UFAULU wa kidato cha sita mwaka huu umepungua

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
UFAULU wa mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka huu umepungua kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka jana.

Wavulana wameibuka kidedea kwa kushika nafasi zote 10 bora.

Pamoja na hayo, masomo ya Sayansi, Biashara na Hisabati ni miongoni mwa yaliyoongoza kwa kufaulisha wanafunzi wengi ikilinganishwa na Sayansi ya Jamii na Sanaa, huku wanafunzi wengi wakifeli zaidi katika masomo ya lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Akisoma matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, alisema , asilimia 87.24 ya wanafunzi waliofanya mtihani walifaulu mtihani huo, ikilinganishwa na asilimia 88.85 ya mwaka jana.

Hata hivyo waliofaulu kati ya daraja la kwanza na la tatu ni asilimia 78.53 tu ya waliofanya mtihani. Mchanganuo wa Necta unaonesha kuwa daraja la kwanza waliofaulu ni asilimia 7.25, daraja la pili (20.23%), daraja la tatu (51%), daraja la nne (13.51%) na waliopata sifuri ni asilimia 7.97 ya wanafunzi wote.

Kwa mtazamo huo, kwa vigezo vya awali vya wanafunzi watakaopata udhamini wa Serikali kuingia vyuo vikuu ni asilimia 27.48 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo kwa maana ya waliopata daraja la kwanza na la pili.

Tofauti na ilivyokuwa katika matokeo ya kidato cha nne, katika matokeo ya kidato cha sita sekondari za Serikali zimejitokeza zaidi kutoa wanafunzi bora.

Dk. Ndalichako aliwataja walioshika nafasi ya 10 bora katika mtihani huo kuwa ni Muhagachi Chacha wa Kibaha, Samweli Katwale (Mzumbe), Amiri Abdallah (Feza Boys), Aron Gerson na Shaban Omary wa Tabora Boys na Kudra Baruti (Feza Boys).

Wengine ni George Assenga wa Majengo Sekondari, Comman Nduru (Feza Boys), Francis Josephat (Tabora Boys) na George Felix (Mzumbe).

Kutokana na nafasi zote 10 bora kuchukuliwa na wanaume, Dk. Ndalichako alisema Necta ilitengeneza orodha maalumu ya 10 bora ya wasichana peke yao.

Katika orodha hiyo, wasichana walioongoza ni Doreen Kabuche wa Benjamin Mkapa, Rahabu Mwang’amba (Kilakala), Mary Moshi (Kifungilo Girls), Nuru Kipato (Marian Girls), Zainab Hassan (Al-Muntazir Islamic).

Nafasi ya sita kwa kundi hilo maalumu ilichukuliwa na Catherine Temu wa Ashira, Anthonia Lugomo (Usongwe), Cecilia Mville (Kifungilo Girls), Mariam Matovolwa (Kilakala) na Suzana Makoi (Tarakea).

Shule bora iliyoongoza kwa kufaulisha katika kundi la shule zenye wanafunzi zaidi ya 30 ni Marian Girls iliyofuatiwa na Feza Boys, Kifungilo, Kibaha, St Mary’s Mazinde, Ilboru, Tabora Boys, St Mary Goreti, Mzumbe na Mafinga Seminari.

Kundi la shule bora zenye wanafunzi chini ya 30, lilikuwa na shule nyingi za seminari zikiongozwa na Seminari za Uru, St James, Same, Maua na Dungunyi. Nyingine ni DCT Jubilee, Parane, St Joseph-Kilocha, Mlama na ya Wasichana Masama.

Somo lililoongoza kwa kufaulisha wanafunzi wengi ni Uchumi lililofaulisha asilimia 93 ya watahiniwa na kufuatiwa na Biashara (88.7%), Advanced Mathematics (81.5%), Kemia (80.3%), Fizikia (67.03%), Basic Applied Mathematics (50.69%) na Jiografia (9.65%).

Baraza limefuta mitihani ya watahiniwa 12 kutokana na udanganyifu kati yao watano ni wa shule na saba wa kujitegemea ambapo pia watahiniwa 218 matokeo yao yamesitishwa hadi watakapolipa ada ya mitihani.
 
ikitokea msichana kaongoza basi.. orodha maalum ya top 10 haitengenzwi... ikitokea msichana yoyote hayumo top ten wanalazimisha kutengeneza orodha maalu.

kwa mtindo tunawapa picha gani watoto wetu wa kike...?!!! na hii inaendelea hadi ngazi ya taifa vit maalum. Ina maana wasichana hawawezi ku compeate na wanaume mpaka wapewe nafasi maalum...? kuna umhuhimu gani kuwategenezea orodha malum jst bcz hakuna msichana aliye topten..
 
UFAULU wa mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka huu umepungua kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka jana.

Wavulana wameibuka kidedea kwa kushika nafasi zote 10 bora.

Pamoja na hayo, masomo ya Sayansi, Biashara na Hisabati ni miongoni mwa yaliyoongoza kwa kufaulisha wanafunzi wengi ikilinganishwa na Sayansi ya Jamii na Sanaa, huku wanafunzi wengi wakifeli zaidi katika masomo ya lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Akisoma matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, alisema , asilimia 87.24 ya wanafunzi waliofanya mtihani walifaulu mtihani huo, ikilinganishwa na asilimia 88.85 ya mwaka jana.

Hata hivyo waliofaulu kati ya daraja la kwanza na la tatu ni asilimia 78.53 tu ya waliofanya mtihani. Mchanganuo wa Necta unaonesha kuwa daraja la kwanza waliofaulu ni asilimia 7.25, daraja la pili (20.23%), daraja la tatu (51%), daraja la nne (13.51%) na waliopata sifuri ni asilimia 7.97 ya wanafunzi wote.

Kwa mtazamo huo, kwa vigezo vya awali vya wanafunzi watakaopata udhamini wa Serikali kuingia vyuo vikuu ni asilimia 27.48 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo kwa maana ya waliopata daraja la kwanza na la pili.

Tofauti na ilivyokuwa katika matokeo ya kidato cha nne, katika matokeo ya kidato cha sita sekondari za Serikali zimejitokeza zaidi kutoa wanafunzi bora.

Dk. Ndalichako aliwataja walioshika nafasi ya 10 bora katika mtihani huo kuwa ni Muhagachi Chacha wa Kibaha, Samweli Katwale (Mzumbe), Amiri Abdallah (Feza Boys), Aron Gerson na Shaban Omary wa Tabora Boys na Kudra Baruti (Feza Boys).

Wengine ni George Assenga wa Majengo Sekondari, Comman Nduru (Feza Boys), Francis Josephat (Tabora Boys) na George Felix (Mzumbe).

Kutokana na nafasi zote 10 bora kuchukuliwa na wanaume, Dk. Ndalichako alisema Necta ilitengeneza orodha maalumu ya 10 bora ya wasichana peke yao.

Katika orodha hiyo, wasichana walioongoza ni Doreen Kabuche wa Benjamin Mkapa, Rahabu Mwang'amba (Kilakala), Mary Moshi (Kifungilo Girls), Nuru Kipato (Marian Girls), Zainab Hassan (Al-Muntazir Islamic).

Nafasi ya sita kwa kundi hilo maalumu ilichukuliwa na Catherine Temu wa Ashira, Anthonia Lugomo (Usongwe), Cecilia Mville (Kifungilo Girls), Mariam Matovolwa (Kilakala) na Suzana Makoi (Tarakea).

Shule bora iliyoongoza kwa kufaulisha katika kundi la shule zenye wanafunzi zaidi ya 30 ni Marian Girls iliyofuatiwa na Feza Boys, Kifungilo, Kibaha, St Mary's Mazinde, Ilboru, Tabora Boys, St Mary Goreti, Mzumbe na Mafinga Seminari.

Kundi la shule bora zenye wanafunzi chini ya 30, lilikuwa na shule nyingi za seminari zikiongozwa na Seminari za Uru, St James, Same, Maua na Dungunyi. Nyingine ni DCT Jubilee, Parane, St Joseph-Kilocha, Mlama na ya Wasichana Masama.

Somo lililoongoza kwa kufaulisha wanafunzi wengi ni Uchumi lililofaulisha asilimia 93 ya watahiniwa na kufuatiwa na Biashara (88.7%), Advanced Mathematics (81.5%), Kemia (80.3%), Fizikia (67.03%), Basic Applied Mathematics (50.69%) na Jiografia (9.65%).

Baraza limefuta mitihani ya watahiniwa 12 kutokana na udanganyifu kati yao watano ni wa shule na saba wa kujitegemea ambapo pia watahiniwa 218 matokeo yao yamesitishwa hadi watakapolipa ada ya mitihani.

Vipi hapo kwenye red ni sawa hii kitu mkuu?
 
ulaya hakuna mambo ya namna hiyo kabisa mie nashangaa kweli kwanini wanawake wa africa wazembe sana na wamekua wakibebwa sana pia pamoja na upendeleo bado wanashindwa inabidi waache uvivu wakaze msuli kwa nchi za ulaya daladala zinaendeshwa mpaka na wanawake ila bongo mwanamke akiwa konda tu ni soo!
wakina mama huu upendeleo mpaka lini? yaani kuongoza kwa wavulana kuna andaliwa list nyingine?mbona kidato cha nne haikuandaliwa list ya wavulana?tafakari chukua hatua
 
Wanawake kataeni upendeleo huu wa orodha maalum ya wasichana kwani mnazidi kudhaifishwa.
 
Baraza limefuta mitihani ya watahiniwa 12 kutokana na udanganyifu kati yao watano ni wa shule na saba wa kujitegemea ambapo pia watahiniwa 218 matokeo yao yamesitishwa hadi watakapolipa ada ya mitihani.

Kwa hiyo in maana hizi takwimu na recognition wanazotoa zinaweza kubadilika? Kwa mfano katika hao 218, haiwezekani kukawa na mmoja aliyefanya vizuri kuliko hao waliotajwa kwenye kumi bora?
 
Ndiyo maana yake - mabadiliko yanaweza kutokea.
 
SHULE YA SEKONDARI MAURICE inawatangazia wazazi na walezi wote kwamba tunapokea wanafunzi kidato cha kwanza mwaka 2019, nafasi za kuamia kidato cha kwanza na cha pili pia tuna kituo cha mitihani kwa watahiniwa wa kujitegemea na Q.T. Vile vile pia tunapokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa michepuo ya ECA, HGE, HGK, HKL na HGL. ADA ni nafuu sana. Shule ni ya kutwa na bweni kwa wavulana na wasichana. Shule ipo Dar es salaam wilaya ya temeke, eneo LA mbande kisewe. Simu 0785907371. Wote munakaribishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom