Ufahamu kuhusu nyota za angani

Mkuu Kifyatu kwenye kusoma soma kwangu wanasema kwamba kuna aliens ambao tayari tuna uhusiano nao (friend aliens) wanasema zaid kwa miaka 1900 dunia ilikuwa kwenye giza na maarifa yalikuwa kidogo, ila walipata kufika dunian kuanzia 1950 ndo wametupatia knoledge kubwa!, kwa miaka 50 unaweza kuwa shahidi technology ilivyobadilika mpk hapa tulipo...unazungumziaje hizo conspiracy mkuu??
 
uploadfromtaptalk1464118376636.jpeg

Mercury,venus and Saturn in line with the pyramids,this occurs once every 2373 years,
 
Mkuu Kifyatu kwenye kusoma soma kwangu wanasema kwamba kuna aliens ambao tayari tuna uhusiano nao (friend aliens) wanasema zaid kwa miaka 1900 dunia ilikuwa kwenye giza na maarifa yalikuwa kidogo, ila walipata kufika dunian kuanzia 1950 ndo wametupatia knoledge kubwa!, kwa miaka 50 unaweza kuwa shahidi technology ilivyobadilika mpk hapa tulipo...unazungumziaje hizo conspiracy mkuu??
Kifyatu habari za jion mkuu
 
Sikua nimeliona hili swali lako la jana.

Kuhusu aliens hata mimi nina shauku sana kujua ukweli uko wapi. Wacha hatua tulizopiga kitaaluma tangu 1950 lakini ukiangalia maajabu kama ya pyramids na accuracy ya ujenzi wake, technolojia za waMayans, Einstein alikuwa anaota nini mpaka kutuletea mahesabu yake ya relativity, nk. Utaona mara kwa mara kunakuwa na mlipuko wa elimu mpya inayotokea na inayotusogeza mbele kitaaluma na sijui ni kwa nini.

Mkuu inawezekana hata wewe na shauku zako za kujua mambo inawezekana unakamkono ka hawa aliens (jokes).

Mimi niko open kabisa kujuzwa kuhusu hawa eliens.
  • Pengine ni malaika?
  • Au ndio mkono wa Mungu mwenyewe?
  • Hivi ni kweli katika universe yote hii hakuna viumbe wenye kufikiri na maarifa kama au zaidi ya sisi?
  • Pengine aliens tunao lakini hatuwaoni (sio carbon-based kama sisi)?
  • Inawezekana kuwa wanatubadilisha (wanatuumba) kwa kutufanyia genetic-mutations (kama jua letu linavyotufanyia) badala ya genetic cross-overs (yaani kuzaa na sisi) kama tunavyozaana?

Maswali ni mengi mkuu. Kuna mengi hatuyajui na ndio maana sipuuzii dhana yoyote ile nitakayoisikia.
 
Tuanze hapa: Muda (time) ni relative na speed yako. Kadri speed inavyoongezeka ndio muda (Time) wako unavyozorota (slow-down). Dhana ni kuwa ukisafiri katika speed ya mwanga basi muda (au umri) wako unasimama ukilinganisha na uliowaacha duniani. Kwa hiyo ukirudi duniani wewe utakuwa kama ulivyoondoka (ki-umri) lakini dunia na watu wake watakuwa wamezeeka. Kwa hiyo wewe utakuwa unaona mambo ya siku za mbele ukilinganisha na umri wako (travel to the future). Hii ya kuwa ukisafiri kwa kasi umri wako unazorota imekwisha thibitishwa kisayansi kwa kuwatumia astronauts.

Sasa mkwara unakuja hapa. Kinadharia, kama utaweza kusafiri kwa kasi zaidi ya speed ya mwanga, basi muda (time) wako sio tu kuwa unasimama bali utakuwa unarudi nyuma (travel back in time). Tatizo hapa ni kuwa ukiweza kufanya hivyo na kukutana na wazazi wako walipokuwa watoto na ukaweza kuwaua, je wewe umepatikanaje. Hii ndio paradox ya kusafiri into the past.

Kwa maoni yangu ni kuwa kusafiri into the past haitawezekana. Sababu ya kwanza ni kuweza kusafiri kwa kasi kubwa zaidi ya kasi ya mwanga. Sababu ya pili ni hicho kiini-macho cha kuweza kubadilisha historia (mfano, umuue Hitler alipokuwa kichanga).

Naendelea kukusoma Mkuu tangu mjadala huu ulipoanza, nimenufaika na kuelimika vya kutosha. Hongera sana. Allah akupe afya njema na akuzidishie ilmu. Hii elimu unayoitoa ni ile sadakatu l jaaria tunayoambiwa siku zote katika Uislam.
Shukran.
 
nyota ni ndogo sana kuliko dunia, ni kama mwezi. zinategemea mwanga wa jua. na nyota ulizoona zinazobadilika kutoka rangi kutokea ya blue kwenda ya kijani ni kutokana na kuzibwa na miti na bahari .na ukiona nyekundu ujue hapo kuna radi na mvua inanyesha.:(:(:(:(:D:D:D
 
Naendelea kukusoma Mkuu tangu mjadala huu ulipoanza, nimenufaika na kuelimika vya kutosha. Hongera sana. Allah akupe afya njema na akuzidishie ilmu. Hii elimu unayoitoa ni ile sadakatu l jaaria tunayoambiwa siku zote katika Uislam.
Shukran.
Nakushukuru mkuu. Nakumbuka tulianza pamoja mada ilipoletwa. Asante kwa kufuatilia. Nitajaribu, Inshaallah, kuelezea concept ngumu za sayansi kwa lugha rahisi inayoweza kueleweka na wote.
 
Kifyatu shikamooo wewe ni noumaa kwa mtu kama mm niliesoma shule za kata na nikapata division 4 kidato cha nne nakuona kama wewe kama n Jini vile
 
Mkuu kifyatu natanguliza shukrani zangu za dhati kwa elimu unayotoa.

mkuu hapa juzi juzi nimeona kuna uvumbuvi wanasema "the new kind of light " kitu kama neutrinos ivi nlisoma soma wakanichanganya unaweza kutupa mwanga kidogo mkuu...
 
Asante mkuu. Jibu langu litakua refu kidogo. Ni matumaini yangu sitawapoteza watu.

Kwa anaetaka kujua kwa kitaalam zaidi kuhusu Neutrinos anaweza kupata taarifa hizi kwenye internet (search for it). Hapa nitajaribu kuelezea kwa lugha rahisi haya yafuatayo:
  • Neutrino ni nini?
  • Neutrino zinatengenezwaje?
  • Neutrino zina faida gani kwetu?
  • Je neutrino zina madhara kwetu?
Neutrino ni nini?
Tulijifunza kwenye sayansi ya sekondari kuwa atom ina viambata vitatu navyo ni:
  1. Protons (+ve charged na zina uzito),
  2. Neutrons (haina chaji na zina uzito), na
  3. Electrons (-ve charged na karibuni hazina uzito - lakini zinao kidogo).
Ukweli ni kuwa kuna chembe chembe (sub-atomic particles) nyingi zaidi kuliko hizo tatu tulizojufunza.

Neutrino (ziko za aina 3) ni moja ya hizo chembe (sub-atomic particles) ambazo hazina chaji kabisa na uzito wake ni mdogo sana kuliko hata wa electrons (uzito wa neutrino milioni moja ni sawa na uzito wa electron moja).

Neutrino zinatengenezwaje?
Kukiwa tu na mlipuko wa ki-nyuklia (kama vile kwenye jua letu, nyota, super nova, mabomu au mitambo ya nyuklia) basi neutrino zinatengenezwa. Popote pale atom zinapopasuliwa (fission, kama mabomu ya nyuklia) au atom zinapounganishwa (fusion, kama kwenye jua au nyota) basi neutrinos zinatengenezwa. Jua letu linatumwagia neutrino billion 65 kwa sekunde katika kila eneo la sentimita moja ya mraba hapa duniani.

Tofauti na mwanga wa kawaida au hata ultra-violet na X-rays, neutrinos hazizuiwi na chochote kile. Zikitua hapa aridhini basi hupita moja kwa moja mpaka upande wa pili wa dunia kwa kasi ya mwanga na kuendelea. Kwa hiyo hata wewe hivi tunavyosema unalabuliwa na neutrino 65 billion kwa sekunde katika kila eneo la sentimita moja ya mraba ya mwili wako (na hiyo ni kutoka kwenye jua tu - na kuna za ziada kutoka sehemu nyingine).

Usifikirie kuwa usiku utakuwa salama, la hasha. Jua likiwa upande mwengine wa dunia hizo neutrino zake zitapenyeza mpaka upande wa pili ambako ni usiku na kukuzaba tu. We kaa mkao wa kula tu mkuu.

Neutrino zina faida gani kwetu?
Kwa kuwa neutrino hazina chaji basi haziathiriwi na nguvu za smaku (electromagnetic fields). Wakati hatuwezi kutumia mwanga wa kawaida kuchunguza kilichopo ndani ya jua letu au nyota na galaxies nyingine, tunaweza kutumia hizi neutrinos kama kurunzi (tochi) ya kuchungulia pasipoweza kuchungulika kwa sasa. Bado utafiti unaendelea wa kutengenezea hizi kurunzi za neutrinos.

Pia kama hizi kurunzi zitapatikana inawezekana tukaachana na upigwaji picha hatarishi wa matibabu kama vile X-rays, MRI (wanasema sio hatarishi lakini sijui), n.k. na tutumie neutrino-scans badala yake?

Unaona utamu huo mkuu.

Je neutrino zina madhara kwetu?
Hili sina uhakika nalo bado lakini nawaza tu. Kama neutrino nyingi kama hizi zinapita kwenye miili yetu, ya wanyama, miti, na viumbe hai vyote, je inawezekana kutubadilishia (mutations) maumbile ya DNA zetu? Kama ni kweli je tunaweza kutengeneza ngao au mwemvuli (neutrino shields) wa kujikinga nazo?

Sijui, lakini hapa ndio tunapofikia utamu wa sayansi.
 
Daah I salute....
 
Kifyatu nasikia kuna Dubwana linakuja kwa kasi sana kuigonga dunia ilo dubwana linaitwa x je habar iz zinaukweli wowote??
 
Kwa maoni yangu ni kuwa usiogope kuhusu Planet X (au Nibiru). Wanajimu wa kiSamaria waliitabiri na kuna wanaoamini kuwa inachukua miaka milioni 27 kulizunguuka jua na ina ukubwa wa mara kumi wa dunia yetu.

Mara kwa mara utasikia huu utabiri wa mwisho wa dunia (year 2000, kalenda ya waMaya na Desemba 21, 2012, n.k.) kutoka makundi mbalimbali. Usibabaike. Walituambia April mwaka huu ndio hilo dubwana litatuzaba lakini mpaka leo tunadunda.

Isipokuwa kuna ushahidi wa sayari ya tisa (planet 9, sio pluto) ambayo inachukua miaka 15,000 tu kuzunguuka jua letu. Hii sayari nayo pia ni kubwa na inatembelea ukanda wenye comets nyingi (Kuiper belt). Kama gravity ya hii sayari itatungua baadhi ya hizi comets na kuangukia duniani basi tunaweza kuathirika. Lakini mkuu usipoteze usingizi wako kuhofia hivi vitisho.
 
Kwa maoni yangu ni kuwa usiogope kuhusu Planet X (au Nibiru). Wanajimu wa kiSamaria waliitabiri na kuna wanaoamini kuwa inachukua miaka milioni 27 kulizunguuka jua na ina ukubwa wa mara kumi wa dunia yetu.

Mara kwa mara utasikia huu utabiri wa mwisho wa dunia (year 2000, kalenda ya waMaya na Desemba 21, 2012, n.k.) kutoka makundi mbalimbali. Usibabaike. Walituambia April mwaka huu ndio hilo dubwana litatuzaba lakini mpaka leo tunadunda.

Isipokuwa kuna ushahidi wa sayari ya tisa (planet 9, sio pluto) ambayo inachukua miaka 15,000 tu kuzunguuka jua letu. Hii sayari nayo pia ni kubwa na inatembelea ukanda wenye comets nyingi (Kuiper belt). Kama gravity ya hii sayari itatungua baadhi ya hizi comets na kuangukia duniani basi tunaweza kuathirika. Kalini mkuu usipoteze usingizi wako kuhofia hivi vitisho.

Asaante mkuu kwa kunitoa hofu

swal lingine iv radi nkimaanisha ule mwanga ambao unaweza kuunguza miti mikubwa na had kuua mtu pamoja na zile nguromo uwa zinatokana na nn uko juu?
 
Mkuu Kifyatu hivi hii inawezakana hawa wajenga ma pyramids walikuwa wanafuata unajimu,au zilikuwa zinawakilisha stars,planets and other objects
Ukisoma namna hizi pyramids zilivyojengwa na kupangiliwa utaona maajabu kwa kweli. Inaelekea hawa wajenzi walikuwa na elimu ya hali ya juu sana kuhusu nyota na mahesabu. Sasa sijui walikuwa ni Waarabu hawa hawa wa Misri au walipata msaada kutoka viumbe wengine. Ningekushauri usome vitabu au uangalie documentaries zinazozungumzia maajabu ya taaluma zilizotumika kujengea hizi pyramids.

Kitu kimoja hakina utata. Pyramid zilijengwa na mafarao walizikwa humo ili waweze kuishi milele (after life). Hii ni kweli na inatokea sasa. Sote sisi tunawazungumzia na kujifunza hawa mafarao kuliko hata tunavyowajua mababu zetu. Huko ndio kuishi katika after-life.
 
Mkuu wa Egypt ya kale kwenye swala la astronomy na hesabu hawa jamaa walikuwa vizuri kuna baadhi hata ya formula za hesabu zina mizizi yake huko.
 
Back
Top Bottom