UDSM: Rais Kikwete atunukiwa PhD ya heshima katika sheria

Mimi ni mmoja wa wahitimu, tuko hapa Mlimani City, kwa mujibu wa kitabu cha majina ya wahitimu ukurasa wa 74 unaonyesha kuwa JK atalamba PhD ya Heshima kwenye Sheria wakati Museveni atapata ya fasihi. Vyanzo vingine vinathibitisha kuwa JK alizomewa Nkrumak sasa tatizo hapa ukumbini ni Elders tu sidhani kama watasemaje! Kaazi kweli kweli

Ya fine/performing arts angalau ingekuwa halali.
 
Nakutafuta ulipo..kama upo ndani hapa lazima nikubebe. Huwezi kuwa unatoa habari za kipuuzi kama hizi hapa JF

Hahahaha, mtu mzima hatishiwi nyau Kaka, njoo ilipo camera, mbele, tafuta bango lililoandikwa MASTER OF SCIENCE IN RENEWABLE ENERGY. Niko hapa mkuu, karibu unisaidie huu ujinga wangu unaousema! Nimevaa joho jeusi na skafu ya orange! Uko pande za wapi??
 
Wanaomzomea jk wametumwa na chadema.

Hongera uongozi wa Ud kutambua mchango wa jk. Hongera jk kwa kupokea gamba.
 
Ya fine/performing arts angalau ingekuwa halali.

Hahahahahaaa FPA ndio zinazomsaidia eeh! Ili aweze kutudanganya akiwa na smiling face. Mtaona atakapokuwa anavishwa joho hapo baadae
 
Hongera sana mh Jakaya.
Unastahili kabisa kutokana na kazi yako nzuri unayoifanya

Kazi gani aliyoifanya? Kuhongwa suti na mwanamme wenzake? au kuwalinda mafisadi na kusaini mikataba ya kipumbavu na kuuza ardhi yetu? Kama huna lakusema bora unyamaze kuliko kutibua hali ya hewa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mhhhh! Heshima hiyo kwenye sheria amekuwa nayo tangu lini? Amefanya lipi katika kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa mpaka astahili kupata tuzo hii!? USANII MTUPU!
 
Wanaomzomea jk wametumwa na chadema.

Hongera uongozi wa Ud kutambua mchango wa jk. Hongera jk kwa kupokea gamba.

Kumbe na wewe upo kazini? Walioanza kukataa ni UDASA na waliozomea (sikuwepo) walizomea kwa mtazamo wao na sio CDM.
 
Kazi gani aliyoifanya? Kuhongwa suti na mwanamme wenzake? au kuwalinda mafisadi na kusaini mikataba ya kipumbavu na kuuza ardhi yetu? Kama huna lakusema bora unyamaze kuliko kutibua hali ya hewa

chuo cha dodoma umejenga wewe. Hizi shule za kata ni zao la nani. Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.
 
Wanaomzomea jk wametumwa na chadema.

Hongera uongozi wa Ud kutambua mchango wa jk. Hongera jk kwa kupokea gamba.

Dah! Kwa kuwa madudu anayoyafanya tangu aingie madarakani ikiwemo kuruhusu ufisadi wa kutisha, nchi kuwa gizani, kupanda kwa gharama za maisha kwa kiwango cha kutisha, kuacha rasilimali zetu ziporwe n.k. yanawaathiri tu wale ambao ni supporters wa CHADEMA!!!! Wale wa magamba wanakula kuku kwa mrija hivyo hawaoni sababu ya kumzomea msanii!!!!
 
Hahahaha, mtu mzima hatishiwi nyau Kaka, njoo ilipo camera, mbele, tafuta bango lililoandikwa MASTER OF SCIENCE IN RENEWABLE ENERGY. Niko hapa mkuu, karibu unisaidie huu ujinga wangu unaousema! Nimevaa joho jeusi na skafu ya orange! Uko pande za wapi??
Hongera kwa kupata degree ya uzamili. Mwenzako kikwete aliipata hiyo long time sana. Jitahidi na wewe unaweza kuja kupata PHD ya heshima kama JK
 
Wewe kwa kuongozwa na fikra zako za kitumwa umeshindwa kuutambua mchango wa jk.
 
chuo cha dodoma umejenga wewe. Hizi shule za kata ni zao la nani. Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.

Sifa za kijinga, laiti ungefika ukaona majengo ya UDOM yalivyojaa nyufa, laiti ungeona shule za kata zinavyosikitisha!! Hakuna walimu, madawati, vitabu wala nyumba za walimu! Shule za kata ni magenge ya wahuni na malaya, naongea kitu ninachokijua na ukitaka tuanzishe mjadala wa shule za kata....utaniliza Mpwa naomba niishie hapahapa maana maisha ya watoto wetu yako rehani.
 
Kwenye kitabu kuna Jina la Eliezer Feleshi, anapata PhD ya sheria, huyu amesoma sasa sijui ndio Feleshi yule yule au labda ni majina tu!

Ndiye huyo huyo yes alikuwa anasoma PhD lakini kaanza juzi inakuwaje fupi hivyo ?
 
Kwenye kitabu kuna Jina la Eliezer Feleshi, anapata PhD ya sheria, huyu amesoma sasa sijui ndio Feleshi yule yule au labda ni majina tu!

Feleshi deserves it sio ya ubweche kagonga buku kweli
 
Dah! Kwa kuwa madudu anayoyafanya tangu aingie madarakani ikiwemo kuruhusu ufisadi wa kutisha, nchi kuwa gizani, kupanda kwa gharama za maisha kwa kiwango cha kutisha, kuacha rasilimali zetu ziporwe n.k. yanawaathiri tu wale ambao ni supporters wa CHADEMA!!!! Wale wa magamba wanakula kuku kwa mrija hivyo hawaoni sababu ya kumzomea msanii!!!!

kwahiyo ulikuwa unataka apewe Slaa anaye hamasisha vurugu kila siku.
 
Hongera kwa kupata degree ya uzamili. Mwenzako kikwete aliipata hiyo long time sana. Jitahidi na wewe unaweza kuja kupata PHD ya heshima kama JK

Asante sana Mpwa ila JK sio mwenzangu, mimi ni mimi na mwenzangu ni mke wangu! Mimi sio gamba ati, nashukuru kaka, uje basi tusalimiane baadae sio saa hizi ili tutete mawili matatu Mpwa
 
Sifa za kijinga, laiti ungefika ukaona majengo ya UDOM yalivyojaa nyufa, laiti ungeona shule za kata zinavyosikitisha!! Hakuna walimu, madawati, vitabu wala nyumba za walimu! Shule za kata ni magenge ya wahuni na malaya, naongea kitu ninachokijua na ukitaka tuanzishe mjadala wa shule za kata....utaniliza Mpwa naomba niishie hapahapa maana maisha ya watoto wetu yako rehani.

yeye ndiye aliyesababisha hizo nyufa au ni wachina.
 
Mimi ni mmoja wa wahitimu, tuko hapa Mlimani City, kwa mujibu wa kitabu cha majina ya wahitimu ukurasa wa 74 unaonyesha kuwa JK atalamba PhD ya Heshima kwenye Sheria wakati Museveni atapata ya fasihi. Vyanzo vingine vinathibitisha kuwa JK alizomewa Nkrumak sasa tatizo hapa ukumbini ni Elders tu sidhani kama watasemaje! Kaazi kweli kweli

mimi pia ni mmoja wa wahitimu tunaotunukiwa degree jumanne ila sas hiyo taarifa inanikosesha mud ya kuhudhuria mahafali yang
 
Back
Top Bottom