Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
I have noted with appreciation your positive commentary on AR.
Hapa unafanya kosa jingine kubwa; The Wealth of Nations cha Adam Smith siyo sawa na Azimio la Arusha. Hivi viwili haviko katika usawa mmoja. Kimoja ni kitabu chenye kuelezea nadharia mbalimbali za mfumo wa ubepari na Azimio la Arusha ni tangazo la makusudio ya msimamo wa utawala wa watu huru. AR siyo kitabu cha nadharia za kiuchumi.
Na hata hicho the WN leo hii kinaangaliwa kikiwa na masahihisho mengi sana ya kihistoria na nadharia yake ya Invisible hand imeonekana kuwa haina ukweli kwani hakuna kitu kama hicho. Ndio maana utaona kuwa ukiangalia kwa ukaribu mfumo wa Ujamaa uliopendekezwa na Mwalimu una mvuto zaidi wa ukweli wa hulka ya mwanadamu kuliko the Wealth of Nations (Mwalimu alimsoma sana Adam Smith na kuona mapungufu yanadharia zake).
Ni makosa makubwa kuendelea kuamini kuwa Adam Smith alikuwa sahihi wakati nchi zenyewe za Kibepari zikiachana taratibu na ile form ya pure capitalism.
AR mirrors kazi za kifalsafa za Nyerere. Hivyo tofauti kati Adam Smith na Nyerere ni kuwa kazi za Adam Smith ziliishia kwenye Falsafa tu kwa sababu hakupata nafasi ya kuwa mtawala. Lakini na yeye angepata nafasi ya kutawala, basi angetoa perspectives za jinsi ya kujitawala ambazo zingekuwa na uhusiano na falsafa zake.
Watanzania hatujawahi kutanga makusudio ya jinsi ya kujitawala. Azimio la Arusha ni intellectual work ya mtu mmoja na ilihusiana na siasa za chama chake cha siasa. Hivyo kulipandisha Azimio la Arusha kuwa tangazo la azimio la kujitawala is a bit of an exaggeration. Imefika wakati wa kuheshimu mawazo ya wananchi na sio kuwapandikizia vitu ambavyo hawavijuhi.