Ufahamu kuhusu nyota za angani

Mkuu hivi dunia inagravity yake? Jua lina gravity yake? Na mwezi pia unagravity yake? If yex kwanini gravity ya jua haiathiri kujaa na kukupwa kwa maji?
Kila kitu chenye mass (hata wewe na mimi) kina gravity yake. Kwa hiyo jua, mwezi, nyota, sayari vyote vina gravity zao.

Gravity ni nguvu (Force) kati ya (tuseme) dunia (yenye mass M1) na kitu kingine kama mwezi (wenye mass M2). Hii force (F) inategemea na umbali kati yao (tuuite R).

Gravity force F = (GxM1xM2)/Rsquared

G ni gravitational constant

Gravity ya jua ndio inayotufanya tulizunguuke na kuwa na majira tofauti.
 
Nashukuru sana wakuu kwa kufatilia uzi huu mengi nimelimika, awali niliona maelezo kuwa nyoto hutoa rangi tofauti kama blue, green, red hicho nimefanikiwa kukiona pia nimejifunza kuhusu binary stars (nyoto pacha) zina spiin light na kutoa wave length zenye kutembea kwa speed, naomba kupata elimu huwaga siku za mawingu au mvua ndogo ndogo naona kitu ambacho tumezoe kukiita upinde (Rambow) ikiwa inajitokeza ktk blue sky(mawingu) naomba kufahamu inafanyikaje? Na Je inahusiana na zile nyota kuspiin light

Upinde wa mvua - rainbow:
Mwanga wa jua (mweupe) tunaouona huwa ni mchanganyiko wa rangi nyingi (Violet, Indigo, Blue, Green, Yellow, Orange, Red). Sasa kama jua linawaka na mvua inanyesha, yale matone ya maji yanakuwa kama vioo (lens au prisms) na yanasambaza mwanga mweupe wa jua kwenye hizo rangi tofauti.
 
View attachment 318903Tazama hii sketch apa hizo ni sayari ambazo kila moja ina mzunguko wake binafsi na kila moja inazunguka jua kwa muda wake tofauti, Mchana na usiku ni matokeo ya dunia kuzunguka katika muhimili wake na mwaka ni dunia kuzunguka jua
Kupitia mchoro huu hivi kwanini hatutafautiani siku na tarehe, ikiwa sayari inajingusha yenyewe kulinguka jua na ndio matokeo ya usiku na mchana, kama vile tunavyotafautiana masaa? Je hii internationa date line zigzag yake ipoje?
 
Majibu:
  1. Uzito mdogo kwenye Mars sio tatizo bali viumbe vitakavyoishi huko vitakuwa na mifupa na musuli hafifu (density).
  2. Uzito sio tatizo bali hakuna hewa ya Oxygen wala maji yanayotiririka kama hapa.
  3. Mwaka wa dunia ni siku zetu 365, mwaka wa Mars ni siku zetu 687. Siku ya dunia yetu ni masaa 24, siku ya Mars ni masaa 24 na dakika 40.
  4. Mars haina pete kama ilivyo Saturn isipokuwa ina miezi miwili Phobos na Deimos. Inatabiriwa kuwa siku za usoni hii miezi inaweza kupigwa dhoruba na vimondo na kuwa vumbi ambalo linaweza kutengeneza pete kama ilivyo Saturn. Kitu hicho kinaweza kutokea hapa kwetu pia kama mwezi wetu utapigwa na dhorubwa kubwa hivyo.
 
Kifyatu Mkuu niambie zaidi kuhusu voyages zilipo fika na taarifa ambazo zimeleta. hapa dunian....je zinaleta taarifa kwa wakati au taarifa zinachelewa Ikifika kutokana na umbali???

2.ikitokea zikakamatwa na another being kwenye universe je tuna namna ya kufahamu!!,

Nin nature ya mission yao!!
Neo
Mkuu Kifyatu umenisahau
 
Mkuu Kifyatu umenisahau.

Kifyatu Mkuu niambie zaidi kuhusu voyages zilipo fika na taarifa ambazo zimeleta. hapa dunian....je zinaleta taarifa kwa wakati au taarifa zinachelewa Ikifika kutokana na umbali???

2.ikitokea zikakamatwa na another being kwenye universe je tuna namna ya kufahamu!!,

Nin nature ya mission yao!!
Neo
Mkuu samahani. Naona nilipitiwa. Nilidhani nimekujibu.

Voyager1 na Voyager2 zilirushwa mwaka 1977 (September 5, na August 20) zikiwa na majukumu mawili kila chombo.

Voyager 1
Jukumu la kwanza:
Kutembelea na kuzichunguza sayari za Jupiter, Saturn (na mwezi wa Saturn uitwao Titan).

Jukumu la pili:
Kuendelea na safari mpaka kutoka nje ya solar system yetu (Heliosphere) na kutuma taarifa za anga la huko.

Iko wapi kwa sasa (May 2016):
Iko kwenye Interstellar space zaidi ya km 21,000,000,000 kutoka hapa. (Ni sawa na umbali wa duniani mpaka kwenye jua mara 136).

Bado inawasiliana nasi?
Ndio. Huchukua takriban masaa 20 hivi kwa ujumbe kutoka Voyager1 kutufikia kupitia mtandao wa Deep-Space-Network.

Lini mwisho wa hii mission?
Nishati ya hiki chombo inapatikana kwa jenerata la nuclear. Inakadiriwa ifikapo mwaka 2025 hili jenerata litaishiwa nguvu na hapo ndio itakuwa mwisho wa mission hii.

Je kikikamatwa na aliens?
Kama watakikamata kabla ya 2025 basi kitatufahamisha. Wakikikamata baada ya 2025 basi tena ndio tutakuwa tumeula.

*******************************************************
Voyager 2
Jukumu la kwanza:
Kutembelea na kuzichunguza sayari za Jupiter, Saturn (na mwezi wa Saturn uitwao Titan), Uranus na Neptune.

Jukumu la pili:
Kama la Voyager1

Iko wapi kwa sasa (April 2016):
Iko kwenye ukingo wa heliosphere zaidi ya km 17,000,000,000 kutoka hapa. (Ni sawa na umbali wa duniani mpaka kwenye jua mara 110).

Bado inawasiliana nasi?
Ndio. Huchukua takriban masaa 17 hivi kwa ujumbe kutoka Voyager2 kutufikia kupitia mtandao wa Deep-Space-Network.
 
Sante mkuu Kifyatu ,
Niambie kuhusu hii vibtation of black hole ambazo zimekuwa detected!, izo vibration ni nini na tunategemea nini kujifunza au kutengeneza kutokana huo ugunduzi!
 
Sante mkuu Kifyatu ,
Niambie kuhusu hii vibtation of black hole ambazo zimekuwa detected!, izo vibration ni nini na tunategemea nini kujifunza au kutengeneza kutokana huo ugunduzi!
Albert Einstein alifanya mahesabu yake na kugundua kuwa nguvu ya gravity ni sawa na mkunjo (curvature) katika mkeka wa space-time (space-time fabric). Pia hesabu zake zilitabiri kuwa kukitokea msituko kwenye mkeka huu basi mawimbi yake yatasambaa kwenye mkeka kama ambavyo mawimbi ya maji yanavyosambaa kutoka pale unapotupia jiwe au kitu kizito.

Blackhole ni sawa na mkunjo mkubwa sana katika huu mkeka. Sasa black-holes mbili zikigongana basi zinaufanya huu mkeka utetemeke sawasawa na bahari itakavyo tengeneza mawimbi (kama sunami) endapo mwamba mkuwa utatumbukizwa majini. Haya mawimbi yatasambaa kwenye mkeka wote. Ni haya mawimbi ndiyo yaliyokuwa detected kama vibrations.
 
Albert Einstein alifanya mahesabu yake na kugundua kuwa nguvu ya gravity ni sawa na mkunjo (curvature) katika mkeka wa space-time (space-time fabric). Pia hesabu zake zilitabiri kuwa kukitokea msituko kwenye mkeka huu basi mawimbi yake yatasambaa kwenye mkeka kama ambavyo mawimbi ya maji yanavyosambaa kutoka pale unapotupia jiwe au kitu kizito.

Blackhole ni sawa na mkunjo mkubwa sana katika huu mkeka. Sasa black-holes mbili zikigongana basi zinaufanya huu mkeka utetemeke sawasawa na bahari itakavyo tengeneza mawimbi (kama sunami) endapo mwamba mkuwa utatumbukizwa majini. Haya mawimbi yatasambaa kwenye mkeka wote. Ni haya mawimbi ndiyo yaliyokuwa detected kama vibrations.
Ahsante Kifyatu nini mategemeo kwenye huu ugunduzi???.
Maana habari za mtaan zinasema we can know universe zaidi coz we can traval through izo vibrations ambazo zina speed kubwa kuliko mwanga!!!...
Zaid wanasema izo vibration zinaweza elezea zaid ya uumbwaji wa ulimwengu!,

Tell me more kikombe changu nimemwaga maji nipe nijifunze zaid
 
Ahsante Kifyatu nini mategemeo kwenye huu ugunduzi???.
Maana habari za mtaan zinasema we can know universe zaidi coz we can traval through izo vibrations ambazo zina speed kubwa kuliko mwanga!!!...
Tell me more kikombe changu nimemwaga maji nipe nijifunze zaid
Hizi vibrations zenyewe sidhani kama zitatusaidia sana kwa sasa.

Mfano: Kukitokea wimbi la sunami baharini na kama wewe una meli yako basi lile wimbi likikufikia litakuinua na kukushusha tu na kamwe hutasafiri nalo. Unaweza hata usijue kama hilo wimbi limekupitia. Lakini ukiwa pwani basi lile wimbi likifika litafanya madhara makubwa sana. Pwani ya bahari ni sawa na ukingo wa huu mkeka wa space-time. Sijui huu ukingo uko wapi, kama upo.

Kwa solar systems au galaxies zilizopo karibu na huo mgongano zinaweza kuathirika (kupoteza routines zake) lakini sidhani zinaweza kusafiri kwa hiyo warp-speed. Ngoja watafiti waendelee kufukunyua.

Nafikiri kumekuwa na excitement kubwa hizi taarifa zilipopatikana kwa sababu mpaka sasa hii ilikuwa nadharia tu katika mahesabu ya General Relativity. Kwa kuwa sasa tunajua ni kweli haya mawimbi yapo basi kazi ndio imeanza upya kabisa. Ni sawa sawa na sisi kujua kuwa kuna mawimbi baharini ambayo baada ya utafiti sasa tunaweza kuyatumia kutengeneza nishati (electric power generation).
 
Sante mkuu Kifyatu
Niambie kuhusu space time.
Wanasema time haiend mbele its constant.
Past, present and future zipo kwenye same line.
Nifunze zaid kuhusu space time na maelezo yake
 
Sante mkuu Kifyatu
Niambie kuhusu space time.
Wanasema time haiend mbele its constant.
Past, present and future zipo kwenye same line.
Nifunze zaid kuhusu space time na maelezo yake
Nitajaribu.

Space (euclidean) ina dimensions 3. Ukiwa chumbani angalia pembe moja na hapo unaweza kufuata ukuta mmoja (mfano kuelekea kaskazini wakati ukiwa sakafuni). Hii ni dimension ya kwanza. Au unaweza kuelekea mashariki (perpendicular na dimension ya kwanza). Hii ni dimension ya pili. Au unaweza kwenda juu kuelekea darini. Hii ni dimension ya 3.

Hizi dimension 3 ziko perpendicular ikimaanisha unaweza kubadilisha position yako kwenye dimension moja bila kuathiri position ya hizo dimension nyingine mbili. Sehemu yeyote ile inaweza kuelezewa kwa coordinates hizi tatu. Einstein aligundua kuwa kujua ulipo kwa hizi dimension tatu haitoshi kuelezea properties nyingi za vitu in the universe. Ni lazima ujue hizo dimensions 3 zilitokea wakati gani.

Kwa hiyo space inaelezeka vizuri sana kama utajumlisha na time. (Hapa namaanisha kuwa space inaweza kuwa finyu au kuwa bwerere kutegemea na muda). Hii ndio maana ya space-time continuum. Properties za Gravity zinaelezeka vizuri sana (kimahesabu) kwa kutumia hizi dimensions 4 (3 za space na 1 ya time). Kwa uelewa wangu time siku zote inakwenda mbele. Bali ukiangalia angani unachikiona kilitokea zamani sana au ni historia.

Sijui kama nimesaidia au ndio nimekuchanganya zaidi?
 
Kifyatu Napata idea ila bado saana!!. Kwa maana iyo unaweza kwenda future au past bila ku afect present? Maana inaonekana vyote vipo kwenye pallale line..haviwez kukutana iLa vinaongozana??
 
Kifyatu Napata idea ila bado saana!!. Kwa maana iyo unaweza kwenda future au past bila ku afect present? Maana inaonekana vyote vipo kwenye pallale line..haviwez kukutana iLa vinaongozana??
Ngoja nikupe mfano mmoja. Nyota ya karibu na sisi (Alpha Centauri) iko 4.4 light years kutoka hapa. Ina maana tunapoiangalia tunaona vitu vilivyotokea zamani (miaka 4.4 iliopita).

Sasa kama tungeweza kwenda kwa kasi ya ajabu na kufika kwenye hii nyota na kurudi mara moja, ina maana tungeona vitu ambavyo vitakujaonekana hapa duniani miaka 4.4 ijayo. Ina maana tutaweza kwenda into the future. Kuna katatizo kadogo tu hapa. Kwa sasa speed limit ya universe ni speed of light. Tukiweza kupata njia ya kusafiri kwa kasi kubwa zaidi ya speed of light basi usafiri kwenda future utawezekana.
 
Mkuu Kifyatu mfano tukipata kitu chenye speed kubwa kuliko mwanga wa jua how is it possible mfn km mwanga wa jua unafika kwa dunia baada ya dakika 8, ikiwa inaweza kufika ndani ya dakika 2 ivyo sawa na kuwa na chombo cha speed ya 2min from sun to earth what will it change??
 
Mkuu Kifyatu mfano tukipata kitu chenye speed kubwa kuliko mwanga wa jua how is it possible mfn km mwanga wa jua unafika kwa dunia baada ya dakika 8, ikiwa inaweza kufika ndani ya dakika 2 ivyo sawa na kuwa na chombo cha speed ya 2min from sun to earth what will it change??
Ilivyo ni kuwa kadri unavyokaribia kasi ya mwanga ndio ukuaji wako unavyozorota kutokana na contraction of space. Sasa kama ulimuacha pacha wako hapa duniani na kusafiri kwenye space kwa kasi ya mwanga, ukirudi hapa pacha wako atakuwa amezeeka kuliko wewe. Ukisafiri katika kasi ya mwanga basi kwako wewe muda (time) unasimama.

Kama umesafiri kwa miaka 30 (ya hapa duniani) ukirudi utakuwa kama ulivyoondoka na kila uliemuacha atakuwa amezeeka kwa miaka 30.
 
Ahsante mkuu Kifyatu
Nlitaka kujua hii paradox ya ukiwa kwenye kax zaid ya mwanga unawexa kwenda kwenye future au kurud past..hii mechanism imekaaje maana inanichanga saana.
Tuanze hapa: Muda (time) ni relative na speed yako. Kadri speed inavyoongezeka ndio muda (Time) wako unavyozorota (slow-down). Dhana ni kuwa ukisafiri katika speed ya mwanga basi muda (au umri) wako unasimama ukilinganisha na uliowaacha duniani. Kwa hiyo ukirudi duniani wewe utakuwa kama ulivyoondoka (ki-umri) lakini dunia na watu wake watakuwa wamezeeka. Kwa hiyo wewe utakuwa unaona mambo ya siku za mbele ukilinganisha na umri wako (travel to the future). Hii ya kuwa ukisafiri kwa kasi umri wako unazorota imekwisha thibitishwa kisayansi kwa kuwatumia astronauts.

Sasa mkwara unakuja hapa. Kinadharia, kama utaweza kusafiri kwa kasi zaidi ya speed ya mwanga, basi muda (time) wako sio tu kuwa unasimama bali utakuwa unarudi nyuma (travel back in time). Tatizo hapa ni kuwa ukiweza kufanya hivyo na kukutana na wazazi wako walipokuwa watoto na ukaweza kuwaua, je wewe umepatikanaje. Hii ndio paradox ya kusafiri into the past.

Kwa maoni yangu ni kuwa kusafiri into the past haitawezekana. Sababu ya kwanza ni kuweza kusafiri kwa kasi kubwa zaidi ya kasi ya mwanga. Sababu ya pili ni hicho kiini-macho cha kuweza kubadilisha historia (mfano, umuue Hitler alipokuwa kichanga).
 
Back
Top Bottom