Ufahamu kuhusu nyota za angani

hivi inakuaje mziga wa nyota kama UY scutti au beltegeuse zinazidiwa uzito na netron star ambazo ni ndogo? hii imekaaje hapo??
Nadhani mkuu Kiranga atakuja kuelezea zaidi au kunisahihisha lakini jibu fupi ni hili:

Neutron Star:
Hii ni tumba inayosalia baada ya nyota kubwa kufa (supernova explosion). Hii tumba inatengenezwa na neutrons zilizopo karibu karibu sana kuifanya iwe very dense. Nyota hai kama UY scutti zina density ndogo kutokana na ujazo mkubwa wa hewa.

Black hole:
Hii ni kama Neutron star bali density yake ni kubwa zaidi. Hii pia hutokea nyota kubwa (UY scutti ni nyota inayoweza kufa na kuwa blackhole) inapolipuka (supernova) na kufa. Kama nyota iliyokufa ni ndogo kidogo tunapata Neutron star lakini ikiwa mzinga kama UY scutti basi tunapata blackhole.

Neutron star na Blackholes zina gravity kubwa sana kwa hiyo hata baada ya kufa zitakuwa zinameza vitu vingi vinavyokuja karibu yao. Kwa njia hii uzito wa hizi gravity centers unaongezeka kula uchweo.
 
kwahiyo mkuu kifyatu hizi neutron star zikishatokea na zenyewe zitafanya fussion ya hydrogen kama nyota nyingine ili kutoa nishati.. na mwisho wake utakuaje?
 
Ukichanganya dini na sayansi unaweza ukatia DOA imani yako kwa kujiuliza maswali mengi tena kwa dini zote mbili.
What if the whole observable universe, yaani galaxies zote ni mbingu ya kwanza, najaribu kui imagine tu mkuu
 
kwahiyo mkuu kifyatu hizi neutron star zikishatokea na zenyewe zitafanya fussion ya hydrogen kama nyota nyingine ili kutoa nishati.. na mwisho wake utakuaje?
Neutron stars zinaanza kama jua letu (isipokuwa linakuwa kubwa zaidi). Linachoma Hydrogen yake kutengeneza Helium. Hydrogen ikiisha inachoma Helium kutengeneza elements zenye uzito mkubwa (Lithium, Beryllium, Boron, Carbon, Nitrogen, Oxygen, ..... ) mpaka itakapokuwa inachoma Manganese kutengeneza Iron au chuma.

Ikianza tu kutengeneza Iron basi ile nuclear fusion inazimika na milipuko ya nuclear inakoma. Hali hii inaondoa ule uwiano uliokuwepo kati ya nguvu ya gravity na milipuko ya nuclear. Hii inaifanya gravity ishinde na kila kitu kinaanguka chini na kulipuka kama supernova.

Tumba inayobakia baada ya mlipuko huu wa mwisho inakuwa na density kubwa sana na baadhi yao zinakuwa neutron stars au kuwa blackholes. Ikishakuwa neutron star au blackhole basi inaranda tu na inaweza kukamata majua na sayari nyingine zikawa katika orbits kuizunguuka kama lilivyo blackhole letu katikati ya milkway galaxy yetu.
 
What if the whole observable universe, yaani galaxies zote ni mbingu ya kwanza, najaribu kui imagine tu mkuu
Wazo zuri sana hilo mkuu. Kuna wanasayansi wanatafiti kuona kama kuna universe nyingine zaidi ya hii yetu. Inawezekana kukawa na multiple-universes au mbingu nyingi. Lako sio wazo la kupuuzwa hata kidogo. Ni aina hiyo ya fikra inayotengeneza wana sayansi waliokubuhu.
 
Hvi mkuu kifyatu tukisema labda nyota iko umbali wa 640 light years tunamanisha nini..? Mimi hua sielew kabisa

04
 
Asante mkuu. Astronomy ni moja ya hobby zangu tu.
Hivi mkuu madukani unaweza kupata telescope ambayo inaweza nikaziona sayari zote kwenye solar system yetu na pia baadhi ya nyota, sayari namaanisha pamoja na physical features zake kama milima, mabonde nk
 
Hvi mkuu kifyatu tukisema labda nyota iko umbali wa 640 light years tunamanisha nini..? Mimi hua sielew kabisa

04
Ina maana hiyo nyota iko mbali kiasi cha kwamba mwanga wake huchukua miaka 640 kutufikia.

Kwa kulinganisha tu, mwanga kutoka jua letu huchukua takriban dakika 8 kutufikia.

Sasa ukichukulia kuwa mwanga unasafiri katika kasi ya kilomita 1,080,000,000 kwa saa, unaweza kupiga mahesabu kujua huo umbali wa 640 light-years ni kilomita ngapi - ni mbali sana.

Mwaka una siku 365
Siku ina masaa 24

Kwa hiyo 640 light-years ni sawasawa na

640 x 365 x 24 x 1,080,000,000 = 606,000,000,000,000 kilomita = kilomita trillion 606 ndio umbali wa 640 light-years.

Na hii ipo karibu nasi. Kuna nyota na galaxies zilizoko thousands, millions, hata billions ya light-years kutoka hapa. Na hizo ni zile tunazoziona tu.

Ulimwengu ni mkubwa sana mkuu. Wewe kula ugali wako umshukuru muumba wako tu.
 
Hivi mkuu madukani unaweza kupata telescope ambayo inaweza nikaziona sayari zote kwenye solar system yetu na pia baadhi ya nyota, sayari namaanisha pamoja na physical features zake kama milima, mabonde nk

Sijui kwa Tanzania ni maduka gani zinapatikana. Lakini kwa kutumia telescope nzuri ya kawaida (kibei) unaweza kuona sayari zote lakini sio milima na mito. Utaiona sayari yenyewe na miezi inayoizunguuka au pete (rings) kama za Saturn. Unaweza kuona mabonde na milima ya mwezi wetu lakini sio ya sayari.

Ulizia UDSM au vyuo vingine kama wana Astronomical club ili uweze kutumia telescope zenye nguvu kubwa ambazo kwa kawaida ni ghali sana kwa mtu binafsi kuzinunua.
 
Ina maana hiyo nyota iko mbali kiasi cha kwamba mwanga wake huchukua miaka 640 kutufikia.

Kwa kulinganisha tu, mwanga kutoka jua letu huchukua takriban dakika 8 kutufikia.

Sasa ukichukulia kuwa mwanga unasafiri katika kasi ya kilomita 1,080,000,000 kwa saa, unaweza kupiga mahesabu kujua huo umbali wa 640 light-years ni kilomita ngapi - ni mbali sana.

Mwaka una siku 365
Siku ina masaa 24

Kwa hiyo 640 light-years ni sawasawa na

640 x 365 x 24 x 1,080,000,000 = 606,000,000,000,000 kilomita = kilomita trillion 606 ndio umbali wa 640 light-years.

Na hii ipo karibu nasi. Kuna nyota na galaxies zilizoko thousands, millions, hata billions ya light-years kutoka hapa. Na hizo ni zile tunazoziona tu.

Ulimwengu ni mkubwa sana mkuu. Wewe kula ugali wako umshukuru muumba wako tu.
Mimi hua naamin ata kwenye hizo galaxy nyingne kuna viumbe wanaishi mkuu...Sitaki kuamini katika galaxy zote ni milk way tu ndo ina viumbe hai...!!

Wacha nikae nile ugali tu mkuu hahah

0404
 
mkuu kifyatu me huwa napenda sana kuangalia discovery channel ila kuna siku nilikuta mada ya anti matter bahati mbaya nilikuta kati muelezaji alikua michio kaku, na alisema tukiweza kutengeneza space vehicle inayotumia anti matter tunaweza tua achieve speed ya light na zaidi kwenye hiyo space vehicles hivyo kupelekea vyombo vyetu kufika kwenye nyota mbali mbali au sayari zinazozunguka nyota kwa muda mfupi, cha kushangaza alisema kuwa mpaka sasa hivi wanasayansi anti matter waliyotengeneza haijafika hata gram 1.

Je, hii anti matter ipoje? kweli physics ni pana sana kila siku mambo mapya yatakuja,hebu nielimishe hapa mkuu na je miaka ya, our descendants wataweza kutengeneza anti matter hata kufikia gram 500 hivi ili tuwe na anti matter space vehicles?
 
Mkuu jua ndio nyota kubwa kuliko zote. So a sun is a star too
Msaada zaidi: just google ''Sun"
Kwenye galaxy waweza kuwa sahihi lakini kiukweli jua ni miongoni mwa vinyota vidogo sana !nawewe tukuelekeze katika kusoma majarida documentary za kisayansi hasa astro physic sio kuishia kwenye muhtsari wa kivivu wa google na wikipedia
 
mkuu kifyatu me huwa napenda sana kuangalia discovery channel ila kuna siku nilikuta mada ya anti matter bahati mbaya nilikuta kati muelezaji alikua michio kaku, na alisema tukiweza kutengeneza space vehicle inayotumia anti matter tunaweza tua achieve speed ya light na zaidi kwenye hiyo space vehicles hivyo kupelekea vyombo vyetu kufika kwenye nyota mbali mbali au sayari zinazozunguka nyota kwa muda mfupi, cha kushangaza alisema kuwa mpaka sasa hivi wanasayansi anti matter waliyotengeneza haijafika hata gram 1,je hii anti matter ipoje? kweli physics ni pana sana kila siku mambo mapya yatakuja,hebu nielimishe hapa mkuu na je miaka ya, our descendants wataweza kutengeneza anti matter hata kufikia gram 500 hivi ili tuwe na anti matter space vehicles??
Katika sayansi ya particle physics (chembe chembe ndogo ndani ya atom) wanasayansi wameona uwezekano wa kuwepo na chembe (particles) zinazokinzana na chembe za kawaida. Tumejifunza kuwa atom ina
  • Protons
  • Neutrons
  • Electrons
Antimatter ina chembe zinazokinzana na hizi za kawaida
  • Anti-protons
  • Anti-neutrons
  • Positrons (Anti-electrons)

Ilivyo ni kuwa Antimatter ikikutana na matter ya kawaida basi zinajimaliza na matokeo yake ni nishati tupu kufuatia kanuni za Albert Einstein kuwa:
Nishati E = mC-squared.

Kwa hiyo kama una antimatter ya kutosha kwenye chombo cha usafiri angani basi kazi yake ni kumeza matter inayokutana nayo njiani na unapata nishati isiyokuwa na ukomo kwa safari yako. Tatizo ni kuwa mpaka sasa wanasayansi hawajaweza kuwa na antimatter ya uhakika (stable).

Cha muhimu kujua ni kuwa swala la antimatter limetoka kwenye nadharia na sasa kilichobaki ni sayansi tu ya kuikusanya ya kutosha. Hii ni kazi ngumu sana na sidhani kama sisi na vizazi vyetu vitabahatika kuweza kutumia hii nishati ya antimatter.
 
Sijui kwa Tanzania ni maduka gani zinapatikana. Lakini kwa kutumia telescope nzuri ya kawaida (kibei) unaweza kuona sayari zote lakini sio milima na mito. Utaiona sayari yenyewe na miezi inayoizunguuka au pete (rings) kama za Saturn. Unaweza kuona mabonde na milima ya mwezi wetu lakini sio ya sayari.

Ulizia UDSM au vyuo vingine kama wana Astronomical club ili uweze kutumia telescope zenye nguvu kubwa ambazo kwa kawaida ni ghali sana kwa mtu binafsi kuzinunua.
hiyo telescope ya kawaida ndo nnayoitaka mie sijui ntaipata wapi aisee
 
Ina maana hiyo nyota iko mbali kiasi cha kwamba mwanga wake huchukua miaka 640 kutufikia.

Kwa kulinganisha tu, mwanga kutoka jua letu huchukua takriban dakika 8 kutufikia.

Sasa ukichukulia kuwa mwanga unasafiri katika kasi ya kilomita 1,080,000,000 kwa saa, unaweza kupiga mahesabu kujua huo umbali wa 640 light-years ni kilomita ngapi - ni mbali sana.

Mwaka una siku 365
Siku ina masaa 24

Kwa hiyo 640 light-years ni sawasawa na

640 x 365 x 24 x 1,080,000,000 = 606,000,000,000,000 kilomita = kilomita trillion 606 ndio umbali wa 640 light-years.

Na hii ipo karibu nasi. Kuna nyota na galaxies zilizoko thousands, millions, hata billions ya light-years kutoka hapa. Na hizo ni zile tunazoziona tu.

Ulimwengu ni mkubwa sana mkuu. Wewe kula ugali wako umshukuru muumba wako tu.
Zaidi ya hapo. Tukisema nyota iko 640 light years away, maana yake tunavyoiona si pale ilipo leo bali ilipokuwa miaka 640 iliyopita.

Tunaiangalia nyota kama ilivyokuwa mwaka 1376 huku kwetu.

Kadiri kitu kinavyokuwa mbali zaidi ndivyo mwanga wake unavyochukua muda zaidi kutufikia.

Kadiri mwanga unavyochukua muda zaidi kutufikia ndivyo tunavyozidi kuona kitu si kama kilivyo sasa, bali kama kilivyokuwa zamani.

Kuna nyota nyingi tunazoziona angani sasa zimeshalipuka kwa mujibu wa saa iliyokuwa adjusted kwa relativity huku duniani, lakini sisi hatutajua hilo kwa mamia ama maelfu ya miaka, kwa sababu tukio la kulipuka kwa nyota hizo limefanyika katika kipindi ambacho ni kidogo zaidi ya kipindi ambacho mwanga unatumia kutufikia.

Kwa mfano. Tunavyoliangalia jua, hatulioni kama lilivyo hivi sasa. Tunaliona kama lilivyokuwa dakika nane na sekunde ishirini zilizopita. Kwa sababu mwanga kutoka kwenye jua unatumia dakika nane na sekunde ishirini kutufikia.

Kwa hiyo ikitokea jua lizimike mara moja sasa hivi, hatutajua kwa dakika nane na sekunde ishirini nzima. Litaonekana linaendelea kuwaka kama kawaida tu.

Sasa ukibadilisha dakika nane na sekunde ishini ziwe miaka 640 kwa nyota iliyo umbali wa light years 640 utaona nyota hii ikizimika leo (supernovae) hatutajua hili leo. Itaendelea kuwaka mpaka mwaka 2656. Watu watakaoishi mwaka 2656 ndio watakaoona hiyo supernovae itakayozima nyota hii. Kwa sababu mwanga wa kutoka nyota hii utachukua miaka 640 kutufikia.

Kuna nyota zimezimika jana lakini tutaendelea kuziona kwa mamia ya miaka.
 
Wazo zuri sana hilo mkuu. Kuna wanasayansi wanatafiti kuona kama kuna universe nyingine zaidi ya hii yetu. Inawezekana kukawa na multiple-universes au mbingu nyingi. Lako sio wazo la kupuuzwa hata kidogo. Ni aina hiyo ya fikra inayotengeneza wana sayansi waliokubuhu.

Kuna mbingu nyingi mno, na ndio maana Biblia Takatifu inasema 'Mbinguni' means kuna mbingu zaidi ya moja.
ila katika hizo zote, kuna Moja ambayo ndio Mbingu kuu, ALIPO MUNGU MKUU.
 
Zaidi ya hapo. Tukisema nyota iko 640 light years away, maana yake tunavyoiona si pale ilipo leo bali ilipokuwa miaka 640 iliyopita.

Tunaiangalia nyota kama ilivyokuwa mwaka 1376 huku kwetu.

Kadiri kitu kinavyokuwa mbali zaidi ndivyo mwanga wake unavyochukua muda zaidi kutufikia.

Kadiri mwanga unavyochukua muda zaidi kutufikia ndivyo tunavyozidi kuona kitu si kama kilivyo sasa, bali kama kilivyokuwa zamani.

Kuna nyota nyingi tunazoziona angani sasa zimeshalipuka kwa mujibu wa saa iliyokuwa adjusted kwa relativity huku duniani, lakini sisi hatutajua hilo kwa mamia ama maelfu ya miaka, kwa sababu tukio la kulipuka kwa nyota hizo limefanyika katika kipindi ambacho ni kidogo zaidi ya kipindi ambacho mwanga unatumia kutufikia.

Kwa mfano. Tunavyoliangalia jua, hatulioni kama lilivyo hivi sasa. Tunaliona kama lilivyokuwa dakika nane na sekunde ishirini zilizopita. Kwa sababu mwanga kutoka kwenye jua unatumia dakika nane na sekunde ishirini kutufikia.

Kwa hiyo ikitokea jua lizimike mara moja sasa hivi, hatutajua kwa dakika nane na sekunde ishirini nzima. Litaonekana linaendelea kuwaka kama kawaida tu.

Sasa ukibadilisha dakika nane na sekunde ishini ziwe miaka 640 kwa nyota iliyo umbali wa light years 640 utaona nyota hii ikizimika leo (supernovae) hatutajua hili leo. Itaendelea kuwaka mpaka mwaka 2656. Watu watakaoishi mwaka 2656 ndio watakaoona hiyo supernovae itakayozima nyota hii. Kwa sababu mwanga wa kutoka nyota hii utachukua miaka 640 kutufikia.

Kuna nyota zimezimika jana lakini tutaendelea kuziona kwa mamia ya miaka.
mkuu supernova ya mwisho ilitokea lini na kwanini inaweza kukatika miaka hatuoni supernova wakati zipo nyota zilishazeeka tokea miaka mingi nyuma ambapo kwa miaka hii tuliopo kwa speed ya mwanga wake tugeshuhudia supernova nyingi tu?
 
hiyo telescope ya kawaida ndo nnayoitaka mie sijui ntaipata wapi aisee
Kwa sasa sipo Tanzania lakini unaweza kuzipata kwenye internet. Telescope nzuri zinaanzia kama Tsh laki moja hivi. Lakini ukishop around kutoka China au India unaweza kupata bei nzuri.
 
Zaidi ya hapo. Tukisema nyota iko 640 light years away, maana yake tunavyoiona si pale ilipo leo bali ilipokuwa miaka 640 iliyopita.

Tunaiangalia nyota kama ilivyokuwa mwaka 1376 huku kwetu.

Kadiri kitu kinavyokuwa mbali zaidi ndivyo mwanga wake unavyochukua muda zaidi kutufikia.

Kadiri mwanga unavyochukua muda zaidi kutufikia ndivyo tunavyozidi kuona kitu si kama kilivyo sasa, bali kama kilivyokuwa zamani.

Kuna nyota nyingi tunazoziona angani sasa zimeshalipuka kwa mujibu wa saa iliyokuwa adjusted kwa relativity huku duniani, lakini sisi hatutajua hilo kwa mamia ama maelfu ya miaka, kwa sababu tukio la kulipuka kwa nyota hizo limefanyika katika kipindi ambacho ni kidogo zaidi ya kipindi ambacho mwanga unatumia kutufikia.

Kwa mfano. Tunavyoliangalia jua, hatulioni kama lilivyo hivi sasa. Tunaliona kama lilivyokuwa dakika nane na sekunde ishirini zilizopita. Kwa sababu mwanga kutoka kwenye jua unatumia dakika nane na sekunde ishirini kutufikia.

Kwa hiyo ikitokea jua lizimike mara moja sasa hivi, hatutajua kwa dakika nane na sekunde ishirini nzima. Litaonekana linaendelea kuwaka kama kawaida tu.

Sasa ukibadilisha dakika nane na sekunde ishini ziwe miaka 640 kwa nyota iliyo umbali wa light years 640 utaona nyota hii ikizimika leo (supernovae) hatutajua hili leo. Itaendelea kuwaka mpaka mwaka 2656. Watu watakaoishi mwaka 2656 ndio watakaoona hiyo supernovae itakayozima nyota hii. Kwa sababu mwanga wa kutoka nyota hii utachukua miaka 640 kutufikia.

Kuna nyota zimezimika jana lakini tutaendelea kuziona kwa mamia ya miaka.
Asante mkuu kwa ufafanuzi mzuri zaidi.
 
Kuna mbingu nyingi mno, na ndio maana Biblia Takatifu inasema 'Mbinguni' means kuna mbingu zaidi ya moja.
ila katika hizo zote, kuna Moja ambayo ndio Mbingu kuu, ALIPO MUNGU MKUU.
Inawezekana ingawaje mimi sina ujuzi wa maandiko matakatifu.
 
Back
Top Bottom