Ufahamu kuhusu nyota za angani

Mwamba028

JF-Expert Member
Nov 15, 2013
4,546
3,545
Napoangaliaga angani wakati wa usiku huwa naona nyota zingine ambazo hazina mwanga wa rangi moja,yan inabadilika badilika mara nyekundu,kijan,bluu.
Je hizi nyota ni za aina gani? mana kuna mtu katika stori za utoto alinambia eti zile ni satelaiti
Pia nyota chanzo chake cha mwanga ni kipi?
Karibuni wadau wa Sayansi ya anga

Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakini ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au, jua liko umbali wa 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (kwenye constellation ya Centaurus) ambayo iko umbali wa 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa majua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko uzito wa atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haipotei bali hubadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni ya mkulu Albert Einstein kuwa E=mC2. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fission) atom nzito kama za Urani (Uranium). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fission ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua kupitia fusion.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary-stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wave-length ya rangi ya bluu.) Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wave-length ndefu (wave-length ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, Nyekundu na bluu . Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowasilisha mada yake kwenye kongamano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawasilisha.

I am sorry if this is an overkill.

Kama nilivyo ahidi ifuatayo ni ile nyongeza.

Nyota zinazaliwaje?
Kabla ya nyota kuzaliwa inaanza kama sayari ya kawaida wakati vumbi na hewa (sana sana hydrogen) ikijikusanya. Kadri hii hewa na vumbi vinavyoongezeka basi gravity nayo pia inaongezeka. Tukichukulia ukubwa/uzito wa jua letu kama kiwango (solar-mass) basi mkusanyiko wowote ule wa vumbi na hewa chini ya 0.013 solar-mass (1.3% ukubwa wa jua letu) hiyo itakuwa ni sayari (planet) tu. Kuanzia ukubwa wa 0.08 solar-mass na kuendelea gravity inakuwa kubwa sana (kilo moja hapa duniani ukiipeleka huko itakuwa na uzito wa kilo bilioni 100 na zaidi). Huu mgandamizo mkubwa wa gravity unafanya joto kupanda zaidi ya nyuzi milioni 15 celcius. Hili joto na mgandamizo wa gravity ndio kibiriti kinachofanya hydrogen ichanganyike ketengeneza helium na kutoa nguvu hizi za nyuklia (fusion). Hivi ndio jua linavyozaliwa.

Nyota zinakufaje?
Maisha ya nyota yanategemea sana na ukubwa wake. Nyota ndogo zinaishi muda mrefu sana (zinachoma hydrogen yake taratibu taratibu) kuliko nyota kubwa. Kwa mfano, nyota ndogo kama jua letu inategemewa kuwaka kwa miaka bilioni 10 wakati nyota kubwa sana kama Betelgeuse zinategemewa kuwaka kwa miaka million 10 tu.

Wakati nyota inawaka kunakuwa na uwiano (equilibrium) wa nguvu ya gravity na nyuklia. Gravity inakandamiza chini wakati milipuko ya nyuklia inasukuma vitu nje. Uwiano huu unaendelea hata baada ya hydrogen ikiisha. Baada ya hydrogen kuisha helium nayo italipuka kinyuklia kutengeneza Carbon na Oxygen. Baadae carbon nayo italipuka kunyuklia kutengeneza iron (chuma). Mara tu nyota inapoanza kutengeneza chuma (iron), mchezo umekwisha. Chuma ni kama maji yanayouzima huu mlipuko wa nyuklia mara moja. Milipuko ya nyuklia ikiacha, ule uwiano (equilibrium) wa gravity na nyukilia unakuwa haupo tena na gravity inashinda. Kila kitu huanguka chini na mlipuko mkubwa sana wa mwisho hutokea na mwanga mkubwa sana (super nova) huonekana.

Vitu viwili vinatokea wakati wa hii super nova. Kwanza, madini nzito zaidi ya chuma (iron) yanatengenezwa kama vile dhahabu, urani, nk. Hii ndio maana dunia yetu pamoja na sisi tunaitwa vumbi la nyota (star dust) kwa saababu kama hizi super nova zisingetokea basi dunia yetu na sisi tusingekuwepo. La pili linaliotokea baada ya kishindo (collapse) ni kuwacha tumba (core) ndogo sana lakini yenye uzito (density) mkubwa wa ajabu. Hii tumba ndio ijulikanayo kama BLACK HOLE.

(For correctness sake, not all stars die and turn into black holes. For instance, our sun is too small to turn into a black hole. When it dies it will collapse into a dense core with properties nowhere close to those of black holes)

Black holes na makaburi ya nyota.
Black holes zinazotokea baada ya nyota kubwa sana (super massive stars) ku-collapse ni vitu vya ajabu sana. Chupa moja ya bia (ujazo wa 0.5 lita) ya hii black-hole ina uzito wa zaidi ya tani 3,000,000,000,000. Gravity inayotokana na hizi black holes ni kubwa kiasi ya kumeza kitu chochote kile (majua, sayari, nk) kinachoikaribia. Hii gravity ni kubwa kiasi cha kumeza hata mwanga (even light cannot escape it) na ndio maana zinaitwa BLACKHOLE kwa sababu hazionekani (mwanga pia unamezwa). Kuwepo wa black hole kunajulikana tu kwa vitu inavyovimeza au vinavyo izunguuka. Usiku ukitoka nje angalia juu. Ukiona ukanda wa nyota nyingi basi huo ndio mkusanyiko wetu wa nyota (Galaxy yetu) unaoitwa MILKYWAY. Katikati ya hii galaxy yetu lipo hili black hole moja ambalo jua letu na nyota nyingine zote zilizopo kwenye hii galaxy yetu zinalizunguuka. Ukitaka kujua hii blackhole yetu iko wapi angalia juu na kama unaijua constellation ya Virgo basi usawa huo ndipo lilipo.

Natumaini hii itasaidia pa kuanzia katika kuzijua nyota.

cc. Mwamba028, 2013 Globu
Iron Lady
 
Nyota zinajizalishia mwanga zenyewe bila kutegemea kutoka kwenye biggest star[ Sun]. Kila nyota inazungukwa na sayari nyingi tu. Kwa sisi galaxy yetu inaitwa milky way galaxy ambapo ndipo inapopatikana sayari yetu ya dunia.

Kiufupi kuna billions of stars na kupelekea kuwepo kwa billions of billions of planets. Zingine ziko kwenye galaxy za mbali ambapo kuzifikia itamchukua binadamu light years [ miaka isiyohesabika/billion of years]. Na nyota zingine hatuwezi kuziona kwa macho bila msaada wa telescope.

Ni kweli zingine zinazooneka juu ni setelite.
 
Napoangaliaga angani wakati wa usiku huwa naona nyota zingine ambazo hazina mwanga wa rangi moja,yan inabadilika badilika mara nyekundu,kijan,bluu.
Je hizi nyota ni za aina gani? mana kuna mtu katika stori za utoto alinambia eti zile ni satelaiti
Pia nyota chanzo chake cha mwanga ni kipi?
Karibuni wadau wa Sayansi ya anga

Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakini ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au, jua liko umbali wa 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (kwenye constellation ya Centaurus) ambayo iko umbali wa 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa majua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko uzito wa atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haipotei bali hubadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni ya mkulu Albert Einstein kuwa E=mC2. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fission) atom nzito kama za Urani (Uranium). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fission ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua kupitia fusion.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary-stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wave-length ya rangi ya bluu.) Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wave-length ndefu (wave-length ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, nyekundu na bluu. Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowasilisha mada yake kwenye kongamano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawasilisha.

I am sorry if this is an overkill.
 
Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakizi ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au liko 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (constellation ya Centaurus) ambayo iko 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa mjua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haupotei bali unabadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni za mkulu Albert Einstein kuwa E=mC[SUP]2[/SUP]. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fision) atom nzito kama za Urani (Uraniun). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fision ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wavelength ya rangi ya bluu. Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wavelength ndefu (wavelength ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, Nyekundu na bluu . Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowakilisha mada yake kwenye mkutano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawakilisha.

I am sorry if this is an overkill.

Mkuu asante kwa udadavuzi mzuri na wa hali ya juu. Ningeomba utudadavulie kidogo hapo kwenye uranium na nguvu za nyukria
 
Nyota zinajizalishia mwanga zenyewe bila kutegemea kutoka kwenye biggest star[ Sun]. Kila nyota inazungukwa na sayari nyingi tu. Kwa sisi galaxy yetu inaitwa milky way galaxy ambapo ndipo inapopatikana sayari yetu ya dunia.
Kiufupi kuna billions of stars na kupelekea kuwepo kwa billions of billions of planets. Zingine ziko kwenye galaxy za mbali ambapo kuzifikia itamchukua binadamu light years [ miaka isiyohesabika/billion of years]. Na nyota zingine hatuwezi kuziona kwa macho bila msaada wa telescope.
Ni kweli zingine zinazooneka juu ni setelite.

Jua ni star ndiyo lakini siyo the biggest star mkuu!Ila jua ni nyota iliyo karibu zaidi na dunia

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakizi ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au liko 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (constellation ya Centaurus) ambayo iko 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa mjua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haupotei bali unabadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni za mkulu Albert Einstein kuwa E=mC[SUP]2[/SUP]. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fision) atom nzito kama za Urani (Uraniun). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fision ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wavelength ya rangi ya bluu. Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wavelength ndefu (wavelength ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, Nyekundu na bluu . Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowakilisha mada yake kwenye mkutano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawakilisha.

I am sorry if this is an overkill.

Duuuh! Kwel hyo ni overkill mzee,,shukrani sana kwa mchango wako,uko deep mkuu,,basi binadamu tumeumbwa kwa mfano wa ajabu sana,tuna uwezo wa kuona kitu ambacho kiko a million no of years to reach it. God is great
 
Vp kuhusu mwezi nao,,nao una enegy yoyote mana mwezi pia hubadilika,siku nyingine unaouona mwekundu,siku nyingine km wa kijani fulan ya kung'aa,siku nyingne una rang nyeupe ya kufifia,wakuu mwezi una any source of energy?na nn kinafanya mwez uwe na rang na size tofaut tofauti
 
@ MTANGOO mi shabiki wako mkubwa khs mambo ya nyota na huwa napenda sana masomo yako unayodadavua khs nyota for a first time niliku note kupitia media ulikuwa na kipindi kihusianacho na nyota ulikuwa ukii host usiku kama sikosei ni saa 4mpk5 ndo nikawa nakupata(nakuelewa) vizuri,unakaribishwa hapa.Hili dimba lina kuhusu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
afadhali nimeuona huu uzi hata mimi huwa na swali najiuliza siku zote kuhusu nyota, hivi ni kweli zina umbo kama ambavyo tunazichora (kwa maana ya star shape) hata huko angani zilipo au ni za duara, au umbo lake likoje, naomba kufahamishwa kwa anayefahamu?
 
Mkuu jua ndio nyota kubwa kuliko zote. So a sun is a star too
Msaada zaidi: just google ''Sun"

There are quite a number of stars bigger than the Sun. In July 2011, a huge star approximately 320 times the size of the sun was discovered. Stars appear to be small because of their great distance from the Earth. The Sun is the nearest star to the Earth.
 
Ukichunguza utakuta Huyu ni mwalimu anayefundisha taifa la kesho.

kaongea kweli tupu Nivea

There are quite a number of stars bigger than the Sun. In July 2011, a huge star approximately 320 times the size of the sun was discovered. Stars appear to be small because of their great distance from the Earth.

The Sun is the nearest star to the Earth.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom