Umma wa Tanzania ambao ndio wenye dhamana yote KIKATIBA na wenye kugharamia kila kitu kifedha kupitia kodi zetu) inajitokeza kuwa ni mteja na kwamba Jopo lile la Wataalam waliobobea katika Sayansi ya Tiba pale Apollo Hospital wao pamoja na vyombo vyao vya kisasa ambavyo vilipata kukiridhisha serikali yetu, wao ni waajiriwa katika mtiririko mzima huu.

Hivyo mwisho wa siku wakatoa RIPOTI YA KIUFUNDI WA SAYANSI YA TIBA ILIOTUKUKA ZAIDI DUNIANI PALLE APOLLO HOSPITAL na kuikabidhi kwa serikali hii ya JMT kwa niaba yetu ili sisi kama wateja tujiridhishe nini kinachomsibu mgonjwa wetu (Dk Mwakyembe) ambaye
Umma wa Tanzania tunacho cha kupoteza kwa kiasi kikubwa endapo atadhurika zaidi na hata pindi inapotokea kibahati mbaya akapoteza maisha.

Sasa kunapotokea mtu au watu wanajipenyeza katikati ili watu tusipate kujiridhisha na ripoti hiyo ambayo serikali iliipewa tayaari nadhani hili huenda tukaidai vizuri zaidi kupitia mahakama ili mwajiriwa wetu huyo wa kumtibu Dk Mwakyembe aje akaitoe yote yote bila hata ya nukta kufutwa kwenye ripoti hiyo; and that is a fact to come sooner than later anyway!!

Naam, kitendo hiki kilitokea mara baada ya Madaktari Bingwa na Wataala wote wa Maswala ya Ngozi nchi KUKIRI KWA LUGHA YA MATENDO yao, pale hospitali yetu ya rufaa Muhimbili, kwamba kuhusu sakata la ki-afya ya Dokta Mwakyembe wao ama imewazidi utaalam au kule kukosekana kwa zana za kisasa zaidi ya sayansi ya tiba hapa nchini hivyo serikali ikalazimika kumpeka huyu kiongozi wetu huyo kwa tiba zaidi huko nje ya nchi.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba kuna taasisi bora za tiba zaidi ya milioni moja kote duniani, kitendo cha serikali ya JMT kuamua kumpeleka mtumishi wetu Apollo Hospital na wala si kwingineko maana yaake ni kwamba kuna umakini wa hali ya juu ulitumika kufikia chaguo hilo.

Ndio, tungependa kuendelea kuamini hadi sasa kwamba serikali nayo iliamini sana chombo hicho cha hapo nchini India kwa utaalamu wake wa sayansi ya tiba, mazingira na vyombo vyake vya kisasa zaidi ya hali hlisi tulionayo kokote kule hapa nchini hivyo hata kunapotokea wao kutukabidhi RIPOTI YAO YA KIUCHUNGUZI JUU YA AFYA YA MGONJWA WETU DK MWAKYEMBE, ni imani ile ile inatarajiwa kuewndelea hadi kutafuna yale yaliomo mle ndani ya faili ile ya mgonjwa wetu.

Sasa kama hali hali ni kwa serikali ya JMT kulazimika kukidhi matarajio tajwa hpo juu kuhusiana na ripoti ya Dk Mwakyembe toka kwa wataalam wa saynsi ya tiba waliosifika kote duniani sasa hili la kuibuka mtu kama vile katoka usingizini au kwenye sayari nyingine, na ghafla tu eti anaanza kutunatangaia kundi lingine kufanya kazi ile ile ambayo tayari wao kama serikali walishawaajiri wataalam wa Apollo Hospital kufanya na kutoa hitimisho ya yote, ni nani anajaribu kuchezea akili ya nani hapa na kwa kuteketeza rasimali adimu ya taifa kwa sababu gani hadi hapo????????

Wananchi kote nchini sasa ni wakati mwafaka kusema NO kwa hilo kundi la pili la WANA-SAYANSI UCHWARA WA WAZIRI VUAI NAHODHA eti kwenda kuendesha uchunguzi juu ya uchunguzi wakati maswali zaidi yanayolilia majibu mapya yanaendelea kubaki bila kushughulikiwa.

Kero kubwa zaidi tena juu ya WANASANSI WA VUAI NAHODHA ni kwamba wao tunaambiwa kwamba WATATUMIA MUDA USIOJULIKANA kurudia kazi hiyo hiyo. Hivi tunafanyia ngonjera uhai wa mtu mzito kama Waziri wa nchi na Mpiganaji kwa fida ya wanyonge wa nchi hii kiasi hiki?


II. UCHURO WA NGONJERA ZA MAAFISA WAANDAMIZI SERIKALINI KUHUSU RIPOTI YA GOGORO LA AFYA YA DK MWAKYEMBE


KUHUSU sakata la mgogoro wa afya na 'Ngonjera na Midura Mirefu' inayoendelezwa na Maafisa Waandamizi ndani ya serikali ya Kikwete juu swala nyeti linalogusia uhaai wa Naibu Waziri wa Miundombinu, Mbunge wa Kyela na Mwanaharakati dhidi ya ufisadi nchini, Dk Harrison Mwakyembe, wananchi sasa tunasema HATUTAKI MBICHI HIZI tena!!

Katu haingii akilini hata kidogo DCI ambaye ndiye Mchunguzi Mtaalam Mkuu nchini Tanzania, awe tu amekurupuka na ki-jiripoti mbele yake tena kwa kuzingtia maelekezo ya weledi wa kazi yake inavyosema, halafu leo hii mtu aibuke na kusema bila aibu eti 'mimi kama Waziri Mwenye dhamani sikujua'.

Mchezo huu maafisa waandamizi wa serikali hii ya Kikwete wa kutupiana mpira kushoto kulia juu ya ripoti ya kitaalam toka Hospitli ya Apollo nchini India hivi sasa unakera kuliko kawaida. Mambo yalianza na Blandina Nyoni wa Wizara ya Afya kushonea faili yenye majibu ya afya ya Dr Mwakyembe kwenye gauni lake ikawa ni vigumu kupakitaka.

Waziri Mwenye dhamana ya Afya, Dk Mponda naye akageuka bubu ghaafla juu ya ripoti hiyo, na wananchi tuliposhinikiza uchunguzi wa NANI ALIYEFADHILI Dk Mwakyembe kutiliwa sumu ili tujue ukweli wa mmbo, hapo ndipo akaibuka Mtetezi wa kujitolea kwa MAFISADI kwa jina la DCI Manumba aliyeendesha uchunguzi ndani ya wiki moja na kuweka mambo hadharani kwa jinsi upeo wake unavyomwelekeza - jibu likawa HAKUNA SUMU HAPA.

Sasa leo hii kaibuka afisa mwingine serikalini kwa jina la Vuaai Nahodha ambaye mpaka hivi majuzi wengi tumekua tukimuona tu kama Waziri sawa tu na picha ukatani (kwa kipindi chake ndio kumetokea mauaji mengi zaidi ya raia mikononi mwao dola wa nchi hii kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii), nae sasa ana-bullshit kila jitihada zilizofanywa na kijana wake Manumba na kuanza kutuaminisha juu ya uchunguzi mwingine juu ya uchunguzi ambao hata wajumbe wake hatuwajui, hadidu za rejea kwao hatuzijui, taaluma zao na uzoefu hakuna anayejua, muda gani na upana wa uchunguzi wao ni swala la kufikirika tu hewani.

Kwa kadiri tujuavyo sisi huku mitaani, DCI Manumba au Saed Mwema anapofanya kazi yoyote ile ni kwamba anayefanya kazi hiyo kimsingi ni Waziri wa mambo ya Ndani ambaye ni Vuai Nahodha. Vile vile, nae huyu waziri naye u waziri mwingine yeyote yule naye anapofanya kazi yoyote kwa jina la serikali yetu hii by extension ni kwamba mwenye kupokea pongezi na au lawama ni Rais wa nchi ambaye ndiye hasa wanayemsaidia kazi zake hizi.

Sasa kwa mtaji wa mizunguko hii yote, kupoteza kote muda zaidi juu ya swala hili sasa tunasema kweli mbichi hizi htuzitaki teeena!!

Kimsingi songombingo hizi zoote zilianzia pale mara baada ya kurejea nchini Dr Mwakyembe kutoka matibabuni nchini India, wananchi tulimbana mbavu kisawasawa AKATUAMBIE KULIKONI juu ya afya yake na kwamba wataalam huko wameona nini?

Kutokana na utaalam wake wa mambo ya sheria na pia maelekezo tu ya Malaika wanaomlinda kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, Dk MwakyembeHapo nyuma kidogo

Hivi kweli enyi maafisa waandamizi wa serikali hii inayofanya kazi kwa niaba ya maelekezo, udhibiti na faida ya MAFISADI waliokubuhu nchini, leo hii mnadiriki kuchezea kamari kweli swala linalogusia uhai wa KIPENZI CHA WANYONGE wan nchi hii kiasi hiki!! Hivi kweli mnajua matokeo ya Ngonjera kama haya ya kutupiana mpira kwetu sisi wananchi huku mtaani kitu gani huenda kikafuatia kweli???????????


III. HITIMISHO JUU YA NGONJERA ZA SERIKALI KWA UHAI WA DR MWAKYEMBE

Wananchi kote nchini sasa ni wakati mwafaka kusema NO kwa hilo kundi la pili la WANA-SAYANSI UCHWARA WA WAZIRI VUAI NAHODHA eti kwenda kuendesha uchunguzi juu ya uchunguzi wakati maswali zaidi yanayolilia majibu mapya yanaendelea kubaki bila kushughulikiwa.
 
Hoja kwa Rais Kikwete; mdharau mwimba miguu huota tende, sakata la Dr Mwakyembe isije ikageuka kijisehemu na fundo la kamba kukatikia jumla endapo wananchi hakuna wa kutusikiliza.

Uchunguzi zaidi usiwe tena juu ya 'sumu au la' hapa bali twende mbele zaidi kutafuta wenye kutenda kosa hili la ajabu sana katika historia ya taifa letu.
 
Kwa yeyote anyechezea swala la Dr Mwkyembe na hata kudiriki kuvuta rushwa juu ya hilo ili kufunika ukweli wa mambo ajua anakizika taratibu Chama Cha Mapinduzi ambacho mpaka hivi sasa kimeshinwa KJIVUA GAMBA LA MAFISADI ambao hsa ndio wanaoaminika na kila mwananchi kwamba wanahusika na hili 'Gogoro la Afya la Kuchonga' kwa Mhe Mwakyembe.
 
MUUNGANIKO KATI YA SHUGHULI ZA CCM KWA KUCHANGANYIKANA NA SHUGHULI ZA KISERIKALI KUNAFILISI HAZINA YETU YA TAIFA NA KUDIDIMIZA KABISA MATUMAINI YA MAENDELEO YA NCHI ZAIDI YA WALIVYOWEZA KUBAINI EUROPEAN UNION KWENYE UCHAGHUZI 2010
ccccm.JPG


ccccm1.JPG

JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012

Surely, President Kikwete how do you just call-street party meetings into a government state house and you just do this without any bit of gult or shame??

Majuzi tu mkuu umetumia ndege yetu, posho zetu na muda wetu wa kufanyia serikali kazi ili mshahara wako wa February uingie ki-halali, kwenda na jopo kubwa la wana-CCM kwenye shughuli ya kichama na kucheza Makirikiri kule Botswana na wala hukuhisi huo UFISADI uliotendeka kwa kubaka rasmali ambazo kimsingi huna uhalali nayo kwa shughuli kama hiyo.

Makamu wako Bilal ilikua ni mpaka wananchi wamzomee kule Tunduma ndio apate kushtuka kwamba katika ziara ile watu walikua tayari kumsikiliza Makamu wa Rais wa JMT na katu hawakua tayari kusikia hata tone ya hutuba ya Kada wa CCM anayeishi katika ulimwengu wa ndoto akidhani kwamba Tanzania ya leo kila umwonaye barabarani bado eti ni mwana-CCM. Jmani mbona hamjifunziiiiiiiii?????

Mkuu wa Mkoa Stella Manyanya, naye pamoja na usomi wake ule wote bado kapumbazika ghafla tu kwa kushindwa kujua kwamba shughuli za ki-CCM ni tofauti kabisa na zile za ki-Serikali sawa tu na jinsi mambo yalivyo kwenye karakana za Engineering pale UDSM kwamba injini ya trekta ni tofauti kabisa na injini ya toyota saloon pamoja na kwamba yote bado hutajwa kama injini tu.

Prof Button vipi huyu mwanafunzi wako?? Eti anatumia hadhara ya kiserikali kukaribisha watu aliowabatiza jina kuwa ni Wana-CHADEMA kwenda CCM; ama kweli hata msomi akishajiunga huko naye yale yale!!!!!!!!

CCM wameulipa serikali ya JMT kiasi gani cha fedha kutumia ukumbi huo wa hapo state house, kutumia vinywaji na pengine hata kupewa posho?

Tafadhali Mkaguzi wa mahesabu za seriukali tunaomba taarifa juu ya bajeti na matumizi ya ikulu katika kipindi walau cha miaka 3 ya fedha ili tuone usahihi wa matumizi hayo, tija kwa taifa, na iweze kutupa mwanga wa kiasi gani chombo hiki kije kipewe au kisipewe kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Ewe mwanasheria Mkuu ambaye ndiwe mshuri mkuu wa serikali kuhusu maswala ya ki-sheria nchini, tafdhali andaa semina kubwa ajabu na ukamuite Dr Semboja wa chuo kikuu cha Dar es Salaam aje akawapige shule viongozi wetu hawa TOFAUTI KATI YA YALIO YA CHAMA NA YALE YALIO YA KISERIKALI kabla watu hatujaanza kuwaomba mkutano kule mahakamani juu ya matumizi mabaya ya ofisi na rasilmali ambazo hata wana-KAFU nao wamelipia.

Yaani hata wewe Januari Makamba tunaoaminishwa kukaa sana huko ughibuni batu tu tunakuona ukikata shingo kwenye THAT PAROCHIAL PARTY MEETING BUT USING STATE RESOURCE BELONGING TO MEMBERS OF ALL OTHER POLITICAL parties in the country yet without any shame on your face??

Hivi ndivyo mnavyotupigia kelele kila situ eti mnataka utawala wanchi hii iwe mikononi mwao baadhi ya WATANZANIA WANAOJIKWEZA KAMA VIJANA sasa wakati mienendo yao ndio kama hivi ya kizee kwelikweli hivi sawa tu na Mzee Pius Msekwa kwenye kikao hichop hicho?? Sasa ubani na mwarobaini ya ujana mnaoringia kila siku iko wapi hadi hapo??

Chonde Mhe Rais Kikwete, kabla haujafanya jitihada za kutenganisha kofia za U-Bunge na U-NEC huko ndani ya chama chenu ili kumdhibiti Lowassa na kumleta chaguo lako dhaifu kuja kuongoza nchi kwa kisingizio cha jinsia tu, hebu kwanza katutenganishie kofia ya kiserikali iwe mbali kabisa na ile ya kichama hata kabla hatujaingiza hili kwenye katiba mpya ijayo.
 
RAIS KIKWETE ANAPOMPIGA VITA MWALIMU JULIUS NYERERE KABURINI LEO HII KWA KUHIMIZA 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ALILOTUKATAZA WATANZANIA LICHA YA MADHARA MAKUBWA TUNAYOYAVUNA HIVI SASA KWAKE MWENYEWE HIVI SASA, YOTE NI KWA FAIDA YA NANI?

Rais Kikwete kamwe hawezi kurusiwa kwa mara ya tatu kufanyia majaribio ya kimaabara maisha ya WaTanzania kwa misingi ya kukamatishwa mawazo ya kiayawani barabarani kila kukicha huku taifaa likiendelea kuangamia kwa kiasi kikubwa kwa kila Jaribio la Kisiasa analolifnya ama ndani au nje ya chama chake.

Mpaka hivi sasa, ni jambo lililo dhahiri kwa Watanzania waliowengi taifa limefikia hapa tulipofika kutokana na mambo matatu mazito ya kimajriobio hayo hayo.

Kwanza, madhara mazito yalioifikia taifa hili ilianza na jaribio la kwanza la kutumika dhna ya 'URAIS WA VIJITOTO' na matokeo yake tukampata Mhe Kikwete kuwa ndiye rais wa JMT licha ya Mwalimu Nyerere kuktalia jambo hili na kuonya kwa nguvu nyingi zaidi watu tusidhubuti kukumbatia jambo hili.

Kiukweli katika nchi hii hakuna hata mtu mmoja atakayeweza kusahau mambo gani ambayo yametupata na yanyoendelea kutupata kutokana na mtaji wa dhambi ya kwenda kinyume na ushauri wa Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere, kwa kukumbatia 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ambayo hivi sasa tena imempata dalali mpya kwa jina la Rais Jakaya M. Kikwete.

Sote hatuna shaka kwamba uongozi wa nchi si sawa na uongozi wa jimbo wala kata hivyo mtu gani akachaguliwe kuongoza WaTanzania zaidi ya milioni 48 si swala la kuchezea chezea.

Inasikitisha mno jinsi ambavyo urais wa nchi hii unavyoendelea kukosa thamani na hata kuanza kurahisishwa kiasi hiki kwa namna mbavyo hata Rais Kikwete anafika mahala anakwenda kujibana mahali kujadilian jambo linalogusa mustakabali wa nchi na vijitoto kwenye mazungumzo binafsi na akina Zitto Kabwe na Januari Makamba kwenye mgahawa na kisha kesho yake kuonelea kuwa sasa hizo ndoto binafsi sasa ziwe ni Mambo ya Ki-Katiba ambayo kila Mtanzania ataswa kuyafuata. Katu hatudanganyiki na mawazo ya barabarani ya aina hiyo.

Hapa chini ni kijisehemu tu cha baadhi ya hatua za kimajaribio ya kimaabara ya Rais Kikwete kudiriki kucheza kamari na mchezo wa potea pata na maisha ya mamilioni y WaTanzania kwa namna isivyofaa hata tone:

1. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijitokeza naa kamari ya kwanza kabisa ya kutuletea kitu walichokiita DAMU CHANGA (kwa maana ya Ndg Jakaya Mrisho Kikwete) kugombea kiti cha urais wa taifa letu.

Sote hivi sasa ni mashahidi jinsi gani kila kitu ndani ya nchi kimepuputika na tumebakiwa tu na janga la taifa kwa kukubaliana na uamuzi huo huo kufanya uchaguzi chini ya DHANA HIYO HIYO POTOFU LA 'URAIS WA NCHI KUKABIDHIWA VIJITOTO' ambao hata kusimamia tu mambo yao ya kimapenzi tu na visichana vyao yenyewe bado ni mtihani.

Kwa nini watu turudie kosa eti kwa jina tu la kuchagua UDOGO WA UMRI kama kigezo ki-kuu mtu kuongoza nchi??

2. Kwa mara nyingine Rais Kikwete mwenyewe, kwa mtiririko ule ule uliojaa MAWAZO YA KUKOMOA MAADUI WAKE, akaja na DHANA POTOFU nyingine kwamba bunge letu ambalo ni mhimili muhimu mno kikatiba kwa kazi ya kutunga sheria za nchi sasa kiongozi wake kwa maana ya spika ili apatikane ni sharti KILA MMOJA WAO AMA AVUE SURUALI AU SKETI KUMTAMBUA JINSIA ALIVYOUMBWA halafu eti kwa kigezo hicho tu ikawa ni leseni kwa baadhi ya washindani kuwashinda wengine kwenye kinyang'anyiro na kuibuka kuwa MA-SPIKA UBWETE AMBAO KILA SIKU UFANYAJI WAKE KAZI NI MADUDU MATUPU NA KAZI NYINGINE NI KUDAI TU POSHO.

Sasa hivi nako chaguo letu kwa kuzingatia DHANA POTOFU LA JINSI nalo linatutokea puani mpaka kinamma wanaharakati kulazimika kuingia barabarani kupinga jinsi gani Spika Anne Makinda anavyowadhalilisha kwa maamuzi yake ya ki-shabiki hata kwa masuala mazito kwa mustakabali mzima wa nchi.

Kweli Rais Kikwete bado tu huoni jinsi gani ulivyotuuza hadi hapo na bunge kuonekana kupwaya ajabu kutokana na mojawapo misururu ya mi-dhana yako yanayopingana na katiba ulioapa kulinda?

3. Kwa jinsi ambavyo Rais Kikwete amedhihirisha wazi kwa umma wa Tanzania kwamba yeye na MAFISADI nchini ni damdam, leo hii anapata wapi uhalali mbele ya uso wa jami na ujasiri uliomshinda kuwavua gamba mafisadi, eti kuja kuliambia taifa na wala si CCM yake kwamba Rais wa Tanzania ajaye atakua ni mtu wa aina hivi mara vile??

Mwenzetu huyu kwa jinsi alivyoongoza kwa KUKUMBATIA MAFISADI Tanzania na kutumia dola kuua wananchi kila kona ya taifa hili, moja kwa moja inamfanya awe ni mtu ambaye hana MORAL AUTHORITY kutuambia wananchi kwamba Rais ajaye atakua ni wa namna gani vile.

4. Isitoshe, masuala ya raia yupi mwenye umri gani ataweza KUWA NA HAKI YA KUZALIWA KUJITOKEZA KUCHAGUA AU KUCHAGULIWA kwa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya mipaka hii ni SUALA NYETI NA LA MSINGI KI-KATIBA ya JMT hivyo hakuna mtu yeyote au taasisi itakayojifurahisha na njozi zake mwenyewe kulivibadilishia vichochoroni huko Magogoni kwa malengo yasio na faida kwa Umma wa Tanzania.

Hivyo, mabadiliko makubwa kama haya eti kwa ajili tu ya HIVI VIJITOTO FISADI ni sharti kwanza tuletewe wananchi kwenye REFERENDUM ILI TUKAIPITISHE KWENYE TNURI LA KIDEMOKRASIA halisi.

5. CCM ikitaka a political showdown wa aina yoyote eti kwa ghiliba hizo hizo wanazozitumia hivi sasa kuzuia baadhi ya watu wenye hamu kubwa ya kugombea urais ndani ya chama chao, na sasa waanze kuvusha ghiliba hizo hizo kwenda kwa vyama vingine kwa kutaka URAIS WA HIVO VITOTO VIWILI VIWAKILISHI NA VINARA WA MAFISADI NCHINI, CHADEMA kipo katika nafasi zuri mara 50 zaidi ya hapo kugeuza ghilib hii mpya kurojeka zaidi ya uji na tena nda ya kipindi kifupi haijawahi kuonekana.


URAIS wa taifa hili kwa msururu wa dhana potofu kama vile JINSIA na au UMRI hauna nafasi hata kidogo kwa nchi hii mpaka mawazo ambayo ni HIGHLY CONTENCIOUS kama hayo yawe yamepitishwa kwenye KURA YA MAONI KITAIFA ikisimamiwa na Tume Huru ya uchaguzi ambalo si hili tume la huyu Jaji wa Mondo, Kondoa.

NOTE:
Na kama huu ndio mkondo mpya wa kutekeleza ile azma ya Rais Kikwete kwamba 'ninapoondoka madarakani uongozi wa nchi simuachii Mtanzania Mkristo ng'o' basi wenye mawazo haya mhesabu kula ya chuya kwa kuwa hamjafaulu bado katika hili la urais wa Januari Maakamba na na Zitto Kabwe!!!

Source: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015 « Zitto na Demokrasia

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015



KABWE ZUBERI ZITTO, MPKIGOMA KASKAZINI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015

Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais'.

Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais.


Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama changu, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.


Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais.

Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu.

Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu.

Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.


Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.


Dar es Salaam29 Februari 2012
 
Mhe Zitto Kabwe, huwezi ukawa CCM na ukwa CHADEMA pia kwa kipindi hicho hicho kimoja; kwa mtaji wa hulka ya aina hii peke yake hufai kuwa kiongozi wa nchi.

Kote unataka na kote unapenda; je CHADEMA kikiamua kucheza karata chafu na wale wana-CCM wasiopendezwa na mienendo yako wewe, Jaanuari Makmba na Rais Kikwete kuwatfutia MAFISADI uhai mwingine katika utawala ujao wa nchi hii, je mtakua wageni wa nani na michezo hii ya kitoto ya kutamani eti kumzuia Dr Slaa asigombee urais ukagombee wewe huku CHADEMA lakini kwa niaba na faida ya MAFISADI??????

Tanzania safari hii URAIS KWA MBELEKO haikubaliki; sote tumeshuhudia madhara ya Urais wa Mbeleko na wal hatutaki kurudia hilo kosa katika maisha haya!!!!
 
Kuwaambia hawa jamaa ni sawa na kuyapigia kelele mawe wala hayatabadilika but me naamini "we have to trust in time to make things better"
 
Swala la kubadilisha UMRI ILI KUMPENDEZESHA nafsi Januari Makamba na Zitto Kabwe, chini ya DHANA JIPYA LA 'URAIS WA NCHI KWA VIJITOTO' kwa niaba y MAFISADI kupata uhakika chini ya utawala ujao wa kulindiwa mali walizotibia, na vile vile kuendeleza MALENGO SUGU YA UDINI nchini kamwe hayakubaliki hata tone Mpaka tukayapitishe mawazo kam hayo ya kihayawani kwenye Kura ya Maoni ya ya Taifa tena chini ya Tume Huru ya Uchaguzi tofauti kabisa na hii Tume ya Lubuva.
 
Masikitiko makubwa kwa baadhi ya wanasiasa ambao huenda bado hawajasoma hali ya hewa kisiasa nchini na pengine kung'amua ni kitu gani kinachojipika kwa wananchi baada ya kuporwa kura ya urais na CCM 2010.

Ukweli wa mambo ni kwamba safari hii na kuendelea, Urais wa JMT katu hautopatikana kwa yeyote kubebwa mbeleko mpaka ikulu.

Kwa yeyote asiyeamini maneno haya niyasemayo, bora ukajiandae na daktari wa presha mapema kabla ya 2015.
 
Nawakumbusha tu yaliyowahi kusemwa hapa jamvini na leo tumejisahaulisha.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom