Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ndio imegunduliwa tu kwa hiyo bado hatujajua kama kweli itaelezea dark matter na dark energy au la. Lakini sisi sasa tuko kiti cha mbele kabisa katika sayansi kuona ni nini kinakuja. Very exciting.
Mkuu Kifyatu hii nguvu mpya ina faida gan kwenye maisha ya kawaida km inavyo Fahamika Kwa electromagnetic,nyukria fission na matumizi yao Ila hii nguvu mpya ukiachana na kuchunguza kuhusu ulimwengu inaweza kuwa na matumizi gan kwenye day to day life!!!?
 
Kifyatu unaamini ama uliwahi sikia kuna wanasayansi wa mambo yaanga walifanya uchunguzi wao na kuishia kusema KWELI MUNGU YUPO??
 
Mkuu Kifyatu hii nguvu mpya ina faida gan kwenye maisha ya kawaida km inavyo Fahamika Kwa electromagnetic,nyukria fission na matumizi yao Ila hii nguvu mpya ukiachana na kuchunguza kuhusu ulimwengu inaweza kuwa na matumizi gan kwenye day to day life!!!?
Swali gumu hili mkuu.

Hii nguvu kama ipo tayari inatuathiri kwa njia moja ua nyingine. Matumizi yake yatakuja baadae. Ni kama Magnetism ilivyogunduliwa hakuna aliejua kuwa itatumika kutengenezea motors, kuzalisha umeme, telecommunications (simu, TV, internet), x-rays, na taaluma zote zinategemea matumizi ya hii magnetism. Tusubiri tu mkuu. Ndio tumefungua tu mlango unaoingia katika nguvu hii mpya. Matumizi yake yatakuja tu. Pengine matumizi yake yasije katika uhai wetu lakini yatakuja.
 
Baadhi ya nyota unazoziona si zote ni nyota zingine ni sayari,ukiamka alfajiri sana kuanzia saa 10 hadi saa 12,kuna nyota huwa zinang'aa sana na kubwa mno kuliko zingine zote,huwa hazizidi mbili,zile ni sayari,hata dunia tuliyomo nayo ni sayari,maajabu ni kwamba ukienda kwenye
Hili lina utata kdg lbd ni kutokana na upeo wng mdogo pengine ningeomba udadavuzi zaidi ktk hii hoja...sayari inawezaje kuwa na mwanga kiasi cha sisi huku tuliopo billions km away kuweza kuziona km nyota vile??
 
Kifyatu unaamini ama uliwahi sikia kuna wanasayansi wa mambo yaanga walifanya uchunguzi wao na kuishia kusema KWELI MUNGU YUPO??
Hapana!

Lakini najua kuwa wanasayansi, kama Higg, wamegundua (na kuthibitisha kuwepo kwa) Higgs Boson ambayo kazi yake ni kuumba (create) matter. Sasa tujuavyo katika dini ni kuwa muumba vitu vyote ni Mungu. Kama hii Higgs boson inaumba basi itakuwa na uhusiano na Mungu. Hii ndio sababu ya Higgs boson kuitwa God-particle.

Kwangu mimi ni uthibitisho wa kisayansi kuwa kuumba (creation) kunawezekana. Huu uumbaji unaweza usiwe kama unavyoelezwa kwenye vitabu vitakatifu (kama Bibilia au Qur'an) lakini ulitokea. Kama unataka kuuita huu uumbaji kuwa ni uthibitisho wa kisayansi wa kuwepo kwa Mungu, unaweza. Mimi sitaki kufika mbali kiasi hicho.
 
JE DARK MATTER IMEGUNDULIWA?
ni:

[*]Strong Nuclear Force
[*]Weak Nuclear Force

Kifyatu Nakosa swali la kuuliza ila nadhani ni dhana mpya Kwangu kuwa na hizi Nuclear force
Nini tofauti zao japo majibu unaweza sema Moja ina nguvu saana nyingine nguvu kidogo
Inakuwaje zinakuwa na nguvu tofauti wakati zote ni Nuclear
Kwenye weak Nuclear huwez kuweka Catalyst kuifanya ikawa strong??
Hizi uranium ndo zinatoa Nuclear power je kuna tofauti kati Nuclear inayotolewa na uranium na Nuclear inayolipuka mfmo Nuclear ya jua??.
Nisamehe Kwa swali langu
 
Hili lina utata kdg lbd ni kutokana na upeo wng mdogo pengine ningeomba udadavuzi zaidi ktk hii hoja...sayari inawezaje kuwa na mwanga kiasi cha sisi huku tuliopo billions km away kuweza kuziona km nyota vile??
Sasa hivi ikifika jioni wakati jua linazama ukiangalia magharibi utaona nyota inayowaka sana kabla ya nyota nyingine kutoka. Hii sio nyota bali ni sayari ya Venus. Na asubuhi kukipambazuka kuna nyota (ya mwisho kufifia) inayowaka sana mashariki, hii siyo nyota bali ni sayari ya Mercury.
 
Weak nuclear force ndiyo inayosababisha radioactive decay inayofanya nuclear material ku-deteriorate.
Strong nuclear force ndiyo inayozishikilia protons na neutrons pamoja katika kiini (nucleus) cha atoms.
 
Weak nuclear force ndiyo inayosababisha radioactive decay inayofanya nuclear material ku-deteriorate.
Strong nuclear force ndiyo inayozishikilia protons na neutrons pamoja katika kiini (nucleus) cha atoms.
mkuu nina swali kuhusu atoms kama kila kitu kimeundwa na atoms why kuna vyenye uhai na visivyokua na uhai mfano wanyama na mawe wakati vimeundwa na mkusanyiko wa atoms zilezile? au kuna atom zenye uhai na zisizo na uhai... swali la pili chembechembe za mwanga nazo ni atoms? kwanini zinatembea speed kubwa sana? samahani kama nitakua nimetoka nje ya mada
 
Swali zuri sana mkuu na wala usiombe radhi. Niko tayari kukuingiza ndani ya ulimwengu wa Kifyatu. Nami nakuomba radhi kwa jibu refu.

Kuna makundi ya aina tatu ya watu:
  1. Wanaoamini uwepo wa Mungu - Theists
  2. Wasioamini uwepo wa Mungu - Atheists
  3. Wasiojua na wanatafuta ukweli uko wapi - Agnostics
Wana sayansi wengi wapo kwenye hili kundi la tatu - Agnostics. Mimi ni agnostic mmojawapo.

Universe:
Unajua, ukiangalia ukubwa wa, na complexity ya, huu uimwengu wetu bado huwezi kuuelezea, hata kwa kutumia sayansi, kuwa ulianzaje. Kulikuwa na nini kabla ya big bang? Je hii Higgs boson (wanaiita God particle) ni ishara ya kisayansi ya uwepo wa Mungu? Unaona. Kuna maswali mengi sana ambayo sayansi bado haiwezi kuyajibu. Kwa hiyo mwanasayansi yeyote yule anaesema yeye ana uhakika Mungu hayupo basi huyo ninamtilia mashaka na hiyo elimu yake.

Dini:
Mimi naziona dini kama vyama vile. Kila moja inavutia upande wake na kujigamba kuwa wao wanamuelewa Mungu kiundani kuliko wengine na kutoa masharti chungu tele ya kuwa muumini. Mimi nimeamua kutoyumbishwa na hizi dini mbalimbali na maelezo yao. Sasa ukiangalia composition ya dini unakuta ina sehemu mbili.

Dini = Spirituality (matumaini au hope au "ucha mungu") + Culture (mila na desturi)

Spirituality ni ile hali ya kuwa na matumaini kuwa utafanikiwa. Hata watu wasio na dini lakini wakiwa katika matatizo watategemea kuwa miujiza (mizimu, lady luck, n.k.) itatokea wasalimike. Watu hawa pia watanunua tiketi za bahati-nasibu wakitegemea watakuwa na bahati siku hiyo ya kushinda. Hii hali ya matumaini kuwa kuna kitu kitaiingilia kutatua matatizo yako ndio SPIRITUALITY.

Kwa wale wenye dini basi hii spirituality wanailinganisha na uwepo wa Mungu mwenye uwezo wote. Binadamu wote wanayo hii spirituality (awe na dini au sio). Ndio njia kuu ya sisi binaadamu tunayotumia kupambana na matatizo ya maisha kisaikolojia (coping mechanism).

Culture au mila/desturi ndiyo inayotengeneza dini.
  • Uislam = Spirituality + mila za kiarabu
  • Ukristo = Spirituality + mila za kizungu/kiyahudi
  • Judaism = Spirituality + mila za kiyahudi
  • Na kadhalika.
Kwa hiyo ukiondoa mila/desturi katika hizi dini basi dini zote zitafanana. Jaribu kufikiria.

Kwa mfano, kama wewe ni mwarabu basi mila/desturi za kabila lako ndio hizo hizo mila/desturi za dini yako. Ikiwa hivyo basi dini kwako ndio mwenendo wa maisha (a way of life) na hujilazimishi. Kwa wengine wote inabidi tujilazimishe tu (kuvaa hijab, kuswali ukielekea Makkah kwa kiarabu, kutokula nguruwe, n.k.) ili tuwe waislam.

Mara nyingi ufuasi wa dini unategemea ulivyokuzwa. Hata wanasayansi, kama wamekuwa katika familia zenye misimamo mikali wa kidini wataamini uwepo wa Mungu kufuatilia imani walizokuzwa nazo.

Mimi:
Hivyo basi mimi katika maisha yangu ni Spiritual lakini sio Religious. Hiki ndicho nilichomaanisha niliposema "sina dini".

Natumaini umenielewa.
Mkuu Kifyatu naomba kutofautiana na wewe katika masuala mawili.
1. Uwepo wa Mungu
2. Spirituality.
Currently niko mobile, nipe masaa machache nikikaa nitaandika.
 
Mkuu Kifyatu mi naomba unifafanulie kidogo kuhusu ulimwengu ulivyo,maana tunaambiwa ulimwenguni kuwa hakuna juu wala chini,japo sisi tunaliangalia jua kwa juu,mwezi kwa juu na sayari zote na vikorokoro vyote tunaviangalia kwa juu hapo ndipo ninapotatizwa ufafanuzi tafadhari.
 
Swali ni kwanini jua linapoanza kuchomoza huwa halina mwanga mkali na jinsi linavyozidi ndio mwanga huwa mkali na pia likaanza kuishia huwa linaanza kupungua ule mwanga mkali????
 
mkuu nina swali kuhusu atoms kama kila kitu kimeundwa na atoms why kuna vyenye uhai na visivyokua na uhai mfano wanyama na mawe wakati vimeundwa na mkusanyiko wa atoms zilezile? au kuna atom zenye uhai na zisizo na uhai... swali la pili chembechembe za mwanga nazo ni atoms? kwanini zinatembea speed kubwa sana? samahani kama nitakua nimetoka nje ya mada
Mkuu hata siku moja usiombe samahani kwa kuuliza swali. Hakuna swali la kijinga bali majibu ya kijinga.

Atom ndio sehemu ndongo inayotengeneza vitu (matter). Sasa hizi atoms zinaweza kujiweka katika mpangilio fulani na ukapata kitu tofauti kabisa. Kwa mfano, atom za carbon zikijipanga katika mfumo wa mabapa (flat structures) unapata graphite (yani penseli) ambayo ni laini sana lakini carbon atoms hizo hizo zikijipanga kama pyramids basi unapata almasi ambayo ni ngumu kuliko vitu vingine.

Sasa atom za aina moja zinaweza kuungana na za aina nyingine kutengeneza molecules zenye sifa tofauti. Kwa mfano, Nitrogen, Hydrogen na Oxygen zinaweza kuchanganyika na kutengeneza molecules zijulikanazo kama Amino Acids. Hizi amino acids ndizo molecule za kwanza kuwepo kabla uhai haujatokea. Hizi ndizo zinazojenga viumbe hai.

Kwa hiyo, katika kujibu swali lako, atoms hazina uhai bali atoms za elements tofauti vinaweza kujipanga na kutengeneza molecule zinazoweza kuanzisha uhai.

Mwanga (au photons) ni baadhi ya chembe chembe (sub-atomic particles) kama zilivyo bosons, neutrinos, electrons, n.k. Photons zina uzito karibu na sifuri na sub-atomic particles za aina hii (kama neutrinos) huwa zinasafiri kwa kasi kubwa. Sijui kwa nini zinafanya hivi bali hiyo ndiyo sifa yake.
 
Mkuu Kifyatu naomba kutofautiana na wewe katika masuala mawili.
1. Uwepo wa Mungu
2. Spirituality.
Currently niko mobile, nipe masaa machache nikikaa nitaandika.
Napenda sana watu wenye fikra tofauti na mimi. Hii ndio njia ninayotumia kujifunza. Nakusubiri.
 
Back
Top Bottom