Mtaala Mpya wa Elimu ya Msingi uko Tayari. Wizara ya Elimu mbona haitaji Lugha rasmi ya kujifunzia?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,784
Wizara ya Elimu imekamilisha mtaala Mpya wa Elimu ngazi ya msingi ambapo Watoto wataishia darasa la Sita huku idadi ya masomo ikiongezeka.

Pamoja na hayo Mtaala inaonesha masomo ya Lugha yatakauofundishwa ni Kiswahili,Kingereza,Kiarabu,Kichina na Kifaransa.

Cha kushangaza ni kwamba Wizara Haitaji Lugha Rasmi ya Kufundishia?

My Take
Kama Lugha ya Kufundishia sio Kingereza basi huo mtaalama msifundishe Watoto Wetu.

--
TAASISI ya Elimu Tanzania imetoa mtaala wa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba 2023.

Muundo wa mtaala huo umebadilika na sasa elimu hiyo itakuwa ni ya miaka sita badala ya saba kama ulivyokuwa Mtaala wa Elimu ya Msingi wa mwaka 2016.

Mtaala huo umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na falsafa ya elimu ya kujitegemea inayosisitiza elimu inayomwezesha Mtanzania ajitegemee na amudu maisha yake ya kila siku.

Muundo wa mtaala unaonesha elimu ya msingi itatolewa kwa miaka sita katika hatua mbili ambazo ni darasa la kwanza na la pili ili kujenga umahiri katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Katika hatua ya pili inaonesha mtaala huo utaanzia darasa la tatu hadi la sita na italenga kuimarisha stadi za KKK na stadi nyingine za maisha.

Mwanafunzi wa shule ya msingi anatakiwa aanze darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka sita na kumaliza darasa la sita akiwa na umri wa miaka 11.

Kwa mujibu wa mtaala huo, maeneo ya kujifunza na umahiri mkuu kwa darasa la kwanza na la pili yamezingatia ujenzi wa lugha, mawasiliano na stadi za hisabati, utamaduni, sanaa, michezo na afya na mazingira.

Kwa darasa la tatu hadi la sita maeneo ya kujifunza na masomo yamezingatia kumjengea mwanafunzi umahiri wa lugha na mawasiliano, hisabati, sayansi ya jamii, sayansi na teknolojia na sanaa na michezo.

Katika eneo la lugha wanafunzi hao watajifunza masomo ya lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kichina, Kiarabu na Kifaransa.

Mtaala umeelekeza kuwa katika eneo la sayansi ya jamii watakuwa na masomo ya historia ya Tanzania na maadili, Jiografia na mazingira, hisabati, sayansi, sanaa na michezo.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Lyabwene Mtahabwa mtaala huo umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023.

Chanzo: Habari Leo
 
Wizara ya Elimu imekamilisha mtaala Mpya wa Elimu ngazi ya msingi ambapo Watoto wataishia darasa la Sita huku idadi ya masomo ikiongezeka.

Pamoja na hayo Mtaala inaonesha masomo ya Lugha yatakauofundishwa ni Kiswahili,Kingereza,Kiarabu,Kichina na Kifaransa.

Cha kushangaza ni kwamba Wizara Haitaji Lugha Rasmi ya Kufundishia?

View: https://www.instagram.com/p/CwCibCyMyZc/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

My Take
Kama Lugha ya Kufundishia sio Kingereza basi huo mtaalama msifundishe Watoto Wetu.

Usiwe brainwashed mkuu. Kwani wakifundishwa kwa kiswahili kuna tatizo gani?
 
Wizara ya Elimu imekamilisha mtaala Mpya wa Elimu ngazi ya msingi ambapo Watoto wataishia darasa la Sita huku idadi ya masomo ikiongezeka.

Pamoja na hayo Mtaala inaonesha masomo ya Lugha yatakauofundishwa ni Kiswahili,Kingereza,Kiarabu,Kichina na Kifaransa.

Cha kushangaza ni kwamba Wizara Haitaji Lugha Rasmi ya Kufundishia?

View: https://www.instagram.com/p/CwCibCyMyZc/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

My Take
Kama Lugha ya Kufundishia sio Kingereza basi huo mtaalama msifundishe Watoto Wetu.

Asa wewe shida yako ni lugha au ujuzi?
 
Kwani wewe kwenu ni Ulaya Au Amerika. Lugha iwe Kiswahili kufundishia kuanzia Msingi Mpaka Chuo kikuu
 
Kama unaijua Kiswahili pekee utakosa maarifa na connection nyingi zama hizi.
 
Kama hujui umuhimu wa Kingereza kafundishe mtoto wako Kiswahili uli ubobee kwenye umbea

Sawa wewe mfundishe kiingereza ili aanze kujifunza ushoga kwenye intaneti akiwa darasa la tano. Nyerere hakuwa mjinga kuchagua kiswahili

Ipende lugha yako ithamini lugha yako.

Burkina Faso wanafuta kifaransa wanaanza kujifunza kiswahili

S.A. Malema na chama chake wanapendekeza kiswahili ndio iwe lugha rasmi ya kufundishia mashuleni.

Wewe mwenye lugha yako unawaza lugha ya mkoloni wako.
 
Back
Top Bottom