Ufafanuzi wako hakika unajitosheleza,labda pia kwa faida ya kufunzana katika jukwaa yapo mambo ya kueleweshana hasa tulikotoka,-ukiacha issue kama hii ya john heche kuwa na majina ya nyumbani utamaduni ambao ni mkubwa kwa makabila mengi tanzania,wapo pia wale waliosoma miaka ya nyuma kidogo kabla ya mfumo wa elimu ya sekondary kupanuka sana,ambapo nafasi za ufaulu zilikuwa finyu sana,na kujikuta mwanafunzi mmoja akifaulu katika darasa la watu mia moja,ikiwa ni sababu hasa ya kutokuwa na nafasi za shule za sekondary za kutosha,hii ilisababisha watu wengi kurudia madarasa ya shule za msingi kwa kupewa majina ya watu ambao mara nyingi walikuwa wakikataa shule,hivyo watu wengi waliosoma miaka ambayo ufaulu ulikuwa kwa kiwango kidogo,walipata kadhia hii ya kutumia majina ya watu wengine,hasa wale watu ambao familiya zao zilikuwa na msisitizo wa kusomesha watoto lakini hawana uwezo wa kuwapeleka private school ambazo pia zilikuwa chache,zaidi ya hapo nakupongeza kwa ufafanuzi mzuri wa john heche,ambao kwa sisi wengine tulijua ni majina yake rasmi,sema siasa za bongo lolote lile ni habari kama ambavyo hao wengine wanaambiwa wameiba majina ya watu,japo huko vyuoni wamesoma na watu.