Nadhani mkuu Kiranga atakuja kuelezea zaidi au kunisahihisha lakini jibu fupi ni hili:hivi inakuaje mziga wa nyota kama UY scutti au beltegeuse zinazidiwa uzito na netron star ambazo ni ndogo? hii imekaaje hapo??
Neutron Star:
Hii ni tumba inayosalia baada ya nyota kubwa kufa (supernova explosion). Hii tumba inatengenezwa na neutrons zilizopo karibu karibu sana kuifanya iwe very dense. Nyota hai kama UY scutti zina density ndogo kutokana na ujazo mkubwa wa hewa.
Black hole:
Hii ni kama Neutron star bali density yake ni kubwa zaidi. Hii pia hutokea nyota kubwa (UY scutti ni nyota inayoweza kufa na kuwa blackhole) inapolipuka (supernova) na kufa. Kama nyota iliyokufa ni ndogo kidogo tunapata Neutron star lakini ikiwa mzinga kama UY scutti basi tunapata blackhole.
Neutron star na Blackholes zina gravity kubwa sana kwa hiyo hata baada ya kufa zitakuwa zinameza vitu vingi vinavyokuja karibu yao. Kwa njia hii uzito wa hizi gravity centers unaongezeka kula uchweo.