Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Mh. Rais tumesikia mengi yanayoendelea katika siri-kali yako. Kashfa juu ya kashfa na hii imepelekea Waziri Mkuu na Rafiki yako kujiuzuru baada ya kuona hana njia ya kuleta mambo ya Kisungura. Vilevile umevunja baraza lako kwa sababu ya huyo Mh. ku-resign. Anyway sababu kuwa ya Lowassa kujiuzuru ni kile kuwa -implicated na Kamati ya Mwakyembe. Lakini tunajua kuwa bado kuna sakata zingine huko hazijatolewa ripoti kama vile BOT, BUZWAGI,SONGAs n.k
Katika report 2 tayari wamemhusisha rafiki yako mkubwa Mh. Rostam Aziz, huyu Mh. sana ambaye hata dola inaogopa kumsogelea ameibia sana wananchi. Hii ni kwa mujibu wa hizo report 2 na si mimi. Watu wako wa karibu wamehusishwa na hizi kashfa Lowassa, Rostam, Amb. Young na wengineo. Mie nilifikiri watanzania wanapenda kujua ukweli na kuaminishwa kuwa WEWE AS EITHER JAKAYA KIKWETE OR THE PRESIDENT OF TANZANIA hujui kinachoendelea juu ya hawa watu. Nashangaa watu hawamzungumzii kabisa Rostam Aziz na biashara zake haramu kwa watanzania lakini halali kwake yeye na kundi lake analolijua ambalo wanagawana hizo Mil. 152 Naamini kwa njia moja au nyingine hizi kashfa zinakusumbua sana kichwa especially zinapowahusisha marafiki zako. So U need to come clean na njia nyepesi kuwaeleza watanzania kuwa wewe hahuusiki kwa njia moja au nyingine ni kuhakikisha kuwa:-
1. Account zao zinakuwa FROZEN (Nje na ndani ya nchi)
2. Wanapelekwa MAHAKAMANI na si kishikaji kama tulivyoona kwa Mzee DITO.
3.Wakionekana Guilty then mali zao pamoja na fedha zitaifishwe na serikali
4. Wafungwe kwa mujibu wa sheria za UHUJUMU UCHUMI.

Vinginevyo urais 2010 utausoma kwenye magazeti tu. Tunajua kabisa kuwa bila utashi wako Kamati ya Mwakyembe isingeenda popote, ingepata findings na kuwa kama kamati zingine. Kwa hilo ninakupongeza sana. Lakini nina wasiwasi kuwa taasisi ambazo ulizipa maelekezi zitafute ukweli kuhusu sakata ya BOT. Hii TAKUKURU sina imani nayo kabisa maana ilidanganya Serikali, Bunge na wananchi kuwa ule mkataba wa Richmond ulikuwa safi na haukuwa na makosa makubwa ya kuiathiri nchi. Leo hii tunaambiwa kuwa kulikuwa matatizo kibao mara ya kubalidili LC, majina ya kampuni, taratibu za kupatikana mzabuni na mengineyo. Sasa tena inapewa jukumu jingine la kutafuta ukweli juu ya BOT, Mh. Rais huoni kama kutakuwa ule mchezo wa kulindana, maana tumesoma katika baadhi ya vyombo habari kuwa ile pesa baadhi ilikwenda kwenye uchaguzi wa CCM ambao ulikupitisha kugombea. Na hawa watu wamewekwa na Chama Tawala kupitia kwako. Mie nilifikiri kuwa tungetumia chombo huru kuangalia undani wake maana siamini IGP, AG (Ambaye ameonyesha UDHAIFU kwenye Mkataba wa Richmond), TAKUKURU wakasema uchafu ulifanyika na fedha zingine zilitumika uchaguzi CCM. Nafikiri hapo hapo watakuwa wamejifukuzisha kazi. Nafikiri tungetumia taasisi za kimataifa zinazoheshimika kwa uchunguzi maana naamini kuna International Transactions took place.
Nafikiri bado una nafasi nzuri ya kujisafisha before 2010. Tanzanians want you to come clean. Kazi unayo Baba Ridhwani maana unatakiwa kusafisha huko BRELA, TAKUKURU hadi hapo IKULU. Na suala la Mkapa na Yona husitake kujifanya kuwa una NTA masikioni au umesahau, hawa watu wanatakiwa kuchunguzwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Watanzania wanaishi kimasikini, kila mtu anapenda unafuu wa maisha, sasa huu sio wakati wa kulipa fadhila eti he fought for you to get The CCM Nomination, pls. Haki isimame kwa kila mtu anayeishi kwenye ardhi ya Tanzania bila kujali rangi au uwezo kipesa. SUALA HAPA NI UHUJUMU UCHUMI, RUSHWA, UFISADI N.K Urafiki sasa hivi weka pembeni vinginevyo U'll pay A PRICE 2010, na hii si utani maana watanzania wamechoka na usanii na ubabaishaji.
Hii mikataba UCHWARA itafutwe jinsi ya kuivunja bila kuiathiri serikali. Itafutwe namna either kupitia bunge na Mahakama pamoja na wahusika wenyewe. Serikali bado inalipa Mil.152 kila mwezi kwa kampuni ya DOWANS ambaye mmiliki wake ni mshirika/rafiki yako ambaye yumo humo humo Bungeni. Jamani kweli hii nchi inaliwa kweli. Na bado huyo mtu anapewa dhamana na IKULU kutafuta watu to work for President. Najua haya mambo yalikuwa ya kibiashara (Richmond & TANESCO) lakini naamini unaweza ku-tight grip na huyu Mh. wa Igunga aka-make something for the sake of the country.
 
Baada tu ya kuapishwa na kuanza kuunda Serikali, Rais kikwete aliwapa nafasi maswahiba zake "washkaji" nafasi katika serikali yake.
Si jambo geni kwani wengi wetu ndio njia ya kusema asante hasa kwa waliokusaidia kwa njia moja au nyingine kufika pale, lakini serikali ya Kikwete imejaa washkaji kila mwenye nafasi ni jamaa au mshkaji wake wa kari jambo ambalo linampa wakati mgumu sana kama kunatokea uwajibikaji inasababisha kuoneana haya!! Najribu kufikiria suala la EL linavyomuumiza kichwa nini cha kufanya, maana bado hajasema ni hatua gani watachukuliwa!!

Utamfanya nini mtu kama Rostam aliyeta Bilioni mbili kuipa CCM kwenye uchaguzi? Leo hii anakula matunda ya mchango!!!

Mkapa aliweza kuwapa nafasi watu wengi hasa baada ya kimshinda Kikwete kwenye Uchaguzi wa nani mgombea wa CCM na alitaka kuwapa nafasi hasa walikuwa kambi Pinzani yaani kambi ya Kikwete ili aonekane amevunja makundi kwa mantiki ya "Ngoja tuwape tuone watafanya nini...!!" hii iliwafanya kufanya kazi kiadilifu (Ingawa wapo walipotea tena sana tu).

Ninachotaka kusema ni hivi Wengi wa Maswahiba wa kikwete Watamtenda na bado wanakuja ngoja Ripoti ya Madini nayo ije?
Na Zitto akicheza karata zake uzuri yao mengi yataibuka hasa baada ya hizi Kafara 3 za mwanzo, wenyewe wataanza kutajana!!
 
Let try to monitor our president from today on his daily activities. Let start with this one. I'll try my best update this thread!

HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA UMOJA WA AFRIKA WAKATI WA MKUTANO WA KUMI NA MOJA WA WAKUU WA NCHI WA UMOJA WA AFRIKA UTAKAOFANYIKA
SHARM EL SHEIKH MISRI TAREHE 30 JUNI 2008

Mheshimiwa Hosni Mubarak, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri;
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Afrika;
Mheshimiwa Jean Ping, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika;
Mheshimiwa Asha-Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa;
Waheshimiwa Waalikwa;
Mabibi na Mabwana:

Naomba nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya Misri kwa kukubali kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Kwa niaba ya Umoja wa Afrika na kwa niaba yangu binafsi napenda kumshukuru Rais Hosni Mubarak na Serikali ya Misri kwa mapokezi mazuri na kwa kutuangalia vizuri tangu kuwasili kwetu katika mji huu mzuri wa Sharm el Sheikh. Napenda pia kuwashukuru kwa maandalizi mazuri ya mkutano na kutupatia mahali pazuri pa kufanyia mkutano wetu. Naamini hayo yatatuwezesha kufanya mkutano wetu kwa mafanikio.

Niruhusuni niitumie nafasi hii kuwapongeza viongozi wapya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika chini ya uongozi wa Mheshimiwa Jean Ping kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya. Huu ni mkutano wao wa kwanza wa ngazi hii kusimamia. Pamoja na ugeni wao, Kamisheni imeweza kuandaa mambo yao kwa ufanisi wa hali ya juu. Ni mwanzo mzuri. Endeleeni na ari hiyo hiyo kwa siku zijazo ili Umoja wetu uweze kufikia lengo lake.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi;

Mwezi Januari 2008 mlinichagua kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Katika kukubali heshima kubwa mliyonipa niliahidi kutetea maslahi ya Umoja wa Afrika na ya Bara letu kwa uwezo wangu na kwa kutumia vipaji vyangu nilivyojaliwa na Mwezi Mungu. Katika ajenda yalikuwepo mambo yahusuyo kuimarisha Kamisheni ya Umoja wa Afrika, migogoro mbalimbali inayolikabili Bara letu na kushughulikia changamoto nyingine zinazolikabili nchi zetu na watu wake.

Aidha, niliahidi kujitahidi kutafuta fursa zitakazoliletea Bara letu maendeleo na ustawi katika nyanja za siasa, uchumi, ulinzi na usalama, ustawi wa jamii na utamaduni.

Katika kipindi cha miezi sita hii ya kwanza Umoja wa Afrika umeendelea na jitihada zake za kutatua migogoro inayolikabili Bara letu.

Tumeweza kupata mafanikio ya kutia moyo kwa kupata ufumbuzi katika nchi za Kenya na Comoro. Mtakumbuka kuwa ndugu zetu wa Kenya waliingia katika machafuko makubwa baada ya uchaguzi. Umoja wa Afrika ulijihusisha kwa ukamilifu kwa kuwatuma viongozi wake wastaafu Mheshimiwa Kofi Annan, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na Mheshimiwa mama Graca Machel kusuluhisha.

Haikuwa kazi rahisi lakini kwa umakini wa viongozi wetu hao na ushirikiano mkubwa walioupata kutoka kwa Mheshimiwa Rais Mwai Kibaki na Mheshimiwa Waziri Mkuu Raila Odinga suluhu ilipatikana. Serikali ya Umoja iliundwa na Kenya sasa ni shwari. Napenda kuitumia nafasi hii kuwapongeza viongozi wasuluhishi.

Lakini pongezi maalum tuwape Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga kwa moyo wao wa upenda kwa nchi yao na watu wao. Waliachilia mbali ubinafsi wao na kutanguliza mbele maslahi mapana ya nchi yao na watu wao. Ni mfano wa kuigwa na wengi tunaokabiliwa na migogoro katika nchi na jamii zetu.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;

Mtakumbuka uamuzi wetu katika kikao kilichopita wa kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho la Comoro kukomesha uasi katika Kisiwa cha Anjouani na kurejesha mamlaka ya Serikali ya Shirikisho kwa visiwa vyote.

Kama mlivyoelekeza Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika likishirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Serikali ya Comoro iliziomba nchi za Libya, Senegal, Sudan na Tanzania kutekeleza uamuzi wenu. Nchi hizo zilikubali.

Libya, Sudan na Tanzania zilitoa majeshi kwa kushirikiana na Jeshi la Comoro yalifanikiwa kumwondoa kiongozi muasi wa Anjouani Kanali Mohamed Bacar bila ya madhara kwa mali na maisha ya raia wa visiwa hivyo. Mamlaka ya Serikali ya Shirikisho yamerejea nchi nzima. Inafurahisha na kutia moyo kwamba hali katika kisiwa cha Anjouan sasa ni shwari na maandalizi ya kufanyika kwa uchaguzi huru na haki ksiwani humo yanaendelea.

Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba yenu wote kuzishukuru nchi za Libya, Sudan na Tanzania kwa moyo wao wa kujitolea. Uamuzi wao umeupa heshima kubwa Umoja wa Afrika. Nawashukuru na kuwapongeza wananchi wa Comoro na hasa wa Kisiwa cha Anjoaun kwa kuunga mkono uamuzi wa Umoja wa Afrika.

Kuunga kwao mkono ndiko kulikowezesha zoezi hili kutekelezwa kwa salama. Natoa mwito kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kuhakikisha kuwa matayarisho yanakamilika kama ilivyopangwa na kwamba shughuli nzima inatekelezwsa kwa kuzingatia misingi ya kidemokrasi na uchaguzi unakuwa huru na haki ili Anjouan ipate uongozi inaoutaka.

Waheshimiwa Viongozi Wenzangu;

Vilevile Umoja wetu unaweza kujivunia maendeleo ya kutia moyo yaliyopatikana katika jitihada za kutafuta amani ya kudumu nchini Burundi. Chini ya uongozi wa nchi za Maziwa Makuu na usuluhishi wa Serikali ya Afrika ya Kusini hatimaye viongozi wote wa juu wa Kikundi cha PALIPEHUTU-FNL, akiwemo Mwenyekiti, Bwana Agathon Rwasa wamerejea Bujumbura. Hivi sasa viongozi hao wa waasi wanaendelea kufanya kazi na wenzao katika Serikali na vyama vingine vya siasa katika mchakato wa utekelezaji wa Mkataba wa Kusitisha Mapigano.

Umoja wa Afrika ufuatilie kwa karibu yanayoendelea nchini Bundi ili kuhakikisha kuwa mambo yanatekelezwa kama ilivyokusudiwa. Ni mategemeo yangu kwamba pande zote husika zitaelekeza juhudi zao katika kutekeleza makubaliano yao ambayo yanafungua ukurasa mpya wa amani iliyopotea Burundi tangu mwaka 1993. Aidha, natoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, kusaidia juhudi hizi kwa kutoa mchango wa hali na mali kuisaidia Burundi kuvuka kipindi hiki kigumu.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali, Mabibi na Mabwana;

Pamoja na mafanikio hayo na mengine ambayo sikuyataja bado Umoja wa Aflrika unakabiliwa na changamoto za kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Jimbo la Darfur na kubwa likiwa kufanikisha mazungumzo ya makundi ya waasi na upelekaji wa wanajeshi wa Jeshi la Mseto la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Kadhalika, bado Somalia mambo hayajakaa sawa hususan upatikanaji wa kuzitaka nchi wanachama kujitolea kuchangia wanajeshi kwenye Jeshi hilo.

Hali ya kutokuaminiana na kuhasimiana baina ya Chad na Sudan inahitaji kuendelea kushughulikiwa ili kuzuia hali kuharibika zaidi.

Umoja wa Afrika hauna budi kuendelea kufuatilia kwa karibu hali ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa nia ya kuisaidia nchi hiyo ifanikiwe kumaliza matatizo kadhaa ya kiusalama yaliyopo huko.

Wakati huo huo Umoja wa Afrika ufanye kila iwezalo kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliozuka baina ya Eritrea na Djibouti. Ni mgogoro ambao haustahili kuwepo na hivyo haustahili kuendelea kuwepo.

Katika kipindi hiki pia tumeshuhudia uchaguzi wa kihistoria ukifanyika nchini Zimbabwe. Uchaguzi huo ambao umefanyika kwa awamu mbili umekuwa na mazuri yake na changamoto zake. Awamu ya kwanza ilikuwa shwari na kupata sifa nyingi. Awamu ya pili ilikuwa na changamoto nyingi kuanzia kabla ya kampeni za uchaguzi, wakati wa kampeni na wakati wa uchaguzi wenyewe.

Na changamoto za baada ya uchaguzi wa juzi. Napenda kutumia fursa hii kuzipongeza nchi wanachama wa SADC hususan Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini kwa jitihada kubwa ya kujaribu kusuluhisha mgogoro wa Zimbabwe. Umoja wa Afrika uendelee kufanya kila linalowezekana ili kuwasaidia ndugu zetu wa Zimbabwe kupita katika kipindi hiki kigumu kinachowakabili kwa salama na amani. Umoja wa Afrika ushirikiane kwa karibu na SADC katika jukumu hili.

Jitihada za makusudi zinahitajika kutafuta ufumbuzi wa kudumu utakaomaliza migogoro Barani Afrika. Ni mingi mno na mingi haina sababu za msingi kuwepo. Inasababishwa na sisi viongozi kwa sababu zetu ambazo nyingi hazina maslahi kwa wananchi tunaowaongoza. Wananchi wa Bara la Afrika wameteseka sana kwa migogoro. Hakika wamechoshwa na migogoro hii ambayo ni kikwazo kikubwa cha kupatikana maendeleo katika Bara letu. Bila amani hakuna maendeleo. Sisi viongozi tunao wajibu wa kuwaondolea wananchi tunaowaongoza mateso hayo.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;

Kwa upande wa uchumi, tumeendeleza juhudi za kutafuta fursa za kuendeleza na kukuza uchumi wa Bara letu. Umoja wa Afrika umeendelea na jitihada zake za kupata marafiki zaidi wa kushirkiana na washirika wa kiuchumi ili kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo katika Bara letu. Katika jitihada hizo tarehe 9 Aprili 2008, Umoja wa Afrika na India zilianzisha rasmi ushirikiano wa kiuchumi.

Ushirikiano ulioanzishwa unalenga maeneo ya kilimo, biashara, sayansi na teknolojia, miundombinu, elimu, utamaduni na michezo. Katika kutekeleza ushirikiano huo, Afrika na India zimekubaliana kuwa na Mpango Kazi(Action Plan) moja. Kamisheni ya Umoja wa Afrika ilipewa jukumu la kusimamia mchakato wa kuandaa Mpango Kazi huo.

Naamini nawasemea nyote nikisema kuwa matumaini yangu kwamba kazi hiyo itakamilika mapema iwezekanavyo ili nchi zetu zianze kufaidi matunda yake. Katika kipindi kilichobaki cha Uenyekiti wangu tutaendelea na jitihada hizi kwa kukutana na Uturuki mwezi Agosti, na nchi za Amerika ya Kusini mwezi Novemba.
Kwa upande mwingine tumeendelea kuimarisha uhusiano wetu na washirika wetu wa zamani. Kwa ajili hiyo, Mkutano wa Nne wa Ushirikiano kati ya Afrika na Japan (TICAD IV) ulifanyika mjini Yokohama, Japan, tarehe 28 hadi 30 Mei 2008.

Ushirikiano huu unalenga katika kuweka utaratibu wa kuisaidia Afrika kukuza uchumi wake na kujiletea maendeleo. Katika mkutano wa Nne wa TICAD Japan imetangaza fursa kadhaa za kusaidia kukuza uwekezaji na biashara baina ya Japan na Afrika. Kadhalika Japan imetangaza nia yake ya kuongeza misaada maradufu ya maendeleo Barani Afrika katika kusaidia kuendeleza huduma za kiuchumi na kijamii hususan miundombinu, afya, elimu na hifadhi ya mazingira. Hii ni fursa nyingine ambayo hatuna budi kuchangamkia kuitumia ili kuongeza kasi ya kupunguza umaskini na kuleta maendeleo.

Waheshimiwa Viongozi wenzangu;

Ni jambo la kutia faraja sana kwamba katika miaka ya hivi karibuni uchumi wa Afrika umeonyesha dalili nzuri za kuimarika. Hata hivyo, mafanikio hayo yaliyopatikana kwa jitihada kubwa za watu wetu yanatishiwa na matatizo yanayoukabili uchumi wa dunia.

Kwanza lipo tatizo la kupanda sana kwa bei ya mafuta na wala hakuna muelekeo wa kupungua. Bei ya mafuta katika soko la dunia imeongezeka kutoka dola 50 kwa pipa Decemba, 2005 na sasa inakaribia dola 150 kwa pipa. Tatizo la pili ni kupanda sana kwa bei za vyakula kulikosababishwa na kupungua kwa uzalishaji wa mazao ya chakula hususan nafaka.

Kulingana na takwimu za Shirika la Kilimo Duniani (FAO) kati ya nchi 37 zilizoathirika zaidi duniani 21 ziko Barani Afrika. Bei za vyakula duniani zimepanda kwa asilimia 75 tangu mwaka 2000 na hakuna dalili za kushuka katika siku za hivi karibuni.

Athari za bei kubwa za mafuta na chakula duniani ni kubwa sana kwa watu wote duniani lakini ni kubwa zaidi kwa nchi maskini na zinazoendelea (nyingi zikiwa Barani Afrika). Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kutokana na kupanda sana kwa gharama za maisha. Uwezo wa Serikali zetu kuwahudumia wananchi wake unazidi kuathirika. Matatizo hayo ukichanganya na lile la kutetereka kwa mfumo wa fedha wa dunia lililoanzia Marekani na kuenea Ulaya yanatishia kudhoofisha kasi ya kukua kwa uchumi wa dunia nzima.

Ili kukabiliana na changamoto hizi, nchi za Afrika hazina budi kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano. Bila kushirikiana itakuwa vigumu kwa nchi zetu kushinda changamoto hizi kutokana na uchanga wetu kiuchumi. Wahenga wamesema “Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu”. Hatuna budi kushirikiana kudai mageuzi ya mfumo wa fedha duniani na upangaji wa bei za mafuta. Kwa sasa hakuna mtu wala chombo kinachosimamia.

Mambo yako mikononi mwa wajanja wachache wasiojali maslahi au mateso ya wengi. Soko huria tunalitaka lakini mambo yasiachwe holela kama ilivyo sasa. Hali hii isipodhibitiwa uchumi wa dunia unaweza kuangamizwa. Watu wanateseka hasa katika nchi zinazoendelea. Nafurahi kwamba matatizo ya bei za mafuta na yale ya upungufu wa chakula na bei kubwa ya vyakula yatazungumzwa katika mkutano wetu huu. Nawaomba wenzangu tuyape uzito unaostahili.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;

Katika mkutano wetu wa Januari, 2008 tulikubaliana kuwakabidhi viongozi wenzetu 12 kutafakari kwa kina suala la kuundwa Serikali ya Umoja ya Afrika. Nafurahi kutoa taarifa kuwa viongozi hao wameifanya kazi hiyo na taarifa yao itatolewa.

Ni matumaini yangu na maombi yangu kwenu kuwa tutayapokea na kuyajadili mapendekezo hayo kwa utulivu na busara ili tuweze kufikia maamuzi yatakayotusogeza mbele zaidi katika safari yetu ya kuelekea kwenye taifa moja la Afrika. Tuepuke jazba na kushutumiana. Mambo hayo hayatajenga bali yatatugawa.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;

Naomba nihitimishe hotuba yangu kwa kugusia kidogo mada kuu ya mkutano wetu ambayo itahusu suala la Maji Safi na Maji Taka. Maji ni rasilimali muhimu na adimu ambayo inapaswa kupewa kipaumbele cha kipekee.

Nchini Tanzania tuna usemi usemao maji ni uhai, ikimaanisha kuwa maisha ya viumbehai yanategemea sana maji. Bila maji hakuna uhai.Licha ya Bara letu kuwa na vyanzo vingi vya maji, takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa rasilimali hiyo inapungua siku hadi siku kutokana na kuongezeka kwa matumizi na uharibifu wa mazingira. Mijini na vijijini upatikanaji wa maji umekuwa ni tatizo kubwa.

Kwa mfano, takwimu zinaonyesha kuwa katika nchi 27 za Afrika, watu watatu kati ya 10 hawapati huduma ya maji safi. Kutokana na hali hii wananchi wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hii.

Pale yanapopatikana mara nyingi maji hayo yanakuwa sio safi na salama kwa matumizi ya binadamu na hivyo yamekuwa chanzo cha magonjwa mengi ya milipuko. Asilimia 40 ya vifo vya watoto duniani vinavyosababishwa na ugonjwa wa kuhara hutokea Barani Afrika. Chanzo chake kikuu ni watu kutumia maji yasiyo safi na salama.

Hivyo ni matumaini yangu kuwa mkutano huu utatoa mapendekezo mazuri kuhusu uendelezaji matumizi mazuri ya rasilimali hii adhimu na adimu kwa ajili ya uhai wa watu wetu na maendeleo ya bara letu.

Lakini, tunaijadili mada hii ikiwa ni moja ya Malengo manane ya Milenia yaliyoamuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2000. Kama tujuavyo Septemba 25, 2008 kutakuwa na kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuzungumzia utekelezaji wa Malengo ya Milenia katika Bara la Afrika. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameendeleza juhudi za kusaidia Afrika kupatiwa misaada inayotakiwa ili iweze kutekeleza malengo hayo.

Taarifa iko tayari na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametufafanulia. Natumai katika kikao hiki tutajipa nafasi ya kuzungumzia hali ya utekelezaji wa malengo ya Milenia ili kujiandaa kwa kikao cha Septemba, 2008 huko New York.
Baada ya kusema hayo sasa natangaza mkutano umefunguliwa rasmi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.
 

Attachments

  • 080630 SPEECH AU 11th Summit - MISRI.doc
    64 KB · Views: 111
Brilliant Idea! I can see where this is going. All the top ministers, then all key public figures.
 
Tutegemee nini katika hii thread? Hotuba, ratiba?
Unategemea mchango wowote toka kwa wana jf?
 
Misri ni jamhuri ya kiarabu, je yafaa kuwa sehemu ya Afrika?

mipaka tulioachiwa urithi na wakoloni, tuna nguvu ya kuipinga?
kwanza kuna mtu anataka kupingana na hali ilivyo?
kama makabila yalivyotengwa nchi mbili tofauti wamasai, wahaya, wachaga nk
 
Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine. Katika pita pita yangu na kuchunguza nimegundua kuwa asilimia 65.78 ya uongozi wa Kamati Kuu ya CCM ni watu wa dini moja. Kama udini ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani, tunaweza kusema kusema kuwa Kamati Kuu ya CCM ina udini? Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?

Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.

Katika siasa, tukitumia "Wangwe's Doctrine" kuwa endapo asilimia 50 ya watu wenye sifa hizo wakakutwa mahali pamoja ni ukabila/ukanda basi ni wazi mahali ambapo pana asilimia 65 ya watu wenye kulingana sifazao kutofautishwa na wengine basi napo patakuwa na tatizo, in this case udini (yaani idadi ya watu wa dini moja mahali pamoja ambayo haina maelezo ya kuridhisha).
 
Mzee Mwanakijiji naona sasa kijijini umeamua kufuatilia kotekote kujua kile kinachoendelea ndani ya siasa za Tanzania.

Swali kubwa sana ambalo limekuwa linaulizwa hapa bila kupata majibu toka kwa wana ccm. Kama kuna uwezekano wa kuangalia majina ya watu na kujua makabila, mikoa, lugha, wake/waume, wakwe, watoto, dini na mengine mengi katika chama kikubwa cha upinzani Tanzania - CUF au chama kinachochipuka cha Chadema, basi kipimo hicho chaweza kutumika kabisa kujua kama kuna udini au hata ukabila ndani ya chama tawala cha ccm.

Kazi kweli kweli Mzee Mwanakijiji.
 
Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine. Katika pita pita yangu na kuchunguza nimegundua kuwa asilimia 65.78 ya uongozi wa Kamati Kuu ya CCM ni watu wa dini moja. Kama udini ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani, tunaweza kusema kusema kuwa Kamati Kuu ya CCM ina udini? Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?

Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.

Katika siasa, tukitumia "Wangwe's Doctrine" kuwa endapo asilimia 50 ya watu wenye sifa hizo wakakutwa mahali pamoja ni ukabila/ukanda basi ni wazi mahali ambapo pana asilimia 65 ya watu wenye kulingana sifazao kutofautishwa na wengine basi napo patakuwa na tatizo, in this case udini (yaani idadi ya watu wa dini moja mahali pamoja ambayo haina maelezo ya kuridhisha).

Dini haielezi utofauti wao, nafikiri kwa kuwa asilimia zaidi ya 90 ni waumini wa dhehebu jipya linaloitwa mafisadi. Hivyo tusiogope uislamu au ukristo wao, isipokuwa imani yao isiyotetereka juu ya ufisadi ambayo kwao ni dini takatifu kabisa.
 
Vigezo alivyotumia mwanakijiji kufikia kusema kuwa kamati kuu ya ccm ina udini ni dhaafu kabisa, yani ikutmia vigezo kama hivyo karibu kila idara ya serikali ya Tanzania utasema in udini.
 
Tatizo ni Zenji Factor. Nadhani Zenji wanachangia 50% ya members wanaoingia kwenye CC. Hapo sijaweka wale ambao wanaingia huko kwa heshima ama kwa nyadhifa zao (viongozi wakuu wa Chama wa pande zote mbili, marais wastaafu na wazee wa chama kama akina Kawawa).

Ukishaweka hiyo Zenji factor automatically lazima utaishia kwenye conclusion ya Mwanakijiji.

Labda swali la kujiuliza ni kwanini Zenji inapewa nafasi sawa na Bara?
 
Vigezo alivyotumia mwanakijiji kufikia kusema kuwa kamati kuu ya ccm ina udini ni dhaafu kabisa, yani ikutmia vigezo kama hivyo karibu kila idara ya serikali ya Tanzania utasema in udini.

Je kuna tofauti kati ya hivi vigezo na vile vinavyotumika kusema kuwa CUF ni chama cha kidini?
 
Tatizo ni Zenji Factor. Nadhani Zenji wanachangia 50% ya members wanaoingia kwenye CC. Hapo sijaweka wale ambao wanaingia huko kwa heshima ama kwa nyadhifa zao (viongozi wakuu wa Chama wa pande zote mbili, marais wastaafu na wazee wa chama kama akina Kawawa).

Ukishaweka hiyo Zenji factor automatically lazima utaishia kwenye conclusion ya Mwanakijiji.

Ukweli ni kwamba, ukianza kuchunguza maeneo au majina au makabila ya watu ili kuangalia kama kuna udini au ukabila basi utajikuta unakosa kanuni kamili ya kufikia hitimisho lako.

Kwa msingi huu, mimi nilisema hapa muda mfupi baada ya uchaguzi wa ccm kuwa ccm ni chama cha kiislam kwa vile viongozi wake asilimia 75 (kwa hesabu zangu na ufahamu wangu) ni waislam.
 
Tatizo ni Zenji Factor. Nadhani Zenji wanachangia 50% ya members wanaoingia kwenye CC. Hapo sijaweka wale ambao wanaingia huko kwa heshima ama kwa nyadhifa zao (viongozi wakuu wa Chama wa pande zote mbili, marais wastaafu na wazee wa chama kama akina Kawawa).

Ukishaweka hiyo Zenji factor automatically lazima utaishia kwenye conclusion ya Mwanakijiji.

Sasa isn't that a grand example of upendeleo usio wa lazima. Iweje CCM Zanzibar ichangie asilimia 50 ya wajumbe wa NEC?
 
Sasa isn't that a grand example of upendeleo usio wa lazima. Iweje CCM Zanzibar ichangie asilimia 50 ya wajumbe wa NEC?

kwi kwi kwi,

labda ccm ni "chama cha wazanzibar" kama "chadema kilivyo chama cha wachaga" au "cuf kilivyo chama cha wapemba" kama wengine wanavyosema hapa.
 
Huyu bwana Mwanakijiji anataka kuturudisha kwenye enzi za zama za mawe!!!!!. Kesho utatuambia hata Taifa stars imejaa udini..... Ushauri wangu: tuangalie uwezo ktk utendaji and not otherwise. Au unataka kuwa-criticize CCM (aka chama cha mafisadi) wanapotumia hoja ya kibaradhuli kwa kusema Chadema au CUF ni vyama vya udini ....kwa wewe nawe kujifanya baradhuli? Mbwa akikung'ata na wewe utachuchumaa umng'ate?????
 
Wakati mnaendelea na mjadala, wajumbe wenyewe ndo hawa hapa:

1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Moh'd Yussuf - Mjumbe
 
baada ya vyama vya siasa inatakwenda kwenye wizara na ofisi za serikali kucheck kama kuna bias ya dini au kuna equal presentation. Huu ubaguzi utakua bila kujua. JF ni influencial na one have to be very careful in articulating topics, everyone should be responsible for his actions.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom