Hawa vijana wa chuo kikuu sielewi uchaguzi wanaozungumzia ni upi. Kama ni ule wa viranja wao pale mlimani, sioni kama hiyo ina nguvu za kutosha kutushughulisha hapa jamvini.
Kama kuna wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa kuhatarisha usalama, nadhani kuna utaratibu wa kushughulikia masuala ya kinidhamu chuoni, na kama utaratibu huo haujakiukwa sioni haja ya kupiga kelele. Watueleze undani wa hao waliosimamishwa, walikosa nini, na nini kinawafanya waone kuwa chuo hakijatenda haki katika utaratibu wa kuwasimamisha, na waeleze hatua za KISHERIA walizochukua ikashindikana ndipo wengine tuingilie kati kusaidia, vinginevyo kama sisi JF tutakuwa tunavamia kila tunaloletewa hapa hawa watoto wataanza kutuchezea, wanafanya madudu huko chuoni halafu wanataka sisi ndio tuuvae mkenge wao!
Kama kuna aliyelikoroga shuleni huko lazima alinywe! Kama anaonewa wekeni details wazi ieleweke. Huko vyuoni mnadanganyana sana, mtu anachaguliwa kuwa kiranja na cheo chake kinaitwa "waziri mkuu" wa serikali ya wanafunzi, basi nae anajisahau anajiona ni waziri mkuu kweli sawa na Mizengo Pinda, matokeo yake anakuwa arrogant na kutumia lugha za kebehi na vitisho kwa wakuu wa chuo, sasa hapo unategemea nini?
Nakumbuka kwenye mgomo mmojawapo hapo mlimani niliwahi kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa "rais" wa wanafunzi alimpa ultimatum Rais Kikwete atimize madai yao katika muda wa siku tatu, la sivyo watafanya nini sijui! Yaani alishajisahau kabisa, kajiona nae ni rais sawa na Kikwete! Hii arrogance haiwasaidii wanafunzi, badala yake inazidi kuwadidimiza na kuifanya jamii iwaone hamnazo!
Nitasimama kuwatetea wanafunzi iwapo kuna taratibu zimekiukwa ama haki haijazingatiwa katika kusimamia masuala yanayowahusu, lakini kama ni suala la kuimarisha nidhamu na utendaji bora kwa kuzingatia kanuni na sheria za uendeshaji wa chuo, hapo namuunga mkono mkuu wa chuo, na tena namshauri akaze uzi kabisa.
Kama wanastahili kutimuliwa, timua kabisa wala usione aibu wala huruma! Usitulelee mijitu itakayokuja kuendeleza ufisadi na ubabe.
Hatutaki mijitu isiyokuwa na nidhamu wala ustaarabu.