Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Hivi kuna majina ya kikiristo duniani?

Yapo tena mengi,kwa mfano nina ndugu yangu anaitwa kokubanza james kiiza lakini baada ya kubatizwa akaitwa Priscillah James Kiiza kwa hiyo hapa jina Priscillah ni la kikristu je una la ziada dada?
 
Ndugu wanaJF,

Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.

Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.

Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.

Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.

Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.

Sasa nije kwa John Heche Suguta:
Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.

Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.

Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.

John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.

Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.

Nawatakia jioni njema.
Mkuu wewe ndio Suguta mwenyewe nini?
 
Asante kwa ufafanuzi Ndg. Mwita Maranya. Ila nadhani bado sijaelewa vizuri ufafanuzi wako. Kama Wegesa Suguta ndiyo jina lake "Official" na ndilo amelitumia kwenye "official" documents zake kwanini kwenye matamko yake "official" ya kimaandishi anajitambulisha kama "John Heche", jina ambalo siyo "official"? Amesharasimisha jina "John Heche" pia kwa mujibu wa sheria? Sihukumu kwamba anagushi jina, nataka kuelewa vizuri tu.
 
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu,napita naona kuna watu hapa wanataka nipigwe ban!
 
Asante kwa ufafanuzi Ndg. Mwita Maranya. Ila nadhani bado sijaelewa vizuri ufafanuzi wako. Kama Wegesa Suguta ndiyo jina lake "Official" na ndilo amelitumia kwenye "official" documents zake kwanini kwenye matamko yake "official" ya kimaandishi anajitambulisha kama "John" Heche, jina ambalo siyo "official"? Amesharasimisha jina lake la asili kwa mujibu wa sheria pia? Simaanishi anagushi jina nataka kuelewa vizuri tu.
Mtoa mada ameelezea majina ya kikuria kirahisi rahisi mno na maelezo hayo hayawezi kusimama mbale ya sheria.Kisheria mtu anakuwa na majina matatu ambayo hayatambui dini ya mtu bali majina hayo.Sasa mheshimiwa Mwita Maranya katoa ufafanuzi wa jinsi Wakuria wanvyokuwa na parallel names ambazo kisheria ni aliases.Kwa hiyo tuhuma zilizopo haziwezi kuelezwa kirahisi hivyo.
 
Hivi kuna majina ya kikiristo duniani?

Jaribu kuhangaisha ubongo wako hata kwa ku google tu,kua kwako ni kada wa chama chenye wengi wa wenye akili mfu basi na wewe ushindwe hata kushughulisha ubongo wako japo kidogo!
 
mbona mnajibu vitu vdogo na kuacha mambo makubwa yaliyohojiwa na Shonza?
hebu tupeni ufafanuzi juu ya vifungu alivyolalamikia Shonza kwamba vmekiukwa! hebu tuambieni vigezo vilivyotumika kumwadhibu Shonza na kumuacha Mamuya wakati wote hawakuhudhuria kikao, hebu tuambieni juu ya mshahara wa Heche na kwann kodi ya nyumba yake inatoka kwa katibu mkuu?
hebu tufafanulieni juu ya gari la BAVICHA na dreva wake.
CHHADEMA acheni kujibu hoja nyepesi na zisizohitaji kujibiwa wakat kuna hoja znahtaj majibu yenu na hapo sijawauliza kwann hamjamfukuza Zitto kwa sababu najua Zitto sio BAVICHA!
 
Kwani we mwita ni nan ake wegesa, kwanin yy aloiba majina asije hapa kufafanua? Mwaka wenu huu kwakweli.
Mwizi wa kingwangwala na mwigulu wote wanadai majina yao ya rudishwe lakini Wegesa ni jina alipewa na baba yake kama wewe ni mwana wa kuzaliwa wa nje na mzee heche basi utakuwa unajua kuwa baba yenu alimpa jina hilo
 
Mwita Maranya mbona unapindisha ukweli? si uwaambie ukweli kuwa jina hilo ni la kike ndio maana huyu jamaa halipendi jina hilo, kwa kuwa hana cheti chenye jina la John mshauri atumie jina lake la wegesa hata kama la kike.

WEGESA ni jina la kikurya la kike wanalopewa watoto wa kike wazaliwao wakati wa mavuno, na Magesa la kiume kwa wazaliwao wakati huo. Kama hapendi jina hilo aende mahakani aape

Kweli siku yako haijafika. Hujui asili na utaratibu wa majina ya kikurya usipotoshe bora uulize usaidiwe.
Kuna wanawake wanaitwa Marwa, Chacha ama Mwita ambayo ni majina ya asili ya kiume na kuna wanaume wanaitwa Bhoke, Ghati ama Rhobi ambayo ni majina ya asili ya kike.
Kuna majina kama Wegesa, Matinde, Nyamhanga, Nyangi, Mogesi n.k ambayo yanatumika na jinsia zote kutokana na sababu maalum wazazi wanaamua kumpa mtoto jina fulani.
Mathalani bibi yake na baba yangu anaitwa Mogesi lakini sasahivi familia yetu inawapa jina hilo watoto wa kiume kutokana na familia kuamua hivyo kama kumuenzi.
 
Mh! Bado umeniacha njia panda kama kwenye vyeti vya shule anatumia Wegesa Charles Saguta, why kwenye siasa anatumia John Heche, je kwenye huo udiwani wapiga kura wake walimchagua kwa jina gani?

Wapiga kura wa Tarime mjini wanamfahamu kwa majina yote mawili John na Wegesa lakini wengi hupendelea kumuita John Heche Suguta.
 
asante sana mwita maranya.... aibu yao PM7..... Tatu bila mpka sasa, ngoja wakajipange tena mr leka du tigite
 
Machafuko ya hali ya hewa kwenye siasa au vyama vya siasa si jambo geni mahali popote duniani. Ni vizuri tukajifunza kuwa usaliti ni jambo la lazima kwenye siasa. Sema usaliti mwingine ni wa kijinga sana - mikakati ya kijinga na ya kitoto. Huyu Juliana anayaweza au ndio remote control kashikilia mtu mwingine (Na yeye hana ya kwake)

Wajifunze kufanya research kabla ya kutupa mawe!
 
Kweli siku yako haijafika. Hujui asili na utaratibu wa majina ya kikurya usipotoshe bora uulize usaidiwe.
Kuna wanawake wanaitwa Marwa, Chacha ama Mwita ambayo ni majina ya asili ya kiume na kuna wanaume wanaitwa Bhoke, Ghati ama Rhobi ambayo ni majina ya asili ya kike.
Kuna majina kama Wegesa, Matinde, Nyamhanga, Nyangi, Mogesi n.k ambayo yanatumika na jinsia zote kutokana na sababu maalum wazazi wanaamua kumpa mtoto jina fulani.
Mathalani bibi yake na baba yangu anaitwa Mogesi lakini sasahivi familia yetu inawapa jina hilo watoto wa kiume kutokana na familia kuamua hivyo kama kumuenzi.

Mkuu achana na huyo masalia mbona hata majina ya kiswahili yapo yanayo tumika kwa wanaume na wanawake,mafano: Neema,Furaha,bahat,ombeni,ombi,maombi,fikiri,sikujua,maisha,n.k
 
Back
Top Bottom