Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Mwita Maranya sasa kamanda mbona mnakaba mpaka penati?Hawa Masalia nadhani mnataka kuhakikisha wote wanapata Heart attack na kujifia kabisa, hongera sana kwa ufafanuzi huu muruwa mpaka Ritz amepata kiwewe.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wanaJF,

Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.

Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.

Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.

Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.

Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.

Sasa nije kwa John Heche Suguta:
Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.

Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.

Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.

John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.

Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.

Nawatakia jioni njema.

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza, masalia wanatapatapa tu, wanashindwa kuelewa kuna watu waliosoma na heche wamo katika chama na humu JF wapo wengi tu. Uchu wa madaraka unawasumbua.
 
Mh! Bado umeniacha njia panda kama kwenye vyeti vya shule anatumia Wegesa Charles Saguta, why kwenye siasa anatumia John Heche, je kwenye huo udiwani wapiga kura wake walimchagua kwa jina gani?
 
Mkuu Mwita Maranya ,

Kwenye orodha weka na jina hili : Thomas Nyambari Nyangwine

Huu ufafanuzi ni mzito sana. Ya majina ya shule na majina ya nyumbani. Ni tofauti sana na wale walioripiti na kutumia majina ya watu.
 
Last edited by a moderator:
Mwita Maranya mbona unapindisha ukweli? si uwaambie ukweli kuwa jina hilo ni la kike ndio maana huyu jamaa halipendi jina hilo, kwa kuwa hana cheti chenye jina la John mshauri atumie jina lake la wegesa hata kama la kike.

WEGESA ni jina la kikurya la kike wanalopewa watoto wa kike wazaliwao wakati wa mavuno, na Magesa la kiume kwa wazaliwao wakati huo. Kama hapendi jina hilo aende mahakani aape
 
Hawa masalia wanatu-keep biz bila mpango, lakini hakuna kuwaachia wasaliti wakubwa hawa. Agenda zao na mambo yao ni ya hovyo kabisa.


So we gonna smoke them out completely!
 
Mh! Bado umeniacha njia panda kama kwenye vyeti vya shule anatumia Wegesa Charles Saguta, why kwenye siasa anatumia John Heche, je kwenye huo udiwani wapiga kura wake walimchagua kwa jina gani?
Ujaachwa njia panda bali Elimu yako ni ndogo na ndiyo iliyokuacha njia panda na hujui hata kazi ya Affidavit.

Angalia hawa wengine walivyokuchanya

Mike Tyson = AbdulMalick.

Clay = Muhamad Ally.
 
Kila mtu anaweza kuja na huo utetezi! Nisaidie kujibu haya:-

i. Wewe ni nani wake?
ii. Umemfahamu wapi na wapi, na alikuwa akitumia majina yepi?
iii. Kipi kilimlazimu kubadili majina kutoka majina ya shule mpaka huku kwenye Siasa.
iv. Mifano uliyoitoa mingi ni ya majina matatu, lakini naona kama kuna majina zaidi ya matatu kwa Heche, vipi unaweza kutupa ufafanuzi?

Ni hayo tu.
 
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza, masalia wanatapatapa tu, wanashindwa kuelewa kuna watu waliosoma na heche wamo katika chama na humu JF wapo wengi tu. Uchu wa madaraka unawasumbua.

Mkuu mimi wenyewe nashangaa kwa sababu Ndugu zake nawafahamu na Mmoja ni mwenyekiti wa BAVICHA tarime na naitwa Chcha Heche, Kuna Malaya wa Siasa anakuja na Hoja mfu hapa akitaka kuwaaminisha Wajinga fulani kwamba JOHN HECHE SI JINA LAKE NA jINA LAKE HALALI NI hili analo komaa nalo,
 
Mwita Maranya sasa kamanda mbona mnakaba mpaka penati?Hawa Masalia nadhani mnataka kuhakikisha wote wanapata Heart attack na kujifia kabisa, hongera sana kwa ufafanuzi huu muruwa mpaka Ritz amepata kiwewe.

huyu Ritzsijui yukoje!

:focus:

MASALIA :A S 103::A S 103::A S 103:
 
Last edited by a moderator:
Hahahaha, umenikumbusha Story ya Muha na Msosi wa moto ile mbaya. Akachukua Bonge la nyama na kuliweka mdomoni ila ndiyo moto kwelikweli. Ghafla baada ya kuzungusha kushoto na kulia, uvumilivu ukamshinda na akaanza kutokwa machozi kwa maumivu makali (Kama Juliana Shonza vile) na hapo watu wakamhoji kulikoni:

Swali: Vipi tena, cha moto?
Muha: Ndiyo.
Swali: Tema basi.
Muha: Niteme chakura.
Swali: Meza basi.
Muha: Nimeze cha moto.
Swali: Kunywa maji.
Muha: Niharibu raza (ladha).

Huyu unabaki tu kumwangalia anavyolia na nyama yake ya moto mdomoni. Itapoa na atameza na kujiondokea.
Masalia wanahaha, maji moto, ugali moto, mboga moto,
 
Sasa mtu kuitwa jina lake ndio upotoshaji kama ana majina mawili mtu anahaki kumwita lolote kati ya hilo au kuna kosa kuitwa jina wegesa
 
samahani mkuu! nilishawahi kusikia kuwa ulishawahi kulaniwa. Sasa nilikuwa naomba kuuliza:
hivi laana uliyonayo inatoka kwa wazazi wako ama kwa walimwengu?
Kama ni wazazi kawalilie watakusamehe! Ni hayo tu mkuu!

Dunia ili mlaani huyu...
 
Back
Top Bottom