UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

Hawa vijana wa chuo kikuu sielewi uchaguzi wanaozungumzia ni upi. Kama ni ule wa viranja wao pale mlimani, sioni kama hiyo ina nguvu za kutosha kutushughulisha hapa jamvini.

Kama kuna wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa kuhatarisha usalama, nadhani kuna utaratibu wa kushughulikia masuala ya kinidhamu chuoni, na kama utaratibu huo haujakiukwa sioni haja ya kupiga kelele. Watueleze undani wa hao waliosimamishwa, walikosa nini, na nini kinawafanya waone kuwa chuo hakijatenda haki katika utaratibu wa kuwasimamisha, na waeleze hatua za KISHERIA walizochukua ikashindikana ndipo wengine tuingilie kati kusaidia, vinginevyo kama sisi JF tutakuwa tunavamia kila tunaloletewa hapa hawa watoto wataanza kutuchezea, wanafanya madudu huko chuoni halafu wanataka sisi ndio tuuvae mkenge wao!

Kama kuna aliyelikoroga shuleni huko lazima alinywe! Kama anaonewa wekeni details wazi ieleweke. Huko vyuoni mnadanganyana sana, mtu anachaguliwa kuwa kiranja na cheo chake kinaitwa "waziri mkuu" wa serikali ya wanafunzi, basi nae anajisahau anajiona ni waziri mkuu kweli sawa na Mizengo Pinda, matokeo yake anakuwa arrogant na kutumia lugha za kebehi na vitisho kwa wakuu wa chuo, sasa hapo unategemea nini?

Nakumbuka kwenye mgomo mmojawapo hapo mlimani niliwahi kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa "rais" wa wanafunzi alimpa ultimatum Rais Kikwete atimize madai yao katika muda wa siku tatu, la sivyo watafanya nini sijui! Yaani alishajisahau kabisa, kajiona nae ni rais sawa na Kikwete! Hii arrogance haiwasaidii wanafunzi, badala yake inazidi kuwadidimiza na kuifanya jamii iwaone hamnazo!

Nitasimama kuwatetea wanafunzi iwapo kuna taratibu zimekiukwa ama haki haijazingatiwa katika kusimamia masuala yanayowahusu, lakini kama ni suala la kuimarisha nidhamu na utendaji bora kwa kuzingatia kanuni na sheria za uendeshaji wa chuo, hapo namuunga mkono mkuu wa chuo, na tena namshauri akaze uzi kabisa.

Kama wanastahili kutimuliwa, timua kabisa wala usione aibu wala huruma! Usitulelee mijitu itakayokuja kuendeleza ufisadi na ubabe.

Hatutaki mijitu isiyokuwa na nidhamu wala ustaarabu.
 
wanafunzi na uongozi wote wanamatatizo,mara nyingi ukiona familia ina watoto wakorofi sana wewe jaribu kuangalia malezi yao yalikua je?
 
Kama wanastahili kutimuliwa, timua kabisa wala usione aibu wala huruma! Usitulelee mijitu itakayokuja kuendeleza ufisadi na ubabe.

Hatutaki mijitu isiyokuwa na nidhamu wala ustaarabu.
Mwe! Prof. Kithuku hapa umeua kweli kweli.

Dah, ukweli unauma... Labda kuna mwenye kuwa na madai yao kwa mapana yanayoonyesha kuonewa waziwazi.

UDSM Students: JF na wanachama wake hawataweza kuingizwa mkenge bila kujua madai yenu yakoje. Come out clean with your allegations and people will lead you into the right place.

Invisible
 
Halafu wakishatuingiza mkenge, kesho utawaona kwenye TV wakiikana JF huku wakidai ina lengo la Kuwagombanisha na Uongozi wao, hawa jamaa siwaamini kabisa, kwani ni mara ngapi wamewakana wanaharakati waliojaribu kuwatetea kipindi wamerudishwa nyumbani kwa ajili ya 40% na pesa za matibabu
 
Kwa upande mkubwa, Watanzania bado hawajatambua kwamba wanasiasa si wakweli. Wanapenda kuwahadaa watu na kuwatumia kwa manufaa yao. Pindi umuhimu wa hao wanaotumiwa unapokosekana, kwa mfano kutowahitaji kwa kura zao, basi, 'rangi' halisi ya wanasiasa hao hujitokeza.

Nilishangaa nilipowaona wanafunzi wa Chuo Kikuu kule Diamond Jubilee, wakishangilia CCM, 'wakipendeza' kwa t-shirt, khanga, vitenge vya njano na kijani. Nikasema, iko siku watakuja kuumbuka hawa. Leo nimeyaona. Mmeumbuka. Poleni.

Kilichobakia? Nendeni Mahakamani, mkadai haki zenu. Kuna wanafunzi wenzenu waliobobea kwenye sheria, wenye uwezo wa kuandika hizo plaints, affidavits na chamber summons.

Kwa wenye uwezo zaidi hapa JF watawasaidia. Wamesikia kilio chenu.

Poleni kwa yote. Hatutawatupa.

./Mwana wa Haki

P.S. Kinachotakiwa kwa ufisadi kufanikiwa ni wazalendo kukaa kimya bila kupinga. Kwa wazalendo, hii ni changamoto mojawapo dhidi ya ufisadi...
 
Migomo iliyopita hapo Mlimani ilikuwa haihusishi kuhatarisha mali au maisha ya jamii ya Chuo. Mgomo wa mwaka huu uliohusisha kuharibiwa kwa mali za Chuo, kuvamia nyumba ya VC na hata kuvunjwa kwa mabweni ya wasichana (hatukuelezwa kuwa kulikuwa na ubakaji au la).

Hizi ni tabia unazotegemea kutoka kwa vibaka wa Manzese au mabaradhuli waliokubuhu! Sio kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu.

Hilo la uchaguzi, waende mahakamani na sio kutafuta sympathy.
 
SHY !

Naomba ufute kauli yako hapo juu ambayo ina lengo la kupotosha wana JF hapa.
Hakuna mwanafunzi aliyegoma mpaka muda huu naandika post hii na hakuna mwanafunzi aliyefungiwa kwenye chumba cha computer chochote kile (COMPUTER LABS) zote zipo wazi na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida sasa we unasema upo chumbani chumba kipi?? Post comments zenye uhakika na si kubahatisha tu nenda sasa hivi zunguka labsa zote kuanzia za falcuties ambazo wanafunzi husika wa kitivi wanatumia free na mpaka computer labs za kulipia kama utakuta kuna lab yeyote imefunga.

BACK TO THE THREAD.
Huyu kitu mtui jamani mimi namfahamu vizuri sana ni mtu mwenye kupenda vurugu ni kijana ambaye anapenda sana kuona machafuko ndani ya chuo na aliuwepo pia kwenye vurugu za kudai maji juzi juzi tu hapa sasa sijui hata kipi kinachomfurahisha.

SIKUBALIANI NA HOJA YAKE YA KUJA KUOMBA MSAADA HAPA JF HATA KIDOGO, ZAIDI ZAIDI NINACHOWASHAURI WAKAE CHINI WAFIKIRIE KILICHOWAPELEKA CHUONI NA SI KUTANGA TANGA NA MIGOMO KILA KUKICHA KAMA KWELI WANASOMA ILI WAWE WATETEZI WA TAIFA HILI WAANZE KUJITETEA KWA HOJA ZINAZOENDANA NA USOMI WAO SI KWA KUANDAA VURUGU NA MIGOMO KILA KUKICHA.

NOTE:-
MIGOMO ALWAYS INAKUWA KIPINDI MITIHANI INAPOKARIBIA SASA HAPA MUST BE THERE IS SOMETHING
 
Jamani eeh this is too much. Wanafunzi wameenda diamond lakini walioenda hawazidi 1000 na chuo kizima kina watu zaidi ya 10000. Na kwa taarifa na nina uhakikia kila mtu anafahamu kuwa Mukandara amewekwa pale na JK kwa manufaa ya chama kwa sababu wameshaona kuwa UDSM hawapati sapoti wanayoihitaji. Sasa wapo hao wachache ambao hawana tofauti na wote ambao wapo hata JF ambao ni Makada wa CCM. Ila wapo ambao lengo sio tu kuongezea posho bali kuhakikisha Huyo Mukandara anaondoka hapo alipo. Na kwa taarifa tu ni kwamba Mukandara hajawahi kuwa hata head wa department Leo ni VC.

Na hapo ndio tunahitaji msaada. Mahakamani it wont work.

Mwaka jana tulijaribu kusimamisha uchaguzi lakini kesi ikapangwa kuanza kusikilizwa wiki 2 baada ya uchaguzi. Tunajua hawa jamaa wapo everywhere ndio maana tunataka msaada kwa ambao wanauzoefu nao katika kupambana nao.
 
Nafikiri Wamwombe Kikwete Awasaidie, Ndo Hawahawa Walisukuma Gari Yake Alipotembelea UDSM. Ni Rafiki Yao Sana. Hawezi Kuwaangusha.

Pia, Wanagomaga Tu Na Kuonyesha Msisimko Pale Bumu Litakapokuwa Haliji, Au Maji Yakikatika Hostel. Lakini, Hawajui Kuwa, Kugoma Kuzuri Ni Kugoma Na Kuandamana Kupinga Kina Chenge, Lowassa Na Mafisadi Wengine. Hao Ndo Wanaiba Hela Hadi Mnakosa Kupata Bumu Zuri.

Sasa, Kwasababu Ninyi Mnateteaga Mambo Yenu Ya Kibinafsi Tu, Sio Mambo Ya Kitaifa,itabidi Mubebe Mzigo Wenu Peke Yenu, Hasa Ikizingatia, Mliandamana Na Kuharibu Vitu Pasipo Busara Wala Hekima. Kwasasa, Wana Jf, Tuelekeza Mawazo Yetu Kwenye Ufisadi Na Kumwelekeza Kikwete Afanye Nini Kwa Mustakabali Wa Taifa In The Future. Thanks.

Samahani Kama Nimewaudhi, Lakini Hiii Ndo "period"
 
Jamani eeh this is too much. Wanafunzi wameenda diamond lakini walioenda hawazidi 1000 na chuo kizima kina watu zaidi ya 10000. Na kwa taarifa na nina uhakikia kila mtu anafahamu kuwa Mukandara amewekwa pale na JK kwa manufaa ya chama kwa sababu wameshaona kuwa UDSM hawapati sapoti wanayoihitaji. Sasa wapo hao wachache ambao hawana tofauti na wote ambao wapo hata JF ambao ni Makada wa CCM. Ila wapo ambao lengo sio tu kuongezea posho bali kuhakikisha Huyo Mukandara anaondoka hapo alipo. Na kwa taarifa tu ni kwamba Mukandara hajawahi kuwa hata head wa department Leo ni VC.
Na hapo ndio tunahitaji msaada. Mahakamani it wont work.
Mwaka jana tulijaribu kusimamisha uchaguzi lakini kesi ikapangwa kuanza kusikilizwa wiki 2 baada ya uchaguzi. Tunajua hawa jamaa wapo everywhere ndio maana tunataka msaada kwa ambao wanauzoefu nao katika kupambana nao.

Mbona hutaki mahakama ?? mtu anaweza chaguliwa na kesi inaendelea mkishinda kesi si anafutwa?? wabunge wangapi wamenyanganywa ubunge na mahakama??

Ama mnajisitukia??
 
SHY !

Naomba ufute kauli yako hapo juu ambayo ina lengo la kupotosha wana JF hapa.
Hakuna mwanafunzi aliyegoma mpaka muda huu naandika post hii na hakuna mwanafunzi aliyefungiwa kwenye chumba cha computer chochote kile (COMPUTER LABS) zote zipo wazi na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida sasa we unasema upo chumbani chumba kipi?? Post comments zenye uhakika na si kubahatisha tu nenda sasa hivi zunguka labsa zote kuanzia za falcuties ambazo wanafunzi husika wa kitivi wanatumia free na mpaka computer labs za kulipia kama utakuta kuna lab yeyote imefunga.

BACK TO THE THREAD.
Huyu kitu mtui jamani mimi namfahamu vizuri sana ni mtu mwenye kupenda vurugu ni kijana ambaye anapenda sana kuona machafuko ndani ya chuo na aliuwepo pia kwenye vurugu za kudai maji juzi juzi tu hapa sasa sijui hata kipi kinachomfurahisha.

SIKUBALIANI NA HOJA YAKE YA KUJA KUOMBA MSAADA HAPA JF HATA KIDOGO, ZAIDI ZAIDI NINACHOWASHAURI WAKAE CHINI WAFIKIRIE KILICHOWAPELEKA CHUONI NA SI KUTANGA TANGA NA MIGOMO KILA KUKICHA KAMA KWELI WANASOMA ILI WAWE WATETEZI WA TAIFA HILI WAANZE KUJITETEA KWA HOJA ZINAZOENDANA NA USOMI WAO SI KWA KUANDAA VURUGU NA MIGOMO KILA KUKICHA.

NOTE:-
MIGOMO ALWAYS INAKUWA KIPINDI MITIHANI INAPOKARIBIA SASA HAPA MUST BE THERE IS SOMETHING

SHY at work once again . Huyu mtoto ana kichwa kibovu.Tumetoka kumkataa Brazamen na uongo leo anakuja na hadithi zile zile ? Hawa ndiyo wanao tumiwa kuandia ujinga ama kuacha kuandika habari za wananfunzi hawa .

Nawashauri sasa wana UDSM tafute nondo likisheni hapa .Kuanzia na Mgaya hadi Mukandara aweza kuzomewa nje na atakufa kwa pressure .JF spread the message .
 
Ila Wanafunzi majority wa Chuo kikuu wanudhi sana, leo wanalia wanaonewa kesho Makamba akiitisha mkutano Diamond Jubilee hawa jamaa watavalishwa Tshirt za Kijani Wakiwa wamepandishwa kwenye Mabasi wakiimba nyimbo za Kumsifu Makamba, ni lazima kwanza wabadilike hawa Watoto,
NI KWELI KBS TENA HUWA VIONGOZI HUPEWA HELA KIDOGO NA HUPOKEA JE WANASOMA NINI? ELIMU YAO INAWASAIDIA NINI TOFAUTI NA MTU AMBAYE HAJASOMA? VIPI NA HAO WALIOKAMATWA WAKIVUTA BANGI TUWATE TEE VIPI? MNATIA AIBU FAMILIA ZENU KAMA MLIVYOKRI NI ZA KIMASIKINI NA NI WATOTO WA WAKULIMA JE WAZAZI WENU NDO WANAOWAPA HIZO BANGI? KWA NINI MSISOME NILISIKITIKA SANA KUPATA HIZI HABARI ULEVI NA UASHERATI PIA MMEZIDISHA TUMIENI BUSARA KU-SOLVE MATATIZO YENU. USHAURI ZUNGUMZENI NA DARUSO WATAWASAIDI KUANDIKA BARUA KWA MUKANDARA WENZENU WARUDI KUSOMA NJIA MLIOTUMIA NI SAWA NA YA WATU AMBAO WAMEIISHIA DARASA LA SABA.
 
Mbona hutaki mahakama ?? mtu anaweza chaguliwa na kesi inaendelea mkishinda kesi si anafutwa?? wabunge wangapi wamenyanganywa ubunge na mahakama??

Ama mnajisitukia??
Mtu mwenyewe anakaa madarakani Mwaka 1 tu.
Kesi ikihairishwa mara 2 mwaka umeisha
 
Mimi nina interest na hizo allegation za MaProfessor wa chuo kikuu kuhonga waandishi wa habari ili habari zao zisiandikwe kwa usahihi.

Je tunaweza kupata ushahidi wa hili? Kama ukipatikana ushahidi hapa patakuwa pazuri pa kuanzia kuwa discredit hawa ma professor.
 
Unajua siku zinavyozidi kusonga nazidi kuwa na Hofu juu ya hawa wana UDSM. Sasa kama mtu ameleta hoja then anashindwa hata kuijengea nyama hiyo hoja yake tutamuita huyo ni msomi wa chuo kikuu?

Pia nakumbuka kuna jamaa yangu alikuwa ndio waziri wa Elimu pale UDSM akawa ananipa mipangilio yao ya migomo so hii migomo yao inamahusiano na Mitihani na Bumu... Mbona hawajagoma kwakuwa walimu hawaingii madarasani?

Nadhani kama funzo mumepata. Ninyi ni Tegemezi la Taifa sasa lazima muwe Active kila idara kama wasomi.
 
Mimi nina interest na hizo allegation za MaProfessor wa chuo kikuu kuhonga waandishi wa habari ili habari zao zisiandikwe kwa usahihi.

Je tunaweza kupata ushahidi wa hili? Kama ukipatikana ushahidi hapa patakuwa pazuri pa kuanzia kuwa discredit hawa ma professor.

The said prof
 
Mimi Niko Hall 6 Hapa Na Muda Mwingi Niko Hapa Eneo Hili Sasa Uliza Mtu Wowote Aliyekuwa Hapa Au Kule Yombo Atakwambia Wanafunzi Wamefanya Nini Kama Ni Uwongo Hawakujaribu Kuingia Katika Internet Cafe Moja Hapo Hall 6 Na Kurusha Mawe

Sisi Wote Tuko Udsm Sasa Wewe Sema Uko Eneo Gani Au Unaambiwa Tu Unakanusha ??
 
Mtu mwenyewe anakaa madarakani Mwaka 1 tu.
Kesi ikihairishwa mara 2 mwaka umeisha

kwa hiyo ninyi mnatafuta suluhisho la mda mfupi ok Well done

Mimi nilikifiri mnatafuta suluhu la kudumu.Na kama sio mahakama basi ufuateni uongozi wenu wa chuo muapigie magoti mfanye dialogue nao.But if u think its too expensive ok then CU
 
SHY at work once again . Huyu mtoto ana kichwa kibovu.Tumetoka kumkataa Brazamen na uongo leo anakuja na hadithi zile zile ? Hawa ndiyo wanao tumiwa kuandia ujinga ama kuacha kuandika habari za wananfunzi hawa .

Nawashauri sasa wana UDSM tafute nondo likisheni hapa .Kuanzia na Mgaya hadi Mukandara aweza kuzomewa nje na atakufa kwa pressure .JF spread the message .

HILI NI JUKWAA HURU KUMBUKA LUNYUNGU YAANI UPO SIJUI DUNIA GANI WEWE MZEE

DAH NYIE MAFISADI MNATIA HATA HURUMA
 
Back
Top Bottom