Uchunguzi wangu unaonesha wanaume tunaongoza kuwafanyia ukatili, kuwaumiza na kuwasaliti wanawake

Mkuu una pwenti kubwa sana na ndo hivyo tuko on point of no return, hamna kurudi.

UOVU NA UENDELEE azawaiz biblia itakuwa inasema uongo.

ZILE NYAKATI ZA TAABU ZILIZOTABIRIWA NA ZISHAMIRI ili neno litimie.

Eeh ubinafsi
tamaa ya fedha,
majivuno,
kujiona,
kumtukana Mungu,
kutotii wazazi,
kutokuwa na shukrani,
uovu,
kutokuwa na upendo moyoni,
kutokuwa na huruma,
uchongezi,
ulafi,
ukali,
kuchukia chochote kilicho chema,
uhaini,
ukaidi,
kujaa kiburi,
kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu....

Wooote na muendelee kwaaana imeandikwa:

"Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa namna yoyote ile, Maana siku hiyo haitakuja mpaka kwanza ule uasi utokee na yule Mwovu aonekane, ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa.
(2 Wathesalonike 2:3 BHN)

Jamani mwisho hauji mpaka uasi utokee kwahiyo mliochagua fungu hilo tunawaoomba mpambe moto Ili Mwokozi wetu arudi!

Yes it was written:

"Let the evildoer still do evil, and the filthy still be filthy, and the righteous still do right, and the holy still be holy.”
(Revelation 22:11‭ ESV)

Sahihi
 
Kwema Wakuu!

Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa linapokuja swala la kupasuana, kuumizana, kutesana, kukatiliana na kusalitiana kati ya mwanaume na mwanamke basi sisi wanaume ndio tunaongoza.

Sio habari mwanaume kumcheat Mwanamke. Hiyo sio habari. Wanaume tuna ubinafsi katika suala la kihisia. Kwamba sisi ndio tunaumia tuu lakini wanawake hawaumii. Kwamba sisi tunaona sawa tunapofanya usaliti kwa kulala na wanawake wengine. Lakini wanawake wakifanya hivyo inakuwa ni habari ya swala kula simba.

Sio habari Mwanaume kumfukuza mkewe au mwanamke wake nyumbani tena mikono mitupu tena wakati mwingine bila sababu ya msingi.
Ni unyama, ukatili, ushetani, ubaya, roho chafu ya giza.
Lakini Mwanamke akifanya hivyo ni habari.

Ni kitu cha kawaida kwa sisi wanaume kuwafukuza wanawake ambao labda wameshindwa kutuzalia watoto, au baada ya kuzaa maumbo yao yamebadilika na kuwa tukunyema.
Lakini sisi ndio tunakuwa wakwanza kupiga kelele pale Mwanamke anapotukimbia tunapofilisika.

Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa hakuna kiumbe mnyanyasaji na mkatili kama sisi wanaume. Sisi wanaume tunapopata vijisenti au kwa kigezo cha kuhudumia familia. Tunataka tuabudiwe kama miungu fulani. Hata tunapokosea hatuonyeshi kujishusha na kuwa wanyenyekevu. Tunaona ni kujidhalilisha. Ni kama tunageuka Mashetani maana shetani ndiye anakiburi cha uzima.

Unapokuwa mnyenyekevu au kuomba msamaha haiathiri uanaume wako, ubaba wako na ufalme wako. Isipokuwa unazidi kuonyesha wewe ni Mwanaume bora uliyekamilika. Unayejiamini na mwalimu bora wa kuigwa.

Hivi wewe ukikosea alafu badala ya kutafuta suluhu na kuomba msamaha hautaki, unategemea huyo mkeo au hao watoto wanajifunza nini? Unategemea mkeo naye akikosea akuombe msamaha? Thubutu! Labda huyo mke awe boya fulani, lakini Binti za Tibeli Wana react vile unavyowachukulia na kuwa-treat.

MKE mwema na bora hawezi kuwa mnyenyekevu kwa mwanaume mwenye kiburi na Mpumbavu. Binti za Tibeli nilishawaagiza nini chakufanya wanapokutana na Scenario za namna hiyo.

Kiburi cha uzima ndio unaita uanaume.
Uanaume ni akili na maarifa, upendo na Haki na kuhakikisha mambo yanaenda Sawa.

Hamtaki Wanawake washike amri ya Mungu mkuu ili wawe watumwa wenu. Amri ya kufanya kazi ndio amri pekee ambayo inamfanya mtu aweze kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Kwa sababu mtu atajitegemea na kuwa huru kuitenda haki na Kweli.

Binti za Tibeli nilishawaeleza na kuwaagiza kuwa ni lazima wafanye kazi ili waweze kumuabudu Mungu kwa roho na kweli kuliko kuabudu Wanaume wasio na Akili.

Binti Elewa, kama hutofanya kazi kuna hatihati ya kunyanyaswa na kuabudu mwanaume badala ya kumwabudu Mungu wa kweli.

Kupata Wanaume bora wa viwango vya juu ambao wanaupendo, Haki, akili na Kweli ni nadra.
Najua kuna Watu hawatanielewa!

Vijana wa Tibeli tunajua hatukuumbwa wanaume ili tuabudiwe. Hatukuumbwa wanaume ili kuwatesa wanawake kwa uanaume wetu.
Tunahudumia Wake zetu sio kwa sababu sisi ni Wanaume bali kwa sababu ya Upendo. Kama wao wanavyotuhudumia sio kwa sababu ya uanamke wao bali kwa sababu ya upendo.

Unam-cheat na kumdhulumu haki Mkeo alafu hapohapo unategemea awe anakupa tendo la ndoa. Hivi hizo akili mnatoleaga wapi?
Elewa mapenzi kwa mwanamke ni Hisia.
Mwanamke ukishaziumiza hisia zake hupoteza hisia za mapenzi. Ni lazima apone ili zirudi.

Yaani kwa akili zako ndogo, umekutwa na sms ya mchepuko, au amekufumania akaumia unategemea vile ulivyoomba msamaha na maneno yako mawili matatu basi ndio moyo wake umetulia na imeisha. Unaumwa wewe!

Usijepe Haki ya kufanya makosa. Usijepe uhalali wa kumuumiza mtu mwingine.
Usije haki ya kufanya makosa kwa Mkeo.
Kwamba kwa vile wewe ni mwanaume unaruhusiwa kuoa au kulala na wanawake wengi zaidi ya huyo uliyenaye. Kwa vile wewe ni mwanaume unahaki ya kuongea neno lolote bila kujali zuri au baya mbele ya mkeo, kwa vile umwanaume basi unarudi nyumbani utakavyo alafu muda huohuo umeweka sheria ya mkeo arudi saa ngapi. Ukiona wapi utawala wa hivyo kama sio kwa mashetani tuu? Huo ni Ushetani na kutokujali hisia za mtu mwingine. Ni ubinafsi.

Jambo lolote ambalo linakuumiza chukulia pia litamuumiza Mkeo.
Kama wewe hutaki mkeo awe na wanaume wengine, elewa hata yeye hataki. Mwanamke ni mfano wa mwanaume. Vile ulivyo ndivyo naye alivyo. Utofauti upo lakini ni mdogo. Ukilinganisha na mambo mnayofanana.

Wanawake wamejifunza tabia mbaya ya ubinafsi kutoka kwetu Wanaume. Ukisikia wanawake ni makatili au wanyanyasaji au matapeli elewa kuwa mwanaume ni mara mbili yake. Sisi wanaume ndio tumewafundisha hizo tabia za kutu hawa wanawake.

Walionielewa waendelee kunielewa. Wale ambao hawajanielewa na hawataki kunielewa hiyo ipo juu yao.

Acha nipumzike

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Uko sahihi kabisa. Kama suala la kuchepuka wanaume ndiyo tunaongoza halafu mke akisimama na mwanamme barabarani tunachukuwa hatua kali.
 
Kiranga ni kilaza wa mwisho jf kwa mujibu wa mtibeli 😂😂😂.

Mtibeli imani yako inaminya uhuru wa wengine, hebu jirekebishe na ufikiri sawasawa.
Hata mimi naamini Mungu yupo ila sio sahihi kubeza na kutweza kile wengine wanaamini.
Mengine hapo upo sahihi.

Haki ipi Unazungumzia?
Kutambua uwepo wa Watu wasio na akili kwani sio Haki?
Kutambua watu wasio na akili ni kuminya Haki zao?

Labda sijui Unazungumzia Uhuru upi?
Mimi sijakataa wala sijazuia Watu wengine kumkubali au kumkataa aliyewaumba.

Ikiwa wapo wanaowakataa wazazi wao waliowazaa wanaowaona sijashangaa sembuse wanaomkataa aliyewaumba ambaye hawamuoni.
Wana haki kwa sababu hawana ile akili ya kuona uwepo wa Mungu.

Zingatia, kinachoona ni akili(Ubongo) na sio macho.
 
Uko sahihi kabisa. Kama suala la kuchepuka wanaume ndiyo tunaongoza halafu mke akisimama na mwanamme barabarani tunachukuwa hatua kali.

Sisi ndio tunawatoa Bikra hawa wanawake na kuwazalisha na kuwatelekeza ili tuje kuwabeza.

Ingawaje pia yapo makosa ya wanawake lakini mzizi mkuu ni mwanaume kwa sababu sisi wanaume ndio chanzo cha wanawake
 
Me nadhani mwonevu wa kwanza ni yule aliewanyima hulka hio muhimu ya kiutawala...Na kama itabidi kuumia rohoni bac tambua kuwa MEN ARE GOD'S REPRESENTATIVES ON EARTH, WE ARE SACRED.

Kinyume cha God ni Satan sijui kama unajua hivyo.
Mwanaume akiwa mwema huwa ni Mungu akiwa Mwovu hugeuka Shetani.

Mada hii Unazungumzia ushetani wetu.
Umekubali kuwa sisi ndio watawala na katika utawala kuna utawala wa Mema na utawala wa maovu. Na kote huko mwanaume ndiye namba moja
 
Haki ipi Unazungumzia?
Kutambua uwepo wa Watu wasio na akili kwani sio Haki?
Kutambua watu wasio na akili ni kuminya Haki zao?

Labda sijui Unazungumzia Uhuru upi?
Mimi sijakataa wala sijazuia Watu wengine kumkubali au kumkataa aliyewaumba.

Ikiwa wapo wanaowakataa wazazi wao waliowazaa wanaowaona sijashangaa sembuse wanaomkataa aliyewaumba ambaye hawamuoni.
Wana haki kwa sababu hawana ile akili ya kuona uwepo wa Mungu.

Zingatia, kinachoona ni akili(Ubongo) na sio macho.
Akili inaonaje na wewe mtibeli mbona unazidi kupuyanga, wewe unatumia hisia unasema unatumia macho, tangu lini akili ikaacha kufikiri ikaona??

Kumuita binadamu mwenzio hana akili ilhali hujathibitisha ni sawa??
Yaani kisa mna mawazo tofauti basi umuite hana akili?

Ccm amuite chadema hana akili, chadema amuite ccm hana akili, alieoa amuite aiseoa hana akili nk.
Hapo kutakua na kuheshimu mawazo ya wengine kweli??

Mtibeli, mtu mzima akivuliwa nguo huchutama.
 
Unaweza ukawa na macho usione.
Ila huwezi ukawa na akili alafu usione.
Akili/ubongo ndio huona. Macho hayaoni.

Akili unakuwa huna kama utashindwa kutambua jambo fulani ambalo mwingine analitambua na lipo.
 
Jamaa yangu kuona ni kufanyaje, au kuna maana zaidi ya moja ya neno kuona bila kuhusisha macho?

Utambuzi hufanywa na ubongo, kuona kunaafanywa na macho.
Baada ya kuona akili ndio hufanya utambuzi kujua kile kilichoonwa na macho.

Kipofu huwezi sema kaona, ila anahisi kwa njia mbalimbali, nae pia akihisi akili hufanya utambuzi.

Mambo ya Mungu yanakupotezea ufikiri ndgu mtibeli, wakati mwingine tumia akili yako na sio hisia zitokanazo imani yako mpya/uliyoificha kwa kipindi kirefu.
 
Kinyume cha God ni Satan sijui kama unajua hivyo.
Mwanaume akiwa mwema huwa ni Mungu akiwa Mwovu hugeuka Shetani.

Mada hii Unazungumzia ushetani wetu.
Umekubali kuwa sisi ndio watawala na katika utawala kuna utawala wa Mema na utawala wa maovu. Na kote huko mwanaume ndiye namba moja
cjui kama nakupata vizur ....Me nafkir hulka ya kimungu huwa haina makosa ndo mana mungu akikuumba na macho mawil tnasema yupo sawa lakn akikufanya kipofu pia tnasema mungu hakosei ..Kwa mantiki hii mwanaume kama mwakilish wa mungu hawez kuw n ushetani vinginevyo kanuni yako ianze kushughulika na mungu aliewapa mikono hawa na kuwanyima chakula wale.
 
Jamaa yangu kuona ni kufanyaje, au kuna maana zaidi ya moja ya neno kuona bila kuhusisha macho?

Utambuzi hufanywa na ubongo, kuona kunaafanywa na macho.
Baada ya kuona akili ndio hufanya utambuzi kujua kile kilichoonwa na macho.

Kipofu huwezi sema kaona, ila anahisi kwa njia mbalimbali, nae pia akihisi akili hufanya utambuzi.

Mambo ya Mungu yanakupotezea ufikiri ndgu mtibeli, wakati mwingine tumia akili yako na sio hisia zitokanazo imani yako mpya/uliyoificha kwa kipindi kirefu.

😃
Mkuu nafikiri haya mambo yanahitaji uwe mzuri wa falsafa.
Kuona ni kutambua. Na macho hayawezi kutambua taswira ambayo macho yametazama.

Ubongo/akili ndio hutoa tafsiri, hutambua, husikia, huonja, hunusa.

Akili au ubongo wako ukigeuzwa iwe kwa madawa au kufanywa ndondocha unaweza ukawa na macho lakini usione.
Ubongo ndio unataswira
 
Jamaa yangu kuona ni kufanyaje, au kuna maana zaidi ya moja ya neno kuona bila kuhusisha macho?

Utambuzi hufanywa na ubongo, kuona kunaafanywa na macho.
Baada ya kuona akili ndio hufanya utambuzi kujua kile kilichoonwa na macho.

Kipofu huwezi sema kaona, ila anahisi kwa njia mbalimbali, nae pia akihisi akili hufanya utambuzi.

Mambo ya Mungu yanakupotezea ufikiri ndgu mtibeli, wakati mwingine tumia akili yako na sio hisia zitokanazo imani yako mpya/uliyoificha kwa kipindi kirefu.
Leo mtibeli kaingia cha kike
 
Hivi ukatili ni nini.?!maana siku iz mwanaume ukiwa na misimamo thabiti juu ya mwanamke tayari unaitwa mkatili,sasa neno ukatili kwa sasa mara nying linafujwa!!wanaume wenzangu tusimame imara,vita ni vikali lakini tutavishinda, full stop

Msimamo sio kitu kibaya.
Hasa msimamo katika mambo Mema.
Lakini sio mambo ya kipuuzi na akili za kijinga.
 
Back
Top Bottom