Ufafanuzi kuhusu kasi ya ndege inapopaa

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
821
2,070
Ufafanuzi mwepesi.
Ndege inapokimbia kwenye barabara yake (#runway) kwaajili ya kupaa, kuna kasi tofauti ambazo Rubani msaidizi '#First_Officer au Rubani kiongozi #Captain anataja ili anayehusika kurusha ndege (Pilot in command) afahamu maamuzi aliyonayo katika mwendo husika.

Ndege (hasa kubwa) inapoanza kukimbia (rolling) rubani mmoja atataja kasi zifuatazo ili rubani mwenzake mwenye majukumu ya kupaisha ndege ili atambue yupo katika wakati gani wa kufanya maamuzi kati ya kupaa au kusimama.

Mfano; 80 knots/100 knots
Kutegemea na aina ya ndege kati ya #Boeing au #Airbus. Hii ni kasi ya awali ya taarifa iliyo kati ya kilomita 140-150 kwa saa ambayo kama ndege inatapata hitilafu/dharura rubani anaweza kusimamisha ndege salama katika barabara iliyobaki mbele yake.

V1 (Decision speed)
Hii ni kasi ya maamuzi ya kupaa inayozidi kilomita 150 kwa saa ambayo zaidi ya hapa rubani kiufundi haruhusiwi kusimamisha ndege hata ikipata hitilafu/dharura. Kujaribu kusimamisha ndege katika kasi inayozidi hapo unaweza kupasua tairi zote na bado ndege isisimame mahala salama.

Vr (Rotation speed)
Hii ni kasi ambayo ndege inatakiwa kuacha ardhi na kunyanyuka. Katika kasi hii tayari ndege inakuwa imezalisha mkandamizo wa hewa ya kutosha katika mbawa kuweza kunyanyuka (lift) hivyo kiuhalisia inakuwa tayari inaelea elea tu ikusubiri maamuzi ya rubani kuinua pua ili kupaa rasmi.

V2 (Airborne)
Hapa ndege inakuwa tayari angani. Hii ni kasi salama ya ndege kuendelea kupaa hata kama injini moja imefeli.
Katika hii kasi mara nyingi utaona ndege inaanza kupandisha 'Flaps' zake kwenye mbawa na kuingiza tairi ndani.

Kumbuka ndege tofauti na gari.
Ina hesabu nyingi sana za kufahamu ili iweze kupaa salama mfano, ikiwemo kufahamu hali ya hewa, Joto, Uelekeo wa upepo, uzito wa mzigo, umbali unaohitajika kupaa, kuseti visaidizi vya kupaa. Pia hesabu za upangaji sahihi mizigo, mafuta na mengineyo.
 

Attachments

  • Polish_20240506_143512918.jpg
    Polish_20240506_143512918.jpg
    192.3 KB · Views: 1
SOmo zuri sana nakupongeza je unaweza kututafsiria zile alama zilizoko uwanjani kila moja inamaanisha nini?

Je, ni njia gani hutumika kuwafanya warusha ndege wasigongane wala kupigana pasi pale uwanjani na hasa ndege moja inapokwenda kuruka unakuta ghafla imesimama nyingine inapita zinapangana msururu wanapeana zamu kuruka au kutua
 
Back
Top Bottom