yeah halafu ni profesa aliyebobea kwenye kiswahili.
mbona mnajadili kwa utani suala nyeti kama hili? Mtu mmoja ajitolee kutoa maelezo ya kina ili rais alipate vizuri. Tuko kwenye wakati wa safisha serikali. Tuko serious na mambo yanayotuharibia hatutaki tena. Huyu mtu hawezi kutajwa kila siku kwamba ni tatizo halafu anaendelea kuwepo kuwa madarakani. Udom ni legacy ya rais kama kuna mtu anaiharibu kwa maslahi binafsi asiachwe hapo tena. Kikwete tembelea udom, tuma watu wako wa usalama, takukuru, polisi na cag kwa pamoja haraka pale kamuondoe huyo kidudu mtu. Hao ndio wanaotuletea shida nchi hii yenye kila neema kadiri ilivyojaliwa na subwana wa taala. Eee mungu umjalie kikwete uwezo wa kumwondoa mlacha. Au mpaka watoto wagomeeee kama madaktari kwa mponda? Au mpaka kamati kuu ya ccm ikushauri? Hapana kikwete inuka chukua hatua dhidi ya kiswahili specialist huyo wa udom.