Hakuna juu wala chini. Popote ulipo ule upande unaovutwa na gravity ya dunia ndio chini (kwa sababu vitu vinaanguka kuelekea chini) na ule upande mwengine ndio juu. Mfano, kama kuna watu wawili, mmoja yuko north pole na mwengine yuko south pole. Upande anaouita juu alieko north pole basi utakuwa ni chini kwa alie south pole.Mkuu Kifyatu mi naomba unifafanulie kidogo kuhusu ulimwengu ulivyo,maana tunaambiwa ulimwenguni kuwa hakuna juu wala chini,japo sisi tunaliangalia jua kwa juu,mwezi kwa juu na sayari zote na vikorokoro vyote tunaviangalia kwa juu hapo ndipo ninapotatizwa ufafanuzi tafadhari.
Watu wanavutwa kuelekea katikati ya dunia. Kwa hiyo popote ulipo duniani upande unaoelekea katikati ya dunia ndio chini na ule mwengine ndio juu.